FFU wa Ngoma Africa band wapakua mpya za mwaka 2010
*Kuna "Bongo Tambarale" pia wameipua jikoni "SUPU YA MAWE"
Na Ripota wa Globu ya Jamii, Ughaibuni
The Ngoma Africa Band aka FFU wa Ughaibuni a.k.a Wazee wa kukaanga mbuyu wameustua ulimwengu kwa kupakua nyimbo mpya ambazo zinasemekana ni moto wa kuotea mbali.
Nyimbo hizo ni pamoja na "Bongo Tambarale" wimbo huu ni pendekezo lake Ankal, ambaye alitoa kitandawili kwa FFU wa Ngoma Africa, Je, Bongo Tambarale kweli au Wizi mtupu?
FFU nao wamjibu kwa njia ya gwaride lao "Bongo dansi" na kupakua kitu kipya kilichobeba jina la "BONGO TAMBARALE"
Laini kama kawaida yao nao wamepika "SUPU YA MAWE" utunzi wake kamanda wa kikosi iko Ebrahim Makunja aka Ras makunja akiimba pamoja na Soloist Chris-B.
"Supu ya Mawe" imepikwa kwa kuni za viungu na viungo vya Chumvi ya mawe, izari ya mawe, yama za mawe, ila kiungoni mawe matupu unaambiwa!
Ras makunja alidokeza mtandao wa jamii kuwa wimbo huu "Supu ya Mawe" ukinywa utapata vitamini ya nguvu za mawe una ujumbe kuwa "Maisha yataka uvumilivu" ni sawa na kupika "Supu ya Mawe" ambayo inachukua mda kuivya!
Maisha yataka uvumilivu ni sawa na kunywa "Supu ya Mawe" kunywa kwa papara ni hatari tupu! Sadaka ya "Supu ya Mawe" itawafikia watu wote.Nyimbo hizo "Supu ya Mawe" , "Bongo Tambarale" zitaongozana na kuelekea redioni wakati wowote kuanzia sasa!
Pia nyimbo kama "Furaha ya maisha iko wapi?" "Baba wa kambo" itaongozana na nyimbo mpya "Kizabi zabina" (si mtu mwema) nazo zitaongozana katika vituo mbali mbali vya redio hili kukupa raha kuwapa raha washabiki na wadau ambao ndio wamiliki wa bendi,wanamziki ni watumishi tu.
Dekshia mwenyewe hapa:
http://www.myspace.com/thengomaafrica
pia unaweza kuwasiliana na FFU wa The Ngoma Africa band thru: ngoma4U@googlemail.com


jamaa walitulia,hapa wamestarabika kidogo, inelekea walikuwa mapuziko,maana naona watoto wenyewe wa mbwa mwitu walikuwa wamepumzika
ReplyDeletedu! vichaa wazee wa kukaangaga mbuyu,mko wapi?vichaa mbona kimya kama miezi 2 sasa
ReplyDeletemichu michu wacha hizo mwanangu sasa ughaibuni wapi huku hawa wazee wazima wanatubuiza ili niende, tutafanuliye mwanangu wee na acha usaini huu wa kibitoz toa maelezo kamili sawa mwanangu.
ReplyDeletemdau wa new york, newalaaa.
unajua ngoma afrika mara nyingine wanakuwa wastarabu,hila sema tu kuna watu wapenda kila wakati kusikia vichaa wetu aka watoto wa mbwa mwitu wanabwaka,jamani ujerumani kuna barafu wacheni vichaa wapumue
ReplyDeletekaka kamanda ras makunja,sasa hii supu ya mawe? mbona unaleta baraha?supu ya mawe,tutakunywa vipi?
ReplyDeletesasa machizi wetu,hii supu yenu ya mawe,naona ni hatari tupu.unaweza mtu kung'oa meno au ikakukwama kooni? harafu tukisema kuwa nyinyi
ReplyDeletemmefyatuka kichwani,mnadai kuwa mnachokozwa
Duh mimi jukwaani tu hapo. pametuliiiia. si mchezo.
ReplyDeleteMdau wa pajazzz+titizzz
kasheshe bongo tambarale? mmmmm kweli tambarale na maisha yenyewe kama wanavyoidai wakali hawa,yataka uvumilivu kama vile unakunywa supu ya mawe
ReplyDeletekaka braza makunja jamani hii supu ya mawe sasa mtu atakunywa vipi?
ReplyDeletekama si ukurofi kimziki.
Mdau Stockholm
Naomba kuliza,utamu wa supu ya mawe ukoje?
ReplyDeletePalitulia barazani hapa sasa ffu watoto wa mbwa wameshaingia,milio na kelele za ajabu zitasikika sasa hivi.
ReplyDeleteHebu nijiondoe
mstarabu UK.ukerewe
Ras?sasa hii supu ya mawe nije bakuli la shaba au kibuyu,maana unywaji wake?kamanda hili si baraha jipya unalianza?mwanzoni mwaka tu.
ReplyDeleteaya tutafika kwa tabia zako hizi za kutisha wenzio
IPR Royalty ya Dube itakula kwako
ReplyDeletemaisha kweli yataka uvumilivu supu ya mawe,supu ya mawe tunaingojea
ReplyDeletedu umenikumbusha mbali sana, nikiwa kwenye basi naelekea moshi. big up wachaga
ReplyDeletebongo tambarale kulamba maelfu ya vichwa bongo? mie naingojea supu ya mawe,sitaki tena vipapatio wa vipaja
ReplyDelete