Ankal pole na kazi za kulijenga Taifa letu
Kwanza napenda nikushukuru mwenyewe kwa kazi nzuri ya kutuletea habari za nyumbani na kwingineko.
Kwanza napenda nikushukuru mwenyewe kwa kazi nzuri ya kutuletea habari za nyumbani na kwingineko.
Juzi nimeona kwenye blog yako clip moja au mbili zilizorushwa na TBS kutoka kwa Mr Jerry Muro kuhusuiana na askari wa barabarani ( traffic)
wa check point kua wanakula rushwa.
Ukiangalia vizuri zile clip hakuna rushwa ilitolewa pale ni fikra tu za huyo mwandishi na wengine . Lakini ukweli ni kwamba akiambiwa atoe vithibitisho nadhani hatakua na ushahidi na kama hana ushahidi unaothibitisha anapokea hela kazi yake HAPO INA KASORO / DOSARI.
Pili sina uhakika kama kazi za Police traffic anazijua sawa, maana ukimsimamisha dereva lazima uulize leseni ya udereva na uombe kadi ya gari, na ndicho kilifanyika pale kama utaangalia vema .
Walisimamishwa wakasimama na kutoa karatasi “Kadi ya gari” na wengine leseni ya udereva sikuona pesa pale. Sawa amehisi ni rushwa Je, kabla hajakimbilia kwenye luninga kutaka sifa alifanya upelelezi wa kutosha akajua chanzo cha hayo yote ni nini na kama kweli wale madereva walidaiwa hongo?
Ningefurahi saana kama angefanya hizo harakati zake uwanja wa ndege DIA, Bandari ya Dares-salaam, n.k . Mimi naona amezidi kuwaonea hawa police kila wakati wanakula rushwa, wanakula rushwa .
Ningefurahi saana kama angefanya hizo harakati zake uwanja wa ndege DIA, Bandari ya Dares-salaam, n.k . Mimi naona amezidi kuwaonea hawa police kila wakati wanakula rushwa, wanakula rushwa .
Ningefurahi kama angesema wanasababisha usumbufu wa geti mara kwa mara hapo ningeelewa lakini sio kuwalaumu hawa Askari wadogo kua wamekula rushwa na kukimbilia kwenye vyombo vya habari. Ninaomba uiwakilishe hii kwenye blog yako na watu wachangie Ili kutafuta dawa ya kudumu ili mambo kama haya yasitokee tena, Kwa kumalizia ninafikiri Bwana Muro anapaswa kuwaomba msamaha hao askari kwa kuwadhalilisha namna Ile.
Kwa leo naomba niishie hapa na ninatanguliza shukrani zangu za dhati ni mimi mdau wako mkuu.
Kwa leo naomba niishie hapa na ninatanguliza shukrani zangu za dhati ni mimi mdau wako mkuu.
Mdau Tokyo


Mdau Wa Tokyo,
ReplyDeleteAmka na uone mwanga, upate ujasiri wa kuona kijiko na kuita kijiko.
Network Engineer (NE),
Reading, UK.
we sijui kama ni mzima wa macho rafiki yangu? au na wewe ni mmoja wapo? acha hizo kila kitu kiko live pale acha utetezi usio wa maana, sasa we unadhani jerry alienda pekeake? au unamuona yule ni mwendawazimu? tafakari kwanza
ReplyDeleteMdau wa Tokyo, naona wewe ndio unatakiwa uangalie zile video vizuri kabla ya kukurupuka na kuanza kumlaumu yule muandishi wa habari. Kwa kawaida trafiki au polisi akiomba leseni na kadi ya gari huwa anaangalia na kurudisha kwa dereva. Lakini kwa mujibu wa zile video, kuna vijifurushi wale matrafiki wanaonekana kupokea halafu haionekani wakirudisha kitu! Sasa kama si rushwa ni nini???! Nampongeza yule muandishi kwa kuyaweka wazi maovu haya, na ni matumaini yangu kwamba wakati tunatafuta suluhu basi tusisahau pande zote mbili za tatizo hili. Pande ya kwanza ni mishahara mibovu, ambayo inaleta njaa kwa polisi wetu. Pande ya pili, ni maadili mabovu ya kazi kwa hawa pilisi wetu. Kama mambo haya makuu mawili yataangaliwa na kurekebishwa basi tutafanikiwa kulitatua tatizo hili.
ReplyDeleteMdau USA
WEWE MDAU WA TOKYO UPO HUKO NA WALA HUKUWEPO KWENYE TUKIO UMEJUWAJI AU UMEONAJE, KUWA VILIVYOTOLEWA NI MAKARATASI YA GARI NA LESENI, KWANZA SI DHANI NI SAHIHI KUTEMBEA NA MAKARATASI YA GARI GARINI! HIYO NI SHERIA YA WAPI, UNACHOTAKIWA KUTEMBEA NACHO NI LESENI NA KUMBANDIKA STICKER YA BIMA TU, ZIPO SABABU ZA MSINGI AMBAZO HUTAKIWI KUTEMBEA NA KADI YA GARI GARINI, PIA KAMA HUJUWI HATAKA KAMA NI MAKARATASI YALITOLEWA NI KWAMBA WANAKUELEKEZA KUWA WEKA PESA NDANI HAYO MAKARATASI ILI WATU WASIZIONE HILO LINAFANYIKA SANA, USIWATETE POLISI WA BARABARANI HIZO NDO ZAO NA NDO WANAONGOZA KWA RUSHWA TANZANIA, JAMII TUNATAKIWA KUIKEMEA HII KWA NGUVU ZOTE TULIZONAZO KISHERIA, NILISOMA RESEARCH MOJA JUZI JUZI ILIYOFANYWA NA SHIRIKA MOJA HAPO TANZANIA NA WAKAONA NI POLISI NA MAHAKA NDO WANAONGOZA KWA RUSHWA TANZANIA, JAMANI TUWAKEMEE HAWA WATU ILI TUWE KAMA RWANDA SWARIIIIIII
ReplyDeleteMDAU WA TOKYO,KWANZA KICHWA CHA HABARI KIMENIFURAHISHA(UKIKICHIMBA VIZURI),ILA KIUKWELI UNA POINT YA KWELI KABISA AMBAYO INAWEZA KUWA DOWNFALL YA HUYU MWANDISHI KAMA HAWA JAMAA(TRAFFIC POLICE)WAKICHUKUA LAWYER,ITAKUWA NGUMU KUTHIBITISHA KWAMBA WAMECHUKUA RUSHWA.UMEGUSA ANGLE ZOTE SINA CHA KUONGEZA.
ReplyDeletemdau wa tokyo nadhani unahitaji miwani na kama unayo kaicheki inaweza ikawa imeisha lenzi,kwenye video tumeona gari moja tu ndio iliotoa kama karatasi na hata hiyo karatasi hajaisoma akirudisha, lkn mengine nimkono tu kama wanasalimiana lkn pale ndio wanapokea hela, hata ungekuwa wewe unapokea rushwa lazima ufichefiche kidogo,vipi kuna ndugu yako nini unajaribu kumtetea hahaha! hiyo point yako ya uwanja wa ndege ni nzuri pale napo pamezidi sana natabia ya kufungua mabegi ya watu siyo nzuri mbona viwanja vya wenzetu hawafanyi hivyo? wanatakiwa wanunue vifaa ile ni aibu kubwa.
ReplyDeleteuko sahihi mdau.inajulikana kabisa kuwa trafiki ni hatari kwa rushwa ila hata mimi nilikuwa na wasiwasi kuwa unaweza kutoa ushahidi wa hizo lips.
ReplyDeleteSORRY MDAU! SIO MAKOSA YAKO KTK LUGHA.
ReplyDeleteTHANK YOU.
mdau kutoka tokyo, mbona sijakufahamu pale uliposema
ReplyDelete"Je, kabla hajakimbilia kwenye luninga kutaka sifa alifanya upelelezi wa kutosha akajua chanzo cha hayo yote ni nini na kama kweli wale madereva walidaiwa hongo?"
kwani kuna vyanzo ambavyo vinakubalika mtu kudaiwa hongo? mimi nilidhani hongo ni hongo tu, na kwa mujibu wa sheria za nchi hongo ni marufuku.
Wewe nafikiri huna hoja ,ila unachotaka uonekane umeandika kitu kwenye blog ya bwana michuzi basi,hivi uliangalia vizuri kweli?,je na wale watu wliohojiwa nao uliwasikia vizuri huwa wanatakiwa watoe bei gani ndiyo wapitishe bidhaa zao!?,au unataka ushahidi wa kinyamwezi?,au tuambie wewe kwa utalaamu wako unataka ushahidi upi hasa?,je ulimsikia msemaji wa jeshi la polisi(Abdallah Msika)alisema nini?!au alihitaji ushahidi upi zaidi ya huo ulionekana,ulimsikia mkuu wa polisi wa mkoa alisema nini!??,baada ya kuona hayo matukio waliitana wote kujadiliana hatua zipi za kinidhamu zichukuliwe juu ya hao askari
ReplyDeletehivi nikuulize wewe kweli uko japan au unaishi mtaa wa japan??!!
Mdau wa Japan asante sana kwa kujaribu kutetea rushwa, lakini mimi sikubaliani na wewe katika baadhi ya malezo yako. Kama kweli wewe unaijua vizuri hii nchi yetu, basi hauhitaji kuambiwa ni wapi RUSHWA imeshamiri au wapi inatendeka. Katika utezi wako unadai kwamba askari kwenye video alikuwa anaomba LESENI, sasa swali ni kwamba, kwa nini aiweke leseni ya dereva mfukoni mwake? Kwa mujibu wa shria, askari alitakiwa aangalie ile leseni,na kama inamatatizo ndio achukue hatua, lakini kinachoonekana ni askari anapoka halafu anaweka mfukoni.
ReplyDeletePili hakuna ushahidi wa rushwa zaidi ya maelezo ya MADEREVA wa malori ambao walihojiwa na wakaeleza jinsi wanavyo pata taabu kutoka kwa TRAFFIC polisi.
Kwa mtazamo wangu, ingaa ni kweli kwaamba rushwa ipo kila sehemu: bandarini, Airport, na Serikalini kwa ujumla, Mr.Jerry Muro anastahili pongezi kwa hatua yake hii ya kishujaa ya kupambana na tatizo hili la taifa.
Binafsi hii mara ya kwanza kabisa kuona ruswha ikitendeka kwenye NATIONAL T.V . Laiti kama mpiga picha angekuwa na CAMERA nzuri yenye zoom kubwa, ingethibitisha kwamba wale traffic walichopokea na kutia mfukoni ni RUSHWA, na sio leseni kama anavyotea mdau wa TOKYO.
MR. MURO, I APPLAUD YOU MY BROTHER. ONE MORE THING; FIGHT CORRUPTION EVERYWHERE YOU SEE IT, kama ni Bandarini, Airport, au Barabarani usichague, AND THAT'S WHAT YOU DID.
THANK YOU.
hizo video clips zinaonyesha 100% mazingira ya rushwa,lakini hazionyeshi jamaa akipokea hela, kwa hapo kisheria kuna LOOP HOLE ambayo huyo traffic anaweza kupenya,hata mimi naamini kuwa huyo traffic alikuwa anachukua mshiko lakini kuthibitisha ni ngumu,labda tupate mdau ALIESOMEA SHERIA atusaidie
ReplyDeleteUSHAHIDI NI MUHIMU SANA,NDIO MAANA TAKUKURU WAKIWEKA MTEGO WANAKUPA HELA ZAO WALIZOREKODI NAMBA ILI WATHIBITISHE HUYO MTUHUMIWA AMEKATWA NA HELA YA RUSHWA,MWANDISHI AMEFANYA KAZI NZURI LAKINI CLIPS ZAKE HAZIONYESHI POLISI AKIPOKEA HELA INAONYESHA ANAPOKEA BAHASHA AMBAYO YAWEZA KUWA NA HELA,DOCUMENT ZA MZIGO AU GARI,NACHUKIA SANA ASKARI WALA RUSHWA LAKINI HAPA MWANDISHI ANA KAZI YA KUTHIBITISHA KUWA ASKARI KAPOKEA RUSHWA NA WALE MADEREVA INABIDI NAO WASHTAKIWE NA WATHIBITISHWE WAMETOA RUSHWA,MIMI BINAFSI ASKARI BRBRNI AKINISIMAMISHA HUWA SITAKI MANENE NAMPA BAHASHA YENYE CERTIFIED(BY LAWYER)COPY ZA DOCUMENT ZOTE ZA GARI HADI TRA/REGISTRATION,KWAHI MWANDISHI AKINIREKODI ANAWEZA KUSEMA NIMETOA RUSHWA...NAKUBALIANA NA JAMII NZIMA KUWA ZILE CLIP ZINAONYESHA MAZINGIRA YA RUSHWA ILA KUSEMA NI RAHISI KUTHIBITISHA NI ANOTHER MATTER,POLISI WA UK WAKIKUKAMATA HIGHWAY WANAKUITA NDANI YA GARI YAO KWA MAHOJIANO KWASABABU YA USALAMA JE TZ UKIHOJIANA NA POLISI NDANI YA GARI YAO SI MTASEMA WALIKUWA WANAOMBA RUSHWA?? HII KESI NI NGUMU KUTHIBITISHA KULIKO TUNAVYODHANI
ReplyDeleteRESPECT KWA WADAU WOTE.
acha kufagilia ujinga wewe,ile mikono ya askari ilikwenda mfukoni kutafuta nini?au unataka ujulikane uko Tokyo ovyoo.
ReplyDeletewewe lazima itakuwa kuna jamaa yako ni askari kama sio mjoba basi kaka yako au dada yako au shangazi yako au shemeji yako, halafu eti unazungumzia air port na badari kwani huko airport na bandari wanaochukua rushwa si hao hao police, unachojaribu kuwatetea ni nini sasa, njooo siku moja na mnasimu yako ya kuokota na laptop kutoka huko japani then ukititoa kitu kidogo coustum na police nje wanakungoja nao wanadai zao..... uatakomaaaaaa ww ndau wa japani
ReplyDeleteHIVI TAKUKURU WANAOPATA PESA ZA WALIPA KODI WANAZIDIWA KAZI NA MWANDISHI MMOJA?WAKIWA CREATIVE RUSHWA ITAPUNGUA SANA TU ILA WANAKULA POSHO TU
ReplyDeleteDU! WE MDAU WA TOKYO ACHA KUJIFANYA KANA KWAMBA HUJUI KINACHOENDELEA BAINA YA ASKARI WA BARABARANI NA MADEREVA, WAKATI MWINGINE SIO LAZIMA UTOE HOJA YA HAJA UKIJIONA HUNA HOJA YA MAANA NI BORA UENDE UKAJIFUNZE KARETE AU TAIKONDO HUKO ULIPO KULIKO KUTUCHEFUA NAMNA HII. WATU TUNALIA JUU YA RUSHWA ZINAZO DAIWA KILAZIMA NA HAO MAASKARI HALAFU WEWE UNAKUJA NA HOJA AMBAYO HAINA KITAKO. HEBU SIKILIZA PALE DEREVA ANAPOTOA ILE KARATASI AU LESSENI NA KUMPA POLISI ANAAMBATANISHA NA PESA, NDO MANA HUWEZI KUONA KAMA ANACHUKUA HATA SEKUNDE KUMI KUIPITA ILE KARATASI. MIMI NIMESHASAFIRI SANA NA MALORI KUTOKA DAR KWENDA MBEYA NA HAYO NIMEYASHUHUDI KWA MACHO YANGU MAWILI. NB, KWA HIYO TOKA UENDE HUKO TOKYO UMEKUWA BLIND MINDED KUHUSU TZ, YAANI TAYARI UMESHA LOWEKA---- POLE SANA
ReplyDeletekaka kama ni leseni au kadi ya gari ameomba kwa nini aiweke mfukoni???
ReplyDeleteHata mkimlaumu mdau wa Tokyo lakini mawazo yake ya ukweli kwa kiasi fulani. tusiende kimkumbo tu, bali kinachotakiwa ni kutafiti na kujiridhisha kabla ya kutoa hukumu.
ReplyDeleteHakuna cha mdau wa tokyo hapa wewe huenda uko bongo tu na nahisi ni miongoni mwa askari walioumbuliwa na Jerry!!
ReplyDelete