Mchungaji Christipher Mtikila

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar imetoa amri ya kuwekwa rumande Mchungaji Christopher Mtikila ambaye anakabiliwa na kesi ya kumkashifu Rais Jakaya Kikwete kwa kukiuka amri ya mahakama na kukiuka masharti ya dhamana mara mbili

Mch. Mtikila alishtakiwa Oktoba 22 mwaka jana baada ya kumwita Rais Kikwete 'gaidi na muhuni'. Hakimu mkuu mkazi Waliarwande Lema alitoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa chama cha upinzani baada ya kutofika mahakamani asubuhi, akiwa nje kwa dhamana.

Hakimu Lema aliamuru mshtakiwa awekwe rumande hadi January 25, mwaka huu wakati kesi yake itapotajwa. Upande wa mashtaka umesema upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika.

Mapema asubuhi, wakati kesi hiyo ilipotaka kuanza kusikilizwa, Mch. Mtikila alikuwa hayupo mahakamani.Wakili wa serikali, Beatrice Mpangala, aliiomba mahakama kutoa amri ya kukamatwa kwa mshatkiwa kwa kukiuka masharti ya dhamana kama ilivyokuwa Oktoba 22, mwaka jana ambapo inadaiwa haukutokea mahakamani.

Hakimu alilikubali ombi hilo na kuamuru polisi kumkamata mshtakiwa mara moja. Na Mch. Mtikila hatimaye alipowasili mahakamani hapo baadaye akajikuta anatiwa nguvuni mara tu baada ya kukanyaga viunga vya mahakama ya Kisutu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Kiongozi gani huyo anamtukana rais wa nchi yake, hafuati sheria za nchi na anakiuka amri ya mahakama?! Dgarau hizo!! Nikifikiria ufisadi uliopo natamani upinzani wangeshika nchi, Lakini nikifikiria viongozi hawa wa upinzani, Mhh!!

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli democrasia ipo mbali sana Tanzania. Ukiona ambavyo huku Marekani wanavyo mwita Obama kila jina gaidi, hitler, kila aina ya maneno yenye mauzi lakini jamaa wala hamaindi kwani kuna msemo kuwa "saying so doesnot make it so" kama kweli nchi yetu inaamini katika demokrasia basi huyu mtikila si wa kumshitaki kwa maneno yake bali ni kumpuuza ama kuonesha kuwa anayoyatenda si kweli kwa kuyapinga na kutolea ufafanuzi.

    huu mchezo wa kupelekana mahakamani kwa kuwa fulani kasema uongo ni ukosefu wa ukomavu wa kisiasa nchini na kujipendekeza kwa wakubwa wale wenye dhamana ya sheria. Hakuna kesi hapo bali ni kushusha hadhi ya mahakama zetu. Kesi za ujambazi zinachukua miaka kumi kwisha. Sick of my country

    ReplyDelete
  3. AH MCHUNGAJIII, Angalia tena maandiko najua unayaelewa ila umesahau, muheshimu basi kiongozi wako na wafuasi wasome nini toka kwako,Sweka jela hyo atajifunza zaidi.

    ReplyDelete
  4. mmmh manake hata kama humpendi raisi wako kaa KIMYA sasa atakiona huko jela watam*****a ile mbaya manake ni kachokoza nyuki. Binadamu lazima tuelewe hakuna aliekuwa sawa mpaka OBAMA pia anakosolewa ila ulaya kuna "Freedom of speech" lakini africa hatuna haya. Ulaya bosi hawezi kukukaripia sababu anajua wazi kuna sheria ila africa mtu yoyote akiwa mkubwa kwako ndio mwenye sheria.
    Mtikila uliyatafuta haya matatizo mwenyewe sasa utakiona. Na ukibahatika kutoka acha mambo ya chama ni hayakufai manake ukipatwa na FURSA ya kutuongoza utatufanyia maajabu kama haya.

    JK Ni Raisi wetu utake usimtake

    ReplyDelete
  5. hawa police na mahakama hawana kazi ya kufanya wanaonekana au wanafanya kazi bila kuelewa sheria na kujipendekeza tuu,alichosema mtikila ndio kina obama wanaitwa kila siku na wala sio kosa,kama kamwita gaidi ni opinion zake tuu na sio lazima iwe kweli na hakuna mtu anamwamini mtikila alichosema ni siasa tuu....upuuzi mtupu na kupoteza muda tuu

    ReplyDelete
  6. mimi binafsi mtikila ni mtu wa ovyo kuliko wana wa upinzani wote walio katika nchi hii anacho kikundi cha vijana kanisa lake ambacho ni wasema hovyo yeye ni mkuu wa msafara huo hukaa pembeni na kuratibu shughuli za kundi lake na mwishoni hufanya hitimisho ukisiliza pointi zake ni hovyo kabisa hazifai hata kwa dawa ni siasa za chuki zaidi kuligawa taifa letu kueneza udini bahati nzuri watz walishaelewa mambo kama hayo siku nyingi hatudanganyiki.
    mtu mzima lakini msema ovyo.

    ReplyDelete
  7. No freedom of speech at all? Does that qualify for deformation of character?

    ReplyDelete
  8. Jamani mbona maneno ya kawaida hayo, sioni tusi.

    mnamtafutia umaarufu tu wakati tayari alishakwisha.

    ReplyDelete
  9. Pamoja na udhaifu wa sheria zetu hapa bongo, Mtikila naye amedhoofu sana kisiasa kwa muda huu. Hiv kanisa lake likowapi?? na siku za ibada hapo ni lini?? hakika wafuasi wake mmedanganika - kwisha kazi yenu.Aswekwe ndani ama asiswekwe hana jipya!

    ReplyDelete
  10. Kukiuka amri ya mahakama nayo ni freedom of speech? Kwa vile marekani au france kumtukana mtu/kiongozi/Rais 'ni kitu cha kawaida', hiyo ndiyo hulka ya kuiga?! Acheni hizo Wabongo, igeni amendeleo, sio ujinga!

    ReplyDelete
  11. Kidumu chama cha mapinduzi, mahakama iliundwa na nchi ili kukilinda chama chetu cha mapinduzi na Rais wetu, vyama vya upinzani havina nafasi katika nchi yetu ya Tanzania.

    ReplyDelete
  12. Mtikila - kibaraka wa yeyote mwenye pesa!!!

    ReplyDelete
  13. wewe mtoa maoni EXHANI,
    Unatushangaza unaposema Demoklasia iko mbali !unachanganya Demoklasia kuwa ni Uniform!? Demoklasia hawezi kufanana kama sare za shule,
    Demoklasia ya Marekani hawezi kufanana na ya Tanzania,na Demokrasia ya Uarabuni hawezi kuwa sare na ya Japan,lazima ufahamu nini?maana ya demokrasia? sasa demoklasia ya marekani inaruhusu kumwita kiongozi jina lolote! ndio Tanzania nayo tuige hivyo?
    Marekani inaruhusu ndoa za mashoga!sasa unataka Tanzania nayo tuige mfumo huo au?
    Mchungaji Mtikila kadharau Mahakama,na mahakama ni chombo cha umma,pia kakiuka masharti ya mahakama! na huko marekani pia kama utadharau chombo kinachochunga sheria ya nchi yaani mahakama,lazima utatiwa mashakani.
    Jaribu kufanya utafiti na kujua nini?maana ya demokrasia haiusiani kabisa na uvunjwaji wa sheria au utaratibu wa nchi ulipangwa na chombo au baraza la kutunga sheria.
    Pia neno hilo Demoklasi sio neno la Kingereza au Kirumi ni neno la KIGIRIKI jaribu kulitafiti neno hilo na ujue maana yake kamili.
    Pia katika utendaji wake demoklasia haiwezi kuwa sare kwa kila nchi.Tanzania ina sheria na utaratibu wake,na kumkashifu au kumtusi mtu ni kinyume cha sheria.
    Unamwita mkuu wa nchi muhuni!maana yake unamtusi mtu aliyechaguliwa na wananchi,na kuwatusi waliomchagua kuwa hawana hakili?
    Sasa kwanini ? mtikila asifikishwe mahakamani? na kutuhakikishia Uhuni wa rais wetu hupo vipi?

    ReplyDelete
  14. wee anon wa hapo juu wewe ndio wa ovyo kwasabababu huijui democrasia, kwa taarifa yajko watu kama mtikila ndo waliochangia leo hii kwa baadhi ya viongozi wa ccm walioko serikalini kupigana na ufisadi na nk, sasa nasema wewe ndio wa ovyo..

    ReplyDelete
  15. Candid ScopeJanuary 12, 2010

    Watanzania tunaweza sema mengi na kushuhudia mengi lakini cha msingi tujue hali hiyo inatokana na athari za siasa za mfumo wa ujamaa tuliojengeka nao hapo awali. Mfumo wa ujamaa unaongozwa kwa misingi ya chama kimoja na viongozi kuabudiwa kama miungu. Usiseme cho chote kuhusu serikali au viongozi wa serikali bali waimbie nyimbo za kuwasifu hata wanapojinufaisha ndo haki yao
    Ukweli uhuru wa kusema katika mantiki ya demekarasi tuko nyuma sana na ndo maana hatukubali kukosolewa na kama unakosoa unaonekana msaliti.
    Tuna kazi sana ya kujikomboa kifikra na kidemokrasi ili kujenga haki katika serikali na jamii, vinginevyo tutaendelea kuwalinda viongozi kwa kuwapinga wale wakosoaji.
    Vyombo vya sheria na vya usalama wa raia na taifa vinatumika zaidi kulinda hieralikia ya uongozi badala ya kudumisha haki na demokrasia ya wananchi na taifa.
    Kwa mantiki hiyo mfumo wa vyama vingi ni kushabikia serikali na chama tawala na viongozi? Au kukosoana ili kuenzi taifa na maendeleo yake kisiasa na kiuchumi ni kumvunjia kiongozi heshima yeke?
    Je tunajua kupambanua nini maana ya kuvunja sheria na nini maana ya kukoksoa ili kujenga hoja ya utendaji mzuri serikalini?

    ReplyDelete
  16. Obama anaambiwa sio raia wa u.s. na ahamaki sembuse wewe Kikwete? Kuna jamaa flani alishawai kumwambia Obama muongo live na akuchukuliwa ha2a yoyote. kum2kana rais ni kosa ila kumkashifu rais sio kosa. Kidemokrasia kumwambia Rais wako vyovyote unavyojisikia sio kosa. Ila kosa alielifanya Mtikila kutokwenda mahakani. I don't care ata kama serikali yako lazima uwende mahakani. Wewe ni nani usiende mahakani? Mwache anyie debe mpaka tarehe yake ya mahakani. Sheria ni msumeno na kwa wote

    ReplyDelete
  17. We anon hapo juu unayejifanya unajua maana ya demokrasia hata kuspell hilo neno hujui sio DEMOKLASIA ni DEMOKRASIA yaani accent yako ya kilugha inasikika mpaka kwenye maandishi yako....

    ReplyDelete
  18. Anka,
    Mimi nawashangaa waTZ. Bwana Mtikila hana kosa lolote hadi chombo cha sheria ktakapothibitisha hilo. Hata hiyo kuambiwa amedharau mahakama haijathibitishwa na kama imeshathibitishwa basi ahukumiwe kwa hilo kosa. Mtikila anaweza shinda hizo tuhuma zote na akadai fidia kibao. Kwa hiyo si vyema kumhukumu Mchungaji huyu.

    Pili.

    swala la kuga au kutoiga demokrasia is no longe a big issue,Sheria za nchi zinatoa uhuru wa kuzungumza katika mfumo wa vyama vingi. Mbona wanakatuni kina kipanya walikuwa wanachora uncle Ben Mkapa mara kibao lakini kwa kuwa alikuwa mshua fulani alikuwa bize na ishu zake za maendeleo ndo maana enzi zake uhuru wa habari ulikuwa fresh. Sasa mtikila akikuita muhuni unakimbilia mahakamani wakati kesi za maana kibao hazishughulikiwi. Na najua huyu mdingi atashinda hiyo kesi na kuvuta mshiko kibao wa fidia. Tanzania haiigi kila kitu, inaiga hili la kuwasema viongozi kama sehemu ya kuichambua serikali na viongozi wake kama wamefanya makosa. Kazi ya upinzani ni kukosoa/watch dog waacheni waongee jamani. Mbona lipumba alimwita rais hana uwezo wa kuongoza/kutoa maamuzi...akasema anamfahamu kuwa ni dhaifu...does that mean nalo ni tusi au si tusi...au kashfa...

    Ankali sipendi watu wanaomwandama Mshua Mtikila

    ReplyDelete
  19. mama HellenasraJanuary 13, 2010

    yaani katika viongozi ninaowakubali basi ni mtikila,ana uchungu na hii nchi mpk imepitiliza anajikuta anasema chochote si unajua mtu ukikasirika hujui litalotoka mdomoni kupoza machungu?
    huyu bwana huwa anaongea point tupu,ktk hotuba zake hapo nyuma kipindi cha kampeni aliongelea sana khs mikataba ya madini na akasema bwana Ben na wenzake wameleta makaburu kuchimba madini na kutuachia mahandaki,watu wakampuuza lkn sasa tunaona ooh kuna mikataba bomu ya madini kibao.
    haya mambo ya mikataba feki kaanza kuzungumzia siku nyingi lkn kila mtu anamuona km chizi.
    kwa ushauri tu,nawaomba wadau mzisikilize sana hotuba zake halafu km mtu una uzalendo na uchungu na nchi yako,utaona hata jina alilomuita mtikila alilipunguza makali tu,we unaweza kutoa zaidi ya hilo

    ReplyDelete
  20. Wewe Anon wa Tue Jan 12, 05:48:00 PM

    Nimeshakufahamu. Wewe ni MUHINDI na hakika wahindi hawampendi MTIKILA kwani wanajua wazi fika ana agenda moja ambayo alitakiwa aifute kwenye maandishi kabla ya kupatiwa usajili wa kudumu nayo ni kuhakikisha MAGABACHORI wanashughulikiwa kwa kuifilisi nchi. Agenda hii aliifuta kimaandishi ila bado ipo kichwani kwa MCHUNGAJI mungu ampe maisha marefu siku akishika nchi mmekwisha.

    Sasa veve nasema "demoklasia" hapana fanana kila nchi, basi sisi Tazania iwe hapana fanya chaguzi bali pitisha ongozi ya nchi kurisisha toto zao wao abao ongoza nchi tu sisi iwe na tawala ya kitemi tu basi

    Ukweli utabaki palepale unapojiita unafuata utawala wa kidemokrasia maana maamuzi yanafanywa kwa faida ya wengi, sasa watanzania wengi hawaoni athari za maneno ya mtikila katika maisha yao bali wao wanataka maendeleo. UHURU WA MAONI UHESHIMIKE, Mbona utabiri wa Sheikh Yahya wameuheshimu ilitakiwa naye ashitakiwa kwa kutishia maisha pale aliposema atakaye mpinga JK atakufa Ghafla. Je kama mtikila naye alikuwa anatoa utabiri wake kwa utawala wa JK kuna ubaya?.

    ReplyDelete
  21. watz hapo tatizo si kutukana tatizo ni kutokwenda mahakamani kama dhamana yake ilivyo watz tuwe watu wa kulewa jamani.

    ReplyDelete
  22. Mama Hellenasra umenifikisha ndugu yangu.........

    Thank youuuuuu!!

    ReplyDelete
  23. watanzania kwa kesi za kuku wanazitilia mkazo lakini wanaoiba mamilioni ya pesa wako mitaani wanakula kuku kwa mirija. serikali yetu siku zote inawapa wapinzani kesi zisizoisha,wapinzani wanajikuta kila siku kazi kwenda mahakani tu na kuacha shughuli za siasa.UJANJA HUO TUNAUJUA. hizo mahakama na sheria za nchi zingekuwa zinafuatwa hivyo kama wanavyodai kwamba mtikila hakuja mahakani siku ya kesi yake basi tungekuwa tunaona haki inatendeka hapa nchini na kwa watu wote. mbona kuna kesi kubwa tena za uharifu mkubwa miaka na miaka hazijapatiwa hukumu? nyingine hata hawajui files zilipo? na miaka nenda wanadai uchunguzi haujamalizika? hebu mtupe data kuna watu wangapi mnawashikilia kwa kutofika mahakani? kama si mtikila peke yake? na tunajua siku akimsifia rais kesi zote mtazifutia mbali. tutaendelea kusema kwa nguvu pale pasikuwa na haki. speak out loudly MTIKILA MPAKA NA VIZIWI WASIKIE.

    ReplyDelete
  24. kama haujawahi kuwa na kesi subiri siku uwe kiongozi kenye kambi ya upinzani, ccm watakupa kesi moja baada ya nyingine mpaka siku ya kufa. kwani kuna watu wangapi umeshapeleka mahakani eti wamekuita "MHUNI"? chungu nzima siyo!!! mbona kesi zote ni kwa wapinzani tu? hivi ccm wao ni malaika hawatendi makosa? wadau msitetee uozo hapa,hizo sheria na mahakama mbona zinafanya kazi upande mmoja tu kwa wapinzani? kesi ya mtikila ni blah....blah tu. hakimu na majaji hebu tafuteni kazi za kufanya siyo kila siku MTIKILA BIN MTIKILA.

    ReplyDelete
  25. si mtikila peke yake anayetukana viongozi wapo wengi mitaani kwani ukipita mitaani utasikia huyu kiongozi wetu kama msengelema yaani hana lolote analofanya na hawa nao wakamatwe

    ReplyDelete
  26. si huyuhuyu mtikila ndiye aligombania issue ya mgombea binafsi akashindaaa,si huyuhuyu mtikila alipigwaga jiwe akabak akishangaa teh teh sasa leo anaizarau mahakama.Huyu jama ukifanya sensa ameshawekwa lupango mara ngap itakua zaid ya mara 50 lakin bado hakomii alishawah mpaka kufungwa mwaka mmoja lakin hasikii ni mgumu kwel.

    ReplyDelete
  27. Jaman hizo hela za walalahoi tunazotumia kukimbizana na mtikila si serikali ingetafuta kijiji kimoja chenye matatizo ya maji wachimbe angalao kisima wanakijiji wasisafiri umbali mrefu kuchota maji?

    ReplyDelete
  28. P.S. NALITOLELAJanuary 14, 2010

    KWANI UBISHI NI WANINI HUMU KWENYE BLOG YA JAMII? KWANI MICHUZI KAKAMATWA? MBONA SIJAPATA HIZO HABARI ZA KUVUNJA SHERIA AMA NI NDOTO ZENU TU ZINA WAFANYA MBISHANE? MICHUZI YUPO HAI TENA HURU WALA HATAFUTWI NA MAHAKAMA WALA POLISI SASA HIZI HABARI SIJUI MMEZISOMA WAPI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...