FFU wa Ngoma Africa band wapakua mpya za mwaka 2010
*Kuna "Bongo Tambarale" pia wameipua jikoni "SUPU YA MAWE"

Na Ripota wa Globu ya Jamii, Ughaibuni

The Ngoma Africa Band aka FFU wa Ughaibuni a.k.a Wazee wa kukaanga mbuyu wameustua ulimwengu kwa kupakua nyimbo mpya ambazo zinasemekana ni moto wa kuotea mbali.

Nyimbo hizo ni pamoja na "Bongo Tambarale" wimbo huu ni pendekezo lake Ankal, ambaye alitoa kitandawili kwa FFU wa Ngoma Africa, Je, Bongo Tambarale kweli au Wizi mtupu?

FFU nao wamjibu kwa njia ya gwaride lao "Bongo dansi" na kupakua kitu kipya kilichobeba jina la "BONGO TAMBARALE"

Laini kama kawaida yao nao wamepika "SUPU YA MAWE" utunzi wake kamanda wa kikosi iko Ebrahim Makunja aka Ras makunja akiimba pamoja na Soloist Chris-B.

"Supu ya Mawe" imepikwa kwa kuni za viungu na viungo vya Chumvi ya mawe, izari ya mawe, yama za mawe, ila kiungoni mawe matupu unaambiwa!

Ras makunja alidokeza mtandao wa jamii kuwa wimbo huu "Supu ya Mawe" ukinywa utapata vitamini ya nguvu za mawe una ujumbe kuwa "Maisha yataka uvumilivu" ni sawa na kupika "Supu ya Mawe" ambayo inachukua mda kuivya!

Maisha yataka uvumilivu ni sawa na kunywa "Supu ya Mawe" kunywa kwa papara ni hatari tupu! Sadaka ya "Supu ya Mawe" itawafikia watu wote.Nyimbo hizo "Supu ya Mawe" , "Bongo Tambarale" zitaongozana na kuelekea redioni wakati wowote kuanzia sasa!


Pia nyimbo kama "Furaha ya maisha iko wapi?" "Baba wa kambo" itaongozana na nyimbo mpya "Kizabi zabina" (si mtu mwema) nazo zitaongozana katika vituo mbali mbali vya redio hili kukupa raha kuwapa raha washabiki na wadau ambao ndio wamiliki wa bendi,wanamziki ni watumishi tu.

Dekshia mwenyewe hapa:

http://www.myspace.com/thengomaafrica

pia unaweza kuwasiliana na FFU wa The Ngoma Africa band thru: ngoma4U@googlemail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. jamaa walitulia,hapa wamestarabika kidogo, inelekea walikuwa mapuziko,maana naona watoto wenyewe wa mbwa mwitu walikuwa wamepumzika

    ReplyDelete
  2. du! vichaa wazee wa kukaangaga mbuyu,mko wapi?vichaa mbona kimya kama miezi 2 sasa

    ReplyDelete
  3. michu michu wacha hizo mwanangu sasa ughaibuni wapi huku hawa wazee wazima wanatubuiza ili niende, tutafanuliye mwanangu wee na acha usaini huu wa kibitoz toa maelezo kamili sawa mwanangu.

    mdau wa new york, newalaaa.

    ReplyDelete
  4. unajua ngoma afrika mara nyingine wanakuwa wastarabu,hila sema tu kuna watu wapenda kila wakati kusikia vichaa wetu aka watoto wa mbwa mwitu wanabwaka,jamani ujerumani kuna barafu wacheni vichaa wapumue

    ReplyDelete
  5. kaka kamanda ras makunja,sasa hii supu ya mawe? mbona unaleta baraha?supu ya mawe,tutakunywa vipi?

    ReplyDelete
  6. sasa machizi wetu,hii supu yenu ya mawe,naona ni hatari tupu.unaweza mtu kung'oa meno au ikakukwama kooni? harafu tukisema kuwa nyinyi
    mmefyatuka kichwani,mnadai kuwa mnachokozwa

    ReplyDelete
  7. Duh mimi jukwaani tu hapo. pametuliiiia. si mchezo.
    Mdau wa pajazzz+titizzz

    ReplyDelete
  8. kasheshe bongo tambarale? mmmmm kweli tambarale na maisha yenyewe kama wanavyoidai wakali hawa,yataka uvumilivu kama vile unakunywa supu ya mawe

    ReplyDelete
  9. kaka braza makunja jamani hii supu ya mawe sasa mtu atakunywa vipi?
    kama si ukurofi kimziki.
    Mdau Stockholm

    ReplyDelete
  10. Naomba kuliza,utamu wa supu ya mawe ukoje?

    ReplyDelete
  11. Palitulia barazani hapa sasa ffu watoto wa mbwa wameshaingia,milio na kelele za ajabu zitasikika sasa hivi.
    Hebu nijiondoe
    mstarabu UK.ukerewe

    ReplyDelete
  12. Ras?sasa hii supu ya mawe nije bakuli la shaba au kibuyu,maana unywaji wake?kamanda hili si baraha jipya unalianza?mwanzoni mwaka tu.
    aya tutafika kwa tabia zako hizi za kutisha wenzio

    ReplyDelete
  13. IPR Royalty ya Dube itakula kwako

    ReplyDelete
  14. maisha kweli yataka uvumilivu supu ya mawe,supu ya mawe tunaingojea

    ReplyDelete
  15. du umenikumbusha mbali sana, nikiwa kwenye basi naelekea moshi. big up wachaga

    ReplyDelete
  16. bongo tambarale kulamba maelfu ya vichwa bongo? mie naingojea supu ya mawe,sitaki tena vipapatio wa vipaja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...