wasifu wa simba wa vita wakati waq mazishi ya Simba wa Vita Mzee Rashidi Mfaume Kawawa nyumbani kwake Madale jijini Dar leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ahsante Bwana Michuzi pamoja na wote walioshiriki katika kutoa hii video ya Mazishi ya Simba wa Vita. Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi.

    ReplyDelete
  2. Hapa Bwana Mithupu umecheza kama drogba sasa tutafutie clip nzima na sisi wabeba box huku tuone mazishi ya Mzee Wetu
    Mungu ailaze roho ya marehemu pahali pema peponi

    ReplyDelete
  3. ankal,
    asante kwa clips hizi nasubiria part 3

    ReplyDelete
  4. MZEE HAPA UMECHEZA KAMA STEVEN GERRARD WA BWAWA LA MAINI, MASHUTU YA NGUVU YA MBALI KITU KINATINGA, SASA TULETEE YOTE MWANZO HADI MWISHO

    ReplyDelete
  5. kaka michuzi kiwango bado bwana cha shooting next time inabidi kazi kubwa kama hii uifanye mwenyewe....

    ReplyDelete
  6. kaka michuzi part one ni out of focus kabisa kaka...lakini lazima nikupongeze kwa kazi kubwa uliyofanya japo ilikuwa out of focus lakini jitihada nimeona...big up kaka. Ila tu next time jaribu kupata wide angle, medium shots, close up etc si unajua tena? vinginevyo utamu wa video unaondoka kama clip yote is too general...lakini nakupongeza kaka

    ReplyDelete
  7. Ankal,

    Thank you for the coverage.

    RIP Mzee Kawawa.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  8. "KAKA MICHUZI UMEVUKA MIPAKA YOTE"

    Kwa mara nyingine tena umetuhakikishia kama una kipaji cha kuzaliwa katika "libeneke" la wanahabari.
    Shukrani kubwa kwa sisi ndugu zako tuliokuwa mbali kwa kutukaribisha tuwe karibu katika mazishi ya mzee wetu simba wa vita,ambayo kimtazamo
    yamehudhuliwa na viongozi wote wa serikali na vyama mbali mbali vya siasa,hii inatupa amani na umoja katika nchi yetu tunapoondokewa na kiongozi yeyote aliyefanya vizuri kwa Taifa.
    Kazi uliyoifanya mbali na vyombo vyote vya habari nchini,wewe ndiye wa kwanza umetuweka karibu kwa kupitia hii "YOU TUBE" video. Wengi baada ya kuusikiliza wasifu wa mzee Kawawa tumebaki na majonzi.
    Mweyenzi Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya mzee wetu Kawawa

    Mickey Jones-Denmark

    ReplyDelete
  9. Ama kweli. Ama kweli. Kama alivosema kaka Mickey Jones hapo juu; blogu yako inasaidia kueneza hizi habari kwetu wote wazalendo ulimwenguni Issa Michuzi. Unafanya kazi nzuri sana hata kuzidi baadhi ya vyombo vya habari. Tunaipata "live" ughaibuni.
    Jambo kubwa lililofukuliwa hapa ni namna ambavyo kazi mbalimbali alizofanya hayati Mzee Kawawa hazikuwa zikijulikana kwa wengi. Mojawapo ambayo haisemwi sana ni namna mathalan alivyokuwa kati ya Watanzania wa mwanzo kuigiza sinema miaka ile ya ukoloni. Alikuwa mwingi na tajiri wa vipaji...
    Na uzuri wake hakujifaragua kwa hilo. Mfano bab kubwa wa kuigwa na kujifunza kwa hawa mafisadi waliostawi kama chawa na viroboto miongoni mwetu, leo.
    Mungu Aiweke Roho yake pema peponi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...