TAARIFA YA KIKAO CHA DHARURA CHA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA KITANZANIA HYDERABAD INDIA (TSAH)

Ndugu Watanzania na Wanajumuiya ya Watanzania wanafunzi Hyderabad nchini India.

Kama mnavyojua, hali ya kisiasa katika Jimbo la Andhra Pradesh si shwari kutokana na vurugu za kisiasa za kuishinikiza Serikali ya India itenge Jimbo huru la Telangana. Vurugu hizi zimetawala zaidi katika vyuo Vikuu hususan Osmania (Osmania University) ambacho watanzania walio wengi wanasoma katika Chuo hiki.

Kufuatia hali hiyo, Mitihani ya Semister imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara tangu Mwezi November, 2009. Takribani miezi miwili na nusu sasa. Aidha kumekuwa na migomo ya wanafunzi (wahindi) kuingia madarasani hadi hapo Jimbo hilo litakapotengwa. Hali hii imetuathiri kwa kiasi kikubwa kisaikolojia ambapo hadi sasa haijulikani mitihani hiyo itafanyika lini na lini hasa wanafunzi (wahindi) watakapokubali kuingia madarasani na kukubali kufanya mitihani. Kutokana na hali hii upo wasi wasi mkubwa wa kufutwa kwa Mwaka wa masomo kama inavyoelezwa na uongozi wa Chuo.

Ni wazi ifahamike kuwa vurugu hizi ni za kisiasa na hazihusishi mwanafunzi yeyote wa kigeni (Foreign students) isipokuwa wanafundi wakihindi wanaoshabikia siasa. Hata hivyo athari za kutofanyika mitihani kwa wakati napengine kufutwa kwa mwaka wa masomo zinatuathiri wote kwa pamoja kama vile kupoteza muda mwingi bila kuingia madarasani, kusoma na kufanya mitihani. Mbaya zaidi tunaweza kupoteza mwaka wa masomo kama dalili zinavyojionyesha.

Ndugu wanajumuiya, kuahirishwa kwa mitihani ni upotevu wa muda na ikitokea kufutwa kwa mwaka wa masomo ni usumbufu kwetu na upotevu wa gharama.

Kutokana na hali hiyo, leo tarehe 20.01.2010 Uongozi wa Jumuiya umefanya kikao cha dharura kujadili suala hili na kuamua kuchukua hatua zaidi ikiwemo kuandika barua maalum kwa Uongozi wa Chuo ili utoe msimamo wake juu ya hatima ya wanafunzi wakitanzania wanaokumbwa na athari za vurugu hizi. Pia kikao kimeazimia kulifikisha rasmi (kwa barua) suala hili katika Ubalozi wetu New Delhi.

Mwenyekiti wa Jumuiya anawaomba watanzania wote kuwa wavumilivu wakati huu ambao suala hili linafuatiliwa na kufanyiwa kazi. Waendelee kujisomea majumbani na kujianda na mitihani muda wowote itakapoamriwa. Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.


ABDILLAH DAUD NKYA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanafunzi wa kitanzania
Hyderabad - India

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. NYIE VIONGOZI WA JUMUIYA ACHE KU-PANIC NA KUANZA KUANDIKA BARUA OVYO NANI KASEMA MWAKA UTARUDIWA WAKATI TATIZO NIKUFANYA MITIHANI YA SEMISTA HII ILI KUINGIA SEMISTA NYINGINE SASA MWAKA UTARUDIAJE.FIKIRIE KABLA YA KUANDIKA HIZO BARUA KULIKO KUKURUPUKA.

    ReplyDelete
  2. THE KOOOOOOOOP a.k.a U'LL NEVER WALK ALONE,10 points behind MAN U an CHELSKI
    IN RAFA WE TRUST

    ReplyDelete
  3. Kweli Michuzi sikuwezi uko juu sana. Yani leo nimetafakari ulikanza Kuitwa ''Mkuwa wa Wilaya ya Nanihii'', akaitwa mkuu wa libeneke, ukaitwa uncle, na sasa unaitwa Ankal!!! mh kweli we kiboko. afu hili la ankal ndo linatambaa kwa kasi ya ajabu. anyway mi napenda sana lile la ''Mkuu wa Wilaya ya Nanihii''

    ReplyDelete
  4. HIKI KIINGEREZA CHA KIHINDI KINATAFUTA NINI KWENYE BLOG, HATA HIVYO KAMA HAPA NYUMBANI TUNAFANYA VIBAYA KWENYE MITIHANI KISHA HUKO INDIA TANZANIANS ARE READ IN ACADEMY! NINATEGEMEA TUTAVUNA EMBE KWENYE MINAZI.

    ReplyDelete
  5. kuhusu swala la hyderabad sasa ni gumu kisiasa hasa kwa wale wanaofuatilia siasa za india kwani wanajua ni jinsi gani wanasiasa wa huku walivyokuwa na nguvu ya umma na wale wanaleta plopadanga kuwa awawezi kurudi loky sabha yaani bungeni kwao ka mtu analeta ujanja ujanja km kwetu tanzania sasa kwa taarifa ambayo ni mpya mitihani yote imearishwa na badala yake tunaendelea na masomo na pia km masomo yatashindikana kwa muda muafaka kuanzia tarehe 22 january mwaka lazima turidie huyo ni vice chansela wa osmania pia tunaweza kufanya mitihani hiyo mwezi wa tano km hali itakuwa shwari na jana risasi za moto na mabomu ya machozi yametembea osmania universitykwa india ni khari mbaya sana na aijawai kutokea kwa zaidi ya miaka 20 sasa atulewi itakuwaje khs hilo km je tutakaa darasani na kufundishwa?
    pia naomba niseme ukweli juu ya wasomi waliopo hapa hasa kutoka tanzania ni kuwa wengi wao si wakweli na ni waoga sana awapendi habari za huku kujua wazazi wao sijajua ni kwanini? na km wasomi hawa ndio wanakwenda kujenga taifa la tanzania baada ya miaka kadhaa ijayo ni kwanini wawe waoga na kusema ukweli kwa wazazi wao kuwa atujaenda shule zaidi ya miezi 2 wazazi wao wakawa wanajua kama mzazi akaelewa suala zima
    pia suala la kumuogopa ubalozi na mpaka tupeleke barua ni kwanini asiende mwenyekiti kuonyesha ni suala zito?
    kwakweli hali ya osmania sio mzuri kimasomo mpaka sasa lkn khari ya kiusalama ni ya asilimia 100% kwa wanafunzi wa kigeni hila je tuendelee kukaa ndani kwa muda gani maana sikukuukwa india ni karibia kila wiki lazima itakuwepo
    tunakuomba mwenyekiti fanya kazi yako vizuri ha uwasiliane na mh.balozi ajue km kitaeleweka sio kukaa tu si tumekuja kusoma hapa

    ReplyDelete
  6. VIongozi ebu acheni mbwembwe basi!!!sisi Beef Biriani la hapa Tolichwoki bado tunalipenda,kule nyumbani Moshi-Rombo hakuna bryani!!!

    ReplyDelete
  7. Nachukua fursa hii kumpongeza M/kiti wa Watanzania wa Hapa Hyderabad kwa hatua iliofikiwa, kisha namueleza huyo Anonymous wa kwanza kabisa kua M/Kiti kafanya sawa kabisa, nyinyi mlio wengi hamuko hku kwa kusoma ni starehe kwenda mbele sasa kuona mambo haya mnayafurahia kweli ila unatakiwa ukumbuke kua "kinga bora kuliko tiba"

    M'funzi Osmania university.

    ReplyDelete
  8. Kesho shule kama kawaida na wenye mitihani mjiandae...someni na vyombo vya hapa kama deccana and Indian Times.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...