Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume(katikati)akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa masuala ya Umeme wa Kampuni ya EHL ya nchini Afrika ya Kusini,Martin Burls, (aliyenyoosha mkono),wakati alipotembelea Kituo cha kupokea Umeme cha Fumba leo.Zanzibar haina umeme kwa takribani wiki tatu sasa baada ya chombo katika kituo hicho kulipuka.Picha na mdau Ramadhan Othman wa Ikulu Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Zanzibar ktk karne ya ishirini na moja! Inakosa umeme nchi nzima na hakuna back up ya aina yoyote; kiza kila upande!!! na bado inajinasibu nchi? Kazi kweli kweli!!!

    ReplyDelete
  2. nilikuwa sijui kama zanzibar wanategemea umeme wa bara

    ReplyDelete
  3. what???ipo kazi jamani

    ReplyDelete
  4. Jamani hii inatia simanzi. Zanzibar yetu basi hata vijenereta vya umeme katika sehemu nyeti za mji mkongwe tunashindwa! Au ndiyo tunangoja wafadhili waje tena kutugaia misaada? Aibu hii.

    ReplyDelete
  5. jamani mbona haibu serikali ya zanzibar kukicha inaleta wasomi nje mbona sioni ubunifu wao.Solutions mbona nyingi tu SOLAR,WIND MILL n.k
    M ndio hapo nachoka naviongozi wetu kwann tunang'ang'ania vitu vya zamani vilishachoka hivyo AAAH!Ibane na hiyo kaka michuzi lkn ndio ukweli wenyewe.

    ReplyDelete
  6. mtamkumbuka commandor mwaka, enzi zake, saa hizi keshakopa generator siku nyingi, taarabu kama kawa bwawani!!!

    ReplyDelete
  7. alafu mnataka kuvunja muungano mlivyokuwa na vichwa vibovu, think twice!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...