Mkuu wa blog ya jamii leo nilikuwa nataka kuzungumzia hii kitengo cha akili muhimbili ambacho ndio tegemeo kubwa kwa jiji la Lukuvi(Dar) lakini pamesahaurika kwa muda mrefu sana na wahusika wanajifanya kama hawausiki sasa uncle michuzi ukiweka kwenye blog hii ya jamii hata wale wakubwa wao wanapita hapa na wataona habari hii.
Kwa jinsi jiji la dar lilivyo kubwa na wodi ya wagonjwa wa akili iko hiyo tu muhimbili na imekuwa na wagonjwa wengi kuliko uwezo wake na vitendea kazi kama wodi za wanaume na wanawake ni vichekesho kwa kweli na hata idadi ya manesi na wataalam wa akili pale wanafanya kazi ya ziada na wahusika wamesahau umuhimu wa kitengo kile.

Mambo ambayo nilikuwa naomba wahusika waweze kuyatilia kipaumbele ni ubora wa majengo kama sio mengine hata rangi basi ipigwe kila baada ya muda fulani na ukija kwenye wauguzi idadi yao ni ndogo sana na wanahitajika wengi kuweza kukidhi mahitaji ya wagonjwa,ulinzi kwenye hii wodi ni hafifu sana kiasi wagonjwa wanatoloka na kama inavyojulikana mgonjwa wa akili ni hatari akiwa nje bila kupona
Kwa yale makampuni makubwa kama vodacom,zain,Tigo,Bp,Ipp na mengine mengi ya hapo nyumbani walio mstari wa mbele ktk kusaidia jamii hii sehemu imesaulika sana na tunaomba wakiweza wapitishe msaada wao mara moja au mbili kwa mwaka na watakuwa wamesaidia sana wagonjwa husika.
Nimeambatanisha na picha za kitengo cha akili muhimbili na picha ya kwanza ni jengo lenyewe sehemu ya kuingilia na milango yake naona toka enzi ya mkoloni,ya pili ni sehemu ilipaswa kuwa bustani lakini ni bora wagepatengeneza maana siku za kliniki panakuwa na watu wengi kama uko sokoni vile na inakuwa sio pazuri hata kidogo
Picha ya tatu ni jengo lenyewe tena kwa nje mbele na ya nne ni sehemu ya mapokezi na jinsi panavyofungwa kwa kukosa ulinzi mzuri.Wahusika jaribuni kuwajali wagonjwa wa akili na sio kusahau huduma hii ni muhimu kwa jamii.
Ni hayo tu mkuu na wadau waweze kuona hali halisi ya milembe ya dar.
Mdau wa Libeneke




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Pamoja na kwamba hapo panahitaji marekebisho ili kuborehswa. Niliona maajabu makubwa pale hospital ya Ocean Road ambapo panatolewa matibabu ya bure. Kuna choo kimoja tu ambacho kinatakiwa kutumiwa na wanawake na wanaume humo ndani ya choo kuna choo cha kukaa na kuchuchumaa na hata huwezi kuvuta maji mabomba baada ya kutumia mabomba yameharibika. Kwa kweli kiafya hapafai kabisa. Ule upande wa kulipia una vyoo lakini wewe uliyekuja kwa bure huruhusiwi kwenda.

    ReplyDelete
  2. Hayo majengo yamenikumbusha mbali sana,kipindi nilichokuwa namsindikiza rafiki yangu clinic,
    Ni kweli mdau hayo majengo yanatakiwa yaboreshwe zaidi

    ReplyDelete
  3. Kweli ni majengo ya watu wasiokuwa na akili yenyewe yatakuwaje na akili?
    Nantombe

    ReplyDelete
  4. hahah kwa sirikali ya bongo haya majengo ni brand new hayapo ktk bajeti ya bunge kabisa lol

    ReplyDelete
  5. kuna wodi ya mapokezi yaani mgonjwa akifika tu ndio anaanzia huko ukiona mdau utazimia watu wanafungwa kamba kama mbwa na iwe jua iwe mvua hao watu wako hivyo na mwaka jana wamekufa watu wawili kisa akijuliakni ila joto la daa mtu unawezaje kumfunga masaa yaote 24 bila kufunguliwa??na vyoo ni balaa tupu.

    ReplyDelete
  6. Baba SangaraJanuary 26, 2010

    Ni Kweli marekebisho makubwa yanatakiwa hapo.. Kwa mtazamo wangu shida sio wakurugenzi wa Hospitali... Shida ni mtazamo wetu watanzania kuzingatia mgonjwa ya akili.. Tukikutana na mtu ambaye "kachanganikiwa" mtazamo wetu ni " jamaa 'kachizi'", "kazidisha bangi", "katenda mabaya huyo 'karogwa'" na kadhalika... Kwa sababu ya mtazamo wetu huo wa kiujumla tunashindwa kuamini au kukubali kwamba ugonjwa wa akili ni kama malaria, TB nk...Tunakataa kukubali kwamba mgonjwa wa akili hakuutaka au kuuchagua ugonjwa huo... Tunajidanganya kwamba sisi hatuwezi kupata madhara hayo..

    Majengo hayo yatabaki hivyo hivyo mpaka siku tatakubali kwamba na sisi tunweza kukabiliwa na madhara ya ugonjwa wa akili na tunweza kulazwa kwenye wodi hizo!

    Kwani ugonjwa wa akili unaua?

    ReplyDelete
  7. Ukisema wahusika watakwambia serikali ina mambo mengi sana, hii sababu ni sawa na mzazi anayelalamikia idadi kubwa ya watoto wake! Uza wengine kama wamekushinda!! Ila wadau mi naona swala la uzalendo hakuna kabisa nchini na hivi karibuni jinsi serikali ilivyo salim amri kwa mafisadi ndio inakatisha tamaaaaaa!

    ReplyDelete
  8. Wodi zenyewe hazina hewa ya kutosha. Ndugu yangu alilazwa pale December, alitokwa vipele vya joto mwili mzima. Hata kama ni vichaa, wanastahili kukaa sehemu yenye hewa ya kutosha ukizingatia hawawekewi feni.

    ReplyDelete
  9. Poleni watanzania ,lakini haya ni
    makosa yenu kuchagua viongozi wanaotibiwa nje ya nchi,lakini kura zao zinatoka kwenu,wala msilalamike kabisa.Wazungu hutuambia kweli sisi tu waoga kujaribu kitu kipya, tumezoea mazoea,tutakufa na kauli ya amani na utulivu wakati wanaosema hizo kauli wanaishi peponi kwa kura zenu.

    ReplyDelete
  10. hii ni moja yA sehemu muhimu dsana katika hospitali ya muhimbili,vijana wengi wamepitia hapa.kjutokana na dunia ya sasa vijana wengi wanachanganyikia kutokana na madala ya kulevya na maisha.serikali inatakiwa iwekeze sehemu kama hizi,sio kutegemea hospitali za watu binafsi kama lutindi.

    ReplyDelete
  11. Hili ni gereza au hospitali?

    ReplyDelete
  12. It all boils down to priorities! The same government that doesn’t see the need to refurbish that psychiatric ward has spent more than 2.7 billions shillings to build Mheshimiwa Governor's house. This is really sad....

    ReplyDelete
  13. HAYA NI MAMBO YA KUTOKUJALI KURAAAA YAKO....JALI KURA YAKO KAMA UNVYOJALI UKIMWI....

    ReplyDelete
  14. anony Tue Jan 26, 06:21:00 PM,... more than 2.7 billions shillings to build Mheshimiwa Governor's house maana yake nini? hata kama hatujuwi kizungu lakini tuheshimiane. 1.2 sio sawa na 2.7, punguza chumvi.

    ReplyDelete
  15. MI naona hapa tupaite MAGONJWA PRODUCTION si hospitali

    ReplyDelete
  16. Ushauri wa bure, siku moja tukamate viongozi baadhi tuwafungie humo siku mbili basi wakitoka watashika adabu yao

    ReplyDelete
  17. Anony Tue Jan 26, 08:43 PM, The government built two mansions for his excellency governor and his deputy ...The former cost 1.5 billion while the latter cost 1.2. I hope you can put two and two t'gether.

    ReplyDelete
  18. sasa nyie annons mnaokazana kum"sahihisha"kiinglish mzalendo eti kakosea tu bei 2.5 mna maana gani?
    sii ujumbe umefika billions spent to built 2 houses for governors while important things like this ward (to mention few) are left untouched

    hapo bado hatujataja wanafunzi wanaosomea chini ya miembe,upungufu wa madawa/vitendea kazi hospitalini,mitaro,mishahara ya wafanyakazi (asa waalimu) nk nk

    this is bullshit

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...