MUTARAGARA CHIRANGI – ‘RUBHOJA BHANU’
Tarehe 03, Januari, 2010 inakamilisha takribani miaka mitatu tangu ututoke ghafla. Familia yako na Wanahistoria tunaendelea kukukumbuka kwa mengi uliyotufundisha kwenye njanja mbalimbali katika Uongozi, Uadilifu na Wema wako.
Katika kumbukumbu hii, dhamira zetu leo zinaguswa zaidi na tabia yako isiyokifani ya
UKARIMU ULIOKUWA NAO KWA WATU WOTE PASI KUJALI MAKABILA, ITIKADI ZA KISIASA, IMANI, JINSI, UMRI WALA HALI ZAO ZA KIUCHUMI.
Aidha haikuwa ajali Wanadamu wakati wa ujana wako wakakupa majina ya utani kama vile Rubhoja Bhanu na pia Nyamulila Mwirango utambulisho ulioashiria tabia hii ya kukarimu watu uliyoionyesha kwa vitendo pasipo uzandiki wala masharti kwa manufaa binafsi.
Tunamuomba Mola azidi kutukumbusha nasi leo kuwakarimu wageni na wahitaji kwa jinsi tunavyoweza kuwasaidia maana kwa kufanya hivyo si tu kuwa tutakuwa tunaenzi kauli mbiu
uliyoipenda ya Haki Huinua Taifa bali pia tutakuwa tunawajibika kuwasaidia wenzetu wenye mahitaji mbalimbali kama tunavyotakiwa katika kujali utu na haki za kila Binadamu.
KWA HESHIMA NA SHUKRANI,

KWELI TUTAMKUMBUKA HUYU MZEE KWA MISIMAMO YAKE THABITI.
ReplyDeleteShukrani kwa kutukumbusha maisha ya huyu baba mwanasiasa mwaminifu, mwanamichezo hodari na mwalimu aliyejituma kufundisha na kusimamia maadili ya taaluma kwa nguvu zote.
ReplyDeletemzee mtaragara chilangi huyu mzee ni jirani yangu yaan alikuwa na mtindo wa kuandika vibao mlangoni kwake,kama amelala wanaweka amelala,kama anakula wanaweka kibao anakula kama yuko chooni wanaweka kibao chooni kama yuko free wanaweka free,hahahahah mwalimu chilangi mzee wa msimamo hapo kamunyoge hahaha kijana sema umechelewe bonge la bite
ReplyDeleteA true man of the people - well known for his social work, charity and charisma. His name (correct me if I am wrong) derives from a local dialect verb implying utmost care - one who never drops - and care he offered. To Musomaians he is a legend in many ways - a living landmark that will, almost forever, be associated with the lakeside town.
ReplyDeleteMwaka 1985 nilimpa kura yangu ya ubunge wa Musoma mjini ambayo ilisaidia kumshinda Abel Kiagyunya Mwanga.
ReplyDeleteRIP Mkaruka Chirangi Mtalagala
He was Once the then FAT (TFF) National vice Chairperson & probably also long serving Trustee. An Exemplary Educational Secretary of his time in Mara region.
ReplyDeleteKweli ungetaka kujua mpiganaji wa kweli wa rushwa uliza juu ya huyu Mzee who was also the Musoma CCM Chairpeson. Rest in Peace
Jamani bado iko kwenye rekodi kwamba huyu mzee ni wa kwanza Tanzania kwa jinsi alivyokuwa mjasiri na wa mipango aliwahi kujichimbia kabuli lake mwenyewe mapema sana sijui miaka mingapi wakati haumwi kwa ajili ya kujiandaa.
ReplyDeleteButiama tulijua kuwa Mwalimu Nyerere alimpenda sana kwa kuwa mkweli na simple.
Endelea kupumzika kwa Amani. Kweli alikuwa na vibao nyumbani kwake very well organised huyu baba. Taifa linapaswa kuenzi maisha ya viongozi down to earth kama hawa.
ReplyDeleteMh. RAIS na Mwenyekiti wa CCM-T familia za akina Kawawa, Opiyo, Selemani Kitwara,Mirumbe na ya huyu mzee Mtalagala na wana namna hii usizisahau.
ReplyDeleteHuyu mzee ndiye alikuwa akisimama jukwaani CCM inaunguruma huko Musoma. Muulize mbuge wa sasa Mathayo anajua vinginevyo angekuwa amekula patupu siku nyingi. Hata wa vyama vya upinzani wa awali akina mzee Wandwi, Ukwaju,Kembo Migire walimuheshimu sana huyu mutu.
Zaidi ya yote aliwaunganisha sana wana Mara kimakabila na pia kidini. Binafsi nilimwona mara nyingi akihudhuria kisomo na kusaidia Waislamu, Wahindu sawia na wakristo wenzake ingawa kuna wengine wanasema eti kwa kuwa asili yake alikuwa mwislamu. Ni mfano wa kuigwa maana hatutaki udini wala ukabila Tz.
Al Musoma you said it all the old chap was a living landmark!
ReplyDeleteNamkumbuka huyu mzee, mchapa kazi sana. Kuna wakati alitoa speech pale musoma sec. school miaka kama 1990 hivi wakati sauti imemkauka ikabidi mwenyekiti wa CCM Tawi, Mwl. Mathias akawa kama kipaza sauti. Alikuwa kama Nyerere vile. Viongozi wazuri wote wanaisha wamebaki madungayembe......
ReplyDeletepoleni sana wanandugu!!
Wa Chirangi:
ReplyDeletePumzika kwa yote uliyoyafanya; yatabakia siku zote!
Mara yangu ya kwanza kumuona au kukutana na Mutaragara Chirangi, ilikuwa wakati wa sherehe (hapo mjini Musoma)za kumtawaza Elizabeth Alexandra Mary kuwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza, June, 1953.
Wanafunzi wote wa wilaya ya Musoma (South Mara District Council), toka darasa la pili hadi la nane, tulikusanywa kila darasa watoto watatu kwenda mjini Musoma kwa sherehe hizo.
Nilitokea Bwasi Primary School, Majita.
Tulipiga kambi hapo Musoma Middle School (Mwisenge)kwa malazi na matayarisho ya gwaride.
Head Prefect wa Musoma Middle School alikuwa ni kijana machachari, Mutaragara Chirangi (na Headmaster alikuwa ni Emmanuel Kibila).
Omumura wa Chirangi, isy’omwoyo ku bhyone bhinhu waikoreye Tanzania!
Ni mimi Born Again Pagan
RIP mzee Mutaragara Chirangi. Kweli naungana na anony moja aliyesema mzee huyu alikuwa "well organised". nakumbuka miaka ya 70 nilikuwa naishi BIAFRA- KAMUNYONGE Musoma, nilisoma KAMUNYONGE na tulikuwa tukipita nyumbani kwa Marehemu mzee Mutaragara, mpangilio wa vibao vyake hasa kile cha mlangoni kilichokuwa na maneno"mzee amelala, mzee ametoka, mzee ana mapumziko mafupi" kwetu ilikuwa burudani tosha. Dah, sikuwa na habari za kifo cha mzee wetu Mutaragara. MUNGU AKUPUMZISHE MAHALA PEMA PEPONI-AMEIN
ReplyDeleteMdau Dublin