Heri ya mwaka mpya!!
Bwana michuzi hapa kuna uvumi kuwa bwana mdogo mr Blue kachapwa risasi jana usiku kwenye mkesha wa mwaka mpya.
Mimi nikiwa kama mdau wa blog ya jamii nimejaribu kuingia na kufatilia hii habari nimekuta bado hujaturushia, sasa siamini sana na mimi naiamini blog yangu hii ya issamichuzi!!
Hebu tuweke wazi na kama ilikuwa bado jaribu kufatilia ili utunyetishe wadau kama kulia tulie na pole tukatoe
Mdau MS
-------------------------------
Mdau MS na wengine wote.
Globu ya Jamii imepata tetesi hizo, tena sio kuwa ilitokea usiku wa mkesha bali mapema mchana, na katika kufuatilia kila uchochoro tumekuta hola. Hivyo ukiona kimya ujue hakijalia. Kama ni kweli kipo kitalia tu.
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Bongo kama New York!

    Dogo kama ni kweli pole sana Mungu akunusuru, na kama ni uongo jihadhari sana ndugu yangu, usikute ni information zimeleak, pengine ni kweli kuna mijitu inakukia timing. Maana kuna waja wana roho mbaya utadhani majululi.

    Wimbo wa 50 Cent wa 'many men' (wish death upon me), usindikize huu wosia wangu. Kuwa makini sana dogo.

    ReplyDelete
  2. Hahahaha Michuzi kwahiyo unataka Kilieee? hahahaha Michuzi misemo yako bwana ya Vijana umenifurahisha leo 2010 nimecheka yak wanza ya kutype. Pazi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...