Balozi mpya na mwakilishi wa Shirika la Umoja Mataifa la Elimu ,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Bi. Vibeke Jensen akimweleza jambo Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika mara baada ya kumtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine wamezungumzia uendelezaji wa sekta ya Elimu na Utamaduni pamoja na Programu ya uhifadhi kumbukumbu ya vita vya ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika hapa nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika akisisitiza jambo kwa Balozi mpya wa Jamuhuri ya Cuba Ernesto Go'mez Diaz kuhusu namna Tanzania itakavyoshirikiana na Cuba katika kuendeleza sekta ya Michezo na Afya nchini.Balozi wa Cuba amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kutoa nafasi za elimu na kufundisha wataalam katika sekta ya michezo na Afya.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika(kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Cuba Ernesto Go'mez Diaz (wa tatu kutoka kushoto) na makocha wa riadha na Ngumi kutoka Cuba wanaoendelea kuwafundisha vijana katika michezo hiyo hapa nchini.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.


Ankal, Balozi wa Cuba ni wapili toka kushoto au wa tatu??
ReplyDeletePROJECT NUMBER ONE FOR TANZANIAN --- MAKING THE NATION NUMBER ONE IN THE WORLD FOR SCIENCE AND MATHS TEACHER. FORMALLY WE DEPEND ON TOURISM FOR FOREIGN CURRENCE SOON MOUNT KILIMANJARO WILL BE NO MORE. OUR FOCUS NOW IS TO PRODUCE AT LEAST HALF OF EVERY FAMILY MEMBER TO TO MATHS AND SCIENCE TEACHER OR EXPART SO AS WE CAN TRY TO FILL THE ABUNDANCE OF THE VACANCES RELATED TO THE FIELD IN THE WORLDabout
ReplyDelete