
Kama tulivyoahidi kampeni ya kuchangia waathirika wa mafuriko yanayoendelea nchini ambayo yameshaathiri watu wapatao 40,000 inaingia katika ngwe yake ya kazi baada ya vyombo vya habari kutumika kuhamasisha wananchi kuchangia kuanzia kesho.
Bw. Sanctus Mtsimbe ambaye ni Rais wa Tanzania Professionals Network atakuwa kwenye vyombo vya habari kuanzia saa kumi na mbili asubuhi kuanzisha uhamasishaji huo na baadaye kuwa na mkutano na waandishi wa habari.
Ratiba yetu ya Uhamasishaji huo iko hivi hadi hivi sasa:
- Saa 12:30 - Kipindi cha Kumepambazuko ITV
- Baada ya Taarifa ya habari ya TBC ya saa moja - TBC
- Saa 4.00 za asubuhi mkutano na waandishi wa habari Ofisi za TPN karibu TBC Radio (barabara ya Nyerere). Jengo la TOHS Ghorofa ya Kwanza.
- Jumatano kipindi cha "Power Breakfast" asubuhi M . M. Mwanakijiji atazungumzia kampeni hii na kujadili kwanini ni muhimu kuunganisha nguvu katika suala hili.
M. M. Mwanakijiji
Ratiba yetu ya Uhamasishaji huo iko hivi hadi hivi sasa:
- Saa 12:30 - Kipindi cha Kumepambazuko ITV
- Baada ya Taarifa ya habari ya TBC ya saa moja - TBC
- Saa 4.00 za asubuhi mkutano na waandishi wa habari Ofisi za TPN karibu TBC Radio (barabara ya Nyerere). Jengo la TOHS Ghorofa ya Kwanza.
- Jumatano kipindi cha "Power Breakfast" asubuhi M . M. Mwanakijiji atazungumzia kampeni hii na kujadili kwanini ni muhimu kuunganisha nguvu katika suala hili.
M. M. Mwanakijiji
Kwa maoni yangu sioni tofauti kati ya waathirika wa mafuriko na waathirika wa ukimwi/vvu. kabla ya kuchangamkia tenda hii tujiulize matrilioni ya pesa zilizokwishabwagwa katika janga la ukimwi/vvu yameleta faida gani katika mazingira ya utamaduni huu wa ufisadi tulioulea na tunaoendelea kuulea! ninasita kuhimiza hata niwajuao kuimarisha ufisadi. Kodi tumeishalipa, ni kazi ya anayekusanya kodi kuwapatia huduma waathirika!!! Kama kweli tuna akili timamu, nitaunga mkono uamuzi wa kuahirisha uchaguzi mkuu (ambao sioni faida yake yo yote zaidi ya kuwa mchezo wa karata tatu) hadi 2015 na badala yake hayo mafungu yaliyotengwa kwa 'kamari hiyo' yaelekezwe kusaidia wahanga wa el nino na kukarabati miundombinu.
ReplyDeletechidumu chama cha mapinduzi.
mlalahoi
Kwa mfugamafisadi
Haya ndiyo maneno! Watanzania tumezoea kulalamika na kunung'unika sana sasa hii ni nafasi yetu kuonesha kuwa tunajali na tunaweza. Big ups mwanakijiji na wenzako!
ReplyDeleteTUKO PAMOJA MKUU PIA NA MALALALA MIKO KATIBU MHUHUTASI WAKO MWANAKIJIJI ANAKALIA MAONI YANGU KWENYE JAMVII LAKO KUU NAOMBA ULIFANIE KAZI
ReplyDeleteWazo hili ni zuri lakini tukuulize ndg. Rais wa TPN kwa vile unashirikiana na Mwanakijiji, basi utuelezee wanataaluma na wananchi wa TZ,
ReplyDeleteMWANAKIJIJI NI NANI NA KAZI YAKE NI NINI ILI SOTE TUMFAHAMU TUMUUNGE MKONO PIA.
MAANA MIMI NA FAMILIA YANGU NA MARAFIKI ZANGU HATUWEZI KUUNGA MKONO MTU ASIYETAMBULIKA KAMA MZUKA HIVI AU ZOMBIES AU MKAZI WA SAYARI TUSIYOIJUA AU JINI N.K
SIOMBEI LAKINI NAFIKIRI TU, JE IKITOKEA SIKU ZA USONI LIKAZUKA JANGA AU TUKIO BAYA LINALOMHUSISHA YEYE UTAWAELEZAJE WATANZANIA?
DUNIA YA SASA MAMBO NI WAZI HAKUNA USHIRIKA NA SECRET SOCIETY AU UNKNOWN BEING BILA KUJUA NI NANI WALA MOTIVE YAKE.
TUJIULIZE, KAMA MAAFISA WA USALAMA WA TAIFA WENYEWE AMBAO HAKIKA NI WATUMISHI TUNAOWAITA 'WA SIRI' LAKINI WANAFAHAMIKA WAZI NA OFISI ZAO TUNAZIJUA, JE SI ZAIDI MWANAKIJIJI?
ZAIDI YA YOTE MFANO TU, NA HAPA SIMAANISHI KUMTUSI MTU AU KUMLABEL MTU MAANA MIMI SIMFAHAMU;
JE IKITOKEA WA AJILI YA MCHANGO WANGU MARA NIKAAMBIWA KUWA NIMEKUWA NIKISUPPORT GAIDI NA NINATAKIA KUFIKISHWA MAHAKAMANI, NITAJIBU NINI MAANA KWELI SIMFAHAMU LAKINI MIMI NAKUFAHAMU WEWE SANCTUS? NI BAADA YA MATUKIO MABAYA NDIO UTAONA JINSI VYOMBO HUSIKA VINAVYOANZA KUCONNECT DOTS!
IELEWEKE WAZI KUWA KUNA UTOFAUTI MKUBWA KATI YA ANONY WA KUCOMMENT KWENYE BLOGU NA MITANDAONI NA MTU AMBAYE ANATAKA KUKUSANYA MICHANGO KWA AJILI YA SHUGHULI ZA UMMA.
Michuzi huwezi kuzuia hili swali langu hata kama kuna mtu anafikiri mimi ni mshamba au nina wivu ni sawa tu.
Mdau Juma A. kwani nilazima uchangie kupitia mwanakijiji? si wamekuambia unaweza kupeleka msaada wako kwa Chama cha Msalaba Mwekundu mahali ulipo. Kama wewe una nia ya kusaidia peleka msaada wako huko, nani amekuambia serikali au vyombo vya usalama havimfahamu mwanakijiji? Wanajua hadi kitanda anacholala na wanaheshimu kazi yake. UwT
ReplyDelete