ANAITWA NURDIN LULANGA AMEZALIWA MWAKA 1990 DAR ES SALAAM TANZANIA, HIVYO ANA MIAKA 19.

HISTORIA YA UGONJWA HUU ILIANZA WAKATI KIJANA HUYU AKIWA DARASA LA 6 (SITA NA ILIKUWA NI MAUMIVU YA KAWAIDA TU YA MGUU JUU YA GOTI NA INAFIKIA MDA MWINGINE ANASHINDWA HATA KUTEMBEA.

MAUMIVU HAYO YALIKUWA YANAENDELEA NA KUACHA NA BAADA YA MDA UKAANZA KUVIMBA TARATIBU NA BAADA YA KWENDA KUCHUKUA VIPIMO VYA X-RAY IKAONEKANA KAMA MFUPA ULIKUWA UNALIKA TARATIBU.

BAADA YA KUFIKA FORM SIX (2009 MAY) TERM YA KWANZA MGUU ULIVIMBA GHAFLA KWA KASI YA AJABU NA NDIO IMESABABUSHA ASHINDWE KABISA KUTEMBEA HUU SASA NI MWENZI WA 9 YUKO TU NYUMBANI.

AMESHAPIMA FULL BLOOD PICTURE, ABSOMEN, BONE SCAN (OCEAN ROAD) N.K LAKINI HAKUNA KIPIMO KILICHOONYESHA DIRECT ANAUMWA UGONJWA GANI MADAKTARI WAMETUSHAURI TUMPELEKE NJE YA NCHI NA FAMILIA HAINA UWEZO HUO JAMANI NDUNGU WATANZANIA TUNAOMBA MSAADA WENU ILI TUMSAIDIE HUYU KIJANA KATIKA UGONJWA HUU
NATANGULIZA SHUKURANI ZANGU ZA DHATI


KWA YEYOTE ATAKAE GUSWA NA HILI TATIZO NAMBA ZA SIMU NI
0712 677 977 NURDIN (MGONJWA MWENYEWE)
0715 247 460 MAMA WA NURDIN
0754 247 460
0784 753 312 NA
0773 464 833 KAONEKA (MJOMBA WA MGONJWA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. Pole sana kijana Nurdin,pamoja na misaada ambayo inatakiwa kufanikisha matibabu yako nashauri pia ungepata wasaa wa kufanyiwa maombi na watumishi wa mungu naamini hakuna lisilowezekana kwa yesu,mungu atakusaidia utapona na kuendelea na masomo yako. Upo muujiza kwaajili yako ukiamini.

    ReplyDelete
  2. Mimi ninam-support huyo mdau hapo juu, wakati unasubiri hiyo misaada, nenda kwa watumishi wa Mungu wakakuombee. wapo wengi tu ni wewe tu kuamini kwamba Mungu atakuponya. Mtwalie Mungu utukufu.

    ReplyDelete
  3. At this time on this planet there is almost no disease that is unknown,generally speaking
    Huyu mtoto nampa pole sana, anachohitaji ni Xrays,MMR.CT,biopsies,angiograms etc
    Labda matatizo ni kwamba bongo bado haijaufungua mlango wa jengo la vipimo hivyo
    Allah ye baarik
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  4. YALE MASHIRIKA YA SIMU HAPO NDIO MAHALA PA KUSAIDIA, SIO KUTOA KATIKA MAMBO YA U-MISS NA MENGINE YASIYO NA UMUHIMU

    ReplyDelete
  5. mdau wa kwanza kabisa umenena mie nilipomaliza kuisoma ishu nzima nikaona hapa sasa ni maombi ya nguvu yanahitajika huku wanajamii tukiwa tunafanya jinsi ya kumsaidia kifedha ili akapate matibabu nje ya nchi labda madaktari bingwa wa maulaya watapata ufumbuzi manake wenzetu wana miteknolegy ya hali ya juu

    ReplyDelete
  6. Poleni sana familia ya kijana Nurdin.ushauri wangu mkubwa ni maombi maana kama hospiltal ugonjwa haujajulikana yuko daktari mmoja tu hapa duniani anayeona na anayetibu magonjwa yote.hivyo mimi naishauri familia impeleke kijana wao katika kanisa la Efatha mwenge siku ya ijumaa asubuhi kuanzia saa mbili pale pana huduma ya ukombozi inayoanza saa mbili asubuhi mi naamini kabisa akifika pale lazima apookee uponyaji.wengi wameponywa pale.mungu akupe nguvu na baraka zake ziwe juu yako daima.ibilisi hana mamlaka yeyote na maisha yako is only God has final say to your life.

    ReplyDelete
  7. Ni kweli, hakuna kitu kinachomshinda mungu. Maombi ni muhimu sana katika maisha yetu. Mungu alisema, ombeni mtapewa, Omba kaka yangu na mungu atajibu maombi yako. Na kitu kingine ni kuwa na imani.
    Mungu atakusaidia.

    ReplyDelete
  8. nyie wadau wa juu mnaye mwambie aende kuombombewa kweli mna fikiria.angekuwa ndugu nyenu mngempeleka kwenye maombi au hospital. kumuomba mungu ni kitu cha kawaida na cha kila siku.nimeona wagonjwa wengi wanapelekwa kwenye maombi instead ya hospital wanakufa wakati wangeweza hishi ngali wangepelekwa kwa watalamu.wengi wanao kwenda kwenye maombi badala ya hospital ni kwa sababu ni masikini awajiwezi na awana pesa za matibabu. hingekuwa vyema kama kungekuwa na organization hapo bongo kama azipo ambazo zina wa support watu kama hawa.tuna weza kusaidiana wenyewe watanzania si adi kila siku tuwasubiri wahindi kutusaidia.
    ni maoni tu
    pole kaka mungu endelea kusali mungu hatafungua njia tu. utapata msaada

    ReplyDelete
  9. sasa john mashaka umsaidie huyu ndo anaitaji msaada sio unasaidia mtu ana miguu mikono miwili eti kisa alikwua jambazi..anyway..

    ReplyDelete
  10. hiyo ni kansa jamani tumsaidie ndugu yetu

    ReplyDelete
  11. POLE SANA KUWA NA IMANI NA MUNGU ATAKUPONYA NA WAKATI UNASUBIRI MCHANGO KAMA WALIVYOSEMA MAMA WA MTOTO MPELEKENI KWENYE MAOMBI AKUNA KINACHOSHINDIKANA WATU WANAPONA ,ASANTE MUNGU AWATIE NGUVU

    ReplyDelete
  12. Toeni pesa acheni maneno...ndo shida kubwa hiyo nimeiona hapa. Mtanzania akiambiwa kuchangia mtu akatibiwe anaanza "uswahili" maneno mengi. Mimi nimeshachangia vitu hivi hapa kwenye blogu mara kadhaa. Ila wananiudhi sana watu ambao kazi yao ni maneno tu na ushauri mia...sasa kama Ocean Road wameshindwa na wataalamu wanashauri akatibiwe nje..ninyi maneno yenu yanamsaidia nini. Toeni hela kwanza ndo mlete ushauri mwingine...!! Ingekuwa jirani zetu hapo Kenya Harambee ingepigwa kwa kasi na mambo yangekuwa sawa..ninyi mtaanza maneno hapa hakuna kinachoendelea..leteni pesa kwanza. Mimi nitatoa dola 50. haya na mwingine aendelee kuahidi..na kuotoa....!!

    ReplyDelete
  13. jamani hatuna uwezo wa hata kuchangia dola 10 au pound 10 au krona 10 tu?? tusikalie kusema tu kuwa hakuna ugonjwa ambao haujulikani, mmeshaambiwa kuwa nyumbani wameshindwa kugundua kwa hiyo akija huku kulikoendelea kitabibu labda ijulikana, ni bora tufikirie jinsi ya kumsaidia mwenzetu huyu kuliko kuanza kutoa maoni ambayo majibu yake tayari mnayo. matatizo ni ya kila mtu jamani leo kwako kesho kwangu who knows?? like this was born not the way he is now, kama hayajakukuta wewe yaweza mkuta hata mtoto wa mjomba wako au mwanao kesho. ndugu zangu tumsaide huyu mtoto. mimi naangalia jinsi ya kutuma hata pound 25 na watu mia tukifanya hivi it's not nothing.

    ReplyDelete
  14. jamani pole kijana wetu,john mashaka vip uko wapi? msaada bwana.

    ReplyDelete
  15. Afanyiwe mpango apelekwe India watapata solution, kama unasumbua sana itabidi ukatwe ili kuondoa ile sehemu iliyoathirika. Au apelekwe aombewe kwani Jina la Yesu linaponya kabisa na kama kuna mazingira yoyote yatabainika kwani Jina la Yesu lina nguvu kwa wale waaminio.

    ReplyDelete
  16. kaka micguzi jaribu kumuulizia nchi jirani kama kuna utaalam tujue gharama zake ili tusaidiane..DAWA YA MARADHI NI DAWA NA SIO KUOMBA YESU hiyo ni kuonyesha uzaifu kijana ana maumivu ambayo hatuwezi kuyajua sisi tunaepata usingizi usiku MICHUZI TAFUTA HOSPITALI NCHI JIRANI KAMA TANZANIA HAIWEZEKANI

    ReplyDelete
  17. Anony wa Tarehe Thu Feb 04, 05:58:00 PM, Wewe kweli kiboko hutaki Blaa blaa na Somjo nyiingi zisizo na maana. nakupa tano mwana we ndo umeona mbali, tatizo wabongo somjo za kumwaga hamna lolote la maana. cha msingi hapa ni mshiko mtu akafanyiwe uchunguzi that is the immediate solution. nimesoma ulivyokuwa mkali ikabidi nicheke kwanza. hiyo safi sana mimi nadhani wewe na mimi tunafikiria kimoja kama ambavyo nami nilishatoa maoni hapo juu.
    let's look into ways to help this poor guy jamani.
    Mdau wa P&T

    ReplyDelete
  18. Kamla alivyotangulia mmoja kusema hapo juu, huu ugonjwa "haujulikani" kutokana na kutokuwepo vipimo!!

    Badala ya serikali kununua ma VX na madudu mengine aina hiyo kwanini wasiwekeze katika kununua MRI scanners na CT scanners walau kila mkoa? Au basi kila kanda?

    Hiyo inaweza kuwa osteosarcoma...

    ReplyDelete
  19. Bwana Nurdin pole sana kwa matatizo haya yalokufika na pia tunawapa pole walezi na wasaidizi (Carer)wa ndugu huyu Nurdin.
    Tiba zipo za aina nyingi na Kwa Allah hakuna jambo linaloshindikana, Kwa jina lako linaonyesha wewe ni Musilamu unayeamini Mungu asiokuwa na mtoto, Hakuzaa wala hakuzaliwa na Hapana yeyote mwenye kufanana na Mola.
    Kuna Tiba alizotufundisha Mtume S.A.A.W ambazo huitwa Tibb Ruqyah(Islamic Exorcism) huenda ukawa na mapepo wachafu wenye kukufanya ukawa katika hali hii,Pia Alama Sheikh Ibn Qayyim Jawziyah anaandika kuna tiba Quraan na Tibb Tabriyah Kuna wadau nitakupa namba zao za simu uwasiliane nao ili wakupe nmsaada huo wa WachaMungu Inshallah utakuwa ni mwenye kupona.
    Utaambiwa mengi kuhusu ugonjwa wako , Jiweke katika msimamo Thabiti na wala usimshirikishe Mungu wako , Hakuna Tiba isipokuwa Ya Allah

    ReplyDelete
  20. Dah...Inackitisha sana. Broooo Michu mimi nina swali hv hawa viongozi uwa wanasoma blogu ya jamii? Maana kuna misada mengine serikali inabidi ijitaidi kuwasaidia wa2 kama hawa. Huyu ukimpeleka India sidhani hata $ 10,000 inafika. Serikali ye2 kwa mwaka ina2mia kuanunua magari ata dola laki mbili lakini wanashindwa kuwasaidia wa2 kama hawa na omba omba. Jinsi inch ye2 iluvokuwa omba omba wangekuwa na fungu lao na vilema. Afu wakiweka gozi gozi town mnawakamata na kuwafukuza. Mbona ata U.S.A. omba omba wapo na awaguswi. Kikwete, wa2 kama hawa ni wakusaidia na Serikali ukiondoa na msahada wa jamii yaani wakujitolea. Inatia huruma, natamani hata kulia, bro Michu

    ReplyDelete
  21. Jamani, hata mimi naungana na wachangiaji wanaolaani maneno maneno, ni kweli maombi yanasaidia lakini TOENI pesa, pesa hapa huyu kijana akatibiwe nje ya nchi. hapa msianze kufagilia dini fulani. msimtumie huyu kijana kuwapa watu fulani umaarufu Mungu ni wetu wote, dini zote, naamini hata huyu kijana ana dini, sio lazima akaombewe na binadamu mwingine. huyo binadamu katoa wapi hizo nguvu? Mungu wetu ni Mungu wa upendo, na anamuona huyu kijana, tumpe msaada jamani, kama ni kuomba nina hakika anajiombea pia na Mungu amesikia sala yake ndio maana hata amepata nafasi kwenye hii blog. kupata nafasi ya kuomba michango kupitia kwa Michuzi ndio majibu ya maombi, sasa sisi tufanye kazi moja KUTOA HELA

    ReplyDelete
  22. Jamani siyo kama sioni huruma Huyu kijana, uvimbe aliokuwa nao ,location yake age yake ni 80% osteosarcoma. Cancer inayoanzia kwenye mifupa. Diagnosis yake ni moja kwa moja tunachotakiwa ni kutoa biopsy kucomfirm diagnosis.
    Treatment yake ni Amputation plus chemotherapy lakini ni kachelewa sana prognosis ni very poor.
    Cha maana anatakiwa aende MOI watashauriwa. Hakuna mtu atakayemreffer nje ya nchi sababu ya huu ugonjwa
    Pole sana.
    Wadau ,ukiona mtu anavimba sehemu yoyote mshauri aende hospital mapema .

    ReplyDelete
  23. watanzania viumbe wa ajabu sana mmesikia kutoa mchango basi kila mmoja keshajigeuza mlokole anaruka kiunzi hawa ndio wabongo porojo nyiiiingi kila mmoja mwanasiasa halafu mnawalalamikia viongozi wenu wana porojo wakati hao viongozi wanatokea kwenye jamii hii hii ya wazee waporojo what do u expect??bungeni fix,police fix,serikalini fix mtaani fix..aisee hii nchi hatari sana kumbe puuuuh mi simo..CHAKUSHANGAZA LEO WACHANGIAJI ZAIDI YA 80% WAMEGEUKA WALOKOLE HAHAHAHA..NOMA SANA WAZEE...KIJANA NAMBA YAKO NINAYO MCHANGO WNG UTAKUFIKIA VERY SOON AU KAMA BRO MICHUZI UNAWEZA KUWEKA UTARATIBU WA KUPOKELEA MICHANGO HAPA

    ReplyDelete
  24. Serikali inatakiwa kuweka budget ya MEDICAL AID....(Na wasitumie wao hilo fungu kujitibu) Hiyo iwe kwa misaada kama hii ya muhimu,....Huyu kijana anaumwa na kijana mdogo sana.

    Kama una email yenye PAYPAL ingekua rahisi kwa siye kudump some money there....A little here a little there kijana wa watu akatibiwe.

    Nchi isiyojali raia wake ni tabu sana.

    ReplyDelete
  25. PIA SERIKALI HIYO NI KAZI YAKE YA KUHUDUMIA WANANCHI WAKE NDO MAANA TUNALIPA KODI HATULIPI KWA AJILI YA MISHAHRAYENU TU NI KWA VITU KAMA HIVI PIA.

    ReplyDelete
  26. mdau, ha ha ha, we mdau uliesema wabongo tumegeuka walokole gafla umeniacha hoi nimecheka sina mbavu, u made my day honey...yani kweli wabongo sie, tumeguswa panapoumiza-pochi wote gafla tumekua walokole! Its sad kwa kweli, ushauri wa kuombewa si mbaya iwapo ungefuata after mchango, changa kwanza then shauri! Du! yani nimeshtuka jinsi wabongo livopiga u turn!
    Kijana Mungu atakusaidia mimi nakuchangia $76 ili upate laki kamili, nakutakia kila la kheri/
    NB: Mdau mwingine katoa wazo zuri kumtumia Mdau Michuzi mimi ningependelea kufanya hivo, ili iwe rahisi hasa kwa Michzi kutuambia ngapi zimepokewa au hata kuweka orodha ya watoaji kwani hiyo inaweza kuongeza changamoto kwa wengi kujitolea esp ikiwa inaonekana kiasi gani kimepungua ili gharama itimie, wengine watakua tayari hata kutoa mara 2 kwani kutoa ni thawabu kubwa sana kwa binadamu and theres no greater satisfaction than seeing that you have been of help to someone in great need!

    ReplyDelete
  27. Nimepatwa na mguso sana, najua maombi ni dawa pia mjaribu kwenda ikulu kwa rais kuomba msaada wa serilali, muu ndo muda wake, maana kama inaweza toa misaada nchi jirani itashindwa nyumbani?badala ya kusuburi michango, na hali ndo inazidi kuwa mbaya, kuna magonjwa yameingia ya kisukari, nana fanana na hilo ninalo liona kwako, kaka, hasa huku marekani huo ni ugonjwa sugu, ni kisukari, nenda ofisi ya rais kajieleze.Wakati ukusubiri michango ya pembeni.POLE SANA.

    ReplyDelete
  28. Ni kisukari hicho, hata leo nimeona kwenye OPRA SHOW, UGONJWA huu umezuka kwa ghafla, na hivi mwaka janandugu yangu wakaribu kapoteza mi guu yote miwili kwa imani za kichawi, kwenda INDIA wakeikata yote, michango ni muhimu na mimi naahidi dola 50, sasa sijui nimpe michuzi au wahusika?pole sana.maombi pia ni dawa,usichoke.

    ReplyDelete
  29. HEBU NYIE MNAO JIFANYA MNAMJUA SANA MUNGU WACHENI NGONJERA ZENU MUNGU NDIO ANATAKA AOMBWE TU BILA JITIHADA ZA MATIBABU??MUNGU MWENYEWE NDIE ALIEMUUMBA MWANAADAM NA KUMPA AKILI YAKUVUMBUA DAWA NA AKILI ZA UTABIBU SASA WEWE BAADA YAKUJUA JINSI GANI TUMFIKISHE KWA WATABIBU NAKUPATIWA TIBA UNASEMA TUMKABIDHI YESU ALAAAA,HAPO NI MKWANJA TU DOGO APELEKWE NJE YA NCHI APATE TIBA.MUNGU ATAKUAF INSHAALLAH,POLE SANA KAKA...NIMECHUKUA NAMBA ZAKO.KHERI ITAPATIKANA INSHAALLAH.AAAMIN MDAU GREECE

    ReplyDelete
  30. Michuzi ninaomba ulifanyie kazi wazo la jamaa hapo juu,tunaomba 'uorganize' utaratibu wa kumchangia huyu kijana, hii itaturahisishia sana kumchangia na kujua pia matunda/matokeo ya michango yetu ikiwa ni pamoja na kiasi gani kimepatikana,na matibabu ambayo ameyapata baada ya michango kupatikana.Ikiwezekana hata kutoa orodha ya waliomchangia hii itawahamasisha wanajamii, japokuwa unapotoa siyo lazima ujulikane kwani thawabu halisi utaipata kutoka kwa MUNGU.

    Pole sana kwa maumivu unayoyapata kijana, mtumainie MUNGU na suluhisho litapatikana utapona.

    ReplyDelete
  31. MASUDI NI VEMA HUYU KIJANA ANGEKUWA NA AKAUNTI NAMBA YA BENKI HIVYO TUNGETOA CHOCHOTE TULICHONACHO KUPITIA BENKI HAYA MAMBO YA KUMPA MTU HELA MKONONI YANA MATATIZO YAKE, NADHANI UMENIELEWA.

    ReplyDelete
  32. jamani tulisema aende kwenye maombi huku akiwa anasubiria michango yetu sio kwamba hatutachanga la hasha tutachanga sana tena nitamtumia michuzi moja kwa moja cdn $100 ili awafikishie walenwa straight!!
    mdau canada

    ReplyDelete
  33. Wabongo porojo-maombi is abt to be cheap. Hata mgonjwa na family yake wanaamini mungu na wanaomba pia. Jibu ni pesa na utaalamu vikiendana na sala/maombi.

    Tusioneshe kanisa gani wanajua kuombea bali tujioneshe sisi tuna upendo kiasi gani kwa kutoa michango ya kumsaidia. Tuache uzushi na porojo.

    Serikali ikishindwa sisi tuoneshe upendo wetu kwa kumchangia. Na sio kuitaja serikali wakati ndugu yetu anaumia.

    Kukiwa na program yoyote ya kumpokea nitachangia $10

    Email me mtanzania_2@yahoo.com kwa maelekezo. Ila niko US i dont know hw I can contribute

    Too much bla bla bla
    Wabongo tubadilike
    Upendo haumuhusu muombeaji wala serikali bali ni wewe tu.

    ReplyDelete
  34. Pole sana kijana Nurdin kwa matatizo yaliyokukuta.Lakini kitu kimoja nashidwa kuamini ya kusema kuwa ugojwa wako haujajulikana.na kwa vipimo alivyovitaja hapo ni kweli hawatojua ugojwa wako.kwani biopsy haijafanyika naona na hiyo ndiyo itakayoonyesha ana tatizo gani.ikiwa fine needle or open biopsy na ni kweli vitu hivyo havifanyiki ocean road bali huwa vinafanywa muhimbili na nilipokuwa Muhimbili pale nimeshapoka kesi kama hizo na nyengine zimetoka ocean road na mara nyingi sana biopsy result zao zinakuja wakiwa na Rhabdomyosarcoma.sasa nashidwa kuyaamini maelezo yake na na nina uhakika vitu hivyo vinafanyika Muhimbili na result zake unapata ndani ya eiki mbili.sasa sijui vipi au ni ujanja ambao huwa unafanya na wagojwa au ameshapewa option kusuhu tiba ya huo mguu wake kwa mara nyingi sana kesi kama hizo zinaishia amputation.

    ReplyDelete
  35. naungana na kıjana juu hapo,it looks like he has osteosarcoma,he needs biyopsi for comirmatıon and CT to look for any metastasis to other organs.no need kupelekwa nje ya nchi muhimbili can manage that case,what he needs is aid on(CT scan,or MRİ) and his operation fees

    ReplyDelete
  36. Nampa pole sana huyo kijana kwa matatizo hayo ya kuumwa. lakini nashauri ndugu zake kabla amjafikilia suala la kwenda nje kutibiwa! kwanza mpelekeni hospitali ya walemavu ya CCBRT msasani. anaweza kupona kabisa. wapo wengi nilio waona wakiwa na matatizo kama hayo na mwenyezi mungu kupitia madakitari wa hii hospitali wameweza kuwatibu na kupona kabisa. pale pana wataalam wa hari ya juu, juu ya matatizo ya namna hiyo.

    ReplyDelete
  37. HIVI NYIE MNAOSHAURI MASOCOMA,HOSPITALI, KUOMBEWA NA KAZALIKA MNAELEWA LAKINI POST INASEMAJE? MNACHOSHA TU MNGEJUA KAISHAPITA KOTE MNAKOZUNGUMZIA! NINGEOMBA KAMA MKIJISIKIA KUONGEA MPIGIENI SIMU MSITUCHOSHE HAPA. KAOMBA HELA SIO MAZUNGUMZO NA USHAULI. MI NATOA $50 NA NINGEOMBA ANAEFUATA ADONDOSHE UPETA APA BADALA YA KUHUTUBIA UPUUZI, HAKUNA DAKTARI, SHEHE AMA PASTA HAPA WOTE MNATUZENGUA KAMALIZIENI DIGLII ZENU MTAFUTE KAZI NDO MUANZE KELELE.

    ReplyDelete
  38. wewe kijana hapo juu inaonyesha hata kiswahili hukijui au una tatizo la kufahamu.wewe kama unatoa hela is good for you. lakini ninachokuambia kesi kama hizo tanzania zinatibiwa na tumeshazitibu kibao nilipokuwa.sasa siamini kabisa huyo jamaa anaposema tatizo lake halijajulikana kwani mtu yeyote ambae amepitia medical school anaweza ku kusema ni kitu gani bila hata ya hiyo biopsy.na mimi sina haja ya kumaliza hizo degree kwani nimeshachukua Phd na sasa nafanya fellowship.najua mtu wa hapo juu huwezi kufahamu naongea kitu gani.lakini tupo hapa kwa kumpaushauri na ambao utakuwa rahisi zaidi kwake yeye kuliko kutaka kwenda nje ya nchi.Sikatazi kumchangia kwani hizo hela zinaweza kumsaidia hata kama atatibiwa pale TZ.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...