Balozi wa Benin nchini China, Mhe. Sedozan Jean-Claude Apithy akitia
saini Kitabu cha Maombolezo huku Afisa Ubalozi Mrs. Matilda Masuka akishuhudia.

Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China
kutoka Idara ya Afrika Bw. Zhang Zhuqiang akimshika mkono wa pole Balozi wetu wa Tanzania nchini China, Mhe. Omar R. Mapuri. Nyuma ni Maafisa wa Mambo ya Nje waliofuatana naye.
Bw. Liu Yangfu, Mwakilishi kutoka Ofisi Kuu ya Chama cha Kikomunisti
cha China (CPC) akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo katika kituo chetu cha Ubalozi, Beijing – China, ikiwa ni sehemu ya kuomboleza kifo cha Mzee wetu Mhe. Rashidi Mfaume Kawawa, Simba wa Vita.
Balozi wa Rwanda Mhe. Benjamin Rugangazi na Balozi wa DRC, nao pia
walifika Ubalozini hapo kuwasilisha salamu zao za rambirambi. Kutokana na watu kufika kwa wingi kumkumbuka Simba wa Vita ilibidi vitabu viwili vifunguliwe kwa pamoja kupunguza kero ya kuwafanya wageni wetu kusuburi kwa muda mrefu.

Afisa Ubalozi wa Visiwa vya Maldives, Ms. Fathmath Najuwa akitia saini
Kitabu cha Maombolezo huku Mwambata Fedha wa Ubalozi, Bw. Lusekelo Gwassa akishuhudia.

Mdau John Masuka aliyetuletea taswira hizi nae alihudhuria Ubalozini hapo kuwawakilisha Watanzania waliopo nchini China katika kutia sahihii katika kitabu cha Maombolezo.

Balozi wa Msumbiji Mhe. Antonio Inacio Junior akitoa pole kwa Balozi wetu Mhe. Mapuri, baada ya kutia saini Kitabu cha Maombolezo. Mhe. Antonio alisema Simba wa Vita alikuwa mhimili mkubwa katika harakati za kupigania Uhuru katika nchi yake na hivyo mchango wake utakumbukwa daima

Balozi wa Burundi Mhe. Gabriel Sabushimike akimpa mkono wa pole Balozi wetu Mhe. Omar Mapuri, baada ya kutia saini Kitabu cha Maombolezo.

Maafisa Ubalozi wetu China, Mr. Murobi Magabilo na Ms. Joyce Matai wakiwa mstari wa mbele katika zoezi la kumkumbuka Mzee wetu Mhe. Rashidi Mfaume Kawawa

Mdau Dr. Aman Bura akitia sahihi katika kitabu cha Maombolezo.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. inana lillahi waina illahim rajiun kamfuata mwalimu watazungumza vizuri kuhushu muungano mshitakiye mwambiye kikwete anatanua nchini pamoja na amani karume

    ReplyDelete
  2. MIMI NAOMBA KALE KASHERAI CHA KUNYONGA WALA RUSHA TUU EPA INGEKUWA HISTORIA. MAMBO YA CHINA JAPANI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...