Ndg. Wadau,
Hawa watoto wanakula vyakula ambavyo wengi wengi wetu hawawezi kuvigusa (maharage ya chukuchuku na chai ya mkandaa) ndio chakula chao cha mchana. Hizi picha nilizipiga hivi karibuni katika moja ya vituo vya kulelea mayatima hapa Dar.
Swali LANGU; Sijui ni watoto wangapi kama hawa wasio na makazi wanaoweza kulishwa na kuelemishwa kwa Shillingi Billion Moja?
John Mashaka
Dar –Es-Salaam, Tanzania.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 53 mpaka sasa

  1. Wacha uchochezi wewe. Uza yako uwasaidie.

    ReplyDelete
  2. Shilingi bilioni moja ingetosha kuwahudumia watoto wengi sana yatima siyo kwa chakula tu, hata afya na elimu. Lakini bahati mbaya bwana mashaka, hiyo hela tumeitumia kukarabati nyumba ya Gavana.

    ReplyDelete
  3. ubunnge utapata tu

    ReplyDelete
  4. HAYO NI MAENEO AMBAYO SERIKALI WALITAKIWA KUYAANGALIA KWA KIASI FULANI.

    KWA BAHATI MBAYA AU MAKUSUDI HAWAKO HUKO NA BADALA YAKE WAMEWAACHIA NGOS AMBAZO NDIYO HUWASAIDIA HAO YATIMA KWA MSAADA WA WAHISANI WA NJE AU NDANI.

    SASA KWA KUKWEPA MAENEO KAMA HAYO HATIMAYE HUONA KAMA WANA FEDHA NYINGI ZA ZIADA AMBAZO BAADAYE HUANZA KUZITUMIA BILA UMAKINI WOWOTE.

    MATOKEO YAKE NDIYO HAYO YA KUMJENGEA GAVANA WA BENKI KUU NYUMBA YA BILIONI 1.4.

    ReplyDelete
  5. mzee krismas njema bongo. ndo umekwenda kimoja au uko vekesheni kama analivyojisemea ankal

    ReplyDelete
  6. senkyu SO MUCH MY BrozA NaBiI YOHANA MASHAKA zis is the ril tanzania ya mafisadi AND ZE KORaPTI. heri wewe umesoma MUZUMBE UNAELEWA ZAIDI mkuu asante sana. SASA KAMA WEWE UTAKUWA LAIS utafanya nini FOR ZE PIPO LIKE ME WU IZ NOT ZE MUZUMBE GLADUETI

    ReplyDelete
  7. joni mashaka mkuu umerudi, karibu sana jamvini kutapendeza sana, aisee tumekumisi sana, za wapi naona umeandika dar, huko maeneo gani tutafutane nasi tubadilishane mawazo??

    ReplyDelete
  8. yaani kwa mahesabu yangu ya juu juu, nadhani tungesomesha watoto kama 2,000 kwa shillingi billioni moja ambayo imekarabati nyumba ya gavana. safi mashaka, tuma picha zingine!

    ReplyDelete
  9. Swali la Kizushi?
    Huyu Mashaka analipwa hela kiasi gani, kwa sababu kila baada ya mizi mitatu yuko Tanzania kutoka marakani alafu anagawa u-nan profiti yeye na Hasheem? Nauli najua ni kama $3,500 au $4,000 kwa hiyo atakuwa analipwa hela ngapi wajameni, nielemisheni,hao ndo wale wanakarabati nyumba zao na billioni 1.4??? swali langu mzinimeze!!

    ReplyDelete
  10. Kumbe Bw.Mashaka anaweza kuongea Kiswahili pindi uchaguzi unapo karibia ili wapiga kura tumuelewe...hahahaaa!!

    Ni afadhali umeligundua hilo mapema, kwani makala zako ulizokuwa ukiziandikia kwa kizungu, walielewa watu walioko nje ya nchi tu ambao hawatakuwapo siku ya kupiga kura.

    Haya..kazi kwako kiongozi kuchagua mchele na pumba.

    ReplyDelete
  11. John mashaka ni kijana makini sana Tena mwenye huruma sana. Hana majigambo. Sijui ni vijana wangapi wenye nafasi nzuri Kama Yale wanaoweza kuja nyumbani kula krismasi na mayatima. Huu ni utashi na hekima kubwa aliyopewa bwana mashaka. Namtakia kila la kheri maishani mwane na kwenye shuguli zake huko marekani

    ReplyDelete
  12. IT SAD MASHAKA. HAO WANAOSHINDIA MAHARAGE TU. KUNA AMBAO HATA MAHARAGE HAWAYAPATI TALK ABOUT ONE BILLION FOR HOUSE RECONDITION. HAA ONLY IN TANZANIA NA BADO. TUTAISHIA KWA MICHUZI TU.

    ReplyDelete
  13. Huyo anayelisha mtoto ndo huyo mwenye kapero alebaba mtoto ndo Jon mashaka? Hapo si ni pale msimbazi senta

    ReplyDelete
  14. Jamani ndo chakula cha hao watoto wakati mafisadi yanakarabati nyumba zao na billioni moja. Walahi nchi yetu imehoza na huko siludi wala watoto wangu hawakanyagi. Ngojeni tuwe watumwa UK lakini hayo maisha yanauUnisha sana

    ReplyDelete
  15. Bwana asifiwe. Mashaka kusema kweli mwenyezi Mungu atakulipa kwa ukarimu wako
    unagusa sehemu ambazo wengi wanaziogopa
    endelea malipo yako yako hapa hapa duniani
    waache wajennge hata na maekalu ambazo hazitakuwa na
    Amani ndani.na wala hawatapata usingizi

    ReplyDelete
  16. Mafisadi dhidi ya Wana wa mungu
    mashaka John ubarikiwe

    ReplyDelete
  17. WAPO WATU AMBAO WAMEBARIKIWA NA UWEZO WA KUZUSHA JAMBO DOGO TU NA KUZUA MJADALA MKUBWA SANA. MASHAKA KAUZLIZA BILLIONI MOJA INAWEZA KULISHA WATOTO WANGAPI KUTUMIA PICHA LAKINI NINA UHAKIKA HADI KESHO KOMENTI ZITAKUWA SIO CHINI YA 70. KAWAIDA YA JONH MASHAKA WALA SISHANGAI, HAYA BWANA WENYE NGUVU ENDELEENI

    ReplyDelete
  18. mkuu wa wabeba boxi wewe kweli ni mfano wa kuigwa. mwenzio hasheem thabeet na afuate nyayo zako. muhache kutuletea picha za makamuzi h-towni, mtuletee vita dhidi ya ufisadi ndo nitawakubali

    ReplyDelete
  19. Niliwahigi kutoa comment kwamba Tanzania inahitaji John Mashaka Wanne na Shayo wawili Tu na nchi yetu itaondoka katika dhiki tuliyomo saha hivi
    Hii nchi imekwisha kusema kweli Billioni 1.4 kukarabati nyumba wakati watoto wadogo tena wachanga kama hawa wanashinda njaa?
    Msicheze na maisha ya tu nyie mafisadi. mungu si athumani
    Malipo yatakuwa mabaya, mtalipa hadi vitukuu vyenu kwa vitendo vyenu vya kuwaua watoto wasio na hatia

    ReplyDelete
  20. Shillingi Billioni Ingelipia Benzi la fisadi

    ReplyDelete
  21. mkulu mashaka karibu tena

    ReplyDelete
  22. Hiyo hela ndogo sana, ni vijisenti. Haitoshi hata kujenga nyumba ya gavana 'from ground up'. Tuseme mlo wa siku ni buku tano. Bilioni moja ni mlo wa watu takriban 550 kwa mwaka mmoja.

    ReplyDelete
  23. Bwana Kasema mjijushe muwe kama watoto wadogo. Mashaka kweli umejishusha kiasi cha kwenda kwenye kituo cha mayatima na kumbemba mtoto mdogo asiye na baba wala mama.
    Wengi hawawezi kuamini kwamba yule mwandishi wa makala makali anaweza kukaa na watoto hivi na kuwa mtu wa kawaida, aisee nimekubali mungu anamtumia huyu jamaa.
    naona bahati aliyonayo kapewa ili kutumikia masikini. mashaka mie nipo tayari kuja huko kwenu tarime nikupigie kura ikiwa utagombea ubunge.
    Pengine gavana ataiona roho yako na kuihama hiyo nyumba akaishi kwenye nyumba yake badala ya kutumia hela za hao watoto wanashinda njaa na kula chakula kama hicho
    mafisadi walaaniwe

    ReplyDelete
  24. oh...............my Gosssssssssssshhhhhhhhhhhhh, i cant believe that is all they eat

    ReplyDelete
  25. ,, nawezaje kuchangia kwa hawa mayatima? mie naishi sweden, naweza kutma hela, jamani, this is sad,,

    ReplyDelete
  26. yaani mashaka anakuja likizo kula na mayatima,,, mkuu hii poa sana mie pia nitafanya hivyo mwakani aisee,, hongera you are my hero. sasa mbona kapero tena??

    ReplyDelete
  27. steve kanumba fanya hivyo na wewe tukuone, au unasubiri mtoto wako wa chupa?

    ReplyDelete
  28. Yes mashaka, your message is very simple but strong and very powerful. what can a billion dollar do in this poor and torned country? i have cried to see the food in that plate, yet a billion built our governer's mansion you.

    are my hero and incredible human

    Some cannot find Hope due to the conditions in which they live. In your hometown, your city, your country, your world people die daily from starvation due to the lack of available food.

    This applies to both material food and spiritual food. How can you help? What is waiting at the other side of the rainbow?

    You can discover that each person has a ministry. Individual efforts to fight the world hunger situation we face must be addressed with all that you are given.

    You can personally deliver groceries to those in your city. Others have been blessed with no time; yet have finances, which they can share so others can distribute food.

    Many have no extra money, yet they have God's greatest gifts, which are spiritual. Use what God has given you to feed the needy, both physically and Spiritually.

    Please let the Holy Spirit be your guide! As you are obedient to the Lord, no matter how much or how small your time allotment or gift, you can be used of God to change the world!

    seth, kigamboni

    ReplyDelete
  29. sasa unauliza billioni moja italisha watoto wangapi? wewe yale magari yako yale ukiyauza yatalisha wattoto wangapi, tangu lini kipofu kamuita mwensie kipofu wakati wote hamuoni, Mercedes 2010 inathamni gani Benz E550 Coupe? yale yale, wabongo hawajambo hapa kanajifanya yeye mtu wa chini anayekula na masikini ili apate kura ubunge hupo kwenye kona

    ReplyDelete
  30. Anony Wed Dec 30,08:33:00 AM acha ushabukuku hiyo E550 ni yake kwa jasho la fedha yake na isitoshe anasaidia pia maskini! Hatukatazi watu kutajirika ila isiwe juu ya migongo ya pesa za walipa kodi!

    ReplyDelete
  31. Umeuliza swali la changamoto na la kufikirisha sana Mashaka hasa kwa kuzingatia mauzauza ambayo yamekuwa yakiendelea katika jamii yetu. Nafsi zetu zitatuhukumu hata tukiwa wabishi wa namna gani.
    Fanya uwezalo kwa uwezo ulio nao, mengine yana wengine. Tenda wema na uende zako.
    Naunga mkono juhudi sana na jitihada zako zote ufanyazo katika kuisaidia jamii!

    ReplyDelete
  32. jamani kukarabati nyumba wanazo ila kujenga barabara kama zile za uchochoroni kijitonyama-africa sana, ustawi-sayansi-new bagamoyo road, samnujoma-sinza mugabe, external nyerere rd-ubungo maziwa, external nyerere rd-mburahati, mburahati-kigogo via royora, NIT mburahati-kigogo via sokol amburahati, mbezikavu-mbezi beach via Masana hospitali, Mbezi kavu-wazo via makabe, vitanda vya hospitali ya mwananyamala, Muhimbili, ilala, temeke, tumbi, wajawazito wanaokufa kwa kukosa huduma, dawa zinazouzwa bila wasio na pesa kuwa nazo shule za kata kwa watoto wa masikini, hali watoto wa wenyepesa wanasoma st meriiz halafu wakifaulu division four walipie hali wa wenyepesa waliosoma kwenye st meriiz na kupata div wani wakapata mkopo, hivi vyote haviwezi kutekelezwa kwa kuwa serikali haina pesa ila hela za kukarabati nyumba zipo na twin tower zipo na za EPA zipo na vijisenti zipo na Radar zipo na magogo zipo, na ngorongoro zipo, na maghorofa wilaya za baridi mkoani TA, etc etc

    Ole wako michuzi uniweke kapuni kama ulivyozoeweya weye!

    The 2015 Minister of Science and Technology

    ReplyDelete
  33. Michuzi kumbe hufai kabisa yaani kwa vile comments zangu ni kinyume na wanaomsifu Mashaka unaziminya.

    Unajua kuwa huo nao ni ufisadi wa mawazo ya watu kwa faida yako binafsi.Hakika nimekushangaa sana!

    Nasema kuwa, kama wengine wanavyomsifu Mashaka mimi simsifu maana hapaswi kuuliza maswali ya kizushi. Na mtu anayejinyanyua huwa simfagilii kamwe.

    Huo ni mtizamo wangu kwa nini unizuie na kuachia zile comments tu za kumwita eti nabii, mara ana fedha nyingi sijui amejishusha, sijui ana akili nyingi na upuuzi kama huo.
    Hatutishani lakini nakueleza kuwa kwa trend hii unaonyesha udhaifu mkubwa sana kama mwanahabari.

    Michuzi nimekushangaa sana na unastahili kuniomba msamaha.

    Unaweza minya na hii ukipenda.

    ReplyDelete
  34. Wewe hapo juu unaongelea 2010 E550 coupe Mercedes benz mbona bei yake haitishi ni kama $85,000 na kama una good credit unalipia kwa mwezi $1120 kwa mwezi for about 5 years, wewe huoni ccm wamenunua magari ya zaidi ya millioni mia per vehicle and about 200 vihecles, waambia wao wauze walishe mayatima.

    ReplyDelete
  35. serikali imevaa sura ya hajaliwi mtu! mipango ya hovyo,chukua chako mapema anayeleta fyoko mzime haraka.
    watoto kama hawa haishindikani kuwaelimisha.lakini hata leo hii serikali ikiamua kufanya kampeni kwa kuwasaidia si itaishia kuwatelekeza kama ilivyo telekeza baadhi ya vijana iliowapeleka kusoma ugaibuni? wanapigwa baridi na sijui wanakula snow!so sad and a pity to have such a government. yaani ni aibu kabisa kwa watu wasomi kushindwa kuwa na priorities ktk mambo.

    ReplyDelete
  36. @wewe wadhi kanye. hacha uroho mbaya na wivu wa kike, andika makala yako tukusifie, siyu kumuandama mtu na kumlaumu michuzi, heti umesikitiaka na michuzi kuombe radhi thubutu yako.nenda kale vumbi au kabebe boxi michuzi aombi radhi ng'o. nadhani kinachokuuma ni wanajamvini kumfagilia mashaka. kwa taalifa yako, mashaka atazidi kufagiliwa hadi siku ya kihama kwa hiyo na uzoee, na ukiweka komenti ya kashfa natupwa kapuni, kwani wewe ni special kuliko US-blogger yeye komenti zake ziwekwe kapuni ila kibaka wewe ndo uwekwe hewani?

    ReplyDelete
  37. Gavana wa BoTDecember 30, 2009

    walimwengu ni watu wa ahjabu sana. ukiwa masikini watakucheka na kukusimanga, ukiwa nacho kidogo watasema siku hizi unaringa na unataka umaarufu. mashaka kauliza swali rahisi tu je billioni 1 ingelisha watoto wangapi wengine wameanza kuzungumzia benzi zake, kwani hizo benzi mlizilipia kodi? waacheni wamerakani amuulize kwamba alizinunua na hela gani,,, wizi mtupu

    ReplyDelete
  38. john mashaka big up bro,, you are my hero fo r the good work you are doing for the people of tanzania. i am very proud of you my btoher, dont give up

    ReplyDelete
  39. yanga tuko juu

    ReplyDelete
  40. bongo tambarare.mafisadi ndo wenye maisha, nyumba ya billioni 1 ni sawa na kufuga majambazi 1000 ambao watakuja na AK47 kulivunja na kuchukua roho za mwenye nyumba

    ReplyDelete
  41. mashaka mwenyezi mungu atakuongoza tu wala usihofu hawa wachache, hasa huyu ibaka anayemlahumu michuzi

    wata kama hawa wapo katika kila jamii, sasa sijui hiyo picha inamuuma nini. hivi ulitumia kamera yake kupiga hizo picha? binadamu bwana

    Mswazi

    ReplyDelete
  42. mdau unaeshangaa mashaka kuendesha merc benz e55...kama anafanyakazi wall street as inestment banker na anaendesha hio gari kweli jamaa si mtu FLASHY...in other words hio gari ni ya kawaida sana kwa watu wa wall street

    ReplyDelete
  43. Mashaka angekuwa jirani yangu, ningehama hiyo neighbourhood kwa sababu ya foleni. Hapa hajasema kitu kikubwa lakini wajuaji wakaanza mashambulizi kila kona
    haya Mimi kula siku nasemaga kwamba wenye nguvu wapishe. Dr. Shayo yuko wapi

    ReplyDelete
  44. MASHAKA SEEMINGLY HAS AN ALTRUISTIC PERSONALITY,I COULD SENSE THIS FROM ACTIVITIES HE DOES.I FEEL COMPELLED TO FULFIL THESE SORTS OF RESPONSIBILITIES TOWARDS UNDER PRIVILAGED.

    THE ONE BIL TSH COMES IN FOR SCATHING ATTACKS FROM ADVERSARIES DUE TO ITS POTENTIAL SIGNIFICANCY IN ADDRESSING OPPOTUNITY COSTS AND HOW THE SUBJECTS FAILED REMARKABLY TO TRANSPIRE THE EXTENTS OF THESE COSTS.THERE ARE ENDLESS COMPLICACIES AND NITY-GRITTY OF THE CAPITAL EXPENDITURE DECISION BY THE BOT BOARD,AND SURELY,THERE IS NEED TO REVIEW BOARD MINUTES.

    YOU AND I AND SOME OTHERS,KNOW HOW AND THIS SUBSTANTIAL SUM COULD BE EXPENDED APPROPRIATELY TO BRINGING ABOUT RELIEVES AND CHANGE TO MANY OF ORPHANAGES IF IT WAS ALLOTED FOR THIS SPECIFICITY.

    IF I WERE ASKED,EXACTLY WHAT I WOULD DO WITH THE OUTLAY,SHORTLY,I WOULD THINK OF THE LONGTERM ASPECTS OF THE LIVELIHOOD OF ORPHANS WHISLTLY UPRGADING THE QUALITY OF THEIR BASIC NEEDS AND SPOTTING AND DEVELOPING THEIR CAREER POTENTIALITIES.MY STRATEGIC FOCUS WITH THE EXPENDITURE WILL ENSURE THEIR SUSTAINABLE DEVELOPMENT.

    I COULD PRESENT METHODOLOGIES AND THE INVESTMENT OPPORTUNITIES IN RELATION TO THE OUTLAY IN BUSINESS CONTEXT SUCH AS UNDERTAKING WORTHWILE PROJECTS WITH POSITIVE NET PRESENT VALUES AND ASSESSING RISK,RETURN AND VALUE,BUT I MIGHT BE DIVERTING TO MORE COMPLEX ASPECTS THAT AN ORDINARY PERSORN WOULD NOT COMPREHEND.THIS IS PRESUMAMBLY HOW AND WHY I WOULD PREFER TO TAKE THE LONGTERM ROUTE FIRST WHILE ORGANICALLY ENHANCING THEIR CURRENT STATE.

    ANYWAY,I APPLOUD YOUR EFFORTS AND PHILANTROPIC ACTIVITIES AND I WOULDN'T THINK OTHERWISE IE AS TO WHY YOU'RE DOING THIS.I REQUEST ALL CYNICISM TO CEASE ONLY TO LET YOU GO ON UNSTOPPABLY IN FULFILLING YOUR AMBITIONS.

    TO STRESS KEENLY,IFF YOU FIND THAT HAD YOU BEEN IN A CERTAIN SITUATION OR POSITION TO INFLUENCE THE GVT EITHER THROUGH PARLIAMENT DEBATES OR CORPORATE POWER,YOU'D NEED TO CONSULT BLOGGERS AND 7MIL VIEWERS IN MICHUZI BY FLANKLY DECLARING YOUR INTENTIONS.I WILL SUPPORT AND PROBABLY JOIN YOU.

    HAPPY NEW YEAR TO EVERYONE.

    Mdau(John)uk
    daskim@hotmail.com

    ReplyDelete
  45. mbegu haina ya mashaka ni adimu sana. ni mtu mwenye upendo na badala ya kuwa na watu kama huyo @wadhi kanye ambaye haeleweki ni nani, angejaribu kumuiga na kujifunza kutoka kwake. nchi yetu inaoza na tunahitaji wahamasihsaji

    ReplyDelete
  46. mie nawahita vijana wetu mahiri kama

    John mashaka
    dr. shayo
    January Makamba
    John MdAU (UK)

    na wengine wachache waungane waanze kuivamia hii ufisadi. hawa ndio wakombozi tanzania inaowategemea. nendeni mkawalishe watoto mayatima

    John Mashaka, Hildrebrand Shayo, January Makamba na wengine wachahceh msiogope, umma uko nyuma yenu. vamieni ufisadi unaitafuna nchi na karibuni tutakuwa mifupa tupu

    ReplyDelete
  47. Dr. Shayo
    John Mashaka
    January na Mdau John (UK)
    unganeni mfanye kazi pamoja, taifa linawahitaji, msiogope kwani atakaowalinda ni sisi wananchi. tumechoshwa na mafisadi

    ReplyDelete
  48. Wadhi Kanye acha kuleta ushamba wa Kanye West hapa. Unamshambulia Michuzi bila sababu ya maana.

    Hii blog siyo ya "the utamu" ni lazima awe ana-edit comments.

    Hata mimi huwa anaminya baadhi ya comments zangu lakini baadaye niki-review huwa nagundua kuzidisha ukali wa maneno.

    Kuwa mtaarabu, usituchafulie hali ya hewa.

    ReplyDelete
  49. Huyu wadhi kanye ni mtu mmoja wa ajabu sana. Kinachomsumbua ni wivu siyo mashaka. Hawa ndo wale ambao itakuwaje yeye na siyo mimi. Mashaka ka panchi kwa bidii na ujanja wake wewe utakuwa mungu kumnyang'anya mtu bahati yake. Huyu wadhi kanye ndo Yule tz secret agent. Shenzi jinga sana aishie zake huko heti anamtishia michuzi. Kama anamchafua mashaka basi akaanzishe blogu yake ahache mambo ya wivu na kutumia blogu yetu. Aendelee alafu tumtoe jina lake huyu mjaluo. Mijitu mingine bwana

    ReplyDelete
  50. Libuburu (Mtwara)December 30, 2009

    Hi wasomaji,
    kuna mdau mmoja anauliza Dr shayo yu wapi? Jibu ni kuwa alikuwa tanzania mwezi wa tisa hadi wa kumi na moja. Nilikutana naye akifanya kazi za kujitolea maeneo ya Liwale huko Lindi. Niliweza kumgundua kwa vile niliwahi kuona picha yake kwenye hii blog ya jamii. alikuwa anajichanganya kiasi kwamba huwezi ukaamini ni yule mtoa mada nzito tunazozisoma huku kwenye hii blog ya jamii.

    Mawazo yangu, hawa vijana wameshaona mbali, na kwa kweli wanatupa hisia za kupenda kufanya kazi.

    ReplyDelete
  51. Mbona sinamsikia Dr. US Blogger akisema mawili matatu ama Ankal umemfanyia ufisadi wa comment?

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  52. Mkendya ( Lisbon)December 31, 2009

    Hi, kulikoni Dr shayo kwenda kufanya kazi ya kujitolea Liwale alikozaliwa Marehemu Rashidi kawawa? Kwa nini hukuenda kujitolea kwenu Kilimanjaro?
    au unataka kusema alikuwa karibu na Mzee kawawa?

    ReplyDelete
  53. Huyo wadhi kanye ni wivu tu. Akajinyonge bwana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...