Hi Michuzi,
Jana niliigiza katika mchezo wa kuigiza, The Harlem Renaissance Renaissance Revisited with a Gospel Flavor. Ilikuwa katika ukumbi wa Blackman Theater, katika Chuo Kikuu cha Northeastern hapa Boston. Kwa kweli ilifana sana. Safari hii niligiza kama Mother Africa.
Feedback niliyopata, watu walifurahi mavazi yangu (costume) na kuwa niliongeza na kiswahili humo. Nilivaa khanga na vitenge niliyopata nilivyokuwa Tanzania mwezi Novemba, ungo nilinunua Ubungo. Zaidi walipenda kuwa nilileta uAfrika, maana wengine walioigiza miaka ya nyuma waliigiza kwa lahaja ya kiMarekani na kuvaa nguo za Afrocentric.
Pia niliigiza kama Ms. Thelma, mwanamke anayetaka kushinda bahati nasibu na anatafuta mwanaume amabaye atamwoa. Ms. Thelma anafanikiwa kumpata Joe the Bartender, awali anamkataa lakini baadaye anamkubali.
Waigizaji wenzangu walikuwa na hofu kuwa sitaweza kuigiza baada ya msiba, lakini katika showbiz wanasema, The Show Must Go On!
Wasalimie wote!
Chemi
Waigizaji wenzangu walikuwa na hofu kuwa sitaweza kuigiza baada ya msiba, lakini katika showbiz wanasema, The Show Must Go On!
Wasalimie wote!
Chemi
picha na habari zaidi
I like sana hiyo picha..
ReplyDeleteVipi arobaini ya msiba wa mumeo imeshaisha??
Da Chemi,
ReplyDeletegood to see you keeping yourself busy. Looking forward to seeing you in one of the plays at Nkrumah Hall!!
Habari kaka Michuzi na dada Chemi,
ReplyDeleteNimekuwa nikifuatilia kwa karibu ushiriki wa dada Cehmi katika sanaa ya maigizo huko Marekani. Kwa kweli napenda kumpongeza dada Chemi kwa kuwa balozi mzuri sana wa sanaa ya Tanzania na Africa kwa ujumla huko ughaibuni. Kinachonishangaza, however, ni kwamba sijawahi kulisoma jina la Chemi katika orodha ya wasanii wanaopendekezwa kutuzwa tuzo za uigizaji Tanzania. Kila mara ni majina ya watu wachache tu yamekuwa yakirudiwa katika tuzo hizi. Je waandaaji wa tuzo hizi kweli hawaoni mchango mkubwa wa dada Chemi au kuna ufisadi katika mcahnganuo mzima wa uteuzi wa wasanii katika tuzo hizo? Kusema ukweli sanaa ya Tanzania, iwe ya maigizo au muziki haiwezi kuendelea kama walio nje ya nchi wataendelea kufungiwa mipaka. Sanaa yetu itaendelea kudumaa kwa ubinafsi wetu.
Mdau toka Sydney Australia.
we love you da Chemi,
ReplyDeletesorry you lost your better half. Keep on going and you will be fine.
That is life and there is not much you can do about it.
Take good care of yourself and the ones you love.
Ngowi wa London
safi sana Da Chemi,HUNA SABABU YA KUTOENDELEA na shughuli zako kwani msiba ndio ni mzito lkn maisha yanaendelea bado kusimamisha shughuli zako hakutabadilisha lolote zaidi ya kuzidi kujitia simanzi ni vizuri kuikubali hio hali na kujichanganya na mambo mengine..nakutakia kazi njema na afya bora
ReplyDeleteDa!Chemi
ReplyDeletesafi sana!hii inatupa moyo kuwa upo imara na unaendelea vema,baada ya msiba,songa mbele dada,sote tupo pamoja nawe !
Mungu azidi kukupa nguvu na moyo wa ujasiri.
wadau
The Ngoma Africa band aka FFU
We Michuzi we! Kwani huyu si ndio aliefiwa na Mai hazbend wake hivi karibuni hata mwezi haujapita?
ReplyDeleteKwani EDA imeshakwisha? Au ndo mambo ya uzungu hayo jamani? Mweeh!
marekani utakaa enda siku 40 nani atalipa bills. unapewa siku 3 tu za kuomboleza
ReplyDeleteWale mnaoongelea eda au siku 40 sijui...Kwani manafikiri kila mtu ni dini yenu?
ReplyDeletewadau 11.09 pm na 01.54 am menichekesha apa acha kabisa,,,nilitaka nimjibu ila mmemaliza yooote
ReplyDeleteeti mnafikiri dini yenu,bills nk???
wee unaeshangaa eti wadau km hawa hawatambuliki na izo Tuzo,,weee kwa ufupi DIASPORA HAMTAMBULIKI hamjasikiliza kipindi cha mahojiano TBC1 apa juzi tu???
sirikali hii hata haijui wataalua tu walioko nje watawatambua wacheza ngoma????
Mkware,
ReplyDeleteAcha hayo mawazo yasio kuwa na maana.
Kwa kifupi ni kwamba hii ishu ya arubaini sio ya kila mtu e.g mimi kwenye kabila na dini yangu hakuna kitu kama arobaini wa stini. ukisha zika mambo yameisha..ukiamua kuchukua week au mwezi hio ni juu yako.
usilete zako hapo...keep it to your hayo mambo yako ya arubaini na kumbuka sio kila mtu anafwata hivyo?
KUNA watoa maoni wasio na nidhamu hapa barazani! jamani wanamwingilia mtu katika mambo yake ya kifamilia na imani yake,
ReplyDeleteSasa huu ungwana gani? mnapojadili Eda,Arobaini!sitini,tujalibu kuwa na mtazamo safi,sio kumtusi mtu bila ya sababu,mambo pengine mnavuka mipaka,Msisahau kuwa Da'Chemi yeye ni mfiwa,na pia aliolewa katika ndoa ambayo ni Mult-Cultural?(yaani yenye utamaduni mchanganyiko.Tutilie maanani kuwa yupo ugenini!kwa kipindi iki kigumu anahitaji sana Moral support kutoka kwetu,lakini
hapa waswahili wanaleta maneno ambayo hayajengi bali kubomoa.
Da'Chemi ni Msanii alizima ajiweke bize sasa mnataka ashinde ndani katika kipindi hiki cha baridi?
Pia kwa nini ?haingiliwe katika mambo yake ya Privacy?
watu wanatoa hoja za utumbo utumbo hapa watafute la kufanya kama hawana kazi.
Mimi napenda kuona mtu anaendelea na maisha yake,haya mambo ya kukaa ndani siku 40 yanasaidia nini? Nyuso za huzuni mpaka lini? Marehemu atarudi? Ni kupoteza muda tu. Keep it up Sista Chemi! Wewe ni mfano wa kuigwa.
ReplyDeleteNa kweli hili ni suala la Imani na kila mtu aheshimu yake. Wakristo mtu akifa anaweza kaa hata mwezi kabla hajazikwa. Lakini akishazikwa tu siku tatu za maombolezo watu wanaendelea na shughuli kama kazi.
ReplyDeleteWaislamu mtu akidondoka tu asubuhi jioni anazikwa zege halilali. Halafu majonzi siku arobaini. Hivyo kila mtu ashike lwake.
Waisilamu ndiyo wenye imani na utamaduni wa kukaa eda na kuzingatia siku 40 baada ya kufiwa. Hii ni imani yao. Sisi wakristo hatuna hayo mambo. Sema kuna watu kutokana na elimu ndogo wanafikiri kila mtu ni muisilamu.
ReplyDeleteWake up!
Nstumaini haya maoni yangu hayatazuiliwa.