Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya udalali ya Majembe, Bw. Seth Motto akishughukikia bomba ili kukata huduma za maji katika jengo la Fazal and company lililopo mtaa wa Livingstone jijini Dar leo kutokana madai kuwa na deni la Sh. Milioni 2.3 wanazodaiwa na kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO). Kampuni ya majembe imeingia mkataba wa mwaka mmoja na DAWASCO kwa ajili ya kuwakamata wateja sugu wanaodaiwa na kampuni hiyo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Nafikiri sasa umefika wakati kwa wafanyakazi wote wa DAWASCO kustaafishwa kubakia na wahasibu tu na mafundi wa kutandika mabomba mapya wasiozidi kumi wakishirikiana na MAJEMBE watakaokuwa wanalipwa mshahara mnono. Na Trifiki nao wapunguzwe barabarani wabakie wachache watakaokuwa wameshika bunduki kwa ajili ya kuwalinda vijana wa kazi barabarani. Ikibidi na Wizara ambazo hazifanyi vizuri tuwaachie majembe nazo. Wameshindwa kazi sasa wanaanza kukodisha makampuni binafsi si bora tubinafsishe nchi kwa miaka miatano tu huenda tutakuwa mbali kiutendaji.

    ReplyDelete
  2. kila kitu majembe siku hizi kweli watu wanajua kulishana.wapeni basi na tenda ya kuwakamata mafisadi sio walalahoi tu.

    ReplyDelete
  3. Nimekubali Majembe auction mart kweli ni vijana wa kazi.

    ReplyDelete
  4. HAYA NI MATOKEO YA IDARA ZA SERIKALI KUSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO.

    IT'S GOOD FOR MAJEMBE ANYWAY. NI MTANZANIA MWENZETU.

    JAMAA APEWE KUSHUGHULIA NA YALE MASUALA SUGU YALIYOSHINDIKANA KAMA RICHMOND NA EPA.

    ReplyDelete
  5. Wadaiwa sugu wa nini? Maana maji hakuna ni upepo..kama siku hizi kuna bills za upepo hata Oxygen tutaanza kulipia sasa Tanzania. Wanaletea watu bills wakati maji hayakuwapo...bill ni ya nini? Ohh..nimekumbuka..bill ya bomba na hewa...!! Lol ninyi wanadamu...Itabidi tuanzishe Luku ya Maji..ndo dawa yenu tu...Mdau-USA

    ReplyDelete
  6. Ilichofanya DAWASCO ni outsourcing. Unajua DAWASCO na mbwembwe na kelele nyingi hapo jijini DSM wateja wake ni only 10 per cent. Hawana hata mipango ya expansion. Kule Kinyerezi kuna minudo mbinu ya maji iliwekwa na SONGAS kwa kushirikiana na kampuni ya Estiim. Huwezi amini. Kutokea pale Segerea pana pump ambayo inapokea maji kutoka Ruvu kupitia Kimara. Pump hii inapaswa kuyasukuma maji hadi Kinyerezi mtaa wa Kange ambako kuna Tanki la kuhifadhi lita milion 6 za maji ambazo zinatakiwa kusambazwa maeneo yote ya Kinyerezi. Na kama hiyo haitoshi kuna visima 6 ambavyo vimechimbwa ili maji yasambazwe hapo Kinyerezi. Kiroja cha mwaka ni kuwa DAWASCO hawana habari na mradi huu. Ukiwauliza wanakwambia haimo katika Mpango kazi wetu hadi mwaka 2012. Ukiwauliza SONGAS wanakujibu sisi tunasubiri kuwakabidhi DAWASCO. Ukienda DAWASA. Giza nene. Matokeo mpaka sasa Mradi haujawa commissioned. Huo ndio ukweli. Kwa hio wakazi wa Kinyerezi wasio na uwezo wana visima vifupi. Wenye uwezo wana boreholes. Huo ndiyo ukweli wenyewe. Quite pathetic.!!

    ReplyDelete
  7. Mmmmh, Inaonyesha jinsi gani viongozi (management) ya dawasa ilivyo mbovu,pia ni kupeana kula tuu,rushwa na kila kitu itaishia kwa hao majembe, Tanzania need help big time

    ReplyDelete
  8. Hawa Majembe Auction mart pia wapewe tenda ya kuwasaka watumishi wa umma wenye vyeo ktk vyama vya siasa.

    ReplyDelete
  9. Nafikiri ni poa tu kuchukua huo uchafu i mean hayo mamita yao ya maji maana hamna maji wala nini mji mzima unanuka sasa sijui hata bills zimetoka wapi ikiwa miaka nenda rudi wabongo wanakunywa maji ya kisimani.so majembe hamna mnachokifanya hapo

    ReplyDelete
  10. Hii ni mbaya sana na ni symptomatic ya kwamba tanzania inafanya mambo yake ki-3rd World. Ni retrogression kwa kurudi nyuma.

    Maji ni utility, credit controll yake lazima iwe tofauti na bidhaa zingine kwa sababu utility ni kitu kinachohitajika katika maisha ya binaadamu siku hadi siku. kutokuwa na maji ni sawa na kushusha uwezo wa mtu kuishi - ni sawa na kuweka mazingira ya ki-maafa (e.g mazingira yanayopatikana wakati wa vita au baada ya janga la hali ya nchi). Ndiyo maana makampuni ya utility mara nyingi hupewa monopoly.

    Hawa Majembe Auction Mart wana nafasi yao katika uchumi na jamii, lakini siyo katika masuala yanayokita katika mambo ya shughuli za kila siku za binaadamu. Kazi yao inatakiwa ibaki katika kutekeleza amri za mahakama, zinazotolewa baada ya mahakama kutafakari mazingira yote kwenye kesi husika.

    Kwa watu wanaochekelea tunapoelekea, ni kwa sababu ya upungufu wa uelewa wa namna Court Brokers wanavyofanya kazi. Labda yakiwakuta ndipo wataelewa.

    ReplyDelete
  11. there is absolutely nothing wrong for Majembe to collect on behalf of DAWASCO wengi wetu ni watumiaji wazuri wa maji ambao tunalipia bills kwa wakati lakini wengine they have to be followed up more than 5 times, wakikutana na mfanyakazi mpenda rushwa unampa chochote hakukatii maji.. hii inajulikana !! deni linajilimbikiza to a point where you cant get out of it, kushughulikia kulipwa hilo deni ni changa la macho, that's why MAJEMBE vijana wa kazi wanakuwa commissioned kudai yale madeni sugu ambayo mdaiwa anaweza hata akawa kafa nyumba imepigwa chini kajenga nyumba mtu mwingine lakini deni liko pale.. yes and they do collect...

    ReplyDelete
  12. Ningependa kuuliza, eti hao Dawasco tuwalipe bili za nini? Karibia nusu mwaka kwenye baadhi ya sehemu jijini Dar hatuna maji bombani.

    ReplyDelete
  13. Sasa ukisikia kichaa kapewa rungu ndio this tym..dis guyz navyojua hawacheki na nyani..ngoja niwahi kulipa kimeo changu

    ReplyDelete
  14. waajiriwa wa dawasco wana kazi gani? hapa tutegemee bili za maji kupanda ili kufidia fedha ambazo wanalipwa majembe, nchi inapoelekea sasa ni pabaya maana sijui trafiki wana kazi gani tena kama ndio hivyo basi muwape wamanage na fedha

    ReplyDelete
  15. Se-Mwamoto ndauli bee

    ReplyDelete
  16. TATIZO LA MAJI DAR ES SALAAM HALIJALETWA NA DAWASCO BALI NI DAWASA. NA DAWASA TATIZO LAKE NI UONGOZI MBOVU, KUNA WATU WAMELEWA MADARAKA PALE. WAMEKAA TANGU NUWA LAKINI HAKUNA WANACHOFANYA CHA MAANA.

    VIONGOZI WA SERIKALI KUU NAO WAMEFUMBIA MACHO KABISA HILI TATIZO. VIONGOZI WA DAWASA WANATAKIWA KUBADILISHWA. WASIPOBADILISHWA DAR ES SALAAM ITAENDELEA KUWA NA TATIZO LA MAJI DAIMA.

    MIMI NAAMINI VIONGOZI WAKUU PALE DAWASA WANALENDWA NA VIONGOZI WAKUU WA SERIKALI. THIS IS BECUASE DESPITE THERE HAS BEEN A BIG PROBLEM OF WATER IN DAR FOR MANY YEARS, NOBODY HAS EVER QUESTIONED THE ABILITY OF DAWASA MANAGEMENT.

    JEURI HII NDIYO ILIYOSABABISHA HATA CITY WATER WAKASHINDWA KUFANYA KAZI KWA SABABU VIONGOZI WA JUU WA DAWASA HAWAKUTAKA MABADILIKO.

    HATA SASA HIVI KIONGOZI WA JUU WA DAWASCO AKUBALIKI KWA KIONGOZI WA DAWASA. KUMBUKA KIONGOZI WA DAWASCO ALIFANYA KAZI NZURI SANA ARUSHA NDIYO MAANA AKAJA DAR. KWA BAHATI MBAYA SANA AMEKUTANA NA VIKWAZO VYA DAWASA.

    VIONGOZI WA SERIKALI KUU, JAMANI BADILISHENI UONGOZI PALE DAWASA.

    ReplyDelete
  17. Hawa jamaa nawaaminia. Tuiombe serikali iwape tenda ya kuwashughulikia wanaume wanaopiga wake zao majumbani

    ReplyDelete
  18. HAHAHAH DUH TENDA YA KUKABILIANA MIJIBABA WANAWADUNDA WAKE ZAO...SI BALAA HIYO WANGU...YOTE NI NJAA TU HAMNA LOLOTE...WAMENYANYASA BARABARANI SASA WAMEAUA KUINGIA MAJUMBANI.....MIMI NIEOMBA MITA NA NIMELIPIA MIAKA MIWILI SASA SIJAPATIWA UTADHANI NAIOMBA WAJE KUKATA MAJI YA MGAO KWANGU.....ZIKI ISYO KUWA NA KIKOMO.................

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...