Brother Michuzi,
Naomba niwekee kilio changu kwenye Blog yetu tukufu, please. Asante

Ilikuwa majira ya asubuhi wakati vijana wa shirika la maji Dares salaam walipokuja kwetu kwa madai ya kusafisha mita ya maji. Tupo Magomeni mapipa barabarani katika kituo cha daladala cha kuendea Kariakoo, tunalitumikia taifa kwa kazi ya kulisha chakula , SEABOYS FAST FOOD sehemu nadhifu inayopendwa na wengi na ni pasafi kiasi cha kwamba hatujapata malalamiko kutoka kwa ma-bwana afya.
Vijana wa dawasco baada ya kufika na supana zao waling'oa mita yetu ya maji na kuondoka nayo. Muda si mrefu walikuja na mita ingine (ambayo kumbe siyo ile yetu ya zamani ) na kuipachika pale na mda huo huo wakadai kwamba tunatakiwa tulipe bili ya maji ya LAKI 7 wakati bili yetu ya maji ya mwezi huo ilikuwa laki 180 na ambayo tayari computer zao zinaonyesha ya kwamba tumekwisha lipa.
Uzuri ni kwamba risiti zote za maji za miaka kadhaa ya nyuma tunazo na daima tuko mbele kulipa bili zetu.Hiyo mita waliyotupachikia ilikuwa tayari inasoma unit zilizotumika kibao.
Hatukusita kuwauliza, jamani hii bili ya laki 7 ni ya mwezi gani ??. mpaka hivi sasa naandika barua hii, hatuna maji,yaani walitukatia pale pale. Tuna endesha restaurant katika mazingira magumu.
Ndugu zangu na binadamu wenzangu tunaompenda Mungu na tunaokwenda misikitini na makanisani kusali, swali langu kwenu ni hili JE ?? HUU NI UUNGWANA ?? naomba barua yangu hii iwafikie wapenzi wote wa haki za binadamu.
Tusaidiane kuukemea unyama huu ambao sisi kwa sisi tunaweza kila raia ana majukumu ya kuisaidia jamii. Namaliza kwa kuwatakia mwaka mpya wenye amani na furaha.
Mdau Ezekiel Zebedayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Uungwana ni kitu cha bure nakupa mfano mdogo sana hapa ninapoishi Sweden takriban miaka 24 sasa bili ya maji unasoma mweyewe mita yako na unaituma kwa kupitia mtandaoni kwenye shirika la maji.Hata siku moja hakuna ushenzi kama uliyo kukuta .Hivi majuzi tu mita yangu imebadilishwa na kufungwa mpya na ile ya zamani walipotoa mimi na fundi tumetia sani imesimamia namba gani.Pole sana Bro ni serikali
    ndiyo inawapa watu chance ya kuwaibia raia zake na hakuna litakalofanyika.Unbelivable ndiyo kisa kilichonifanya nisijakanyage TZ tokea nilipoondoka.Poleni ndugu zangu.

    ReplyDelete
  2. kizingo ng amboJanuary 04, 2010

    POLENI SANA WAJASILIMARI,NA HAO JAMAA NI JIRANI ZENU HAPO MLIPO YAANI WAKO NYUMA YA JENGO LENU WENGI WAO WANAKUJA KULA HAPO]SAFI SANA HILI SWALA MLIVYO LILETA HAPA NA TUNALISOMA LAKINI PIA MNGECHUKUA HATUA ZAIDI HASWA KWA WAKUBWA ZAO NGAZI TOFAUTI NA KWA KUWA USHAHIDI MNAO WA MALIPO YENU NAFIKILI MNAWEZA KUSAIDIWA ZAIDI NA BAADHI UWA WANAPITA HAPA MICHUZIII KAMA HAWAJATUMWANA NA HAO MABOSI MAAANA INAWEZA KUWA KESI YA NYANI UKAMPELEKEA KENGEDELE ALIE KOSA HATA TONE LA AIBU,LA NITAKUJA NA GLOUP YANGU TUJUE TUTAWASAIDIAJE POLENI SANA.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA SIO WANAOWAONEA WANYONGE

    ReplyDelete
  3. MiundombinuJanuary 04, 2010

    Bongo ni kuishi kwa kutumia Ubongo.. Hivyo Bwana ZeyB kuwa mpole tu u-solve issue yako kimya kimya. Ukipiga kelele sana utaletewa Msala mwingine wa Mamilioni hapo sasa ndo utajuta zaidi kuwaanika hadharani hao "wajasiliamali" wenye kauli mbiu ya "Utakula kazini kwako"

    ReplyDelete
  4. Pole sana kwa tatizo hilo ambalo linawakabili pia watumiaji walio wengi. Kimsingi nakushauri mambo mawili kama ifuatavyo:
    1. Andika barua rasmi ya malalamiko yako na uipeleke ofisi za DAWASCO ukiambatanisha na ankara zote za malipo, Hakikisha unakuwa na nakala mbili ili moja wakugongee muhuri wa kupokea ili wasijekuruka kuwa hukupeleka malalamiko, kisha uwaulize barua yako itajibiwa baada ya muda/siku ngapi za kazi.Swali hili ni muhimu ili ujue utasubiri kwa muda gani ili uchukue hatua zaidi. Hili ni moja ya maelezo muhumu katika mkataba wa huduma kwa mteja.

    2. Ukipata majibu yasiyo ridhisha unatakiwa kukata rufaa EWURA hawa ni Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji, fika ofisi zao zilizoko mtaa wa Samora jengo la Jmall ghorofa ya sita watakupatia utaratibu mzuri na nakuhakikishia utapata haki yako. EWURA ni mamlaka iliyowekwa kisheria ya kusimamia na kudhibiti huduma za nishati na maji, na pia wanajukumu la kuhakikisha sisi wateja tunapata huduma bora, kulingana na pesa tunazolipia. Nilipata tatizo kama hilo na EWURA waliniwezesha kupata haki yangu na sikutoa chochote zaidi ya nauli yangu ya dala dala.Mama K.

    ReplyDelete
  5. Poleni sana. Kweli inaudhi sana.

    Diwani wa eneo hata Mbunge (sijui kama anasoma hizi comments) ebu fuatilia kero hii maana isiwe mna kazi za kusubiri kuomba kura tu kwa wananchi wakati mkiwa ofisini hamutaki kuwasaidia.

    Vinginevyo kama hakuna msaada tafuteni mwanasheria (nendeni pale mlimani au haki za binadamu muwaeleze) wako watu hata wa kujitolea kusaidia wanaoonewa bila malipo.

    ReplyDelete
  6. mlalamikaji tafadhali weka namba ya account na mita ikiwezekana na mbaya simu ili tukusaidie.

    ReplyDelete
  7. Mdau Zebedayo. Walipokuja kung'oa mita mara ya kwanza kwanini hukuwauliza sababu? Kma una stakabadhi na namba ya mita si uende DAWASCO makao makuu au kituo cha polisi ukafungue kesi? maana kama ni kweli ulichokiandika huo ni wizi na ni kosa kisheria. Ukienda huko ndipo tutakusaidia mawazo. fanya jitihada haki yako ipatikane. Siku nyingine wakija watu wa jinsi hiyo ulizia vitambulisho vyao vya kazi pengine ni matapeli tu, labda kama umewazoea. na kama umewazoea wasingeweza kukufanyia mambo hayo. WAKE UP BRO. Mjini Shule, oohooo!!!

    ReplyDelete
  8. hao mafundi koko sana walishakula mlungula sasa wakaona waje wawabambikieni nyinyi poleni sana ebu jaribuni kwenda huko ewura kama wadau waliotangulia wanavyoshauri na hakika mtafanikiwa kwani mita si huwa zina namba? bili zenu zitakuwa na namba pia hivyo mita yenu mtaipata kwa mpuuzi mmoja nyie fatilielini kwa makini tu msichoke wala kukata tamaa kweli wamewaaribia biashara yenu makusudi kukaa bila maji ni kero ya ajabu nyinyi mafundi mungu awapige radi. na msichoke kusoma blogu ya jamii hizi ndo faida zake kuu kusikiliza kilio cha wanyonge na ishu mbalimbali globu ya jamii idumu

    ReplyDelete
  9. Bwana Zebedayo mbona hao mafisadi wazoefu dawa yao ni ndogo tu!

    1. Nenda kamuone bosi wao tena sio meneja wa branch, ninamaanisha bosi wao mkubwa, itakuwa ngumu lakini wewe ukifika pale sema nina shida ya binafsi, ukisema ya kikazi watajua soo tayari hivyo sekretari atakuzuilia mlangoni, lakini ukisema ya binafsi, watajua ni mjombako umeenda kupiga soga watakuruhusu uingie.

    2. Wakati unaenda kumuona bwanamkubwa hakikisha unayo barua yako ya malalamiko mkononi, ukiambatanisha na vielelezo vyote, namaanisha copy ya bili zako, na hiyo barua yako uitoe copy kadhaa, nakala na viambatanishi mpelekee Katibu Mkuu wizara ya Maji. Mkabidhi barua yako, lau ukishindwa kumuona kabidhi barua yako uliyomwandikia huyo bwana mkubwa (Director General; Managing Director, whatever!!) Masjala lakini waombe wagonge muhuri wa kupokelewa hiyo barua kwenye copy/nakala yako ambayo utabaki nayo kama ushahidi iwapo hiyo barua yako itatupwa kapuni.

    3. Subiri matokeo ya barua yako kutoka huko Dawasco, huku ukienda kufuatilia, (maana wanataka kufuatiliwa kila siku kama vile unakwenda kumeza vidonge vya TB) ili ujue kama umeshughulikiwa au la.

    4. Wape siku 2 au 3 tu, ukiona kimya nenda kamuone katibu mkuu wa wizara inayohusika na maji na umshtakie shida yako wakati huo copy yako uliishaipeleka wizarani siku ilipoipeleka huko Dawasco. Kama hutapata jibu kote huko basi

    5. Ita waandishi wa habari wa TV na radio, wapeleke hapo kulikotokea hilo suala, ukiwa na barua, copy na uwaeleze kila kitu kuhusu hatua ulizochukua na walivyokunyali badala ya kukuhudumia. Kama kesho yake timu nzima haikuhamia kwako sijui, utatupa matokeo humu humu. Na hakikisha unapoongea na watu wa TV mbali mbali waambie wazi kuwa sasa hatua inayofuata ni kwenda mahakamani kufungua mashtaka yafuatayo
    a. Kudhalilishwa kuwa ni mwizi wa huduma ya maji wakati wewe umelipa bili zote
    b. Kuvunjiwa heshima mbele ya jamii
    c. kuharibikiwa kwa biashara yako kutokana na ukosefu wa maji.
    d. Kuvunjwa kwa mkataba bila kupewa taarifa au haki ya kujitetea kati yako na dawasco abruptly, bila warning ambayo ingekuwezesha wewe kutopata hasara na kutafuta njia nyingine ya kupata maji.

    Na ukishawaona wataalamu wa sheria walio makini na wasioweza kununuliwa, wanaweza kukuelekeza ni namna gani unafungua hayo mashtaka.

    NB: Siku nyingine unatakiwa ujue mita yako ni namba ngapi, mita huwa zina identification, lau kama unaweza kupata document walizotumia kufungia mita hapo kwako unaweza kuwapata vizuri maana namba za mita zinatofautiana, mita hiyo unayosema wamebadilisha itakuwa tofauti na mita yako uliyofungiwa zamani.

    Pole sana, mchezo wa kubambikiziana bili uko kila mahali sio Dawasco tu, hata kwenye makampuni ya simu, mtu anakaa zake huko mtaani anaunganishiwa international call bill inakwenda kwa mwingine. Na hata kama ni prepaid wanajua jinsi ya kula pesa yako pia. Halafu ndio wako kimbelembele kupiga kelele za ufisadi wakati watanzania wengi sana wana tutabia twa kifisadi.

    Mswahili!!

    ReplyDelete
  10. Pole sana mdau. Hayo yanaitwa ni "machejo". Kuna mjasiliamali hakulipa maji muda mrefu kawakatia kitu kidogo hao wakora wa DAWASCO wakaona njia rahisi ni kubadili mita yake kwa muda na kuileta kwako ili uilipie then wakae kipindi warudi kuja kuifungua na kumnrudishia mwenyewe, Why kwa kuwa wewe unabiashara so ni logic kukubambikia bili ya laki saba. Kwa kuwa umewabaini wameona waondoke nayo halafu ukipeleka malalamiko yako watajifanya walikosea na kukurudishia mita yako ili so liishe. Sasa kama unataka kuwapa discipline fanya yafuatayo

    1. Kwa kuwa una records zote halali na wewe huwa hufanyi mchezo mchefu kwenye bili yako na namba ya mita yako ipo kwenye records zako na zao, basi funga shughuli mpaka wakurudidhie maji

    2. Siku wakirudisha mita wewe unakuwa tayari umeshamtafuta mwanasheria kufile law suit kwa kutaka wakulipe damages za zifuatazo
    (a) kukosa mapato yako ya kila siku kutokana na kufungwa kwa Hotel, kwani sheria za afya haziruhusu wewe kuendesha biashara bila kuwa na maji
    (b) Kukulipa gharama zote za kesi
    (c) Kukulipa damage itakayo sababishwa na wateja wako kuhama kwani kwa kufunga hotel tayari umeisha wafanya watafute sehemu mbadala ambapo kuwarudisha itachukua muda wa matangazo redioni na nguvu kazi
    (d) wakulipe gharama za kutrain upya wafanyakazi kwani wale waliokuwepo wametafuta sehemu nyingine kwa kuwa hawakufahamu hatima ya maisha yao ambayo hutegemea biashara ya kila siku hotelini kwako
    (e) Kwa kulipe gharama za usumbufu binafsi ulioupata baada ya wao kukata maji, uliacha kufikiria kuendesha shughuli zako na kupoteza muda wa kufuatilia kitu ambacho hukupaswa.

    Kwa ujumla ukiwadai kama Milioni 200 hivi itatosha kuwafanya wajue kuwa, upuuzi kidogo wa mpumbavu mmoka unaweza leta hasara kwa shirika na hivyo management kuwa wakati kwa wafanyakazi wasio waaminifu.

    ReplyDelete
  11. Poleni sana.kujua na kufahamu sheria na stadi za maisha ni muhimu sana kwa sisi sote.
    Wachukulie sheria....mimi niko huku mpaka Wakimbizi wananifundisha mengi sana.
    Vita ilianza kwa kudhulumiwa haki ya mmoja mmoja.

    ReplyDelete
  12. KAKA POLE SANA!

    NAONA UMETUMIA PIA NAFASI HII KUJIPIGIA DEBE JUU YA MGAHAWA WAKO.
    LAKINI SWALA LA MSINGI KWAKO, JE UNAWEZAJE KUENDESHA MGAHAWA WAKATI HAUNA MAJI?
    KWA MSINGI HUU, UNAFIKIAJE VIWANGO VYA UBORA? NA HAYO MAJI UNAYONUNUA UNA UHAKIKA GANI NI SAFI NA SALAMA? USIJE UKAUWA WATU KAKA.

    back to the principle question: HUKU KWA MICHUZI HUTO WEZA PATA UFUMBUZI WA SUALA LAKO. NAJUA KUNA MTANDAO MPYA WA SERIKALI UITWAO MWANANCHI AMBAKO RAIA WANAWEZA WASILISHA MATATIZO YAO NA KUFUATILIA MAJIBU.

    VINGINEVYO WAFUNGIE JAMAA SAFARI NA IKIWEZEKANA HATA WAKUBWA WAO SEMA NAO TU.

    LAKINI PIA UNAYE DIWANI NA MBUNGE WAKO, KWA NINI USIWASHIRIKISHE? THIS SEEMS TO BE A VERY GENUINE CASE, WHY DON'T YOU WANT TO GO THERE?

    mwisho ndugu zangu watanzania tusiwe watu wa kulalama sana. mnapochagua viongozi wabovu mnafikiria nini? sasa imekula kwako unapiga mayowe, subiri wakati wa uchaguzi SASA UFANYE MAAMUZI YA BUSARA.

    Baba Mithambwa
    pemba - MSUMBIJI

    ReplyDelete
  13. HEALTH AND SAFETY FUNGA RESTAURANT YAKO HARAKA SANA KABLA SISI WATU WA AFYA ATUJAKUZUKIA,NI KOSA LAJINAI KUENDESHA RESTAURANT KWA MAJI YA KUBEBA KWENYE NDOO NA HASA UKIWA KATIKATI YA JIJI,USHAURI USIENDE HAO WANATAKA RUSHWA USIWAFUATE FUNGUA KESI YA MADAI NA TAFUTA MWANASHERIA ATAKAE KUSIMAMIA UDAI HASARA ZOTE NA USBUFU SIO CHINI YA MILIONI 100,000.OO0.00 UTAKUWA UMEUWA NDEGE 2 KWA JIWE MOJA AU FIKA OFISI ZETU TAKUKURU KWA MSAADA ZAIDI.

    ReplyDelete
  14. usithubutu kuweka namba yako ya account wala mita.

    ReplyDelete
  15. Nimemwandikia sms mtu ambaye atafikisha ujumbe kwa Raymond Mndolwa kama halijatatuliwa kwa muda wa siku tatu nijulishe kupitia taza_tz@yahoo.com ili tuchukue hatua zingine zinazostahili. Pole sana ndugu yangu

    Taza

    ReplyDelete
  16. Pole sana mdau,mimi nitoa pongezi kwa WAUNGWANA WOOTE WALIOTOA USHAURI, USHAURI WANGU MIMI NINACHOSEMA NAOMBA UJITAHIDI KUWASILIANA NA WATANGAZAJI WA CLOUDS FM WA POWERBREAKFAST ILI WALIRUSHE HILI TATIZO HEWANI MIMI NINAAMINI DAWASCO WATAWAJIBIKA KUKUTAFUTA NA KUWASAKA HAO MAFUNDI WAO NJAA WAMESHAKULA HELA YA FISADI MMOJA HAPO MTAANI ILI WAMPUNGUZIE DENI KWA KUBAMBIKA MITA.

    ReplyDelete
  17. pole sana ndungu yangu kwa mkasa kama huo uliokutokea hasa kwa wakati kama huu wa mwaka mpya.tumempoteze mzee wa vita sasa ukifilia siku za nyuma wa huhai wake, mambo kama haya hakuwepo kama sasa. cha kufanya ndugu yangu, nenda kwa wakili anayejulikana umwelezehe mkasa wako; na pia toa report kwa serikali ya mtaa, polisi, ofisi ya maji taka makao makuu. Pia itakuwa bora zaidi uende court of alpeal iliyopo jirani na kilimanjaro hotel. Kama destuli ya mtu yoyote mwenye kuomba msahada na kutaka kusaidiwa, nenda hapo mahakamani, elezea shida yako na kuomba uwezekano wa msaahada.ukihulizwa kwanini umekuja hapo, sabau uwambie kwamba "unaomba kutumia nafasi hii kuonesha kwamba umeonewa na shirika la maji taka na kwamba wewe ni mteja wao kama wateja wengi hapa TZ. Pia kuonyesha kwamba mteja yeyote aliyefanyiwa kitu kama hiki ajuwe kwamba sheria hipo yakumlinda asife moyo. mimi naona unaweza kushinda vizuri sana kwa maelezo uliyoandika. bill ya laki saba ni sawa na lita ngapi za maji uliyotumia hapo kwenye reustaurant yako.piga mahesabu hayo kwanza utaona ushindi unavyokuja. nakutakia mema kwenye ufuatiliji wako.

    ReplyDelete
  18. Anon wa Mon Jan 04, 03:32:00 PM

    Nakubaliana na wewe kuwa awachukulie sheria lakini njia uliyompatia siyo. Kumwambie aende polisi ni sawa na kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi. Hili ni tatizo kubwa tulilo nalo sisi watanzania, nalo ni kujua haki zetu na mahala pa kuzipata. Hili suala si criminal(jinai) ambayo inahitaji uanzie polisi, hili suala ni Civil (madai) linahitaji mwanasheria (advocate) atakaye file case ya madai moja kwa moja mahakamani bila hata kuwapitia polisi.
    Hebu tujifunze kitu hapa.

    1. Si kila kitu lazima uanzie polisi, haya ni matokeo ambayo watanzania wengi wanakosa haki zao za msingi. Polisi nenda kama una kesi ya jinai (Criminal) ambayo mshitaki ni Jamhuri wewe unakuwa shahidi tu. Hata siku moja mtu akikudhulumu usitumie polisi, kama una ushahidi tumia mwanasheria tu.

    2. Kama case ni Civil (Madai) Polisi watakachofanya ni kukupotezea muda kwa kuchukua rushwa kwako na mdaiwa na kujifanya kusuluhisha, kazi ambayo si yao ni ya mahakama.

    ReplyDelete
  19. Sasa na wew unakuwa kama ndio umeshuka bongo. Hii ni bongo haindi kwa nguvu unaweza umia buree. Hata mawaziri wenyewe unafikiri wanaishije? Lazima ujue kuwatuliza watu kama hao tena unaweza kufanya bili yako iende chini. Wewe ungewapatia msosi wa nguvu na kuwaambia mkiwa na njaa njooni hapa. Basi hapo ndio ulikuwa mwisho. Sasa wewe unataka kuleta ubishi, ona sasa Restaurant siku ya 3 sasa hakuna maji. Hao jamaa njaa tu hakuna lolote

    ReplyDelete
  20. Labda sijui hesabu lakini mbona naona mmepata nafuu kulipa laki 7 kuliko laki 180.

    ReplyDelete
  21. A. MutallabJanuary 04, 2010

    PLEASE PAY, hii nchi itajengwa na wenye moyo pekee.

    Yawezekana mmedhulumiana.

    Inaonekana kulikuwa na kaujanja ka kutemper na mita halafu mmeshindwa kulipana vizuri, sasa ukizingatia tunatokea kwenye sikukuu mfululizo matokeo yake ndiyo hayo.

    Ni mtazamo tu.

    ReplyDelete
  22. Hivi wajameni naomba kuuliza hiyo bili ya maji laki 7 au laki na 80 ni ya muda gani?Au hiyo bili ni ya msikitini?Maana ndio maji kila wakati yanatumika,Uk maji mwaka mzima ni 160-180,ulaya nyengine kama vile Greece 80 euros au less kwa mwaka na nusu tena vipi TZ maji yafikie kiasi hicho?na sasatna kila kitu unalipa online au unasema uwezo wako wa kulipa maji kiasi gani sio

    ReplyDelete
  23. Dole gumba juu kwako TAZA

    ReplyDelete
  24. jamani tanzania tunaenda wapi mbona na nani wakumuamini hapa nyumbani nani wakumlilia kilio chetu sisi maskini inasikitisha sana na aibu watu wa serikalini inamaana hao wakubwa hawajui yote haya au hawasomi haya ya humu ndani hey wanayajua sana na wao ndio wameyaleta yote haya lakini jamani ni time sasa kutoa hadharani watu wayaone haya na pia msisahau hata umeme mambo ni hayo hayoooooo na wanaiba na watazidi kuiba na hata humu ndani wapo wakituchunguza tunavyo lalamika na kutuona wajinga jamani mbona nchini kwetu tunazidi kuumizana jamani lini haki na usawa utakuwapo tanzania way ni nani wakumuamini ni nani wakumlilia jamani hata akienda wapi watamzungusha na kumla zaidi mungu wangu ndio nazidi kuvunchika moyo wa kurudi nyumbani nitaishia huku ulaya do lazima tuwatafute watu wa bbc waone jinsi tunavyotesana jamani namalizia na kusema chagueni marahisi waliosoma nje na mawaziri waliosoma na hawana uroho wa pesa vijana na wanauchungu na mateso tunayo yapata.do amakweli bongo umaskini hautaisha ni mimi mdao mpenda haki na jasho la mtu haliliwi ni mimi mdau wa KUPIGANI HATA YA BINADAMU NA RUSWA STOP.

    ReplyDelete
  25. Pole sana kwa maudhi hayo kaka. Mimi binafsi leo sina mengi ya kuchangia kuhusu hii hoja maana kama ni maudhi siyo idara ya maji tu,bali katika vitengo mbali mbali kama Bandari,Tanesco,wizara ya ardhi,nk.Tunacho hitaji ni sisi wote Watanzania kukemea ufedhuri wa aina yoyote ile pale unapotokea na hasa kwa watanzania wasiyo na uwezo.Ningependa Tanzania isiyo na rushwa,yenye kujali watu wake,yenye kuangalia haki inatendeka ngazi zote.Hii yote kwasababu tanzania baadhi ya sheria hazifatwi na zisipofatwa wenye kulaumiwa wawe wote raia pamoja na viongozi.
    RAIA:
    Tuna haki ya kutokubali kutawaliwa na walafi,wahuni na walarushwa.
    VIONGOZI:
    Tuna haki ya kupewa heshima tunayostahili kulipwa mishahala tuliyokubaliana,
    Wajibu wa kila mtu ni kufuata sheria pamoja na kutoa taarifa pale mambo yasipoenda ipasavyo.

    ReplyDelete
  26. Kaka hiyo ndio fitina bongo!
    mshindani wako wa biashara anahusika hapo!

    ReplyDelete
  27. anon 09.34 sijui mita za wengine lakini kuna mita mpya hapa Dar ukisoma mpaka unashangaa zimeundwaje maana bill utakayo iona hapo ni ya ajabu wakati ni matumizi ya kawaida tu ya nyumbani na maji yanatoka kwa mgawo.

    ReplyDelete
  28. Wadau,

    Hao mafundi wa Magomeni ni MIJIZI. Wamenifungia mita inakwenda mbio kama mohammed transport, yaani kwa siku kama natumia mitakyubu 10 au zaidi kwa nyumbani tu. wala sina biashara ya maji wala nini.

    Baada ya kulalamika kwa fundi, ameniita pembeni na kuniambia tongee kama vipi abane mita yangu. kwa maneno yake mwenyewe eti hapa magomeni "wachamungu" ni wachache, wengi wamebana mita zao.

    ReplyDelete
  29. wewe unayejidai mwanasheria sijui ulisoma wapi. Kesi yeyote lazima ufile report...iwe criminal au civil. Kupata lawyer hayo yote ni baada ya wewe kuwa na case. Lawyer atakuwakilisha wapi wakati huna case? Na pia hapa hawa watu waliobadilisha hiyo mita wamecommite the crime....wamevunja seria...kama huyu mtu anasema ni kweli...

    ReplyDelete
  30. wadau msilalamike sana ukweli utajulikana pengine ametemper namita akashtukiwa kama ana risiti ajitokeze msije mkatetea wakati ukweli kamili haujulikani. dawasco na yenyewe inafanya kazi kwa umakini itakuwaje kama haudaiwi udaiwe laki 7 kwa siku hiyo inawezekana ni illegal connection wakampiga penalty na ofisi ya dawasco si iko hapo nyuma yao kwa nini asiende apate majibu kutoka kwa branch manager. tuache ujanja2 shida ni kwamba hatuna desturi ya kulipia huduma sanasana umeme na maji mdau dawasco

    ReplyDelete
  31. SAFI SANA MSWAHILI ...wengine wamekunya...ila wewe umeharisha kabisa...!!!!! Hii nchi imekuwa na dhulma nyingi dhidi ya watu wa kipato cha chini na cha kati...Fukuza wote hapo dawasco weka watumishi wazalendo wapya!!!

    ReplyDelete
  32. TUJIFUNZE KUPENDA SHERIA, HAPO BWANA NENDA KAMUONE LAMWAI NA MARANDO MVUNGUWE KESI WASHITAKIWA WATUKWA WAWILI NA MAFUNDI NA DAWASCO, DAWASCO AKIWA TAPELI NA HAO MAFUNDI WAKIWA WANASAIDIA SHIRIKA KUIBIA WATU. KWANZA WAANDIKIE BARUA KUWA UNAKUSUDIA KUFUNGUWA KESI JUU YA KITENDO CHAO, USIFANYE MZAA HAWA WATU WANARAKIWA KUKOMESHWA, KAMA UNARISITI ZOTE HIYO SAFI KABISA HUNA TATIZI USIOGOPE MTU NA WALA USITOWE HATA SENTI TANO YA RUSHWA, KWANZA WALIENDA KUSAFISHA KWANI ILIKUWA MBOVU. GANGAMALA NA UFUATE SHERIA.

    ReplyDelete
  33. Hili jambo limeniudhi mpaka nimekaa kazini ninaliwaza. Hivi hii Bongo yetu itaendelea kweli kama mambo yenyewe ni hivi? Halafu watu wanatoa comments za kipumbavu "aah Mjini shule!!" what? Mshikaji hapo gangamaa kabisaa na usitoe hata senti tano. Jamani ndugu zangu, kama tunataka nchi iendelee, inabidi kuwaencourage na kuwaondolea vikwazo wajasiriamali. Yaani nimeboreka ningekuwa hapo Bongo ningekutafuta mshikaji nikakuambia haya twande tukawafuate hao vigogo hata ikulu tungekwenda. This kind of thing is an embarrassment to our nation. Inasikitisha sana kila mtuanaishi kiujanjaujanja tu mtu akifanya biashara halali hatupendi..itikadi ya kijamaa hiyo kikorosho!!
    Hebu Dawasco or whoever the hell you are mfungulieni maji mjasiriamali aendelee kuchacharika. Ndio maana sina haraka ya kurudi nitapigana na mtu ushenzi kama huu. Pole sana Mdau lakini haki utapata tu. Chukua siku moja, nenda kwa mkubwa kabisa Dawasco na pia kamuone waziri.
    Again, hii kitu imenboa sana!!
    Mdau, Boston, US.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...