Kunradhi wadau watukufu wa Globu ya Jamii,
Pamoja na hamu na jitihada ya kuendeleza libeneke la video lakini kwikwi ya spidi ya mtandao bado inafanya kazi iwe na changamoto kubwa kiasi hata inalazimu tupunguze ukubwa wa saizi ya video na kuambulia chenga-chenga.
Video ya Ivory Coast na Taifa Stars iko tayari lakini inapanda taratiiiiiiiibu hadi inakera. Hivyo wadau na tuvumiliane, nia ni nzuri tu lakini vitendea kazi iko jaa kwikwi dani yake.
Fibre Optic inaendelea kusambazwa kila sehemu ila haijakamilika kiiiivyo hivyo bado mtandao sehemu nyingi ni mwendo wa jongoo. Ukikaa sawa tu libeneke litanoga na inshaalla sio mbali sana toka leo!
Nae umezini nikuletee 40gb je unayo laptopppp
ReplyDeleteUsikonde ankal tunaaminia!
ReplyDelete