Naomba michuuu unipeperushie hii kwa wanajamii muone kama kuna uhalali wa hii kero ya A-town.Nafikiri ni hapa tunaweza kujadili na kupata walau msaada au ushauri nini kifanyike.
Kuna hili swala la mtu unataka kupangisha duka au fremu ya biashara kama wanavyoita huku A-town. Kuna hawa madalali ukikutana nae anakwambia kuna fremu mahali ila kama unaitaka ni 300,000/- kwa mwezi na unatakiwa kodi ya mwaka kwa mwenye nyumba.
Halafu utatakiwa utoe kiasi cha kodi ya mwezi mmoja yaani 300,000/- kwa dalali aliyekutafutia chumba hiyo haina shida.
KUNA KITU WANAITA KILEMBA HIYO UNAWEZA AAMBIWA UTOE MILIONI 5 MPAKA 10 MBALI NA YA DALALI KUNA WATU WANASHIKA VYUMBA ILE MARA TU WANAONA NYUMBA INAJENGWA NA WAO SI WAFANYABIASHARA ILA WANASHIKA HIZO NA UNAKUTA NI WENYE UWEZO LABDA ANASHIKA KWA LAKI MBILI NA ANAANZA KUPANGISHA LAKI TATU MPAKA SITA. NDO UNAANZA KUAMBIA KILEMBA MILIONI 10.
JAMANI WAJASIRIAMALI TUTAWEZA NA UKIZINGATIA MTAJI WENYEWE TUMEKOPA PRIDE AU NI MKOPO WA KIKWETE. MTU ANAFUNGUA DUKA BAADA YA SIKU MBILI ANAFUNGA. UNAKUTA MTU AMETUMIA ELA NYINGI NA HAUZI KURUDISHA ELA ALIYOTUMIA, MATOKEO YAKE ANARUDI NYUMBANI. WAHUSIKA TUSAIDIANE JAMANI.
MDAU MJASIRIAMALI A-Taun


MDau unakutana na wrong people na lazima wakuingize mjini inatakiwa kukutana na watu wazoefu wa shughuli za nyumba hapo A-Taun nimekulia A-Taun na ninaijua fika hiyo hela ya dalali ni kawaida ila kilemba ni wanakufanya deal. Kama unahitaji msaada zaidi kuhusiana na maswala ya upangaji nenda Robots Secretarial Services utapata contacts zangu kisha nitakusaidia kupata sehemu za kufanyia biashara. Robot Secretariat ipo kwenye jengo la New Safari Hotel. Kisha jieleze utasaidiwa kuanzia hapo.
ReplyDeleteMdau wa Damu USA
Ubepari ni unyama, ndo soko huria hilo,mtu hujikuna pale anapoweza, kama huwezi achia ngazi.
ReplyDeleteNasikitika huo ndio ukweli wa dunia.
Huo ndio mwanzo ndugu yangu, wewe subiri jumiya ya Africa Masahriki na kati ichanganye. Ningekushauri ukafungue biashara yako Moshi, A- TOWN hapakufai kabisa kama mtaji wako ni mdogo.
ReplyDeleteHUo ni mji wa wala rushwa, wenye migodi, na wafanyakazi wa Mashirika ya KImataifa.
Sululu.
HUO NDIO UJINGA WA TANZANIA NDIO MAANA HAMNA MAENDELEO KWA WOTE NA YA WOTE KWA USAWA, HAYO MAMBO YANAFANYIKA HATA SERIKALINI HUWEZI KUPATA HUDUMA HADI UTOWE RUSHWA, KWA MFANO UNAWEZA KUWA NYUMBANI KWAKO UMEIBIWA UKIENDA POLISI WATAKUAMBIA HAWANA GARI YA KUJA KWAKO PENGINE UKODI GARI NDO WAJE, UKIKUBALI WATAKUAMBIA UWAPE PESA WAKACHUKUWE GARI UKIWAPA, WATAZUNGUKA NA KURUDI NA GARI YA SERIKALI WATAKUAMBIA IMERUDI SASA HIVI NA ILE PESA HAWAKURUDISHII, NA MUKIWA NJIANI WATAKUOMBA PESA ILI WASHUGULIKIA JAMBO LAKO KWA HARAKA, WAKATI NI KAZI YAO NA WANALIPWA MISHAHARA, PIA ARDHI THE SAME STUFF, UNAENDA KUTAKA KUPIMIWA ARDHI YAKO WATAKUAMBIA WAKO BUSY NA KAZI ZA MWAKA 47 UKITAKA YAKO IFANYIKE KIOFISI BASI NGOJA HADI MWAKA 2020 LAKINI WATAKUAMBIA WANAWEZA KUKUSAIDIA WAKATI WAO WA FREE TIME JIONI AU JUMAPILI LAKINI UNATAKIWA UWAPE KIFUTIA JASHO WANAVYOITA WENYEWE, NA NI PESA NYINGI HADI MILIONI WANAWEZA KUKUOMBA, KAMA UNAKUBALI NA KUWAPATIA HAPO HAPO WATANYANYUKA NA KUACHA KILA KITU WALIKUWA WANAFANYA NA KUCHUKUWA GARI YA SERIKALI NA VIFAA VYA SERIKALI NA KUKUFANYIA KAZI YAKO NA KUMALIZA SIKU HIYO HIYO, WAKATI WALISEMA HAWANA MUDA, HII HALI HAITAKWISHA NA MAENDELEO YATAKUWA KWA WACHACHE TU. NI UJINGA NA UPUUZI MKUBWA SANA KIASI KWAMBA NACHUKIA NCHI YANGU MWENYEWE, SIJUWI KWA NINI SIKUZALIWA RWANDA KWA MZEE KAGAME MPENDA WATU KAMA NYERERE
ReplyDeleteHayo mambo hayakuanzia hapo vijana wamesomea biashara na ni kimataifa kila mtu lazima apate chake.
ReplyDeleteJamani Elimu ya biashara imefika mbali sana , Sio wafanya biashara tu .Hata huduma za serikali wanatafuta jinsi ya kuongeza kipato .ndio kila aina ya jina unaisikia . mpaka hotelini ukimwambia ongeza pilipili anakuambia ongeza pesa.
ReplyDelete