



Nimeambatanisha na picha za kitengo cha akili muhimbili na picha ya kwanza ni jengo lenyewe sehemu ya kuingilia na milango yake naona toka enzi ya mkoloni,ya pili ni sehemu ilipaswa kuwa bustani lakini ni bora wagepatengeneza maana siku za kliniki panakuwa na watu wengi kama uko sokoni vile na inakuwa sio pazuri hata kidogo

Ni hayo tu mkuu na wadau waweze kuona hali halisi ya milembe ya dar.
Mdau wa Libeneke
Pamoja na kwamba hapo panahitaji marekebisho ili kuborehswa. Niliona maajabu makubwa pale hospital ya Ocean Road ambapo panatolewa matibabu ya bure. Kuna choo kimoja tu ambacho kinatakiwa kutumiwa na wanawake na wanaume humo ndani ya choo kuna choo cha kukaa na kuchuchumaa na hata huwezi kuvuta maji mabomba baada ya kutumia mabomba yameharibika. Kwa kweli kiafya hapafai kabisa. Ule upande wa kulipia una vyoo lakini wewe uliyekuja kwa bure huruhusiwi kwenda.
ReplyDeleteHayo majengo yamenikumbusha mbali sana,kipindi nilichokuwa namsindikiza rafiki yangu clinic,
ReplyDeleteNi kweli mdau hayo majengo yanatakiwa yaboreshwe zaidi
Kweli ni majengo ya watu wasiokuwa na akili yenyewe yatakuwaje na akili?
ReplyDeleteNantombe
hahah kwa sirikali ya bongo haya majengo ni brand new hayapo ktk bajeti ya bunge kabisa lol
ReplyDeletekuna wodi ya mapokezi yaani mgonjwa akifika tu ndio anaanzia huko ukiona mdau utazimia watu wanafungwa kamba kama mbwa na iwe jua iwe mvua hao watu wako hivyo na mwaka jana wamekufa watu wawili kisa akijuliakni ila joto la daa mtu unawezaje kumfunga masaa yaote 24 bila kufunguliwa??na vyoo ni balaa tupu.
ReplyDeleteNi Kweli marekebisho makubwa yanatakiwa hapo.. Kwa mtazamo wangu shida sio wakurugenzi wa Hospitali... Shida ni mtazamo wetu watanzania kuzingatia mgonjwa ya akili.. Tukikutana na mtu ambaye "kachanganikiwa" mtazamo wetu ni " jamaa 'kachizi'", "kazidisha bangi", "katenda mabaya huyo 'karogwa'" na kadhalika... Kwa sababu ya mtazamo wetu huo wa kiujumla tunashindwa kuamini au kukubali kwamba ugonjwa wa akili ni kama malaria, TB nk...Tunakataa kukubali kwamba mgonjwa wa akili hakuutaka au kuuchagua ugonjwa huo... Tunajidanganya kwamba sisi hatuwezi kupata madhara hayo..
ReplyDeleteMajengo hayo yatabaki hivyo hivyo mpaka siku tatakubali kwamba na sisi tunweza kukabiliwa na madhara ya ugonjwa wa akili na tunweza kulazwa kwenye wodi hizo!
Kwani ugonjwa wa akili unaua?
Ukisema wahusika watakwambia serikali ina mambo mengi sana, hii sababu ni sawa na mzazi anayelalamikia idadi kubwa ya watoto wake! Uza wengine kama wamekushinda!! Ila wadau mi naona swala la uzalendo hakuna kabisa nchini na hivi karibuni jinsi serikali ilivyo salim amri kwa mafisadi ndio inakatisha tamaaaaaa!
ReplyDeleteWodi zenyewe hazina hewa ya kutosha. Ndugu yangu alilazwa pale December, alitokwa vipele vya joto mwili mzima. Hata kama ni vichaa, wanastahili kukaa sehemu yenye hewa ya kutosha ukizingatia hawawekewi feni.
ReplyDeletePoleni watanzania ,lakini haya ni
ReplyDeletemakosa yenu kuchagua viongozi wanaotibiwa nje ya nchi,lakini kura zao zinatoka kwenu,wala msilalamike kabisa.Wazungu hutuambia kweli sisi tu waoga kujaribu kitu kipya, tumezoea mazoea,tutakufa na kauli ya amani na utulivu wakati wanaosema hizo kauli wanaishi peponi kwa kura zenu.
hii ni moja yA sehemu muhimu dsana katika hospitali ya muhimbili,vijana wengi wamepitia hapa.kjutokana na dunia ya sasa vijana wengi wanachanganyikia kutokana na madala ya kulevya na maisha.serikali inatakiwa iwekeze sehemu kama hizi,sio kutegemea hospitali za watu binafsi kama lutindi.
ReplyDeleteHili ni gereza au hospitali?
ReplyDeleteIt all boils down to priorities! The same government that doesn’t see the need to refurbish that psychiatric ward has spent more than 2.7 billions shillings to build Mheshimiwa Governor's house. This is really sad....
ReplyDeleteHAYA NI MAMBO YA KUTOKUJALI KURAAAA YAKO....JALI KURA YAKO KAMA UNVYOJALI UKIMWI....
ReplyDeleteanony Tue Jan 26, 06:21:00 PM,... more than 2.7 billions shillings to build Mheshimiwa Governor's house maana yake nini? hata kama hatujuwi kizungu lakini tuheshimiane. 1.2 sio sawa na 2.7, punguza chumvi.
ReplyDeleteMI naona hapa tupaite MAGONJWA PRODUCTION si hospitali
ReplyDeleteUshauri wa bure, siku moja tukamate viongozi baadhi tuwafungie humo siku mbili basi wakitoka watashika adabu yao
ReplyDeleteAnony Tue Jan 26, 08:43 PM, The government built two mansions for his excellency governor and his deputy ...The former cost 1.5 billion while the latter cost 1.2. I hope you can put two and two t'gether.
ReplyDeletesasa nyie annons mnaokazana kum"sahihisha"kiinglish mzalendo eti kakosea tu bei 2.5 mna maana gani?
ReplyDeletesii ujumbe umefika billions spent to built 2 houses for governors while important things like this ward (to mention few) are left untouched
hapo bado hatujataja wanafunzi wanaosomea chini ya miembe,upungufu wa madawa/vitendea kazi hospitalini,mitaro,mishahara ya wafanyakazi (asa waalimu) nk nk
this is bullshit