(Reverend Douglas G. Whitlow 1951-2010)

Wadau, nasikitika kutangaza kifo cha mume wangu, Reverend Douglas G. Whitlow, kilichotokea nyumbani hapa Cambridge, Massachusetts leo asubuhi (January 18, 2010). Alikuwa na matatizo ya figo kwa muda mrefu.

Mipango ya mazishi ninafanya na nitawajulisha mara ikikamilika. Kwa habari zaidi mnaweza kuwasiliana na mimi:

Chemi Che-Mponda Whitlow

617-497-4353 /617-497-4353

au

Ezekiel Concord Luhigo

781-632-3605
NB: Kwa atakaye piga toka nje ya Marekani tafadhali weka namba namba ya mwito ya nchi +1 mwanzoni mwa tarakimu hizo kumi zilizotolewa.

------------------------------------------------

Kwa niaba ya wadau wote, Globu ya Jamii inatoa mkono wa rambirambi kwa Da'Chemi kwa msiba huu mzito. Ni vigumu kutoa maneno stahili kuelezea masikitiko yetu kikamilifu, ila tuna imani kwamba Mola atawapa wafiwa nguvu na imani kwamba kila alifanyalo Mungu halina makosa.
Pole sana Da'Chemi. Tunamwomba Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya hayati Mchungaji Withlow. AMINA
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. pole sana dada Chemi,
    bwana alitoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amen.

    ReplyDelete
  2. Poleni sana Dada Chemi-Chemponda katika wakati huu mgumu. M/Mungu atawapa faraja.

    ReplyDelete
  3. Pole sana Da' Chemi. Mungu akupe nguvu, uvumilivu na ukakamavu katika kipindi hiki kigumu. Ni Mungu aliyemleta mpendwa wako na ndiye aliyemchukua, jina lake lihimidiwe... Amen

    ReplyDelete
  4. pole sana kwa msiba mzito wa kupoteza mwenza wa maisha,
    may the reverend rest in peace, bwana ametoa, bwana ametwaa na jina la bwana libarikiwe
    AMINA

    ReplyDelete
  5. Mwenyezi Mungu akuongoze katika kipindi hiki kigumu, pole sana Dada Chemi

    ReplyDelete
  6. POle zenu wafiwa, Mungu na awape nguvu katika kipindi hiki kigumu. RIP Whitlow.

    ReplyDelete
  7. Dada Chemi pole kwa msiba huu mzito...

    ReplyDelete
  8. KELAND PRIMARY SCHOOLJanuary 19, 2010

    BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE

    ReplyDelete
  9. pole dada mungu akupiganie

    ReplyDelete
  10. Pole sana Da'Chemi. Hakika huu ni msiba mzito sana. Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  11. pole sana da Chemi,
    Mola awe mfariji wako.

    ReplyDelete
  12. Pole sana Chemi na tunamwomba Mwenyezi Mungu - muweza wa yote - akupe subra katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  13. Asanteni wote kwa walionipigia simu na kunitumia e-mail. Nitawajulisha mipango ya mazishi yakikamilika.

    ReplyDelete
  14. Pole sana dada kemi jamani mme wa kwanza MUNGU alimchukua na huyu tena,I CAN IMAGINE HOW SAD IT IS.

    ReplyDelete
  15. Pole Da Chemi - RIP shemeji

    ReplyDelete
  16. Pole sana Da Chemi,Mwenyenzi ailaze roho ya marehemu shemeji yetu mahali pema peponi Amen.

    ReplyDelete
  17. pole sana Da Chemi,
    kwa msiba huu mkubwa wa kuondekewa na mwenzio,mungu amlaze mahala pema peponi shemeji(RIP).
    wadau
    The Ngoma Africa Band aka FFU

    ReplyDelete
  18. Pole sana DA CHEMI kwa msiba huu ulikukuta.Tunamwomba Mwenyezi Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    mwenyezi mungu aipumzishe roho ya ndugu yetu mahala pema peponi.AMINA

    Tupo pamoja kwenye sala dada yangu

    ReplyDelete
  19. DADA CHEMI,
    POLE SANA KWAKO NA FAMILIA YAKO YOTE KATIKA WAKATI HUU MGUMU. TUNAKUWEKA MIKONONI MWA MUNGU AKUFUTE MACHOZI NA KUKUPA FARAJA.
    FAMILIA YANGU NA WANA CCM (UK)WAKO PAMOJA NAWE KWA SALA NA MAOMBI.

    MAINA ANG'IELA OWINO
    UK.

    ReplyDelete
  20. Pole na msiba Da Chemi. Mungu ailaze roho ya marehemu Reverend Whitlow mahala pema peponi.

    ReplyDelete
  21. Pole kwa msiba mzito, Mwenyezi Mungu akutie nguvu na roho wa ufariji.

    ReplyDelete
  22. pole sana Da Chiku.
    muumba amlaze pema shemeji yetu

    ReplyDelete
  23. Pole sana

    Kazi ya Mungu haina makosa.

    Mwenyezi awape subra.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  24. PLe sana Mrs Withlow , Mungu Amlaze mahali pema peponi Amina

    Hii habari ni wa kusikitisha ila imeniweza kutiririka vizuri na kukueleza kila unachotaka kujua kuhusu Marehemu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...