Ankal Salaams,
Mimi ni mdau toka moshi mjini. Naomba msaada wako kwenye blog yetu ya jamii. kuna hili gari ninauza.

namba yangu ya simu ni 0784925163,
na email yangu ni lshangali@yahoo.com.

1. Gari lenyewe ni
Chevrolet
Model - Chev
Model No. - 14HPG
Body Type - Station Wagon
Colour - Black
Class - Light Load Vehicle
(GMV 3500Kg or Less)
Manufactered - Around 1918

Gari lenyewe lipo Moshi mjini ila limetembea hapa mjini kama miezi sita tu. lilikuwa kwa tajiri mmoja wa zamani hapa moshi akawa kalifungia ndani ndio tukaenda kulichukua nyumbani kwake.

Naliuza sababu kuna gari lingine kwa
mtu la kizamani pia nimelipenda nataka kulinunua.

Kuhusu bei ni maelewano...
Thanks in advance.
Lui.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Gari kama hii huku America ni Antique, they are expensive, all the best in getting the right price.

    ReplyDelete
  2. Hii milango yake itakuwa inafungwa kwa kitasa kama cha nyumba.

    ReplyDelete
  3. Hiyo gari iweke ktk webusaiti www.ebay.com dunia nzima wataiona, labda Hollywoods wakiona watakupa mshiko wa nguvu kutengeneza picha nyingine ya "Once Upon Time in America"

    Mdau
    Robert De Uriyo

    ReplyDelete
  4. Mdau Robert De Uriyo Ushanihariibia sasa mwenyewe nimetoka Ubungo sasa hivi kukata Ticktey ya Bus la Kwendea Moshi alafu wewe tena unampa Wazo zuri la kuweka Picha Ebay? ah anyway kila mtu na Bahati yake weka Ebay.com. Pazi.

    ReplyDelete
  5. MHESHIMIWA IKIWA UMEWEZA KUWEKA PICHA NZURI INAYOVUTIA YA KILA UPANDE INGEPENDEZA SANA UNGEWEKA PAMOJA NA BEI YAKE ILI ATEKAYECHUKUA HIYO CLASSIC CAR AJUE USAFIRISHAJI UTAMGHARIMU VIPI UMPUNGUZIE MTIHANI WA KUPIGA SIMU.NENDA NA WAKATI-

    ReplyDelete
  6. KAKA HAYO NI MATATIZO KAA NAYO MWENYEWE IZIKE NA MWENYE NAYO FULL STOP.

    ReplyDelete
  7. OK, gari ni zuri hasa kwa wale wenye nia ya kuanzisha kampuni za mazishi.

    ReplyDelete
  8. Huu si mwaka wa uchaguzi, unaweza kununua halafu ukalitumia kwenye kampeni kwa sababu lenyewe jinsi lilivyo tayari ni crowd puller.

    ReplyDelete
  9. Antique hiyo

    ReplyDelete
  10. Ili gari hiyo iwe Antique inabidi iwe na Original parts .
    kama imewahi kubadilishia viti au kitasa au modification ya aina fulani,inatoa thamani yake.
    Fanya utafiti,upate unachostahili.

    ReplyDelete
  11. kwa africa magari kama haya hayana thamani.Mtu ukiwa nalo wananchi lazima waseme kwamba umefulia. ma nchi ya mbele kwenye watu walio rithika magari kama haya wana yanunua kama mapambo. Mbongo anataka kuendesha baluni bana si magari ya vilema .

    ReplyDelete
  12. tarehe ya kwenye picha inaweza kuonyesha ni jinsi gani info inaweza kutafsiriwa vibaya.

    ReplyDelete
  13. Bro, Utafiti wangu wa haraka unaonesha kuwa model hiyo ni ya 1930's au 1940's. Najua kuwa Nairobi kuna na watu wananunua magari ya antique na kuyakarabati kwa spare parts original lakini bei zao za kitapeli. Bora uitangaze kimataifa.

    ReplyDelete
  14. Kwa mbeba box hii ni a ticking bomb lakini kwa fisadi hii car ni a keeper...very nice car lakini kama original things havijaguswa....manake kwa gari ya weekend au kwenye shughuli maarufu this is a car....

    lakini hii neno bei ni maelewano....kwanini watu lakini mwapenda hii msemo. kwa vile vitu vingi ni vya kurithishwa hivyo hamjui thamani ya vitu vyenu au mnapenda kwenda na demand and supply...huu ni ulimwengu wa transparency...nyie kalieni kuficha ficha tu...mnakosa wateja...

    ReplyDelete
  15. Du si bora ninunue bajaj siku hizi zina ac, kuliko hilo Antique lako. Kawape makumbusho ya taifa...

    ReplyDelete
  16. A A A A U.S.A.... safisha/osha matairi (DAWA MAALUM), carpet ipo poa sio ? una original title na vitu vyake original vingine gharamia kidogo tu mambo ya ndani BEI YAKE KWA MUNUNUZI MBAHILI NI KUANZIA $50,000.00

    ReplyDelete
  17. Revenge of Al Capone or Public Enemy No 1 with Tommy Machine Gun Maaannn we canmake a classic movie

    ReplyDelete
  18. Gari hii Jay Leno akiiona atainunua kwa zaidi ya $80,000.00 Elfu themanini, Ni kwamba wabongo hatujui tu hiyo ni gari ya nguvu na matajiri wa marekani wakiiona watataka kuinunua kama ina origina parts kama wadau waliotangulia itabidi uiweke kwenye Ebay utapata hela nzuri sana. Tupe bei kisha tutakupa mawazo.
    Nitakupigia simu mdau tuongee.
    Good luck.
    Lakini hiyo gari ni nzuri sana.
    Mdau wa Damu USA

    ReplyDelete
  19. Gari hii ni aina ya CHEVY PANEL 1950`s its depends on how original the car is you are looking at btn $9000-$15000 from original seats to door handles.You might want to try placing an AD on ebay or craigslist africa sana South Africa. Anyways the car looks very clean from the pics Goodluck selling it, hope you get the good value out of it.
    check out the 2010 chevy panel.
    http://www.chevrolet-carz.com/wp-content/uploads/2009/12/2010-Chevrolet-HHR-Panel-Pics-300x186.jpg

    mdau USA.

    ReplyDelete
  20. nice gari but definitely not from 1918! Rather 1948! Its value depends on the technical condition. If it was always maintained properly then it could easily fetch 50'000 USD or more.
    cheers

    ReplyDelete
  21. 1948 chev kali lakini wameharibu kutoboa madirisha hilo kosa mnunuzi anaejua atashusha thamani kwa hilo

    ReplyDelete
  22. Gari ni zuri ila WESE(mafuta)vipi? isije ikawa inabugia kama ngamia. Maana sisi tunaoishi Kitunda kamwe hatutaliweza.

    ReplyDelete
  23. Mdau kuna web ya bure ambayo unaweza kuweka matangazo yako ya kuuza au kuhitaji kununua angalia http://www.swahilinet.com

    ReplyDelete
  24. enzi hizo indiketa za nyuma ilikuwa hamna

    ReplyDelete
  25. Pimp my ride!!

    ReplyDelete
  26. enzi hizo hawakuwa na AC sasa kwa daslama na joto lake hii ni friji ya moto baba, tena rangi nyeusi inafyonza jua kama haina akili

    ReplyDelete
  27. USA KWA MAGARI YA SURA MBAYA NDO ZAO KA KIBOKO, WAMEBADILIKA SIKU HIZI TU KWA KUMUOGOPA M-JAP NA WAO WANATENGEZA ZENYE SURA NZURI ZAMANI NYEE GARI KAMA INATAKA KUJISAIDIA HAJA KUBWA.

    ReplyDelete
  28. subiri kidogo hali ya uchumi duniani itakaporejea utapata wanunuzi sasa hivi matajiri wote wako katika kuhesabu hasara zao. nakushauri baada ya mwaka irudishe picha mtandaoni.

    ReplyDelete
  29. hiyo ni 1948 au zaidi canopy,suburban etc kwa ufupi chevy trucks za around 1948-1950's.utapata mishiko kama vitu vingi ni original,personally body nimeikubali na nitakupigia simu.
    mdau Prescott,AZ

    ReplyDelete
  30. WEWE KIJANA MDOGO HIYO UMEIPATA WAPI? UMERITHI KUTOKA KWA BABU YAKO? HEBU TUJULISHE HUENDA IKASAIDIA KUPANDISHA DAU.

    ReplyDelete
  31. Bwana Biashara unaijua na Gari unajua kuitafuta na la pili unaongeza sasa msaada gani waomba kwa waswahili au unaomba kijicho . Mtu kitu hana wamtamanisha apitishe macho na rai wamekupa. sasa tunaomba msaada wako tufahamishe magari ya kizamani yanapatikana wapi. mimi navojua kuwa mitumba zote zinatoka nje ya nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...