(Reverend Douglas G. Whitlow 1951-2010)Wadau, nasikitika kutangaza kifo cha mume wangu, Reverend Douglas G. Whitlow, kilichotokea nyumbani hapa Cambridge, Massachusetts leo asubuhi (January 18, 2010). Alikuwa na matatizo ya figo kwa muda mrefu.
Mipango ya mazishi ninafanya na nitawajulisha mara ikikamilika. Kwa habari zaidi mnaweza kuwasiliana na mimi:
Chemi Che-Mponda Whitlow
617-497-4353 /617-497-4353
au
Ezekiel Concord Luhigo
au
Ezekiel Concord Luhigo
781-632-3605
NB: Kwa atakaye piga toka nje ya Marekani tafadhali weka namba namba ya mwito ya nchi +1 mwanzoni mwa tarakimu hizo kumi zilizotolewa.
------------------------------------------------
Kwa niaba ya wadau wote, Globu ya Jamii inatoa mkono wa rambirambi kwa Da'Chemi kwa msiba huu mzito. Ni vigumu kutoa maneno stahili kuelezea masikitiko yetu kikamilifu, ila tuna imani kwamba Mola atawapa wafiwa nguvu na imani kwamba kila alifanyalo Mungu halina makosa.
Pole sana Da'Chemi. Tunamwomba Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya hayati Mchungaji Withlow. AMINA
-Michuzi


pole sana dada Chemi,
ReplyDeletebwana alitoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amen.
Poleni sana Dada Chemi-Chemponda katika wakati huu mgumu. M/Mungu atawapa faraja.
ReplyDeletepole we.
ReplyDeletePole sana Da' Chemi. Mungu akupe nguvu, uvumilivu na ukakamavu katika kipindi hiki kigumu. Ni Mungu aliyemleta mpendwa wako na ndiye aliyemchukua, jina lake lihimidiwe... Amen
ReplyDeletepole sana kwa msiba mzito wa kupoteza mwenza wa maisha,
ReplyDeletemay the reverend rest in peace, bwana ametoa, bwana ametwaa na jina la bwana libarikiwe
AMINA
Mwenyezi Mungu akuongoze katika kipindi hiki kigumu, pole sana Dada Chemi
ReplyDeletePOle zenu wafiwa, Mungu na awape nguvu katika kipindi hiki kigumu. RIP Whitlow.
ReplyDeleteDada Chemi pole kwa msiba huu mzito...
ReplyDeleteBWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE
ReplyDeletepole dada mungu akupiganie
ReplyDeletePole sana Da'Chemi. Hakika huu ni msiba mzito sana. Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeletepole sana da Chemi,
ReplyDeleteMola awe mfariji wako.
Pole sana Chemi na tunamwomba Mwenyezi Mungu - muweza wa yote - akupe subra katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeletePole sana da'Chemi.
ReplyDeleteAsanteni wote kwa walionipigia simu na kunitumia e-mail. Nitawajulisha mipango ya mazishi yakikamilika.
ReplyDeletePole sana dada kemi jamani mme wa kwanza MUNGU alimchukua na huyu tena,I CAN IMAGINE HOW SAD IT IS.
ReplyDeletePole Da Chemi - RIP shemeji
ReplyDeletePole sana Da Chemi,Mwenyenzi ailaze roho ya marehemu shemeji yetu mahali pema peponi Amen.
ReplyDeletepole sana Da Chemi,
ReplyDeletekwa msiba huu mkubwa wa kuondekewa na mwenzio,mungu amlaze mahala pema peponi shemeji(RIP).
wadau
The Ngoma Africa Band aka FFU
Pole sana DA CHEMI kwa msiba huu ulikukuta.Tunamwomba Mwenyezi Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeletemwenyezi mungu aipumzishe roho ya ndugu yetu mahala pema peponi.AMINA
Tupo pamoja kwenye sala dada yangu
DADA CHEMI,
ReplyDeletePOLE SANA KWAKO NA FAMILIA YAKO YOTE KATIKA WAKATI HUU MGUMU. TUNAKUWEKA MIKONONI MWA MUNGU AKUFUTE MACHOZI NA KUKUPA FARAJA.
FAMILIA YANGU NA WANA CCM (UK)WAKO PAMOJA NAWE KWA SALA NA MAOMBI.
MAINA ANG'IELA OWINO
UK.
Pole na msiba Da Chemi. Mungu ailaze roho ya marehemu Reverend Whitlow mahala pema peponi.
ReplyDeletePole kwa msiba mzito, Mwenyezi Mungu akutie nguvu na roho wa ufariji.
ReplyDeletepole sana Da Chiku.
ReplyDeletemuumba amlaze pema shemeji yetu
Pole sana
ReplyDeleteKazi ya Mungu haina makosa.
Mwenyezi awape subra.
(US Blogger)
PLe sana Mrs Withlow , Mungu Amlaze mahali pema peponi Amina
ReplyDeleteHii habari ni wa kusikitisha ila imeniweza kutiririka vizuri na kukueleza kila unachotaka kujua kuhusu Marehemu.
R.I.P.
ReplyDelete