President Jakaya Mrisho Kikwete in private talks with former US President Bill Clinton in Davos Switzerland. President Kikwete arrived in Davos yesterday to attend the World Economic Forum Summit. Photo by Freddy Maro.
Asante sana, JK amwambia Bill Clinton
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amemshukuru Rais wa zamani wa Marekani, Rais Bill Clinton, kwa mchango wake katika maendeleo ya Tanzania, na hasa katika sekta ya afya na kupambana na maradhi.
Aidha, Rais Kikwete amemweleza Rais Clinton athari za kiuchumi ambazo zimeikumba Tanzania kutokana na msukosuko wa uchumi duniani na hatua zinachukuliwa na Serikali yake kupambana na msukosuko huo.

Rais Kikwete amemweleza hayo Rais Clinton wakati viongozi hao walipokutana na kufanya mazungumzo usiku wa leo, Jumanne, Januari 27, 2010, kwenye Jengo la Kirchner Museum, kwenye mji mdogo wa Davos ambako viongozi wote wawili watahudhuria Mkutano wa 40 wa Taasisi ya Uchumi Duniani ya World Economic Forum (WEF) unaoanza kesho, Jumatano, Januari 28, 2010.

Rais Clinton alikuwa ameomba kukutana na Rais Kikwete, hata kabla ya kiongozi huyo wa Tanzania kuwasili hapa kwa ajili ya Mkutano wa WEF wa siku tatu unaotarajiwa kuhudhuriwa na viongozi kutoka zaidi ya nchi 30 duniani.

Rais Kikwete na ujumbe wake wamewasili Davos, mji mdogo ulioko milimani nchini Uswisi usiku wa leo, wakitokea Sirte, Libya, ambako Rais Kikwete alisimama kukutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi.

Katika mkutano wake na Rais Clinton, Rais Kikwete amemshukuru kiongozi huyo wa zamani wa Marekani kwa misaada ambayo imekuwa inatolewa moja kwa moja na Taasisi za Clinton, ama kupitia taasisi nyingine, hasa katika sekta ya afya katika kupambana na magonjwa ya malaria, ukimwi na kifua kikuu.

“Tunakushukuru sana Mheshimiwa Rais kwa misaada yako, na napenda kukuhakishia ushirikiano wa Serikali yangu na wananchi wa Tanzania katika kuendeleza ushirikiano huo,” Rais Kikwete amemwambia Rais Clinton katika mazungumzo hayo yaliyochukua kiasi cha dakika 40.
Wakati wa mazungumzo hayo, Rais Clinton alitaka kujua jinsi gani msukosuko wa uchumi duniani ulivyoathiri uchumi wa Tanzania na hatua ambazo Serikali ya Kikwete inachukua kukabiliana na athari hizo.

Rais Kikwete amemweleza athari hizo ikiwa ni pamoja na kushuka kwa bei ya mazao ya kilimo ya Tanzania kwenye soko la kimataifa, kupungua kwa mahitaji ya mazao hayo kwenye soko hilo, kupungua kwa idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania na kupungua kwa uwekezaji katika uchumi wa Tanzania.

“Tulikuwa tunatarajia kuona uwekezaji mkubwa katika uchimbaji wa madini aina ya bati na ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuyenyusha bati, lakini wawekezaji katika maeneo hayo wameahirisha mipango ya uwekezaji wao hadi hali ya uchumi duniani itakaporekebika,” Rais Kikwete amemwambia Rais Clinton.

Rais Kikwete pia amemwambia Rais Clinton kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali yake kukabiliana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na kutangaza Mpango wa Kunusuru na Kuhami Uchumi wa Tanzania uliotangazwa na Rais Kikwete Juni, mwaka jana, 2009.

Rais Kikwete pia amesema kuwa chini ya Mpango huo, Serikali yake italinda mafanikio yaliyopatikana katika huduma za kijamii kama vile afya na elimu, na katika ujenzi wa miundombinu nchini, na hasa barabara kwa sababu ya umuhimu wa huduma hizo katika kuboresha maisha ya Watanzania.

Kesho, Jumatano, Rais Kikwete anatarajiwa kuungana na viongozi wengine kutoka zaidi ya nchi 30 katika ufunguzi wa Mkutano wa 40 wa WEF unaoanza leo mjini hapa, Davos, Uswisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Hii picha ni utata kidogo. Inawezekana huyu clintoni kweli? mbona inasemekana yupo Haiti--akiwa ndio muwakilishi wa Amerika.

    ReplyDelete
  2. Alafu JK muoga kwa wazungu!!

    ReplyDelete
  3. hya tena bakuli hiloooo,jamaa wanasaidia watu wa haiti muungwana weee,hawana kitu sasa baaaa!!!!!

    ReplyDelete
  4. Kwani brother Michuzi Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa hayupo???maana naona kila inapotokea safari za nje anakwenda mwenyewe Mheshimiwa Rais ina maana watendaji wake hawawezi kuzifanya hizo ziara mpaka aende mwenyewe??? Aulizae ataka kujua ni mtazamo tu!!

    ReplyDelete
  5. Mbona nilisikia maraisi wote wameenda huko? Obama, Ahmadinejad, Mwai Kibaki, Kim nk

    ReplyDelete
  6. Wewe anon. wa kwanza hapa picha hiyo haina utata bali kichwa chako ndio kina utata,umeambiwa huyo ni Bill Clinton Rais mstaafu wa Marekani.Kwa kukusaidia aliyekuwepo/kwenda Haiti ni Hillary Clinton waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani ambaye pia ni mke wa Bill Clinton...acha kukurupuka.
    MWALIMU.

    ReplyDelete
  7. Mdau wa Jan 28 11.05 usiwe na wasiwasi. Kutegemeana na madhumuni ya safari anaweza kwenda Rais au Waziri wa mambo ya nje, na mara nyingine huambatana wote katika ujumbe mmoja. Ninavyofahamu ni kuwa diplomasia imebadilika na kuna kazi nyingi ambazo kiasili zilikuwa zinafanywa na mabalozi na mawaziri wa mambo ya nje ambazo marais huzifanya kwa sasa. Hivyo kupelekea kumuona rais kama vile anafanya kazi zisizomhusu.

    ReplyDelete
  8. tumezidi sasa khaaaaaaaaaaaa!!

    baraza la mawaziri kuuuubwa utendaji hata hatuujui,,TUNAITAJI kuzijua JOB DESCRPTION ZAO kwakweli kwa mwendo huu

    na wewe MWALIMU acha kukurupuka ovyo sana,,ni kweli clinton rais mstaafu wa USA alikua Haiti pia...

    i

    ReplyDelete
  9. Siasa ina niudhi sana! Yani kila siku mnakuwa kama mko shule. Picha ineleza kabisa kuwa Bill hakuwa na mazungumzo maalum na Kikwete. Clinton alikuwa amekaa na marais wa nchi masikini walikuwa wanakwenda mmoja mmjoa kumsalimia na kutoa matatizo yao. Kwanza ngalia kuna kikombe kimoja tu cha chai kama Kikwete angekuwa pale kwa muda mrefu kungekuwa na vikombe viwili au walau glass ya maji. Pili Mh. Kikwete tunakuomba ukiwa na Mazungumzo ya hao wakuu wa nchi jaribu kidogo kuonyesha kama na wewe Rahisi wa nchi sio unakaa kama uko na mwalimu mkuu. Kumbuka wewe ni alama ya Taifa sasa kila ulifanyalo linamwakilisha Mtanzania. Hii si mara ya kwanza Mkuu, pitia picha zako zote uone ninachokisema. Kumbuka confidence ndio silaha kubwa!!

    ReplyDelete
  10. WATANZANIA TUNA MOYO WA UPENDO TUNAHUDHURIA KILA MSIBA UNAPOTOKEA HATA KAMA MAREHEMU HAUMFAHAMU VIVYO HIVYO KILA MKUTANO HATA KAMA HAUNA FAIDA KWAKO MRADI KUNA POSHO.

    ReplyDelete
  11. KWA WATAMBUZI WA PICHA KIKWETE ANAONEKANA AKITETEMEKA KWA BARIDI WAKATI MWENZAKE ANAONEKANA AMEIZOEA HALI YA BARIDI IN OTHER WORD YUKO COMFORTABLE.

    ReplyDelete
  12. “The New, World Credit System:

    The Question Before Us”



    Without the Four Powers, Trans-Atlantic Region Is a Doomed Civilization. “What you are seeing in the trans-Atlantic region is a dying civilization, a dying, self-doomed civilization,” Lyndon LaRouche said. “What you are seeing in the trans-Pacific region, especially on the Asian side and the Indian Ocean side of that, you’re seeing progress!”

    We are recommending it as a policy. We are not authoring the policy; we are recommending it. It’s a doctor’s prescription for the patient if he wishes to survive.. We have no power to enforce a prescription; we are simply providing it.”

    ReplyDelete
  13. Huyo jamaa anayemvalisha Kikwete ni wa kutandika viboko...!!sometimes huyu jamaa anajifanya kuwa casual lakini amechanganya tu marangi...!

    ReplyDelete
  14. Inaonekana JK ana umaarufu wa pekee

    ReplyDelete
  15. jamani humu ndani watu wana visa acheni tu nijichekee lol!!

    ReplyDelete
  16. kikwete hapo anaonekana anatetemeka baridi kwa sabab hajapata kahawa mwenzake anashtua na kahawa ikamweka sawa.

    ReplyDelete
  17. Kaka Michuzi
    Nimekuwa nikifuatilia kwa makini sana utendaji wa viongozi wetu na sifa za Tanzania ndani na nje ya nchi. Kwa ufupi sana Tanzania is one of the "politocal power house in Africa". hili kwa asilimia 100 halina ubishi kuwa viongozi/jina la Tanzania kimataifa ni kubwa tangu enzi za ukombozi kusini mwa afrika....na kwa mantiki hiyo Tanzania inaheshimika kila mahali sasa hivi....TATIZO ni Moja

    Tanzania haijabadilika na mazingira...mfano rai ankwenda kuhudhuria Mkutano anu tukio la kimataifa " anatakiwa kwenda na ISHU ambayo anataka dunia au nchi zilizoendelea zimsaidie" Rais/Ujumbe wa Tanzania unatakiwa uende kulobby na kutoa a serious proposal on key developmenetal(not politix) au general statement ya Afrika..afrika...afrika ...Niloitegemea raisi angetoa maneno yafuatayo..."mf. Tanzania inakabiliwa na tatizo la miundombinu kutokana na ukuaji wa uchumi na wingi wa watu... Naiomba jumuiya ya kimataifa/ nchiu zilizoendelea zinisaidie katika yafuatayo
    (1) Upanuzi wa Bandari zetu za Dar, Tanga, Mtwara ili kupanua biashara na kati yetu na nchi zsizona bahari na dunia ya mbali,
    (2) Upanuzi wa Viwanja vya ndege vya Dar, Klimanjaro , Arusha etc kwa jili ya kukuza biashara na nchi zote
    (3) Upanuzi wa Barabara za miji mikubwa DAR, ARUSHA, Mwanza etc ili kuongeza tija ya usafiri mijini
    (4) Miondombinu mipya ya RELI za miojini kwa treni ziendazo kasi...(hapa angewabana Japan, USA, Korea, UK, na nchi zote zenye maendeleo katika eneo hili na kuwapa some trade off ya key interest zao bila kuathirio maslahi ya Taifa,
    (5) Kilimo akataja ka-eneo fulani muhimu
    (6) halafu angeendelea na mambo mengine kam maji safi, afya kwa watoato, upanuzi wa vyuo vikuu...nkl Nina maana kati ya hayo hapo juu Raius/Tanzania ingekuwa na ishu moja au mbili za kuhakiksha inazipata na zinakuwa key ishue ktk mkutano huo na timu yote ingeelekeza nguvu zake kulobby kwa hilo...sasa kunakuwa na general statement afrika, afrika, agrika want this..bla.....hatutafika mahali kwa stahili hii michuzi..lazima tuwasome wenzetu wanafanya nini...
    Kaka michuzi sipendi Rais wangu aonekane kama Mtalii,....na pia nakubaliana na mtoa maoni hapo juu kuwa rais naye lazima awe anaonekana kujiamini...anaonekana kukaa kiwogawoga wakati anmfahamu na amekutana na Clinton mara mingi sana...
    Kaka naomba unikosoe au wadau wanikosoe kama nimesema kitu kibaya ktk haya maoni yangu....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...