NATAFUTA PICHA ZA MAREHEMU DR. RUGATIRI MEKACHA

Wadau, nahitaji msaada. Natafuta picha za aina yo yote za Marehemu Dr. Rugatiri Mekacha ambaye alifariki tarehe 29/9/2001 nchini Japan ambako alikuwa amekwenda kikazi katika Chuo Kikuu cha Masomo ya Kigeni cha Osaka. Dr. Mekacha ndiye alinipa misingi ya isimu wakati ule nikiwa bado mwanafunzi wa shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Nilipopata nafasi ya kwenda kusomea shahada za uzamili (Masters) na Uzamifu (Ph.D) katika Chuo Kikuu cha California, Los Angeles (UCLA).
Dr. Mekacha alikuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili na alihakikisha kwamba ninapata kila kitu nilichohitaji kwa ajili ya safari hiyo. Hata baada ya kufika UCLA, aliendelea kunishauri katika masomo yangu na mambo mengine ya kimaisha. Kwangu Dr. Mekacha hakuwa mwalimu tu bali rafiki na mshauri.

Ni kwa sababu hizi ndiyo maana nimeamua kuhariri kitabu ili kumkumbuka na kumuenzi. Kitabu hiki (ambacho maelezo yake mafupi yapo hapa chini) kiko tayari kwenda kwa mchapishaji. Kitu pekee kinachonikwamisha ni picha. Mchapishaji amesisitiza sana kwamba itapendeza kama kutakuwa na picha ya Dr. Mekacha ambayo itawekwa mwanzoni mwa kitabu hicho. Juhudi zangu za kupata picha zake hata hivyo zimekwama kabisa. Kama ningeweza kwenda Tanzania ningeenda nyumbani kwao Nata Serengeti kuzitafuta.

Kutokana na tabia yake ya ucheshi na uanaharakati pamoja na kutambulika kwake, nashawishika kuamini kwamba lazima kuna wadau wa blogu hii ambao wana picha zake. Kama mpo basi naomba sana mnitumie picha zake zo zote zile kupitia barua pepe ifuatayo: profesamatondo@gmail.com. Pia kama kuna mdau ambaye yuko Musoma/Serengeti na angependa kunisaidia kwenda kijijini Nata Serengeti kufuatilia picha basi naomba tuwasiliane. Nitalipia kila kitu.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Dkt. Masangu Matondo Nzuzullima
Chuo Kikuu cha Florida
(profesamatondo@gmail.com)

KUHUSU KITABU CHA KUMBUKUMBU YA DR. MEKACHA

Kitabu kinaitwa: “Studies in Bantu Linguistics and Languages: Papers in Memory of Dr. Rugatiri Mekacha”.
Ni mkusanyiko wa makala (16) nzuri za masuala ya lugha na isimu katika lugha za Kibantu. Makala hizi zimeandikwa na wanaisimu wenye umashuhuri duniani kote na tunatumaini kwamba kitabu hiki kitatoa mchango mkubwa katika kuzieleza na kuzifafanua lugha za Kibantu ambazo kusema kweli bado zinahitaji kufanyiwa uchambuzi wa kina wa kiisimu kulingana na nadharia za kisasa.
Lugha zilizochambuliwa katika kitabu hiki ni Kiswahili (makala mbili - moja imeandikwa kwa Kiswahili), Kisukuma (makala mbili), Kisetswana (makala mbili - Botswana na Afrika Kusini), Kikurya, Kichewa (Msumbiji na Malawi), Kilungu (Zambia), Kikhayo (Kenya), Kibemba (Zambia) na Kihaya. Pia kuna karatasi nne zinazojadili masuala mbalimbali ya lugha nchini Tanzania; ikiwemo sera mpya ya lugha ambayo inapendekeza kukifanya Kiingereza kuwa lugha ya kufundishia kuanzia shule za msingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Nakupongeza sana Prof. Matondo kwa kuonyesha moyo wa kukumbuka waliokusaidia na kukupa mwongozo hadi ukatimiza malengo yako. Nategemea hapa utapata watu watakaoweza kukusaidia kupata hizo picha ili uweze kumuezi huyu ndugu yetu.Hongera sana. Wako Mkulima wa Army.

    ReplyDelete
  2. I don't normally comment in here but right after reading this I got so touched and was compelled to!

    Dr. Matondo, well done man! Hongera sana kwa hatua hizi nzito na nyeti ulizopiga maishani mwako. I like the way you live and your whole general life style & culture. As a matter of fact, you are such an inspiration to the whole TZ diaspora and everyone else back home. Wewe na yule bwana mwingine huko US (Makulilo Jr) kwakweli mnanitia moyo vilivyo! Please keep it up, I like the whole positive attitude too - like I said - it's really inspiring! It reminds me of the current US presidents Campaign motto in 2008, "THIS IS OUR MOMENT". Naam, no matter how black we may be, no matter how "sukuma" we may be, this is definitely OUR moment! Well done brother and keep it up for all of us.

    You might not remember me coz it's been years since we parted, but I'm still a brother as always. We attended same Secondary School at Sengerema. I remember you as the most active member of our debating club (you and Godwin Simba Ngwillizi). Kama umesahau nitakukumbusha mambo ya SESESCO kidogo, unakumbuka "puto" aka bwalo la bondo :) na mwl. Mhembe je? (revolutionary).

    Mi niko hapa UK mzee ndo kwanza nachukua masters yangu. I know, i know, nimechelewa kweli mzee lakini nikaonelea bora uchelewe kuliko kutofika kabisa..lol. You can hit me back on this mail: survivordeny@hotmail.co.uk

    Well done again Masangu.

    ReplyDelete
  3. Huko alikokuwa anafundisha hawana picha yake?Au unataka za utotoni?

    ReplyDelete
  4. Napenda kumshukuru sana Mzee wa Libeneke kwa kuniwekea tangazo hili hapa. Tayari nimeshapata watu ambao wako tayari kunisaidia katika jambo hili. Asanteni nyote na tuendeleze huu moyo wa kusaidiana.

    Wewe mdau wa SESESCO tutawasiliana. Mdau wa mwisho - picha zake pale mlimani zilikuweko lakini kwa sasa "hazionekani". Nimeshajaribu kila mahali mkuu...

    ReplyDelete
  5. Jamani marehemu alikuwa rafiki yangu na mshauri wako wa karibu kwani hamkupiga picha pamoja miaka yote hiyo?

    ReplyDelete
  6. hongera sana kaka, nimefurahi kuona kuwa bado kuna wa" wenye shukrani ktk dunia hii. wewe mdau wa hapo juu huyo GODWIN SIMBA NGWILIMI na SIYO NGWILIZI.

    ReplyDelete
  7. yani wee mdau mtoa mada sikujui ila umenigusaa sana,,,unaonekana una roho njema na shukrani maana ni wanaume wachahce sana tena sana wa kufanana na roho yako..mwee

    lol

    ReplyDelete
  8. Asante mdau kwa kunikosoa. Najua kama surname yake ni "NGWILIMI" na si Ngwilizi. Ila hiyo ilikuwa ni typo error hivyo kumradhi (samahani) kwa Godwin na mdau yeyote aliyekwazika na hiyo typo.

    Ndiyo maana mimi siku zote hujitahidi kuwa mwangalifu sana na typos, kwani typo inaweza kusababisha misunderstanding kubwa kama si kupotosha maana nzima ya ujumbe kwa jamii, sema tu bahati mbaya this time hiyo sikuiona, so nimeona nichukue nafasi hii kuomba radhi.

    Godwin, kama huwa unapitia hii blog, na kama ukiona hii comment, pls naomba tuwasiliane kupitia e address niliyompatia Masangu hapo juu. Asante mkuu (au kama kuna mdau ana email yake basi naomba anisaidie please). Cheers.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...