Simba iliweka historia katika Tanzania kwa kuifunga Yanga mabao 6 Julai 19, mwaka 1977. Abdallah Kibadeni alikuwa nyota kwa fufunga mabao matatu ( dakika za 10, 42 na 89) Jumanne Hassan ‘Masimenti’ alifunga mabao mawili katika dakika za 60 na 73 na kutokana na ‘kiwewe’ cha Yanga siku hiyo, mlinzi wao Selemani Sanga alijifunga katika dakika ya 20.

Kipa alikuwa - Athumani Mambosasa,
beki wa kulia, - Shabani Baraza,
wa kushoto - Mohamed Kajole,
wa kati Athumani Juma na Alloo Mwitu,
viungo Khalid Abeid, Haidari Abeid,
wing wa kushoto Abasi Dilunga,
kulia Willy Mwaijibe,
washambuliji Abdallah Kibadeni na Jumanne Hassan Masimenti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hivi Simba iliifunga Yanga mabao hayo mwaka 1977 au mwaka 1973? Nakumbuka kama ni 1973 hebu jaribuni kuchunguza kwa makini

    ReplyDelete
  2. Simba ya zamani ilikua inakula nyama, Ya sasa hivi inakula majani naona.

    ReplyDelete
  3. Nakumbuka ilikuwa 1977

    ReplyDelete
  4. KABADA KADINDADecember 05, 2009

    MBONA UMEWASAHAU KINA HALFANI NGASA ERIKI SAGARA JOHN MAKELELE NA MOHAMEDI MWAMEJA WOTE HAO WAMEZALIWA KATI YA MIAKA YA 1973 NA 1977, SIONI LISTI YAO?

    ReplyDelete
  5. Ni 1977,kwani 1973 waliifunga bao moja bila na kutwaa ubingwa wa nchi mfungaji akiwa ni Haidar Abeid"Muchacho".

    ReplyDelete
  6. Wewe uliyesema Simba wa siku hizi anakula majani,Kaa ukijua Simba ni Simba tu usimuone amekaakimya ukadhani ni Kondoo,na usimuone amelala ukamchezee Sharubu.Angalia anavyowagaragaza mwaka huu kwenye hiyo ligi yao.
    Mwana wa Msimbazi-London

    ReplyDelete
  7. Kabada Kadinga
    kama umezaliwa kati ya 1973 na 1977 wakati mechi inachezwa maximum utakuwa na umri wa miaka minne, hiyo ndio sabau hawamo kwenye list, bado walikuwa wananyonya.

    ReplyDelete
  8. Kaka mbona hutaji na list ya Yanga ya Kuokoteza maana ndio wakati huo Yanga iligawanyika first eleven yote ikaondolewa. nawkumbuka wachache waliocheza siku hiyo:
    1.Muhidin Fadhil
    2.Rajabu Tangale
    3.Sefu Matege
    4.Selemeni Saidi Sanga
    5.Omar Jongo
    6.Sam Kampambe
    7.Shabani Katwila
    8.Bonamax
    9.Yanga Fadhil Bwanga
    10.Ezekiel Grayson (Juju man)
    11.Rashid Hanzuruni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...