Seehemu ya wanafunzi chuo kikuu cha Osmania katika mgomo
Hyderabad India,
Vurugu zinazoendeshwa na wanafunzi wa vyuo vikuu katika kile kinachoelezwa kuwa ni kuishinikiza serikali kuu ya nchi hii iweke ukomo wa muda(deadline) katika mchakato wa kuanzisha serikali mpya ya Telengana, zimechukua sura mpya baada ya wanafunzi kugomea mitihani yao ya mwisho na hatimaye kuzichanachana karatasi za mitihani walizogawiwa.

Wanafunzi hao wanaoungwa mkono na wanasiasa wamekuwa katika mgomo wa kuingia madarasani tangu December 2, mwaka jana.

Katika hali ya kukata tamaa, uongozi wa chuo kikuu cha Osmania ulionya kuhusu uwezekano wa kufutwa kwa mwaka wa masomo endapo wanafunzi wataendela kugomea mitihani mapema mwezi December mwaka 2009.

Jitihada kubwa za uongozi wa chuo kuwashawishi wanafunzi hao kufanya mitihani, zikiongozwa na principal wa Art College (Osmania University) Zimegonga mwamba.

Chanzo cha mgogoro huu mkubwa, ni kutotekelezwa kwa makubaliano ya mwaka 1956 yaliyozaa State ya Andra Pradesh inayojumuisha mikoa miwili ya Andra na Telangana, ndani ya India Huru.

Jambo hilo lilisababisha balaa kubwa mwaka 1969 pale wanafunzi katika chuo kikuu cha Osmania walipogoma wakiungwa mkono na vyama vya siasa, na wananchi wengi wanaotokea katika eneo la Telangana. Katika vurugu hizo, wanafunzi zaidi ya 200 walipoteza maisha yao kwa kupigwa na polisi au kujiua.

Mgomo wa sasa ulianza pale kiongozi maarufu wa upinzani Chandrasekhar Rao, alipoamua kufunga kula na kunywa hadi afe, ili mradi tu Telengana haikunziashwa kama State inayojitegema.


Katika hali iliyotarajiwa na wengi, kufunga kwa mzee huyu kulipokewa na wanafunzi wa Osmania na baadaye vyuo viku vyote hapa Hyderabad, kama vile mtu aliyeanzisha wimbo uliokuwa ukisuburiwa kwa hamu kubwa harusini.

Kilichofuatia ni kusigana kwingi kisiasa kati ya uongozi wa State na Serikali kuu ya Delhi. Jambo hilo kwa hakika limekuwa mtihani mkubwa kwa wanafunzi wa kigeni tunaosoma hapa.

Kutokana na sababu za mazoea ya Serikari kuu kusahaulisha, nia inayoonyeshwa na wanafunzi na wanasiasa walio nyuma yao na historia nzima ya mgogoro huu.

Uongozi wa Serikali ya hapa, na ICCR (Idara ya serikali ya India inayoshughurikia scholarship) wamebakia kimya hata pale tunapowauliza kuhusu majaaliwa ya wanafunzi wa kigeni tuliopo hapa.

Nchi kadhaa zenye wanafunzi wengi hapa Hyderabad zimeanzisha mchakato wa kuwahamishia wanafunzi wao katika state nyingine ili kuwaepusha na hasara kubwa na athari kubwa za kitaaluma na kisaikolojia zitakazotokana na kuahirishwa kwa mwaka wa masomo.

Tunaiomba serikali yetu pia, kwa kushirikiana na ubalozi wake hapa India, ianzishe mazungumzo kama hayo, ambayo kwa hakika yanaweza kuwaokoa wanafunzi zaidi ya 200 wanaosoma hapa hapa katika balaa hili.

Lugamba, T. A
Lugamba2001@yahoo.co.uk.
University College of Engineering
Osmania University
Hyderabd,
Andra Prandesh,
India
Tel: +919160412755
-----------------------
NOTE: Kusoma taarifa
za sakata la Osmania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. tuna shukuru sana ankal hila tusaidie kutoa tu hiyo namba ya simu basi maana usumbufu utakuwa mwingi sana tunaomba ushirikiano wako ankal lugamba

    ReplyDelete
  2. Hali ni mbaya kwa kweli maana fikiria leo ilitakiwa mitihani ya semester ifanyike lakini imeshindikana,wanfunzi wamekataa kufanya mitihani na badala yake baadhi walianza kuchana karatasi za mitihani

    Hawa Watelugu hawafai hata kidogo,wapumbavu sana yaani...yaaani leo nimemshuhudia mwanafunzi mmoja kajinyonga hapa main campus kisa anapinga mitihani,mwingine kajimwagia petroli na kujilipua eti kisa anapinga mtihani usifanyike,inakera sana..Kwa kweli leo hali ilikuwa mbaya sana main Campus na Nizam college

    Wanafunzi wa main Campus hatujui hatima yetu ni ipi maana kuna hatari tukaupoteza mwaka wa masomo hivi hivi tukiona...Serikali ya AP nao wako kimya,mabwege sana yaani...Ni vema OU wakaangalia ni jinsi gani wakatusaidia sisi foreign students,hayo mambo ya Telangana ni ya Watelugu,sisi foreigners hayatuhusu kabisa

    Mdau wa OU,University College of Law,Main Campus

    ReplyDelete
  3. Jifunze Kiswahili safi ingawa umejitahidi. Kwenye Kiswahili hakuna "state" ni jimbo, mfano tu.

    Halafu ICCR siyo idara ya serikali inayoshughulikia sijui vitu gani, hii ni Indian Council on Cultural Relations.

    Wasalimie.

    ReplyDelete
  4. poleni sana vijana kwa hali inayo wakabili. wasiwasi wangu ni kuhusu ombi lenu kutekelezwa,maana serikali yetu ukisha kuwa nje ya nchi basi wanajuwa wewe umewin life na hata kama unakufa au kuteseka hakuna anayejali.
    wengine tumekwisha imba wimbo wa kutumiwa pesa za kjikimu huu ni mwezi wa 6 sasa lakini hakuna anayejali,tumeandika barua kila kunakostahili kuanzia bodi ya mikopo hadi unakoweza kutaja lakini wala hilo halimgusi mtu.
    sasa nachoweza kusema tu ni muombe mungu maana nchi yetu si nchi tena.kila mmoja analake hasa wakati kama huu wanapojiandaa na uchaguzi mmh!sijui kaka.
    watu tumetaabika sana lakini ukisema unaokana mjinga tu wanasema si ufanye vibarua utadhani wewe hilo wazo hujawahi kulifikiria na likashindikana kwa sababu zinazoeleweka.
    naona umezungumzia kutolewa simu,je ni simu yako au ya serikalinili?kama ni serikalini nikukatishe tamaa maana watu tumepiga sana simu ilazinaambuliwa kuzimwa au kutopokelewa maaana wanajuwa wanachokifanya wenyewe. kazi mnayo ican feel you guys.

    ReplyDelete
  5. Hali si mbaya sana kama madau huyo anavyojaribu kueleza na Mimi nataka kuwatoa Hofu wazazi na marafiki zetu wote Mlioko kokote ulimwenguni kuwa hali hapa ni salama na watu tuna uhakika wa Maisha kwa 100%,usalama ndani ya Hyderabad ni mzuri na hviyo haitishii Amani ya Mtanzia yeyote alioko hapa kwani huo Mvutano hauna Mapigano yanayojumuisha wananchi/wakazi wa state hii.
    Hivyo nawaomba Ndugu,wazazi na marafiki zetu wote msiwe na wasiwasi sana juu ya mambo yalivyo huku.
    Asante.

    ReplyDelete
  6. kwanza Mdau uliyeleta taarifa Hizi ,mimi nasema Asante...........Kwa uzohefu wangu mimi ICCR haita husika kuwahamisha wanafunzi hapo Mlipo.Na ukizungumzia watanzani wanaosomeshwa na ICCR ni wachache sana hapo HDY hivyo ulikuwa huna haya ya kuzungumzia hilo!!!wewe Zungumzia mambo yanayojili tu hapo hdy.
    Mdau ICCR PUNE.

    ReplyDelete
  7. we mdau uliye toa comment ya tano acha kudanganya hali si shwari,leo kumetokea mapigano kati ya wanafunzi na polisi,wanafunzi maiti za wanafunzi waliojinyonga , labda we husomi Osmania University, au ndo wale wanao soma distance learnning wakiwa ndani ya India,

    ReplyDelete
  8. Kwanza kabisa namshkuru Mungu, kwa kweli hali ya usalama ni njema na maisha yanasogea ila tatizo liliopo ni kwamba tuna miezi miwili sasa hatujagusa shule kwa migomo at the same time tunapoteza hela nyingi tu hususa ss tunaosomeshwa na wazee wetu au kwa kua ww unasoma kwa mkoppo.
    kwa kweli inauma na kusikitisha sana kwa hali tuliyonayo Wanafunzi wote hususan wa kigeni.

    Mwanafunzi Mtanzania
    Osmania University,
    Nizam college.

    ReplyDelete
  9. Namuunga mkono anony wa Jan 20 08:27:00 AM.Hakuna hatari ya maisha kwa watanzania au wageni.Hata idadi ya watu wanaokufa kwa kiasi kikubwa wengi wao wanajiua wenyewe.Kuhusu mwaka wa masomo kupotea haijafahamika rasmi maana colleges nyingi shule zinaendelea kama kawaida na wametangaziwa mpaka tarehe za mitihani ya kumaliza mwaka.Main campus ni baadhi ya walioathirika sana maana mitihani yao ya kumaliza sem ya kwanza haikumalizika.
    Mdau ICCR Hyd

    ReplyDelete
  10. Admision fees LLM bei gani sasa ivi?..mi iko banya LLB hapo bana sasa taka rudi tena ..miss sana beef berian ya tolichok,godflek chotaa alto bana..

    ReplyDelete
  11. Huyo mdau anashangaa mtu kujinyonga mbona wanyarukolo wetu wanajinyonga na huwa hatusikitiki? Ninyi nawaomba mfanye kitu kimoja, mtumeni mwakilishi hapa Delhi aje awasilishe taarifa hizo kwa balozi officially na kama kuna ulazima wa ku-evacuate wananchi wetu ni jukumu la balozi na ninyi kuripoti officially haraka.

    Msitegemee serikali ya India kumwambia balozi wetu kuwa hali ni mbaya, wao hawajali sana kwani kwa India kufa mtu mmoja nobody cares.

    Kitu kingine muwe na nauli za dharula ili hali itakapokuwa mbaya msafiri kuja states zingine walipo waTZ wengine ili mpate hifadhi ya muda.

    Nawakaribisha Uttarakhand State, IIT Roorkee.

    ReplyDelete
  12. mtoa taarifa usichanganye mambo, wanafunzi wa kigeni hamhusiki na hiyo migomo, hamhitaji kuwa na wasiwasi, isipokuwa kama huo mmgomom unaathiri usalama wenu kwa ndiyo ombeni msaada ubalozini. kama kitafungwa , mitihan ikaahirishwa basi mtakuja kufanya mitihani chuo kitakapofunguliwa. kudai kujua hatma yenu toka kwa chuo wakati huu ni kupoteza muda tu. nyie hamhusiki na mgomo. hiyo ni tukio ambalo chuo hakikutarajia, hata chuo kikifungw nyie mtarudi chuoni kufanya mitihani yenu. siyo mnalialia kama watoto wa shule ya sekondari, hatamkipoteza mwaka , nina uhakika hamtalipa ada kwa mwaka mwingine. mnatakiwa kuwa makini siyo kuibuka kwenye vyombo vya habari na kutupa lawama ubalozini, do maana siku mnakuwa na shida makini, watu watasema -a hawa vijana wa india ni zao kulalama ovyo.

    ReplyDelete
  13. Poleni wa hyd dont worry maisha yata songa tuu watelugu should stop being stupid tuko pamajo mdau wa hyd kitambo.kash

    ReplyDelete
  14. we mdau wa kumi nambili sijui unaongea nn "eti mtafanya mitihani chuo kikifunguliwa", "oooh na hta mkirudia mwaka hamtalipa tena ada" unajua uchungu wa utupa MDA wewe au kwakua hayajakufika wewe. Kuwa makini kijana ss hku muda wa masomo umebakia miezi miwili tu kwa w'funzi wa semester na hatujui ln haswa tutaingia shule. Shule imefunguliwa tarehe 18 januari ila mgomo ndo umeanza upya tena kwa kasi mpya.
    Tumeharibika kisaikolojia kiukweli maana mda unakimbia.

    Osmania university.

    ReplyDelete
  15. Being stupid and in stupidity its very different!!!!!!!!!how com?life is short enjoy!!!!!!!charls anamiaka sita aja lalamika kitu gani kurudia mwaka!!mdau,and wadau someni!!!!!!mkicheza mta imba epa mpaka mwisho.........

    ReplyDelete
  16. Na nyie mkome, vyuo vikuu kibao vimejaa Tz, chakuwapeleka India ni nini? Ingekuwa USA, Canada Europe nk, Ingekuwa inaleta akili. Au ili mradi na nyie muambiwe mnasoma nje ya nchi?? Makubwa!!!!!!. Mungu abariki usalama wenu.

    ReplyDelete
  17. Hpa sio suala la kilichotupeleka India nini, are serious? sasa w'funzi wote wa Kitanzania wakiamua wasome nyumbani kweli sote tutapata nafasi hpo? mambo yenyewe ndo hyo Maprofessor wanakataliwa kwa upuuzi kabisa halafu eti someni nyumbani. Ukweli ukiujua utazinduka.
    God bless u.

    Osmania university.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...