Mjumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chipukizi wa UVCCM toka Wilaya ya Morogoro Vijijini kichama , Kasimu Hamis ( kulia) akitumbukiza kura yake kwenye sanduku la kura wakati wa kuwachagua viongozi wa Chipukizi Mkoa wa Morogoro leo kwenye ukumbi wa ofisi ya CCM Mkoa huo
Katibu wa Umoja wa Vijana wa UVCCM Mkoa wa Morogoro, Lucia Mwiru ( wapili kulia) akimnong’oneza Mwenyekiti mpya wa Chipukizi Mkoa wa Morogoro , Masuda Nassoro leo baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo na msimamizi wa uchaguzi , Pili Jabiri ( kushoto) ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa UVCCM toka Mkoa wa Morogoro pamoja na Kamati ya Utekelezaji Taifa. Picha na mdau John Nditi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. sio mbaya kuwapa sumu mapema, ndio wapiga kura wa kesho hao, uwekezaji wa wapigakura wa baadaye

    ReplyDelete
  2. Anything to do with Kingunge Ngombale Mwiru?

    ReplyDelete
  3. Najaribu kupata picha ya huyu "Yanki" akijafikwa na Baleghe itakuwaje, ka leo kshaanza kuvaa magwanda ya namna flani hivi. Dah, huwaga sijui nawaonaje jamaa wanaovaaga magwanda ya namna hiyo na wale wanaovaaga mavazi ya Mgambo au askari wa jiji.

    ReplyDelete
  4. THAT IS VERY DANGEROUS, STOP TOTURING KIDS, THEY NEED TO PLAY AT THAT AGE, DONT CONFUSE THEM WITH UNTHINKABLE AT THEIR TENDER AGES. HUO NI WAKATI WA KUFURAHIA UTOTO, NANI KALETA WAZO MFU HILO, KINGUNGE NINI?

    ReplyDelete
  5. Jamani hebu tuwaache watoto wawe watoto. Kuanza kuwavuruga akili na mambo ya vyama kipindi hiki ni kupandikiza magonjwa tutakayokuja kuyajutia baadaye.

    ReplyDelete
  6. Unazi ulianza hivihivi Ujerumani! Unawalisha itikadi watoto wakiwa Wakubwa hawaoni haki za vyama vyengine

    ReplyDelete
  7. badala ya kujiunga na clubs za maana kama maths club, english debating club, poetry clubs, robotic clubs, wanapeleka watoto kwenye chipukizi.

    ReplyDelete
  8. these people are not serious, kama wanajua umuhimu wa grassroots za CCM, basi na Taifa Stars wangeanza kujenga talent mapema.

    ReplyDelete
  9. Kama Palestina watoto WANAZALIWA NA KUFUNDISHWA KWAMBA WAYAUDI NI ADUI hata kwetu ni hivyo watazaliwa wakijua tu chama kinachotakiwa kutawala ni CCM

    ReplyDelete
  10. huu hi ututusa kabisa!

    ReplyDelete
  11. je, sheria ya kumlinda mtoto iliyopitishwa hivi majuzi na bunge la muungano inalizingatia hili au la? ni unyanyasaji wa wototo chini ya umri wa miaka 18 kuwalisha kasumba ya siasa. wanaweza kufundishwa somo la uraia shuleni na hata kuunda serikali za wanafunzi mashuleni kuwapa misingi ya kupanga mipango na kuendesha shughuli zao lakini sio kasumba ya vyama vya siasa.

    ReplyDelete
  12. Jamani, hawa watoto ni wadogo sana na ni mapema sana kuanza kuwachanganya na habari za vyama.Kwa mtindo huu,watoto wanafungwa akili na kuwa na uelewa mdogo sana kuhusu vyama vingine.Waacheni umri ukifika watashiriki chaguzi nyingi za vyama,acheni kwanza wasome ili waandae maisha yao ya baadaye.

    ReplyDelete
  13. This is wrong! Waacheni watoto wawe watoto. Chipukizi ilipaswa kuwa jambo la watoto bila kuzingatia itikadi za kisiasa. Mtoto mdogo mnaanza kumlisha mbegu za ufisadi. Huu mchezo ukome. Chipukizi inatakiwa kuwa kama skauti.
    Kila chama cha siasa kikianza kujipeleka shule za msingi kutafuta watoto wa kujiunga na 'chipukizi' wao watoto watapata wapi muda wa kujifunza mambo ya darasani na mengine ya kimaisha?
    Asante mkuu wa libeneke kwa kuianika hii. Message sent.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...