Wakati pilika pilika za kutafuta mwanamziki au bendi gani imefanyavizuri katika fani ya muziki 2009 ili ajinyakulie tuzo ya KILI MUSIC AWARD 2010,mambo mengi yanayohusu fani hiyo yanajitokeza,kuachia mbali malalamiko ya bendi za kikongo hapa nchini.


Wingu lingine kubwa ni kuhusu wanamziki wa Tanzania na bendi zao wanafanyia kazi nje ya nchi? Je hawa nao "Kili Music Award" inawafikiliaje? kutokana na mchango wao mkubwa wa kuelimisha jamii kwa njia ya mziki,baadhi ya nyimbo au tungo za wanamziki hao na bendi zao zinasikika na kukubalika katika jamii ya watanzania hapa nyumbani,wanamziki hao pamoja kuwa wapo nje ya nchi lakini wamekuwa mabalozi wazuri sana wa kuitangaza Tanzania kwa njia ya mziki.


Kwa mfano ni hawa www.myspace.com/thengomaafrica ambao baadhi ya nyimbo zao zinafanya vizuri pia kuna Ras Nas www.myspace.com/ras_nas, Fresh Jumbe http://www.freshjumbe.com/ na wengine kibao


Swali ni je kwa nini kipengele cha wanamuziki wa Afrika Mashariki kisiwe kwa wanamuziki wa Tanzania katika Diaspora??? Ama hicho cha East Africa kikiachwa kwa nini kusiwe na Best Tanzanian Musician in Diaspora????


Hakika huu ni ubaguzi wa hali ya juu kuliko huo mnaowafanyia wakongomani.


Mdau Hamburg

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. michuziiiiiiiiiiiii...nimeona hapo juu...one now can read...blogu ya jamanii..in mashaka language aka english teh tehhhh..hongera!

    ReplyDelete
  2. ni kweli waswahili walisema nabii hana utukufu kwao,hatutashangazwa tukisikia bendi kama the ngoma africa,inayoongozwa na kamanda wa ffu ras makunja kuwa wanawekwa kando katika award hii ya Kili!.hizo tabia na destuli zetu kuwapa kipau mbele watoto jirani..na kusahau watoto wetu.
    Kazi za hawa wanamziki wa ughaibuni zimetoa changa moto kubwa kuliko hizi za wakongo

    ReplyDelete
  3. Kili Music Award,itakubalika na watanzania wengi kama itazikubali pia juhudi na mchango unaofanywa na wanamziki wa tanzania walio nje ya nchi,tukiangalia kwa makini hakuna wa kupinga kuwa wanamziki wa kibongo walio nje wameupenyeza mziki wa bongo katika viwanja vya kimataifa na kujinyakulia maelfu ya washabiki.hata katika nyimbo zao zinamchango kwa maendeleo ya jamii,nilikuwa nawasikiliza vichaa wa Ze ngoma africa bendi nikagundua
    mtunzi wa nyimbo ras makaunja ni kichwa kinachochambua matatizo yaliyomo katika jamii za uswahilini,Kili Award lazima iwafikirie wanamziki wa tanzania walio nje

    ReplyDelete
  4. Kili Award kuwapa wanamziki wa bongo wanafanyia kazi ughaibuni?
    kama watafanya hivyo basi watakuwa wamepiga hatua moja kubwa sana sana,kwa kukubali juhudi zilizofanywa na wasanii wa bongo walio nje..ngoma africa bendi na wengineo,lakini Kili Award akipewa mtunzi mwenye uchokozi wa kila aina ras makunja si itakuwa sawa na kumpa rungu kichaa na kumtimulia sokoni?inamaana kichaa huyo wa mziki atahakikisha kila mwaka anachukua Kili Award.

    ReplyDelete
  5. ffu wa ughaibuni ngoma africa band,na kiongozi wao bw.kichwa ngumu ras makunja,jamaa nawakubali kazi wanaijua,nyimbo zao zina ujumbe,japokuwa mara nyingi washabiki wao wanamwekaga roho juu ras makunja

    ReplyDelete
  6. kinacho tuacha midomo wazi tulio wengi,ni utaratibu wa kamati ya Kili Award,kwanini ?hawawi makini,kwa kuzitambua kazi za wanamziki tanzania?tunao wanamziki wengi sana ndani na nje tena wanafanya vizuri sana,kazi zao au nyimbo zao zinapigwa ktk redio za ndani na nje ya nchi,tena zinaeleweka.sasa kuna uzito gani? kwa kamati kuzimabua kazi za wanamziki hawa.kamati inapowapa tuzo best of east africa musician!
    na kuwatosa akina ras makunja na ffu wa ngoma africa band.tulio wengi tunakuwa hatutambui kamati ya Kilimanjaro award ina malengo gani? katika utoaji tuzo hizo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...