Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (katikati) mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa kazi na kamati ya Bunge kujadili maeneo mbalimbali ya mabadiliko katika sheria ya madini ya mwaka 1998 na hatimaye kupata sheria mpya ya madini leo wilayani Bagamoyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hawa jamaaa kila siku wanazungumzia kurekebisha sheria ya madini ni muda mrefu sasa viongozi wetu hawa wanafanya mambo taratibu sanaaaaa hata pale panapohitajika haraka ina maaana madini yanayochimbwa sasa yako chini ya sheria mbovu!!!!kama wameshindwa michuzi waambie kuna kucopy na kupest sheria za nchi nyingine kama botswana na south
    nchi nchi inaangaamia kutokana na sera za CCM kulindana ubinafsi rushwa
    jamani amkeni fanyani mambo harakahara tanzania tunaachwa watu waje kununua madini tanzania sio madini yapelekwe hongkong na kenya ibadilisheni tz iwe kama bangkok

    ReplyDelete
  2. huo uslow wao ndio zuga wapate kubunya kama wanalia vile bongo nchi ya vipofu na viziwi

    ReplyDelete
  3. Mie nimetazama website ya EITI.org kuhusu transparecy ya mikataba, mbona ni nchi masikini ndizo zimeridhia kusaini.

    Sasa makampuni ya Australia, Canada, South Afrika ambao hawajasaini watayabana makampuni yao yaliyowekeza Tanzania ktk sekta ya madini kuweka wazi mikataba, au wataruka kimanga, maana wazungu mkataba(sheria) kwao ndo dini yao huwezi kuwaambia jamani hamuoni haya kutunyonya hivyo, wao watatujibu si mkataba ndo unazungumza kila kitu, sasa sie wakubwa hatujatia saini hivyo hatuutambui.

    Au EITI ni kwa ajili ya kufuatilia Bloody Diamonds yaani madini ynayotoka ktk nchi zilizo ktk vita kama Congo DRC, Sierra Leone?

    ReplyDelete
  4. Kama kuna mtu ana nakala ya mkataba wa madini naomba aitundike online ili wananchi tuweze kupata mwanga kitu gani kinaendelea.

    ReplyDelete
  5. Gwabha KuliaJanuary 19, 2010

    Rais wetu mpendwa:

    1. Tenganisha wizara, Madini na Nishati ziwe mbili.

    2. Katika wizara mpya ya madini,
    pata waziri mpya, katibu mkuu mpya na kamishina mpya wa madini. hao wawe wasomi kweli waliobobea katika sheria za madini na jiolojia na wawe wazalendo ambao hawajawahi kuwa na skandali. Tafuta popote walioko ndani au nje ya nchi.
    Utalikomboa Taifa letu kwa kiwango kikubwa sana kupitia wizara hii. Na wakati GDP/ GNP inapanda kutoea sekta hii unikumbuke kwa jina langu kupitia blogu hii ya wananchi.
    Natoa wosia huu leo tarehe 19 Januari katika mwaka wa ukombozi wa 2010.

    ReplyDelete
  6. NINA MIAKA HAMSINI NA TATU SASA, HAWA WATU TOKA NIKO VIDUDU WANASIKIA SERIKALINI NA BUNGENI HADI LEO WANAKULA TU MWEEEEEEE TUWAACHIAGE NA WATOTO WALE SASA

    ReplyDelete
  7. Wewe unalalamika watu ni wale wale kwani hujui Green Economy ya ku-recycle?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...