SWALI: Kama ungepata nafasi ya kuonana na Mh.Rais ni jambo gani la kwanza ungependa kumshauri ama kuzungumza naye?
MAGAVILLA: Kwa mtazamo wa nje kwanza napenda kumpongeza kwa juhudi zake na ninaamini kazi ya utawala si kazi rahisi nafikiri ugumu wake unakuja pale ambapo hata wale ambao pengine hawapo katika utawala nao wanakuwa wanajijengea dhana ya utawala katika utawala mara nyingi kazi au uchungu wa mzazi ajuaye mzazi.
MAGAVILLA: Kwa mtazamo wa nje kwanza napenda kumpongeza kwa juhudi zake na ninaamini kazi ya utawala si kazi rahisi nafikiri ugumu wake unakuja pale ambapo hata wale ambao pengine hawapo katika utawala nao wanakuwa wanajijengea dhana ya utawala katika utawala mara nyingi kazi au uchungu wa mzazi ajuaye mzazi.
Kwa hiyo mimi siwezi nikamsemea kwa undani yale ambayo anapitia kama kiongozi ila kwa upande wa mambo ambayo nadhania ni muhimu na pengine nikumbushe tu kwa sababu nadhani kuna juhudi nyingi ambazo zimeelekea huko ni suala la elimu na hamasa kwa vijana.
Na mimi namsifu sana Mh.Rais kwa sababu amejaribu sana kuweka ukaribu na vijana na hajawaacha mbali ila ninamuomba aendelee na asichioke katika kuwekeza katika elimu na hamasa kwa vijana hamasa chanya kwa sababu sasa hivi mazingira yalivyo yanawaelemea zaidi vijana ambao hawana mtazamo tofauti.
Haya matukio ambayo wengine wanaweza wakawa wanayapuuzia ambayo wanaweza wakawa wanaufaika nayo kwa nafsi zao hawajui kwamba kwa ujumla wanaokuja kuathirika kwa asilimia kubwa zaidi ni vijana wadogo ambao wao watakuwa wanakosa maarifa. Watakuwa wanakosa ndoto ambazo zinamuono wa mbali na jamii inajengwa kwa kuwa na vijana wenye muono wa mbali vijana amabo wanaweza wakathamini maisha yao ya baadaye kana kwamba wakaona kwamba maisha yao ya sasa ni kitega uchumi kwa ajili ya huko waendako ....
mahojiano kamili
who is this guy?
ReplyDeletejamani tusaidieni wengine
mdau Canada
MENEJA MASOKO WA KAMPUNI YA ZAIN
ReplyDeleteYuko Zain Tanzania, nafikiri ni Meneja masoko (sina hakika sana kama kuna mwenye kufahamu zaidi cheo chake Zain tofauti na hiki aseme).
ReplyDeleteNi kijana hodari na mchapakazi. Ni mtunzi pia wa vitabu vya mambo ya management.
Ila kwa hapa amekuwa too soft!!! Naweza kusema ame-comment kinafiki.
ni nani hiu mmoja hapa jijini daresalamu ndugu yangu ....
ReplyDeletewell mpango wa elimu anaousifia mgavila ni kweli mimi pia nauunga mkono na mwanzoni nilisifia sana plam ya mh.Rais ktk elimu.
ReplyDeletelakini nimekatishwa tamaa na utekelezaji wake,hasa pale serikali yake chini ya watendaji wa bodi ya mikopo wanapoamua sijui ni kwa maksudi au kwa kutokuwa makini ktk kutenda,kuwaweka vijana strandend bila fedha ugenini hadi sasa huku wakiteseka. sasa kama huu ndio utekelezaji wa sera ya elimu ni bora kabisa uchukuliwe utaratibu mwingine wa utekelezaji wa sera hii ila sio huu wa sasa.
kama serikali inaweka malengo,ni bora kuweka malengo inayoweza kuyatekeleza na sio kufanya mambo kwa kulenga campain kisha inayaachilia njia panda hayaja kamilika.
kwasababu logicaly haiji akilini,serikali inatoa changamoto ya kuwasomesha watu wake,inaridhia kuwapeleka nje au ndani ya nchi kusoma chini ya udhamini wake,kisha inawatelekeza bila kujali wanaishi vipi,wanasoma vipi ilikufikia lengo la kuelimisha. si ajabu watendaji wana zile mentality kwamba kusomesha vijana ni favour wanawafanyia,badala ya kutambua kuwa kama ni sera basi ni wajibu wao kuitekeleza sera hiyo,vinginevyo watangaze kuwa sera hiyo haitekelezeki full stop.
maana tumechoka kupokea malalamiko ya vijana wetu toka nje wakidai tufuatilie ktk bodi ya mikopo iwatumie fedha as if bodi haina utaratibu makini unaoeleweka. kama kazi imewashinda kuna watu wengi sana hawana kazi na wanauwezo wa kufanya kazi hiyo.au vinginevyo basi tufahamu kwamba huu ni mradi wa watu fulani unaojiendesha kibiashara au element za kifisadi zimeota pia mizizi kuelekea huko baada ya EPA.na ktk campain tusisikie tena habari za mafanikio ktk sere tajwa.
Katika mtazamo wa kifamilia kwa waliomuulizia hapo juu,huyu ni kaka wa toka ntoke wa Jokate Mwegelo, aliyekuwa Miss Tanzania namba mbili miaka ya nyuma.. Ni kutoka katika familia iliyobarikiwa vipaji mbali mbali kutoka kwa wazazi mpaka watoto. Na kila mtoto amepewa jina lake la ubini.
ReplyDeleteMfukunyuku.
Ukerewe.
Huyu ni mtoto wa Urban Ndunguru aliekuwa Afisa Wizara ya Mambo ya Nje takriban miaka 10 iliyopita hadi walipokombana na aliekuwa Katibu Mkuu wakati huo ikabidi aachie ngazi. Huyu mzee walikuwa classmate na JK huko Tanga form 5 na 6 mwaka 1970 na 1971. Ni mzee mmoja mwenye misimamo na mikogo mingi ambyo kwa kweli ilimponza. Yuko muwazi mno na inaelekea hata mwanae huyo amemrithisha. Sometime mwaka jana au juzi huyu kijana alilaunch kitabu ambacho mgeni rasmi alikuwa mzee Mengi. Nina sababu za kuamini msukumo wa kufanya hivyo alipata kutoka kwa baba yake. Baba yake ni member mzuri sana wa Mango Garden. Ukipita pale jioni huwa anapata bia yake pale. Quite an intelligent man and rhetorical too. Sijui kwa nini hafundishi hata part time kwenye vyuo vyetu kama Open Univerisity.
ReplyDeleteI am encouraging the young to forge ahead kwa vile anaonekana kuwa yuko assertive. Ila he should be careful ili ile laana ya baba yake isimwangukie. Kwa kuwa ni msomi. Namshauri atafute kitabu kilichoandikwa na Robert Green 48 Laws of Power. It is a good handbook ambacho kina kanuni nzuri ya jinsi ya kusurvive katika mazingira ya organisational as well as a political system. It is based on the thoughts of Machiavelli. It is quite helpful.