Mbunge wa viti maalum (CHADEMA), Mhe. Mhonga Said Ruhwanya akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mwamgongo kilichopo katika wilaya ya Kigoma Vijijini mara baada ya kukabidhi vifaa vya umeme wa jua katika kituo cha Afya kijijini hapo.
Mbunge wa CHADEMA
achangia kituo cha Afya Kigoma
Kituo cha Afya cha Mwamgongo kilichopo Kigoma Vijijini, kaskazini mwa Ziwa Tanganyika kimepatiwa umeme wa nguvu ya kujua ili kunusuru mazingira hatarishi yaliyokuwemo katika kituo hicho.
Kituo hicho ambacho kina wadi ya kujifungulia akinamama wajawazito, maabara na jokofu la kuhifadhia dawa hakijapata kuwa na umeme tangu kuanzishwa kwake miaka 14 iliyopita na hivyo kusababisha matatizo makubwa kwa wagonjwa wanaotibiwa hospitalini hapo hasa akinamama wajawazito wanaolazimika kulazwa kwa ajili ya kujifungua.
Hata hivyo, matatizo hayo hivi sasa yameondoka baada ya Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Mhe. Mhonga Said Ruhwanya kujitolea msaada wa vifaa vya umeme wa jua vyenye gharama ya shilingi milioni 27.

Akikabidhi misaada hiyo, Mhe. Mhonga alisema kuwa aliguswa na matatizo hayo na kulazimika kujitolea msaada huo kwa faida ya akinamama toka vijiji saba wanaohudumiwa na kituo hicho, ’’ Nashukuru kwamba kwa msaada huu wagonjwa toka vijiji vya Bugamba,Kagunga, Zashe, Kiziba, Mwamgongo, Mtanga na Kigalye watakuwa wamepata ahueni kwa vile ukosefu wa umeme ulikuwa ukiathiri sana huduma za afya katika maeneo haya’’ alisema.
Aidha, Mhe. Mhonga alisema kuwa msaada wake wa vifaa vya umeme wa jua ni kutokana na kubaini kuwa umeme wa serikali ungechelewa sana,’’ Baada ya majibu ya serikali juu ya upatikanaji wa umeme Kigoma, nilibaini kuwa umeme katika eneo la Mwamgongo hautofika leo wala kesho. Nisingeweza kusubiri kipindi chote hicho huku nikiona wananchi wanateseka’’ aliongeza Mhe. Mhonga.
Mhe. Mhonga ambae kwa sasa ni mbunge mwenye umri mdogo zaidi katika Bunge la sasa pia amekabidhi vifaa vya umeme wa nguvu za jua kwa shule ya bweni ya Bugamba inayohudumia vijiji hivyo saba kwa gharama ya shilingi milioni 35. Vifaa hivyo vimeweza kutoa umeme katika jengo la Utawala, Mabweni na madarasa ya shule hiyo. Akizungumzia msaada huo Mhe. Mhonga alisema anatumai kwamba kwa msaada huo wanafunzi sasa watanufaika kwa kuweza kumudu kujisomea usiku.

’’ Katika ziara zangu kwenye maeneo haya yaliyo kaskazini mwa Ziwa Tanganyika nilibaini kuwa wanafunzi wanajisomea muda wa mchana tu ambao unachanganyika pia na wakati wa masomo na hivyo kuwa na muda finyu wa kujisomea sasa kwa kupatikana umeme hivi sasa, wanaweza kujisomea usiku na pia wafanyakazi wa shule kuweza kutumia vifaa vya kisasa katika utekelezaji wa majukumu yao’’ alisema.
Mkoa wa Kigoma ni moja ya mikoa ya pembezoni ambayo mbali na ukosefu wa nishati ya umeme umekuwa nyuma kwa maendeleo kutokana na kutokuwa na miundombinu ya barabara na reli ya kati kutofanya kazi kwa ufanisi.

Mimi nafikiri wakati umefika kwa tume ya uchaguzi kufanya marekebisho ya kuufanya uchaguziwa wabunge ufanyike kila baada ya mwaka mmoja au mika miwili.Hili litatusaidia kupata misaada kila wakati kampeni zikikaribia kuliko kusubiri kupata misaada baada ya miaka mitano maana hapa ukiuliza huyu mbunge in all those 5 years haya matatizo hakuyaona mpaka uchaguzi unafikia ndio anakurupuka?
ReplyDeleteumefanya vizuri sana mama si kama wale wa chama tawala walotoa sh 190m/= za kampeni kwa ajili ya kulikwamua jimbo la john cheyo, bariadi mash
ReplyDeletembunge kabla hajachaguliwa atoe ahadi atafanya nini ktk miaka 5, watanzania siku hizi ni machangudoa wananunuliwa kwa sh 10,000/= kumpa mtu kura pasipokufikiria wayatendayo.USIBANE PLZ...
Mdau wa kwanza kabisa hapo juu - Mgosi wa Kaya - wazo lako ni zuri sana.
ReplyDeleteMi naunga mkono.
safi sana! we Mgosi wa Kaya acha mtimanyongo! huyo dada ni Mbunge wa Kuteuliwa! huo ni upendo wake mwenyewe!
ReplyDeleteMdau wa kwanza kabisa hapo juu - Mgosi wa Kaya - wazo lako ni zuri sana.
ReplyDeleteMi naunga mkono.
WE HAPO JUU JARIBU KUSOMA VIZURI KABLA HUJARUKIA COMMENTS HUYO DADA SIO MBUNGE WA JIMBO NI WA KUTEULIWA NARUDIA "HANA JIMBO" KWAHIYO HAJATOA KWA SABABU UCHAGUZI UNAKARIBIA
ReplyDeleteHUYU ANGEKUWA MBUNGE WA CCM INGEKUWA SAHIHI KUTOA HUO MSAADA KWANI ISINGEKUWA KAMPENI LAKINI HUYU NI WA UPINZANI NDIYO SABABU NIMELAZIMIA KUSEMA HIVYO NINA CHUKI NAO.
ReplyDelete