Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Eng. Zebadiah Moshi (shoto) akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Veta, Prof. Idrissa Mshoro, kutembelea Chuo cha Hoteli cha Veta, kinachojengwa Njiro nje kidogo ya mji wa Arusha. Mwenyekiti huyo na wadau wa Veta, walifanya ziara ya ukaguzi wa mendeleo ya ujenzi wa chuo hicho mjini Arusha mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Veta, Prof. Idrissa Mshoro, (Kulia) akipokea maelezo toka kwa mjenzi wa Chuo cha Hoteli cha Veta, kinachojengwa Njiro nje kidogo ya mji wa Arusha. Mkurugenzi na wajumbe wa wa Bodi ya Veta, walifanya ziara ya ukaguzi wa mendeleo ya ujenzi wa chuo hicho mjini Arusha mwishoni mwa wiki.
Prof. Mshora akitoa maelekezo
Sehemu ya mbele ya chuo hicho, chini ni bwawa
la kuogelea na chini kabisa ni sehemu ya nyuma

Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi, VETA, imejipanga kuwa mkombozi wa Sekta ya Utalii nchini, kwas kuwekeza katika kujenga uwezo kwa Watanzania, kumiliki soko la huduma za watalii ambalo kwa sasa, linamilikiwa na wageni zaidi kuliko Watanzania wenyewe.

Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki, na Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Eng. Zebadiah Moshi, wakati akiwatembeza wadau mbalimbali wa sekta ya utalii, kwenye Chuo cha Utalii cha Veta, kinachotarajiwa kukamilika hivi karibuni, kilichoko mkoani Arusha, ambacho kitatoa mafunzo ya huduma za utalii na uongozi wa hoteli.

Eng. Moshi amesema, soko la huduma za Utalii linakuwa kwa kasi kubwa kunakopelekea ukosefu wa wahudumu wenye utaalamu wa kati na wa juu wa kuhudumia mahoteli ya kitalii, hali inayopelekea ajira nyingi za kati za za juu kushikiliwa na wageni toka nchi jirani, huku Watanzania tukijikuta kama watazamaji.

Eng. Moshi, amesema kwa muda mrefu kumekuweko na upungufu wa wahuduma na watalaamu wa hoteli na huduma za utalii kwenye mahoteli yetu, ni kwa kutambua hitaji hili, ndipo Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi, VETA, ilipoamua kujikita katika ujenzi wa chuo cha kisasa cha mafunzo ya hoteli na huduma za watalii.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Veta, Prof. Idrissa Mshoro, amesema uamuzi wa VETA kujikita kwenye utoaji wa mafunzo ya hoteli na kuhudumia watalii, umefikiwa kwa kuweka maslahi ya Taifa mbele katika jukumu zima za kujenga uwezo kwa Watanzania kutawala biashara ya utalii kinyume cha hali ilivyo sasa kwa wageni kushika nafasi za juu kutokana na kuwepo kwa Watanzania wachache wenye utaalamu huo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Veta kanda ya Kaskazini, Angelus Ngonyani, amesema chuo hicho kimejengwa Arusha karibu zaidi na soko la utalii, na kitatoa mafunzo ya cheti na Diploma za huduma za Utalii na Uendeshaji wa Hoteli na kitajikita zaidi katika utoaji wa mafunzo kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuendesha hoteli ya kisasa ya kuhudumia watalii.

Wenyeviti na wajumbe toka kwenye kanda zote 9 za VETA, Wenyeviti wa Kamati za Kiufundi za Ushauri (TACs) na wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii walitembelea kujionea hatua mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi nchini VETA katika medani za Utalii. Mwisho.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. hivi jamani hakuna sehemu nyingine ya kujenga vitu kama hivi mbali na dar, mwanza,arusha mfano iringa na mikoa mingine yenye vivutio

    ReplyDelete
  2. Naona kila kitu kinajengwa Arusha, Moshi. Hivi kweli CHADEMA ikishinda uchaguzi, si mpaka IKULU itahamishiwa huko?

    Umefika wakati sasa hilikabila lidhibitiwe vinginevyo tutenda pabaya

    ReplyDelete
  3. sasa mtoa maoni hapo juu nahisi geograf ya tz haiko kichwani kabisa kwa sababu hiki chuo kiko njiro mkoani arusha sasa unasema hakuna shemu nyingine zaidi ya Dar
    unamaanisha nini.kwanza pongezi kwa ujenzi wa chuo hiki pale arusha coz hapo watalii wengi wako north kuliko south saket ni asante VETA Bravo.

    ReplyDelete
  4. nani kakwambia chadema wanaweza kushinda uchaguzi,huo ubunge wenyewe wasahau 2010,maana moshi mjini na karatu zinarudi ccm,kigoma nccr,watabaki na tarime peke yake.

    ReplyDelete
  5. Jamani mkumbuke kujenga hivi vitu pale kwetu Singida. Ardhi ipo tele tu. Karibuni kuwekeza

    ReplyDelete
  6. sehemu zingine vitu kama hivi kujengwa mpaka dar, mwanza na arusha kujae, na kukijaa wanaanza kubomoa vya zamani ili wajenge vipya kwa hiyo nyie wengine mlie tu.

    ReplyDelete
  7. VETA hongera sana. Siku za nyuma niliposoma ilani ya CCM kuwa watajenga chuo cha kitalii Dar sikufurahi maana Dar is too overloaded. Nilitegemea chuo hicho kingejengwa Karatu kwa sababu ingekuwa rahisi kwa wanafunzi kufanya practicals na pia vijana wa pale Karatu wangelipata ajira hasa baada ya kuwa hivi sasa mashamba ni ya taabu na vijana wanaongezeka. Anyway hata hapo Arusha siyo mbaya kwa sababu ni katikati. Nimefurahi sana kwa uamuzi wenu huo. I hope Shamsa Mwangunga supports you.

    ReplyDelete
  8. Kwanza nyerere alikosea sana kubaki ikulu Dar halafu na sera yake ya kuhamia Dodoma.

    Makao makuu ya nchi yalitakiwa yawe Arusha kwa sababu kuna hali nzuri ya hewa.

    ReplyDelete
  9. Sasa Mdau kule Singida chuo cha utalii mbona kitakuwa sio mahali pake? Watalii wengi watakao saidia wanafunzi kwenye masomo yao ya vitendo wapo hapo Arusha zaidi ya Singida.

    Unaonaje Singida wajenge Medical au Agriculture College?

    ReplyDelete
  10. Jamani mbona kila kitu Wachagga ina maana wao ndo Mawaziri na ndo wanaooendesha hii serikali? Na unapo-invest kitu kama chuo kuna vitu vingi huangaliwa kama in CBA kama Human Resources, Logistics mbali na vitu vingi tukiacha hivyo! sasa kama chuo ni cha Utalii, huitendei haki Arusha! Geographical location favours Arusha no. of Hotels that need VETa
    A facilities are enormous! Sasa Singida unategemea watu watoke Dar, Arusha na Zanzibar waje Singita kusoma! Where is the practical in hand facilities? Hizi fikra za kijamaa ndo ziliua miradi mingi kwa vile they turned out to be impractical unaweka chuo in no man land nani atakuja kusoma! Singida wajengewe chuo cha Kilimo that's piece of cake! Otherwise ni wivu usio na kichwa unakusumbua!

    ReplyDelete
  11. Iringa Mbeya,Rukwa kule kwenye sokwe,,,
    ivi bodi ya utalii na izara husika hamuoni aya maeneno ya utalii?adi arusha?kama sio uvivu wa kufikili na poor planning ni nini?

    mnanikera acha tu

    ovyo sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...