Habari kaka.
Mimi ni mmoja wa wadau wa usafiri mrefu wa barabarani. kuna tukio moja lilitokea Jumatatu tarehe 21.12.09 jijini Dar.
Ilikuwa ni asubuhi mapema sana, nilikuwa naelekea kupanda basi kwenda a-taun. kwa bahati mbaya mabasi yote ya hiyo sehemu husika yakawa yamejaa na hakukuwa na nafasi. Lakini kulikuwa na magari ambayo yalikuwa yanapakia watu kinyume na utaratibu wa SUMATRA.
Mimi ni mmoja wa wadau wa usafiri mrefu wa barabarani. kuna tukio moja lilitokea Jumatatu tarehe 21.12.09 jijini Dar.
Ilikuwa ni asubuhi mapema sana, nilikuwa naelekea kupanda basi kwenda a-taun. kwa bahati mbaya mabasi yote ya hiyo sehemu husika yakawa yamejaa na hakukuwa na nafasi. Lakini kulikuwa na magari ambayo yalikuwa yanapakia watu kinyume na utaratibu wa SUMATRA.
Basi moja lenye jina la (jina kapuni), lilikuwepo ila baada ya basi jenzie kujaa ikabidi wafanya kazi wa basi hilo kuingia ndani ya basi na kuanza kuteta kwa muda mrefu sana bila kubugudhiwa na abiria. waliwakataza abiria kupanda kwenye gari kabisa mpaka hapo watakapomaliza maongezi yao.
Baada ya kama robo saa hivi, msemaji mmoja kati ya hao waliojifungia humo alitoka na kusema ''jamani nauli ya kwenda arusha ni sh. 18,000 lakini kwakuwa ni sikukuu itabidi mtupe chetu cha juu ambacho ni sh. 2,000. So jumla ya nauli hiyo ankal ni sh. 20,000.
mwanzoni watu walionyesha mgomo, mshangao na kutokukubaliana na uamuzi wa basi hilo na wafanyakazi wake. ila kwa kuwa hakukuwa na namna nyingine ya usafiri ilibidi abiria kukubaliana na uamuzi huo. wafanyakazi hao wakagawana hizo tiketi na kuanza kusambaza kuziuza.
Cha ajabu na chakushangaza ni kwamba wakala wa usafirishaji SUMATRA walikuwepo wakipita pita na kushuhudia hali iliyokuwa ikiendelea pale lakini cha kushangaza ni kwamba hakuna hatua yoyote ile ya kisheria iliyotendeka japokuwa kosa lilikuwa linaonekana wazi wazi.
Baada ya kama saa 1 hivi baada ya kuwa vurugu za kukata tiketi na kupokea pesa yao kukumilika watu wakaruhusiwa kupanda kwenye gari. Na hapo fujo zilikuwepo pia maana watu walikuwa na wasiwasi wa kukosa siti maana upatikanaji wa tiketi haukuwa na uhakika.
Gari ilipojaa, ikaondoka kwenda gereji kuweka upepo matairi. Na hapo napo tulikaa kama nusu saa hivi ndani ya gari bila kupewa taarifa ya shughuli iliyokuwa inaendelea ili tushuke tukakae kivulini tujinusuru na lile joto na majasho ya Dar.
Hilo halitoshi, huko barabarani basi lilikuwa linatembea kama dala dala, lilikuwa linasimama mara kwa mara. Ikitokea mtu ameshuka na ikapatikana siti itafanyika replacement papo kwa papo ndo maana nikaipa jina la dala dala.
You cant imagine tumeondoka Dar kama saa 4.15 ivi na tukafika Arusha saa 4 usiku. Hivi huu ni utaratibu wa SUMATRA kweli jaman????????????
Kuna watu wanategemea kusafiri kabla na baada ya sikukuu. Je, huu utaratibu wa kusafirisha watu utaendelea hivi kwa muda gani na nani atakayeumia hapa?????
Tunaomba SUMATRA wafanye kitu hapa.
namba za mawasiliano ya hilo gari ni 0755 451633 na 0712720102
(kutoka kwenye tiketi zao)
Ni mimi Mdau niliyeguswa na usumbufu huo.
Mbona unatoa namba za wenye gari tu? Tupe na Namba ya hao waliokubali kulipa 20,000 wakati nauli ni 18,000. Hao ndio haswa, wanaopaswa kuchukuliwa hatua kwa ktutoa rushwa mchana kweupeee, tena kwa ushirikiano. Acheni ubinafsi na chukueni hatua dhidi ya dhuluma. Kama watu zaidi ya 60, wote kwa pamoja mnakubali kunynyaswa mchana kweupe hivyo, hao sumatra ndo nani?
ReplyDeleteUnadai basi lilijaa mithili ya Dala dala la kwenda Mbagala!! Nami kwa kushangaa nyoote mkakubali kutoa rushwa mchana kweupee!! halafu mnalalama kwenye mablog. Sasa nani mwenye kosa, wewe mtoa rushwa au huyo mlanguzi uchwara?? Huo ni unafiki wakutupa, kama lilikuuma ungeripoti kwa hao SUMATRA ulokuwa unawaona, unasubiri ushafika ndo unalalamika, ka una chuki binafsi tutajuaje. tena koma kabisa kutoa simu za watu.
ReplyDeleteKwa nini umepanda? Abiria wengekuwa na msimamo.. yasingetokea. Basi likikimbia sana, abiria ndani kimyaa.. hamna anayesema. Sisi wenyewe ndio wakulaumiwa, sisi kama jamii husika. Basi bovu kabisa hilo.. hata service lilikuwa halina.. linasafiri, na nyie mkapanda
ReplyDeleteNdugu mlalamikaji, ebu jibu maswali yafuatayo:
ReplyDeleteJe wewe ulilipa hiyo nauli ya 20,000?
Je ulipoona huo uovu ulichukua hatua gani?
Je unadhani kuandika kwenye michuzi ndio hatua sahihi ya kuzuia huo uovu?
Je uliwaita hao watu wa sumatra kuwaeleza?
Je ulitoa ripoti kituo cha polisi pale pale stand?
Na kama umeweza kusoma hizo namba za simu kwenye tiketi, je ulijaribu kumpigia simu mwenye gari/au ofisi yao kumwambia hilo jambo?
Unajua ndugu yangu kuwa shujaa sio kuandika kwenye michuzi. Ushujaa ni pale wewe mwenyewe unapochukua hatua dhidi ya hilo jambo.
Ni nani unadhani atafanya hiyo kazi? sumatra? au wananchi? pengine hao sumatra hata hawakujua hiyo biashara, japo unasema walipita. watajuaje bila kupewa taarifa na nyie mnaibiwa? Jua kuwa sumatra wawajibikia vizuri ni vyema wajue kuwa hata nyie mmeona na mmechukizwa mpaka mume-report.
Sasa unatuandikia sisi namba za simu, je unataka tupige simu? ili tuseme nini?
Sikiliza ndugu, kama unataka kuzuia uovu basi chukua hatua palepale, hata kama utaingia hasara ya kukosa kula x-mass kwenu.
Kumbuka mashujaa ndio wafanyavyo. Kama unataka ushujaa basi chukua hatua kisha tusimulie hiyo hatua. Sio kutuandikia ili tuzidi kusikia uchungu.
Chukua hatua!
kwanza ningependa kuwapa pole raia wote wema waliokuwa desparate kusafiri na kulazimika kulipa xtra fair ila pia nataka nimlaumu huyu jamaa aliyeripoti tukio hili kwani alishiriki kutoa rushwa kisha alipofika safari yake ndo akatoa habari,muda wote huo kwanini asingepiga simu polisi ili wadhibiti hali hiyo na kuwachukulia hatua wahusika? na pili ni kwanini asilitaje jina na namba ya basi hilo ili wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na wakati ana ushahidi tosha kabisa wa ticket?.hiyo ni sawa na story ya jamaa mmoja aliyeingiliwa kinyume na maumbile na kisha hakimu akamuuliza mheshimiwa inaonekana ulikuwa unainjoy tukio maana ulionyesha ushirikiano mkubwa muda wote wa tukio lililodumu masaa matano na pia ukaripot tukio siku mbili baadae jamaa anajibu 'nilionyesha ushirikiano ili ushahidi ukamilike'
ReplyDeleteUnajua mojawapo ya matatizo ya customer service Tanzania ni kuwa ninyi Watanzania wenyewe mmekuwa kondoo mno...hamjui haki zenu..sasa wewe unayejua hizo haki ulichukua hatua gani unalalamika tu bure? Kama maofisa wa serikali waliokuwepo hawakufanya kitu..ulichukua hatua gani? unaandika hapa kwenye michuzi it's too late now...Michuzi atafanya nini? Jifunzeni haki zenu wabongo ninyi..Lol...!!
ReplyDeletenakama kweli umeamuakuliweka wazi suala hili ilisheria ichukuemkondo wake mbona hautaji jina la basi hilo?liweke suala zimabayana ilipichakamili ionekane kwajamii pia,ili kama SUMATRA watashindwa kufanya kazi yao basi tujiandae kulipa pesa zaidi next time.weka mambo wazi huu sio wakati wakuendelea kuogopa mbona wewe hawakuogopa kuchukua pesa yako
ReplyDeleteWewe ni mtu mnafiki sana. Kama kweli hilo lilitokea kwa nini ufiche jina la basi? Na swali kuu ni kuwa, kwa nini upande basi lililojaa? Hii inaonesha ni jinsi gani ulivyo kosa maadili. Kama una safari kwa nini usikate tiketi kabla ya muda kwa mabasi yanayoheshimika na yanayofuata utaratibu?
ReplyDeleteMadai yako hayana maana yeyote kwa sasa, kwa kuwa watu wameshadhulumiwa na wewe binafsi ulishiriki kuwadhulumu kwa kufyata mkia wako.
Kaa tu kimya sasa, mjinga ushaliwa.
WABUNGE WANAJILIPA MILLION TANO, WACHATUBANANE KILA MTU NA NAFASI YAKE.
ReplyDeleteZamani kulikuwa na nyimbo ilikuwa na kibwagizo hiki "sema usiogope semaa". Sasa na wewe weka hadharani namba ya gari na kila taarifa iliyopo.
ReplyDeleteNyinyi abiria ndio mulitakiwa kuchukuwa hatua pale, sasa Sumatra anaepita nje atajuwaje kama hamkumripoti huyo dereva?
Wewe mlalamikaji ndiye mwenye matatizo zaidi ya hao wenye basi, badala ya kuchukua hatua ya kuwashitaki wenye basi kwa SUMATRA,Polisi. wewe unaleta malamiko yako kwenye blog na badala ya kutaja jina la gari bado unaweka jina kapuni ili keendelea kufuga uozo. Nini lengo la kuleta malalamiko badala ya kupeleka hayo malalamiko kwa wahusika SUMATRA, majembe. Wakuu wa polisi wametoa namba zao zitumike kuripoti uhalifu unatambua hilo?
ReplyDeleteNi kawaida ya sisi watanzania kusemea pembeni,kila kitu kinaachiwa serikali wakati wanaoumia ni sisi wenyewe huyu ndugu analeta umbea tu humu,sikutarajia kwa mtu mwenye ufahamu kiasi hicho akaripoti hili tukio ni aibu,kwanza nadhani anastahili kutiwa mbaroni kuisaidia polisi
ReplyDeleteWewe mlalamikaji. shukuru ulipata gari kwa siku hiyo, Maana kipindi cha sikukuu kama hii usafiri wa Dar - Moshi - Arusha ni kero tupu, nadhani magari huwa hayatoshi.
ReplyDeleteTuwashauri wachaga waache tabia yao ya kwenda kuesabiwa siku kama hizi maana wao ndo wanasababisha matatizo yote haya.
HAYO NI MATATIZO YA NCHI INASYOENDESHWA BILA SHERIA NA UTAWALA WA HAKI, WANAKUWA NA KIGUGUMIZI KUPIGANA NA RUSHWA, I HATE THIS HABIT, NA INAKUAJE SERIKALI INASHINDWA KUPAMBANA VITU KAMA, HAINGII AKILI KABISA, SIJUWI KAMA KUNA UMUHIMU WA KUWA NA SERIKALI!!! NASITA KUELEWA.
ReplyDelete