Ankal,
pole na majukumu ya kuelimisha jamii.
Nimejikuta nalazimika kuingia katika mjadala ulioanzishwa na ndugu yetu Mdau wa Tokyo bila kupenda. Ni hulka ya wabongo wanapopata bahati ya kwenda ughaibuni na kujifanya kusahau hali halisi ya nyumbani.

Hivi ni nani asiyefahamu usumbufu wa Traffic wa Tanzania hasa kunzia Kibaha hadi unafika Chalinze? Kwa taarifa yako mdau wa Tokyo, Unapoamua kuanza safari lazima uchukue shs. 50,000/= na uchenji katika elfu moja moja au mbili ambazo utazitumia kuwapa traffic njiani hadi unafika unakokwenda. Hakuna asiyelijua hilo! Uliza kaka utaambiwa, au siku ukija nyumbani bongo, kama una ndugu yako ni dereva wa lory, endesha hilo lory toka Dar hadi Iringa ndo utajua Jerry Mulo anastaili pongezi na tuzo aliyopewa.

Nadhani ulianzisha mjadala huu kwa wivu uliokuwa nao juu ya kazi nzuri ya Jerry Mullo.

Naomba kuwasilisha,
Mdau Sinza Mori.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Nchi yetu inanuka rushwa , lakini fact is huwezi kutumia ile video kuthibitisha rushwa ilitolewa.
    Mazingira ya rushwa yalikuwepo ,ndio . Tuliona rushwa iliyotolewa? hapana.
    Hata hivyo hongera sana Mwandishi .

    ReplyDelete
  2. mimi nafikiri kabla ya kujua kama alichukua rushwa au la kwanza tujadili,je wanalipwa mishara bei gani. Na maslam yao ya halali ofisini yanatosheleza kukidhi mahitaji muhimu ya mtu na familia yake?Nafikiri kuanzia hapo tutapata picha halisi

    ReplyDelete
  3. We Mdau wa pili unaongelea kipato kutosheleza, ni kiasi gani kinatosha? Sidhani kama rushwa ina uhusiano wowote na kipato kutosheleza. Mpe mtu baiskeli atataka Bajaji, mpe boat atataka meli, mpe ardhi atataka mbingu!!

    ReplyDelete
  4. Mimi nadhani mdau hakuwa na wivu na jery. alichokifanya ni kutoa changamoto ya kutokukurupuka na kutoa shutuma nzito bila kujiridhisha kwa kina na mapana yake.

    ReplyDelete
  5. nadhani wawaboreshee mishahara hao watumishi wa kazi za hatari kama wanavyowajali wanajeshi ambao kazi zao sizioni, kazi za polisi ni hatari kuliko zote duniani na kwa wenzetu polisi ndio wanapata kipaumbele zaidi kuliko wanajeshi.

    maisha ni magumu na kwa mshahara wa 150,000/= yaani hapo labda usioe na usiwe na familia uishi kambini, hiyo mishahara inawatosheleza kununua chakula tu! kujenga nyumba,kusomesha watoto shule nzuri ni ndoto
    sikatai polisi kila nchi werevu lkn kwetu imezidi wanapokea mpk rushwa ya $1!!

    ReplyDelete
  6. Ninyi watu vipi bwana? Kila siku kutetea uovu tu? Rushwa imetolewa na tumeona, mnatuambia hatujaona. Wanga tu ninyi

    ReplyDelete
  7. RUSHWA HAINA UHUSIANO WOWOTE NA MISHAHARA NI UTAMADUNI ULIOJENGEKA, HATA WAKIPEWA BILIONI MOJA KAMA MSHAHARA BADO WATACHUKUWA RUSHWA YA SHILINGI ELFU MOJA, NA HATA KAMA HIYO NDO HOJA YA MSINGI SI SAHIHI KUCHUKUWA RUSHWA TOKA KWA WANANCHI HAO HAO WANAOLIPA MISHAHARA YAO KUPITIA KODI WANAZOLIPA SERIKALINI, MSHAHARA MDOGO NI JUU YA SERIKALI NA WAO KULIJADILI HILO SI KUUMUZA WANANCHI KWA KUWATOZA RUSHWA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...