UNAKUMBUKA NINI ENZI HIZO HASA UKISIKIA WIMBO KAMA HUU...??
Binafsi nakumbuka mbali sana enzi hizo radio zilikuwa ni National na Philips tu na zilikuwa zinauzwa kwenye maduka ya RTC.
Nakumbuka maduka yale yalikuwa yanaitwa Bora yalikuwa karibu kila mkoa, walikuwa wanauza viatu vikiitwa safari boot, pamoja na raba mtoni zilikuwa zinaitwa Bora.
Nakumbuka enzi hizo daftari za mistari mikubwa na midogo kwa ajili ya kujifunza mwandiko kwa wanafunzi zilikuwa zinapatikana maduka ya Tanzania Elimu Supplies tu.
Nakumbuka pia tulikuwa tunapewa madaftari bure shuleni kila mwaka shule ikifunguliwa na likiisha unakwenda kumuonyesha mwalimu anakupa jingine jipya.
Nakumbuka enzi hizo kulikuwa na mashirika ya uchukuzi kila mkoa Mwanza ilikuwa KAUMA, Kagera ilikuwa KAGERA RETCO, Iringa ilikuwa IRINGA RETCO, Dodoma ilikuwa KAUDO, wadau mtaongezea.. Morogoro, Rukwa na kule kaskazini yalikuwa yanaitwaje..
Namkumbuka nakumbuka radio Tanzania ya enzi hizo na vipindi vyake kama Kahawa ni Mali, sikiliza Bwana Umeme, TTCL simu kwa Maendeleo, General Tyre, Starehe na BP, Malenga wetu.... wadau ongezeeni vipindi mlivyokuwa mnakumbuka enzi hizo...
Nakumbuka enzi hizo kulikuwa hakuna TV watu walikuwa wanakwenda kwenye kumbi za sinema tu kuangalia movies, Dar zilikuwepo kumbi kama Avalon,Drive Inn n.k Dodoma kulikuwa na N.K Disco Teques
Nakumbuka enzi hizo mabasi yalikuwa yakisafiri usiku tu na kulikuwa hakuna ajali nyingi kama sasa. Nakumbuka pia Mabasi maarufu enzi hizo kama SIRI YAKO, SUPER STAR, NGORIKA na wale mliokuwa Dodoma mtakumbuka mabasi yale ya kwenda Tanga kama SIMBA MTOTO, AMEET na zile honi zao kimadaha.
Nakumbuka pia watu walikuwa na ushirikiano sana, jirani alikuwa ni kama ndugu yako.
Mdau unakumbuka nini enzi hizo...??????
Mwenda Pole
Mdau wa Dodoma
Home
Unlabelled
maroon commandos
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
nasilikiza hii nyimbo na mambo uliandika yananipa msisimko niifikiri njinsi mambo yalivyo badilika
ReplyDeleteviatu - BORA
UDA - dar usafiri
SU - magari ya mashirika ya umma
Nakumbuka Maramba JKT,Tanga.Nawaona wazee maarufu kama Mzee Japheth Mbonea, Athuman Kiguru na wengine wanakunywa kahawa.
ReplyDeletePia nakumbuka timu kubwa mkoani Tanga kama Coastal Union na nyingine
Wadau enzi hizo mpira ulikua Tanga, mliopitia Maramba Jkt Mpo....
Asante sana,
Mdau,
Texas, USA
Nakumbuka enzi hizo tangazo la sigara ya sportsman na wimbo wa "Bwana Msafiri anasema hakuna sigara inayofaa ila sportman kubwa inaburudisha".
ReplyDeleteNakumbuka enzi hizo Radio Tanzania kipindi cha Ukulima wa Kisasa na wimbo wa NUTA ulioimbwa "vijiji vya ujamaa haya shime wananchi twendeni..kitu kama hicho.
Nakumbuka enzi hizo tangazo la RTD kipindi cha National Agricultural Products Board kabla ya National Milling na GAPCO kuna kawimbo kanasema hivi "Mazao mazao ni kazi ya Bodi ....nk
Nakumbuka mengi enzi hizo RTC wakiuza changer yaani record player ilikuwa shilingi 750..
Nakumbuka enzi hizo pale jirani na Tiger Motel barabara ya kwwenda Tegeta kuna mmakonde alitaka ninunue plot pale kwa shs 15000 sikumudu. Nilishauriana na mke wangu tuuze fridge na radio cassete tukaambuli shs 3500 tu. Nikashindwa kununua. Sikuwa mlanguzi wala fisadi. Mpaka leo ninapopita pale nakumbuka sana. Hayo ndiyo maisha. Nilipakosa pale lakini Mungu ni mkubwa miaka ilivyozidi kwenda nimepata vingine. Sikuwa na haraka kwa sababu kwa njia ya subira Mungu bado kanipa. Namshukuru.
viatu vya chachacha kaka, tulikuwa tunatofautiana rangi sote tulikuwa wachina, TV utegeshe Zanzibar au kenya, usafiri wa mjini ilikuwa kamata na uda na yalikuwa yanatosha, mabasi yamikoani kama siri yako yalikuja baadae, burudani tulikuwa na bendi kama Afro band sabini, nuta urafiki jazz, kibakora jazz,mwenge jazz, jamuhuri jazz, mororgoro jazz na nyenginezo
ReplyDeleteKweli mdau, vitu kama sukari na mchele tulikuwa tunanunua kwa mstali kwenye maduka ya RTC. Kulikuwa na mashamba ya kijiji vijiwe havikuwepo.
ReplyDeleteKwenye disco usiku muziki ukifikia chorus basi taa zilikuwa zinafifishwa kwa nia njema kabisa basi na kama ni kibatali muungwana mmoja atakizima kwa kukipulizia upepo taratibu. Burudani kama kawa.
That was probably the best time in our life. Ukimwi haukuwepo, free riding. Ukiugua ugonjwa kama gono ulikuwa unaonekana bingwaaa!!
MY FRIEND, UMENIKUMBUSHA MBALI SANA. ENZI HIZO HAPAKUWEPO AIDS AND LADIES WERE NOT COSTLY KAMA ILIVYO SIKU HIZI.
ReplyDeleteNAKUMBUKA SIKU YA USAFI SHULENI,NILIKUA NAFUA SHATI ASUBUHI NA KULIKAUSHA NA PASI.
ReplyDeletemimi kilichokuwa kinaniboa ukitaka kusikiliza mziki hadi usubiri RTD waamue tena miziki yenyewe wanabana kwenye klab raha leo na chaguo la msikilizaji
ReplyDeletenakumbuka pia wagonjwa wengi kwenye kipindi cha wagonjwa RTD walikuwa wanachagua wimbo wa kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe na wimbo wa dr remmy wa kifo hakina huruma
nakumbuka mazungumzo baada ya habari(RTD),nakumbuka tulivyokua tukipanga foleni ya unga wa yanga kwenye maduka yale ya nationalmiling,mgambo wa zone walivyokua wanakimbiza wezi,nakumbuka player ya baba alikua akipiga sana santuri yake(kasongo yeye mobali nangai kasongo mama mobali ngalawee)we acha tu,
ReplyDeleteMAISHA YA ZAMANI YALIKUWA MAZURI SANA SI YA SASA ENZI HIZO UNATOKA BARA UNAKUJA DAR UNAPOFIKA MBEZI UNAHISI KAMA UNAINGIA ULAYA HIVI, UKIKAA MWEZI DAR SIKU UNARUDI NYUMBANI UNARUDI NA MKATE WA SIHA NA HALI YAKO IMEBADILIKA HIVI NA KAWEUPE HIVI NGOZI NYORORO. SIKU HIZI MWEEE. NAKUMBUKA ENZI HIZO WATU WALIKUWA WACHACHE SANA DAR
ReplyDeleteShime wakubwa wenzangu. Nilidhani mie kibopa kumbe papa wengi wamo. miaka hiyo nilikuwa dogo lakini nakumbukia sana yoote yaliyosemwa humu. Kweli dunia yetu ilikuwa tamu wajameni. Mara ya kwanza kuusikia wimbo huu ni pale kaka yangu mmoja alioa, miaka ya themanini (1980) kule rombo Tarakea, tukawa tunaurudia rudia wimbo wenyewe kwenye changer yake aliyokuja nayo toka Jeshini- ilikuwa burudani tosha. Wakati huo ndio nilikuwa darasa la saba na hatukuruhusiwa kuingia kwenye kumbi za kijijini zilizoitwa enzi hizo Madisco. Siye tuliambukia kuangalia wakubwa walivyokuwa wakilisakata rumba (ni enzi za mapekosi na mabugaloo na viatu vya Santana, na mashati ya kubana mbavu, nywele za Afro). Madisco kule Tarakea yalikuwa yanachezwa mchana wa saa kumi hadi saa kumi na mbili na nusu na burudani ilimtoshea kila aliye hudhuria. Mchalii ama mdada alitengeneza pombe ya mbege na kuandaa uwanja kwa kuuziba kwa miti na majani, vijana waalikwa walihudhuria, wake kwa waume, mageti crushers walitolewa nduki. Mziki ukichezwa watu walitulia kumsikiliza mtangazaji ambaye alikuwa anaashiria kama ni wasichana kuwachukua wavulana na kulikuwa na discipline ya hali ya juu. Enzi hizo ikichezwa blues, wasichana walikimbilia migombani kujisaidia na wavulana wanawadaka waliobakia kucheza blues. Jioni ikifika wasichana walitimua mbio kwa makundi kuelekea majumbani kwao. Hapakuwepo na ufuska wala ubakaji.
ReplyDeleteIkiwa mziki uliendelea zaidi ya saa kumi na mbili basi Baba ama mama mwenye nyumba alikuwa anaingilia kati na kudai mziki ufungwe na kila mtu apotee. Ebwana walikuwa wanasikilizwa, hakuna anaye tukana, kila mtu anakitoa kimya kimya.
Kwa upande wa Marangu madisco nayo yalikuwa kama haya haya na yalikuwepo mchana vilevile. Kule kibosho na Machame hali ilikuwa tofauti. Madisco haya yalikuwepo usiku na utashangaa hapakuwepo na uhuni. Kama kulikuwa na ubakaji ni wa nadhra saaana. Bwanaweee. Nimerudishwa mbaliiiiiiiii. wacha we. Wadau wa Kasirwa Mpoooooooooo!
Nakumbuka vipindi vya kuelimisha watu kuhusu Family planning, chakula bora nk kupitia RTD na vipeperushi kibao
ReplyDeleteUkiusikia huwa wimbo asubuhi enzi hizo jua umechelewa namba, bola ujaladie kabisakaisa!!!!
ReplyDeleteNakumbuka wakati wa kipindi cha michezo kila siku saa mbili kasorobo na mtayarishaji wake marehemu Abdul Omar Massoud( R. I P),sote tulikimbilia kwenye redio za watu wachache waliokuwa nazo ili kusikiliza habari mbalimbali za michezo.
ReplyDeleteNakikumbuka kipindi cha majira cha saa moja kasorobo asubuhi ndio ilikuwa jirani yangu anatoka kwenda kazini na siku nisipofungulia redio yangu alikuwa anachelewa kazini.
ReplyDeleteNimesikia kulia. Nakumbuka nilikua ndio kipindi cha wafanyakazi. Ninaanza kunawa ili niende shule. Tulikua tunaingia shule mchana.
ReplyDeleteViatu vilikua vinaunzwa bora...vinaitwa viatu vya mwaka wa watoto. Vilikua vya brown na vyeusi (clogs)...Viliua very soft..Nilibembeleza mama aninunulie alichukua sijui akiba yote bank.
Mdau mbona waniliza! Yaani yote hapo juu wadau mmenikumbusha mbali. Kuwahi namba shule na mchakamchaka.
ReplyDeletePamoja na yote waliyosema wadau hapo juu, naona wamesahau kuwa wakati huo kulikuwa na zile chupi za kiume zinazoitwa VIP. zile zilikuwa ukizi-abbuse zinakutoa nishai maana unaweza ukawa umeivaa inapotakiwa na baada ya muda inakuwa imefika tumboni au kwenye kwapa lol. Good old days!
ReplyDeleteWadau, kumbe kweli maisha wakati ule yalikuwa mazuri.
ReplyDeleteNakumbuka waalimu wetu shuke ya msingi walikuwa nadhifu sana darasani. Kipindi cha kiingereza ilikuwa ni kuongea kiingereza tu. Mwalimu alikuwa hachanganyi kiingereza na kiswahili. Namkumbuka sana mwalimu wetu wa kiingereza, Raynard Sanga (RIP) jinsi alivyokuwa anaringa wakati akifundisha kiingereza, wewe mwenyewe utapenda tu.
Nakumbuka sana kitabu hevi kule Caigo Secondary. Walimu walikuwa commited kufundisha. Hongera Dr Madumula, nakuona hapo UDSM. Nakukumbuka kwa shule yako ya kiswahili, Mofimu, Ngeli, Viunganishi vya sentesi. We acha tu.
Nakukumbuka pia mwalimu wangu wa Ung'enge wakati ule, Azaveli Lwaitama (sasa Dr. hapo UDSM). Huo mpangilio mnaouona wa maneno yake, ndivyo alivyokuwa anatutia darasa la lugha ngeni ya kiingereza. Namkumbuka jinsi alivyokuwa antufundisha ujanja wa kutamka manaeo ya kiingereza (mfano, neno 'type' akisema fikiria maneno kama 'taa ipo' ili uweze kukumbuka. Hebu ona mbinu hizi za kumfanya mwanafunzi apende somo. Lakini siku hizi, mmhhh. Miundo mbinu kibao, lakini hatuishi visingizio. Tunafuma vitambaa maofisini na kuacha vipindi.
Anko, siku zile zitakumbukwa. Wombo huo unanikumbusha mbali sana**''+++"""...**..*** halahu aah
Jamani, hapa nalengwalengwa machozi, yaani nakumbuka mbali sana.
ReplyDeleteKulikuwa na kipindi cha muziki kinaitwa 'Misakato' bendi maalumu zikipewa nafasi kupiga nyimbo zao.
Pia kulikua na kipindi cha Mchana mwema, miziki kibao na salamuz. Wakati ule RTD. Mzee TIDO, unakumbuka enzi zile?
Halafu kulikuwapo kipindi cha Tumbuizo Aslia. Ilikuwa asilia kweli. Aah jamani, Good those old days. Ancle Michuzi, we acha tu.
Mdau wa zamani enzi zile.
santuri mzee alikua atokanazo majuu
ReplyDelete1.donna summer,ABBA,bony M,disco toto nk nk,
2.viatu vya chachacha,nguo za segadanz
na raha za majuu basi