Jerry Muro
Globu ya Jamii kwa niaba ya wadau wanaopenda weledi kazini inatoa pongezi kwa mtangazaji machachari wa TBC Jerry Muro kwa kazi nzuri anayoifanya katika kuleta habari mbali mbali zenye kugusa jamii nchini.
Akiwa Mwandishi Bora wa mwaka 2009 Jerry Muro amewonesha kwa vitendo kwa nini alistahili tuzo hiyo adhimu. Ameendeleza libeneke sio kwa kuganda kwenye mikutano na masemina na makongamano kama ilivyo kawaida ya wengi wetu, bali yeye anaenda eneo la tukio na kwa kutumia weledi wa hali ya juu ameweza kunasa vitendo ama matukio kibao na kuyaweka hadhadarani kama video hizo chini zinavyoonesha.
Hongera Jerry, zidisha juhudi, na endelea kuleta mapinduzi katika kubadili namna ya kuripoti, iwe TV, redioni na kwenye magazeti na mitandaoni. Kama kutakuwa na manenno maneno ya kukukatisha tamaa wala usihofu, kumbuka mwembe mtupu hautupiwi mawe...
-Michuzi
Ninaungana na Mdau Kiongozi wa Libeneke la "Globu ya Jamii" kumpa pongezi za dhati Jerry Muro kwa kufanya kazi hii ya uandishi kadiri wananchi wengi tulivyotarajia. Hii ni sehemu ya kazi yake lakini kwa kuwa ameifanya ikaonesha utofauti na tulivyozoea, pongezi ni jambo la busara sana!
ReplyDeleteHongera Jerr! Kaza buti kijana.
but sasa anatakiwa awe extra care na maisha yake.hawana maana watu wanaopenda kuishi kwa 'shotikati'
ReplyDeleteHongera Jerry Muro na ongeza bidii
ReplyDeleteJerry Kaza Buti, Hao askri wana tumwa na wakubwa wao, kuwa wasipo rudi na kitu wataondolewa barabarani. Kuna dreva asiyejua askari kula rushwa, Njoo mbuyuni hapa kuelekea Tegeta utaona akari na magari yao yamepack pembeni wanazichanga, pale Makongo Jeshini utakuta Traffic wamepack magari yao binafsi wanazichanga, ukienda njiapanda ya Kawe kuelekea Kawe posta pale utakuta wamepack magari yao binafsi wanazichanga, kwani hawa wakubwa unadhani hawajui...wanajua sana nadhani ma OCD, wakuwa vituo wanajua wote ni hao hao tu.kwani hawaoni wanaona sana?
ReplyDeleteThe 2015 Minister of Science & Technology
Muro hongera kwa kazi nzuri sana na ubarikiwe .
ReplyDeleteChangamoto:
Je Muro, au Michuzi, au TBC au Media yeyote mbona hamjatoa laivu mjadala hata kwa majina tu bila picha mnato wa wezi wa mabilioni wa Benki Kuu, Mremeta, Richmond Kagoda na hata wafanya biashara wa madawa ya kulevya nchini nk ambao athari yao ni kubwa sana kwa Taifa.
Sisemi kuwa hii rushwa kwa Polisi wa barabarani si kero au haituathiri la hasha; ila ninachouliza ni, je kipaumbele chetu ni kupambana kwanza na samaki wadogo wa elfu mbili mbili au tuelekeze kwanza nguvu zetu kwa the big fishes wa mabilioni ambao pigo la mmoja wao linaathiri madawa ya hospitali 50 au madawati ya shule za msingi 1000 au kudumaza akili za vijana zaidi ya 500 kwa uvutaji wa madawa ya kulevya na kuvamia watu kila mahali hadi Sullender bridge puani mwa Kituo cha Polisi bila uoga.
HAKIKA MKIRUSHA HEWANI HAYO HATA SIKU MOJA TU NA UPOKEE SIMU, SM, EMAILS TOKA KWA WANANCHI UTAKUWA UMEANZISHA PROGRAM OF THE CENTURY AMBAYO ITALETA MABADILIKO MAKUBWA SANA KATIKA NCHI YETU!
Jerry hongera sana na ama hakika unastahili kuikwa tuzo yako hiyo.
ReplyDeletetatizo moja tu nililonalo kwako ni kujisahau kwako either kwa kulewa sifa ama labda ni toka mwanzo upo hivyo.
nimekushuhudia mara mbili kwenye bar ya hongera na mara moja pale mlimani city ukiongea kwa either minajili ya ku atrract watu ama labda ndio sauti yako ilivyo habari zako hasa hizo za kiuandishi wa kipelelezi mpaka meza ya sita wanasikia tena huku unawaangalia watu wa meza hizo ilihali waongea na watu wa meza yako!
elewa kuwa sio watu wote wanaokupenda..ukimaliza kazi yako basi keep low profile..lakini sio masifa yasio na mipaka.
hiyo mosi, la pili jana nimebahatika kuona kipindi chako cha mahojiano na polisi pale TBC....sio lazima utupe mikono kwa kupitiliza ukiwa unasisitiza jambo...mwisho wa siku mi niliona kama unazidisha chumvi....jaribu haya mawili kuyarekebisha ili na mwaka huu ufunike zaidi.
mdau
Hongera sana Jerry kwa kuonyesha ueledi katika tasnia ya habari na mawasiliano kwa umma.Huu ndiyo uandishi mahiri makini.Wadau wanataka ubunifu unaoweza kuibua kero za kijamii na kuzitafuatia majawabu na siyo stori.
ReplyDeleteAnkal, nami naomba nichukue nafasi hii kuungana na wewe katika kumpongeza Jerry Muro, kwa kweli jamaa anafanya kazi nzuri sana, na anastahili kupewa pongezi.
ReplyDeleteKwa kifupi hii ndio kazi ya uandishi wa habari, sio kutuletea habari za rusha zisizo na ushahidi, hii ni kazi ambayo hata ikiwa presented, unakuwa na hamasa ya kufuatilia.
Kama ulivyosema Ankal, katika kazi kama hii, najua wapo mafisadi ambao wao wanaishi kwa kutumia kazi za rushwa kwa polisi ili wao waishi. Na hao si wengine bali ni baadhi ya polisi wenye vyeo vya juu. Naani kabisa kwao hawa huu ni msumari wa moto, na lazima watajaribu kukuingilia katika kazi yako nzuri, kaza buti mwanaume.
Huu ndio uzalendo wa kweli kwa taifa lako...
KAZA BUTI KIJANA JERY ILA ANGALIA WASIKUMWAGIE TINDIKALI.
ReplyDeletekamua baba,hofu yangu ni maisha yako maana wajomba watakuwa na hasira sana na wewe. big up sana
ReplyDeletemdau CM
Napata wasiwasi na maisha yake sasa.
ReplyDeleteanatakiwa kuwa mwangalifu sana na apate ulinzi.
Kijana apatiwe ulinzi mapema iwezekanavyo.
ReplyDeleteWalikuwapo wakina Sokoine, Amina Chifupa wakapita kama upepo.
Lets see about Muro.
Naungana na wadau kumpongeza Kijana Jerry ingawa bado nina tatizo kidogo, wajomba wa barabarani wanaokota visenti tu je kuna mpango gani na mapapa wanaojenga barabara ya km 1 kwa mabilioni ya pesa za walipakodi? Wanaojenga nyumba ya kuishi mtu mmoja kwa zaidi ya bilioni moja pesa ambayo ingelitosha kujenga hospitali kubwa kuwahudumia walima mahindi na mpunga huko vijijini? Wanaowasadia kina patel na vigogo wa biashara kupitisha makontena yaliosheheni vitu luxurious kwa kodi ndogo tu? Ni kweli trafic wanasumbua namuomba mjomba Jerry atembelee na mahakama zetu je zipo safi? Mahali ambapo tunategemea kupata haki zetu wanyonge zimegeuzwa pango la watu kutajirika! Hospitali zetu za serikali mambo yakoje?
ReplyDeleteJamii yetu imefika mahali ambapo inabidi nguvu za ziada kutuondosha, kila mtu anafikiria ni lini atapata nafasi ajilimbikie mali iwe kwa uhalali au kwa njia haramu, Viongozi wetu wa serikali mna kazi kubwa kujisafisha wenyewe na jamii ambayo inatuzunguka.
Hongera Jerry Muro, huu uwe mwanzo tu kazi kubwa ipo mbele yetu!
Naomba kuwasilisha
Jerry
ReplyDeleteHongera kaka, umekuwa mzalendo wa kweli kwa kufichua uhalifu.
Watakutisha but usihofu ni sehemu ya wanadamu..
USIOGOPE CHOCHOTE FANYA KAZI YAKO SAWA SAWA. TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO. HATA KAMA WATAKUFANYIA MABAYA, DHAWABU YAKO IPO KWA MOLA.
ReplyDeleteWATU WANASHINDWA KUELEWA KUWA DUNIA HII TUNAPITA TU, HAKUNA ATAKEYEISHI MILELE. HIVYO USIOGOPE KUFANYA KAZI YENYE MATUNDA MEMA KWA JAMII YA SASA NA VIZAZI VIJAVYO.
WAANDISHI WA HABARI NI KAMA WANAJESHI, KWANI WANAJESHI WANGAPI WAMEPOTEZA KUPIGANIA NCHI ZAO.
WATANZANIA ZAIDI INABIDI MJITOKEZE KUFANYA MEMA NA KUFICHUA MAOVU SIO KURUDI NYUMA KWA HOFU KUWA MAISHA YATAKUWA HATARINI. KWA TAARIFA TU MAISHA YA WATANZANIA WENGI TAYARI YAKO HATARINI. RUSHWA NI MOJA YA HATARI HIZO. HIVYO LAZIMA TUPAMBANE NA HATARI HIZO.
KAMA NYERERE ANGEHOFU MAISHA YAKE UNAFIKIRI TANZANIA INGEPATA UHURU KIRAHISI.
NELSON MANDELA ANANGEHOFU JUU YA MAISHA YAKE UNAFIKIRI UBAGUZI WA RANGI UNGEISHA AFRIKA.
NCHI ITAJENGWA NA WENYE MOYO. HIVYO KAMA UNA MOYO WEWE NYAMAZA KIMYA SIO KUSEMA MAISHA YATAKUWA HATARINI WAKATI TAYARI YAKO HATARINI.
KWA KUMALIZIA KUMBUKA ILI UPATE HUDUMA KWENYE TAASISI NYINGI ZA SERIKALI INABIDI UTOE RUSHWA KWANZA. NA MAMBO MENGI HAPA TANZANIA YANAPISHWA KWA SABABU YA RUSHWA.
HILI NI TATIZO KUBWA KWA JAMII.
ENDEDELEZA MAPAMBANO.
Kuna mtu aliwahi kusema kuwa ukiona polisi tajiri ujue anashirikiana na waharifu maana hakuna namna nyingine ya askari kutajirika, hiyo imedhihirishwa na kazi hii ya Muro. Pamoja na pongezi kwa Muro twende mbele zaidi na tujiulize hawa askari wengine utajiri wamepataje?
ReplyDeleteHongera Jerry Muro kwa kazi nzuri ambayo umekuwa ukiifanya tangu kipindi kile ukiwa na ITV mpaka hivi sasa,lakini kutokana na umri wako mdogo naamini bado taifa linakuhitaji ktk kufichua maovu mengi yaliyo mbele yetu...nasema hivi kwasababu kutokana na comment za Anonymous aliyepita aliyedai kuwa amewahi kukuona ktk sehemu kadhaa ukiongelea kuhusu kazi yako tena kwa sauti kubwa mbele za wa2..ambao wengi wao sina imani kama unawafahamu vizuri.NAPENDA KUKUPA ANGALIZO kuwa sio wote wanaokuzunguka ni wema na kutokana na kazi yako unaweza kuwa umewaathiri kwa njia moja au nyingine...kaka tunakuomba uwe makini na kauli zako haswa unapokuwa sehemu zenye mkusanyiko wengi,zaidi ya hayo nakutakia kazi njema.
ReplyDeleteDu, nilikuwa nasubiria hicho kipindi, nikapitiwa na usingizi lakini nashukuru umetupitia hako ka clip, tatizo ni internet service ya bongo ipo slow. inakata kata.
ReplyDeleteHata hivyo nampa hongera JERRY MURO, ila awe makini hawa jamaa wapo kama watu lakini sio, wataweza kumfanyia mambo ya ajabu tukalazimika kwenda Diamond jubilee au Karimjee njiani kwena Machame. MUNGU MUWEZA WA YOTE AMWEKEE ULINZI WAKE, MAANAKE WANADAMU NI WANAFIKI, HATA TUKIOMBA APEWE ULINZI , MATUMBO YETU YANA NJAA TUTARUHUSU RUSHWA, SI MNAKUMBUKA WAPO WALIOLINDWA NA WAKAVAMIA ASKARI HAWAPO, ETI SIKU YA TUKIO ASKARI WALICHELEWA KWENYE FOLENI AU ILISAHAULIKA KUPELEKWA.
Big up man, you are so creative. I like your coverage. You always do right things and not things right. That's quality investigative journalism. Iwe somo kwa waandishi wengine kuona umuhimu wa kuuncover evils in our society na kutafuta solution ya tatizo husika. Kama tunahitaji journalism as a profession kuwa recognised na kuheshimika we should really work hard na tuachane na habari ya njaa kufuatilia vibahasha.
ReplyDeleteBravo Muro!
Safi sana Jerry.Ni mfano wa kuigwa,mngekuwepo watano kama wewe tungekuwa mbali katika kuondoa ufisadi jodari (Papa).
ReplyDeleteKijana Jerry endeleza mpambano. You are the best. Usijali maneno na fitna zao. Tuko pamoja na wewe
ReplyDeleteyaani hao viongozi wa takukuru na mwenyekiti wa usalama barabarani mpk huyu msemaji wa jeshi la polisi ni siasa kwa kwenda mbele wote wanajaribu kuilinda serikali, anyway ndo bongo yetu hiyo, ukweli ni kwamba mishahara ni midogo sana ukilinganisha na gharama za maisha
ReplyDeleteNi kweli Muro ni mwandishi mahiri na amefanya kazi kubwa ajabu. Mimi inanipa wasiwasi kidogo anavyo-expose sura yake. Angeweza akaripoti huo uovu, bila ya yeye kuonekana kwenye screen kwani kazi nzuri ananoyifanya haitafurahiwa na wengi. Katika kupekuwa vitabu vingi vya taaluma ya uandishi wa habari, sentensi ifuatayo huwa naiheshimu sana. THERE IS NO STORY WORTH YOUR LIFE. Kwa hiyo mdogo wangu Muro, angalia hili otherwise kazi yako ni nzuri mno.
ReplyDeletehakika Mdau wa Wed Jan 20, 01:20:00 PM you have made my day !
ReplyDeleteoh yes, he has been bold enough to do that exposee, but he really need to learn slowly from the pro's hiyo ya kuongea kutaka misifa ndio mbavu zangu weeee, na hiyo ya kuongea akirusha mikono kwikwikwi
nampongeza kwa ujumla lakini achukue na hizi changamoto, yuko station nzuri atapata safari za nje na mafunzo zitamsharpen zaidi..
Hongera sana kijana kwa kazi nzuri unayoifanya. Tupo pamoja.
ReplyDeleteHongera sana Jery Muro. Ushauri wa bure.
ReplyDeleteJaribu kuwa na kikosi cha "Investigative Journalism" hawa watu wawe ni kana CIA wako vile yaani wasijulikane na wewe uwe unachukua nafasi ya kuwa Kama reporter wa matukio tu ukitoa reference kwa "Mchunguzi wetu aliona" badala ya niliona au nilikwenda. Hii itapunguza risk ya wewe kuwa target kwani wanajua kuwa wewe ni tawi tu hata likikatwa shina bado lipo so there is no need to do that.
Nchi yetu bado sana kwenye usalama wa raia na mali zao. Hivyo wasijepanga kukufunga mdomo jumlajumla god forbid.
Ila nafikiri Tanzania Tukipata akina jery kama kumi kwa kuanzia tuna uwezo mkubwa sana wa kubadili mienendo ya rushwa na uhujumu uchumi na kuleta maendeleo kwa kila MTZ
vyombo vyote vinabidi kuiga mfano.vyombo vya habari huwa vina mchango mkubwa sana sana sana sana ila vya kibongo havijielewi elewi mimi huwa siamini hapa BBC wakiamua kushupalia jambo hata kama ni dogo kiasi gani.
ReplyDeleteUkifuatilia sana koment za Mdau wa Wed Jan 20, 01:20:00 PM utagundua ni Askari wa usarama barabarani.
ReplyDeleteHongera sana Jerry Muro, pia kuna askari mwingine MZANZIBAR, mweupe mnene kidogo yupo pale Ferry (Kivukoni kuelekea kigamboni), yule Trafiki ni mshenzi sana, analazimisha rushwa, naomba Jerry Murro avuke pale muda wa jioni wakati wa foleni then amuone........ mshenzi kabisa yule
ReplyDeletek'dume
Nami naungana na Anonymous wa Jan 22 at 08:22:00PM;kwamba anaporipoti asioneshe kwamba yeye ndiye anayefanya kila kitu, ionekane like its kind of a team work.Kuna watu wengi behind the stories/investigation. Hata mtu akitaka kumdhuru ataona haitasaidia chochote kwani wengine wataendelea na kazi.Pia asilewe sana na sifa,apunguze kdg sifa
ReplyDeleteMungu tunaomba utuongoze watu wako maana hatueleweki sana. Mtu akiwa anafanya kazi vizuri ohh anapenda sifa. Atapendaje sifa?? Anafanya kazi yake inavyotakiwa sio sifa hizo. Kwani sifa zitamsaidia nini? Kama ni hio faida mbona wewe hujitumi? Tusaidiane kwa kweli la sivyo tutabaki nyuma siku zote.
ReplyDeleteKupiga vita rushwa ni kazi sana hasa kwa upande wa askari polisi kwani vitendo hivi vinafagiliwa na viongozi wao wa juu kabisa, huku kwenye Public wanajifanya Oooh! tutawachukulia hatua, wakifika wanawaambia
ReplyDelete"Mnapopokea kuweni makini sana, mnatudhalilisha kwa umbumbumbu wenu wa kupokea hadharani sisi tukiletewa picha zenu tutawabadilisha vituo"
Nakumbuka kuna mdogo wangu alikuwa depo kule moshi siku ya kumaliza Sumaye(wakati huo waziri mkuu)alikuwa ngeni rasmi na Mahita (IGP) wa wakati huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuongea alianza kuongea yeye then akafika mahali akasema naomba mzime hivyo vipaza sauti vikazimwa, maneno aliyoongea huwezi amani kama yanatoka kwa mpinga uhalifu mkuu, namnukuu
"Mtamaliza hapa mtapangiwa vituo na kuanza utendaji mliosemea hapa, ila kuna vishawishi vingi hasa vya pesa pale utakapomkamata muhalifu halafu akataka kukupa pesa, Mimi nasema hivi chukua palepale atakachokupa ila usianze kumtaka akakuletee zingine mahali ati kwa kuwa hizi alizokupa ni ndogo hapo ujue kuwa unaingia pabaya na ukikamatwa sisi tutakukana kuwa ni mwenzetu"
Maneno kama haya yanachochea rushwa zaidi badala ya kupinga. Huu ndiyo mtazamo ndani ya jeshi la polisi ndiyo maana hawa jamaa hata buku anachukua.
IT'S A JOKE - ELFU TANO, KUMI AU ISHIRINI WHAT'S THAT??
ReplyDeleteKUWENI FAIR BASI SIO TU KUWAANDAMA POLISI KILA SIKU!!
KWA NINI WATZ NI WAZURI SANA KUDEAL NA PETTY ISSUES?? WHY??
IT'S AN EFFORT BUT NOT IMPRESSED UNTIL I SEE THE MEGA ONES ADDRESSED, NOT YET.