Mama Maria Nyerere na Mama Sitti Mwinyi wakisoma wasifu na ratiba wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa Sima wa Vita ukumbi wa Karimjee Hall jijini Dar leo
Sheikh Yahya Hussein akisoma Quran
sehemu ya waomblezaji
waombolezaji wakilia
wengi walishindwa kujizuia
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa marehemeu Mzee Rashid Mfaume Kawawa katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar jioni hii. Mamia ya wananchi wamefurika ukumbini hapo kumuaga Sima wa Vita anayetarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Madale kesho Jumamosi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiifariji familia ya Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa muda mfupi baada ya kutoa heshima za mwisho.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. RIP Simba wa vita.Tuta-miss busara na hekima zako.
    By the way-Jamani dini inasemaje juu ya wanawake kuaga mwili wa marehemu?

    ReplyDelete
  2. Wewe Tarehe Sat Jan 02, 01:28:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
    Ni Dini gani unayoiongelea kuhusu kuaga mwili wa marehemu?

    ReplyDelete
  3. Innalillah wainailah rajiun! sisi sote ni wa Allah nasi kwake tutarejea, kwani ni njia ya wote..

    ReplyDelete
  4. Mdau 01:28 hayo ndo wanaita mambo ya kwenda na wakati! Ila nadhani kwasababu haonyeshwi mwili...na si wanawake pekee wanaokatazwa kuaga wmili ila nadhani kidini watu wote hawaruhusiwi! Kwa maoni yangu najua watu watanitoa ngeu...mie sie mwanazuoni hapa ni maoni tu!

    ReplyDelete
  5. inna lilahi waina illaihi raaajiuun,allwahuma gh'firlahum warhamhum waskinhum fil'jannah ,inshaallah tutazidi kumuombea dua mzee wetu hyu .m/mungu amsamehe dhambi zake na sisi pia atusamehe

    swadaqatun jaaria ndio yapasa kumtolea il'hali hakun kingine anachoenda nacho mbele ya haki.

    mdau

    ReplyDelete
  6. kila mtu anaruhusiwa kumuaga mpendwa wao kwa nini wanaume waende peke yao kwani nyie mliumbwa kwa gold??? lol ubaguzi hadi mtu akifa mbona arusini wote mnahudhuria?? kama ni kulia hata wanaume wanalia mwangalieni huyo jamaa hapo juu na ikumbukwe mwanadamu ana arusi tatu za maisha kuzaliwa kuoa or kuolewa na kufa na hizi zooote inabidi watu wote wahudhurie kikamilifu full stop!! michuzi naomba meseji hii ifike jinsi ilivyo !!! heri ya mwaka mpya

    ReplyDelete
  7. RIP simba wa vita, hakuwa na makuu kabisa mzee wetu na wala hakuwa fisadi alikuwa safi,mwadilifu na mpenda nchi. kwa nyazifa zake wala hakutaka kukimbilia kuishi oysterbay masaki alienda kuishi uraiani kwa walala hoi, tafadhalini viongozi wetu fateni nyayo za kawawa na nyerere.
    ufisadi utawapeleka jehanam.

    ReplyDelete
  8. namuona sheikh yahaya akitoa neno la mungu na kwa mbali naona pete la njano

    ReplyDelete
  9. Mithupu!Tunaomba video!Tumsikize Yahya Hussien(Gwiji la Tajweed)ila amekosea kuwa Gwiji la Uganga na Utabiri vinapishana na fani ya Tajweed!Anyway tunaomba Video

    ReplyDelete
  10. mdau hapo juu umeniacha hoi huku kwani hiyo pete ya njano ina nini?

    ReplyDelete
  11. HAKUWA MWIZI, HAKUWA NA MAJUNGU, ALIKUWA MSEMA KWELI, KAMA ATAKA KUSEMA KITU ALIKISEMA MBELE YA MUHUSIKA SI MGONGONI KWAKE, HAKUHOMOLA MAPESA YA SERIKALI, ALIWAPENDA WATU WOTE NA ALIKUWA RAFIKI WA KILA MTU HATA MASIKINI, WALALA HOI NA WASIO NA ELIMU. VIONGOZI WA SASA MUJIFUNZE TOKA KWAKE HAMNA HAJA YA KUIBA PESA ZA UJIRA WAKO ZINATOSHA. TUFANYE KAZIN KWA FAIDA YA WATU WOTE SI PEKE YENU TU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...