Naibu Katibu Mkuu wa UN akitoa heshima zake mbele ya picha ya Mzee Rashidi Mfaume Kawawa mara baada ya kusaini salamu za rambirambia kwa niaba ya Katibu Mkuu wa UN na pia akasaini kwa niaba yake Mwenyewe kama Naibu Katibu Mkuu.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon katika salamu zake amesema, historia ya Tanzania haiwezi kukamilika bila ya kutajwa kwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa, kiongozi ambaye kwa kushirikiana na Baba wa Taifa, Mwaliku J.K. Nyerere waliogoza mchakato wa kudai uhuru wa Tanganyika, akalijenga taifa la Tanzania lenye umoja, amani na maendeleo, akalitumikia taifa lake kwa uadilifu na uaminifu, huku akitoa mchango mkubwa wa ujenzi wa misingi imara ya uzalendo, utaifa na mchikamano misingi ambayo inaifanya Tanzania kuwa hivi ilivyo, alikuwa mnyenyekevu, mkweli na aliishi maisha ya mwanasiasa aliyejitolea maisha yake kulitumikia taifa la Tanzania na watanzania.
Naibu Katibu Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa mataifa, mara baada ya kutia saini kitambu cha maombolezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nawaona wadau Omari Mjenga na Helen Maduhu. Nimefurahi kuwaona jamani kweli kusoma kuzuri!

    ReplyDelete
  2. Mbona wote ni watu wa Tanganyika? Ivi hakuna hata mzenji mmoja ambae ana sifa za kupata kazi hizi?au ndio wawakilishi wa Tanganyika na sio Tanzania?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...