Msanii na kiongozi wa Kundi la Mjomba Band Mrisho Mpoto akiwasilisha ujumbe kuhusu umuhimu wa jamii kutumia vyoo safi ili kuepuka magonjwa mbalimbali akiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Serengeti kutoka wilayani Temeke leo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam wakati wa Kilele cha Kampeni ya Fyatua Choo na Ushinde.
Mkurugenzi Msaidizi wa Afya na Mazingira wa Wizara ya Afya Elias Chinano akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa (katikati),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Aisha Kigoda (wa pili kushoto) na Katibu mkuu wa Wizara hiyo Bi. Blandina Nyoni kuhusu picha mbalimbali za vyoo usafi na vichafu zilizoshiriki Shindano la Fyatua Choo na Ushinde leo jijini Dar

Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akibadilishana hati za makubaliano na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Injinia Christopher Sayi kufuatia Wizara nne kuwa na Ushirikiano katika kutekeleza shughuli za Afya na Usafi wa mazingira wakati wa Kilele cha Kampeni ya Fyatua Choo Ushinde leo jijini Dar es salaam.Wizara zilizosaini makubaliano hayo ni 0fisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamii, Wizara ya Majia na Umwagiliaji na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufunzo.
Makatibu wakuu Bi. Blandina Nyoni wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (kushoto) na Injinia Christopher Sayi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Wizara (kulia) wakisaini hati za makubaliano ya Ushirikiano katika kutekeleza shughuli za Afya na Usafi wa mazingira huku wakishuhudiwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na Naibu wake wakati wa Kilele cha Kampeni ya Fyatua Choo Ushinde leo jijini Dar
Mshindi wa Shindano la Fyatua Choo na Ushinde kwa kuwa na choo kisafi Bi. Fatuma Ally kutoka Dodoma akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa wakati wa Kilele cha Kampeni ya Fyatua Choo na Ushinde iliyolenga kuhamasisha kaya na Jamii kuona umuhimu wa kuwa na choo bora na kunawa mikono kwa maji na sabuni. Picha na Aaron Msigwa wa Maelezo





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. MARA NYINGI NIMEKUWA NIKIONA BENDERA TA TANZANIA INAPOTUMIKA KAMA PAMBO ILE SEHEMU YENYE RANGI YA BULUU HUKUNJWA ILI ISIONEKANE, SASA SWALI LANGU NI JE, RANGI HIYO YA BULUU ILIWEKWA KIMAKOSA KWENYE BENDERA HIYO? PICHA YA JUU INAONESHA WAZI RANGI TATU, KIJANI, NJANO NA NYEUSI AMBAZO ZINATUMIWA NA CCM.

    ReplyDelete
  2. wewe vipi unaagalia rangi za bendera mimi naangalia jinsi mawaziri wetu wasivyo na kazi sasa wanakagua vyoo vya watu..... ni aibu kuna watu mpaka leo hawajui kutumia choo. nenda dar es salaam international airport, after landing now you are at immigration counters unakutana na harufu ya toilet man its a shame. i remember those days when i was in our village we use to burn some leaves to make the toilets kunukia vizuri, sasa siku hizi tuna vitu kama air freshener nafikiri may be abiria huwa wanaondoka nazo (may be ) lakini my point the airport wanalipa pesa nyingi sana kwa wanaopata tenda za ku clean hizo toilet, do they do their job? au wanajaza tu watu airport na kufanya idadi kubwa ya wafanyakazi airport kuwa wengi and kuzidish wizi tu. enzi za mwalimu tulikuwa tunafundishwa kutumia choo and jinsi ya kukiweka safi and tungekuwa and hilo darasa mpaka leo kizazi cha leo sio cha kujifunza kutumia choo na waziri angekuwa na kazi nyingine ya kuleta maendeleo katika jammi yetu,
    waziri hiyo ni kazi ya walimu wa msingi your job is make sure we have good hospital na dawa zipo with good doctors

    ReplyDelete
  3. mwelevu haambiwi, lengo la kuificha rangi ya buluu ni kuoneshakuwa mradi umegharamiwa na chama cha mapinduzi na si vinginevyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...