Mambo vipi mkuu wa nanihii?
Naomba unipostie swali langu kwenye blogu yetu ya jamii.
Nauliza wapi ntapata Appartment za bei affordable hapo Dar kwa siku kumi tu za mwezi wa nne mwaka huu, NB ziwe fully furnished na appliances zote muhimu , nimecheki nyingi online zinapangishwa kwa muda mrefu ambao sitouhitaji na bei zake ni za kitalii zaidi na kwa mimi mzalendo inakuwa matata kidogo kuweza kujikakamua.
Kama Kuna mtu anataarifa au maelezo naomba acomment kwenye post hii contact details za hizo appartment na bei zake kama anafahamu, websites zitakazoonyesha picha mbali mbali za appartment zitasaidia zaidi.
NB: BUDGET YANGU haizidi Tshs 50,000 kwa siku.
Shukran bwana Michuzi,
Shukran bwana Michuzi,
mmhh kweli mambo yako mazuri,kuna tausi gest pale moroco
ReplyDeleteRamada hotel
ReplyDeletekwa nini usiende kulala kwenye gesti/ hoteli nyingi za kizalendo mbona bei poa sana. Tena Tsh 20, 000 kwa siku na vile vile unakula chakula bei poa. inategemeana wee upo wapi?
ReplyDeleteukijibu unataka kukaa wapi hapa dar basi nitakupa sehemu poa.
mdau
siko bongo kwa muda kama mizi 6 lakini sidhani kama bei itakuwa imepanda sana kuna apartment msimbazi centre na bei yake si kubwa na ni rahisi kwa city center movement kama unataka nzuri lakini za bei rahisi pia ujiandae kwa foleni za dar kuna kituo cha masister kinaitwa agape pametulia sana ila ni nje ya muji au mbagala mission ila kote huko foleni mwanangu unaweza ukalia ai utakuwa unawahi asubuhi sana kwenye saa kumi au kumi na moja kasoro kukwepa foleni.
ReplyDeleteJamaa aliyetoa comment ya kwanza yuko right kabisa, Hotel za kinondoni utapata kile chumba kizuri kabisa kwa TZS 40,0000 hadi TZS 50,000. Ila kwa uhakika kabisa ni TZS 40,000 kwani hata mimi nimewahi kuishi kwenye hizo hotel nilivyokuwa likizo. Sikumbuki jina Ila ni hotel moja karibu ya Vijana-kinondoni,bado mpya mpya........I can say, it is value for money!
ReplyDelete$40 apartment fully furnished with all appliances in Dar?? You must be joking!!
ReplyDeleteFor that budget try a normal hotel room in the areas ambazo wadau hapo juu wamekueleza.
Karibu Dar.
Broh,
ReplyDeleteUlizia watu unaowafahamu utafute jinsi ya kuwa roomate for a few days. Watanzania ni wakarimu sana utashangaa....especially kama unatua kutoka nje (LOL). Na asikwambie mtu, watu wengi wata-entertain idea ya kuingiza hela zaidi kidogo kwa siku chache utakazokuwa hapo. Kama ukipata mtu atakayekukubalia, usisahau japo vizawadi vidogo kutoka ulaya...just to show your appreciation and build a friendship bridge, badala ya strictly business. Next time ukirudi they will be the first to extend their invitation to you.
ndugu ,karibu bongo ,nimekuulewa zaidi. unachotaka ni aprtment , mimi ninazo nitakupatia bedroom 1 , kitchen1 livingiroom . dstv , ac , , unasafishiwa nyumba kila siku, shuka zitabadilishwa wiki mara 2 . kwenye apartment hii maximum watu 2 tuu . utapikiwa breafast wewe ni kukunua chakula chako tuu
ReplyDeletesh 50,000 kwa siku .iko kijitonyama
wasaliana nami ili nikutumie picha , greenparkvillage@hotmail.com
mie nina chumba sh 1200.00 kwa siku lakini maji unajichotea kwa jirani sabuni uje nayako lakini bafu ya ndoo au beseni mashuka yako godoro lakoukiondoka unaliacha bei poa nicheki kigogo mwisho jirani yangu ni kibaka kwa usalama wako usiseme ulikotoka
ReplyDeleteSwali kwa mdau wewe ni wa jinsia gani? Ongea vizuri na anko masupu kuna gheto anaweza akakupangishia kwa bei poa kabisa. Lakini wewe mdau unauliza aprtment kwa siku 10 wewe unatania mbona majibu unayo mwenyewe, fikia guest house ina kila kitu, apartment siku 10 there is no way ukapata kwa hizo siku chache! atleast miezi 3 nitakubaliana na wewe! Swali na shida yako haina msingi tena unabahati watu wamekuheshimu wewe anko siku nyingine message kama hizi wala usiangaike kupost watu wanafanya utani sasa na blogu ya jamii ! alaaaaa! Usirudie tena kuuliza swali kama hili!$#@$%*$&&)*@&$!!?
ReplyDeleteMlimani city kuna appartments unaweza kufanya contact nao
ReplyDeleteShukran Sana mdau Tarehe Sat Feb 06, 11:21:00 PM, Naomba usome email yako kwa maelezo zaidi.
ReplyDeleteKUNA HOTEL KIJITONYAMA SAYANSI NI PAZURI HATA WAFANYAKAZI WENZETU WAKIJA KUTOKA NCHI MBALIMBALI WANAFIKIA HAPO NA WANAFURAHI SANA
ReplyDeleteTHE GRAND VILLA
EMAIL: gm@thegrandvillatz.com
simu +255 773 / 715 /784 - 167700
au COLLUBUS HOTEL
EMAIL: info@collubustours.co.tz
kaka unapata shida ya nini, njoo ukae kwangu, nitakuachia room mie nitakuwa nalala sebuleni, housegirl wangu atakuwa anakuandalia kila kitu, utanipa elfu 40 kwa siku, wasiliana nami.
ReplyDeleteSylvia
KWA HIYO PESA USIHANGAIKE KABISA NITA KU-HOST UKISHUKA TUU EAPOTI CHUKUA BAJAJI MPAKA VINGUNGUTI MWAMBIE AKUACHE MACHINJIONI, UKIFIKA PALE UTAONA KUSHOTO KUNA WAMAMA WANAUZA VYAKULA PEMBENI YA BALABALA KATISHA KATIKATI YAO KUNA UCHOCHORO UNAINGIA KWANGU NENDA KAMA MITA ISHIRINI UTAKUTA KUNA GOFU MOJA VIJANA WAMELIGEUZA KUWA CHOO ACHANA NALO KATISHA KUSHOTO UTAKUTA MATEJA WANACHEZA KAMALI(ukifika hiyo sehemu zima simu ifiche) WAULIZE KWA BABA TIZO(fundi saa). WATAKULETA CHUMBA KIPO NA FULUFANISHDI BEI NI SHIRINGI ELFU SABA KWA SIKU JAPO MAELEWANO YAPO. MSOSI FRESH UPO KWA MAMA TABU UKITAKA KESHI AU BILI HAISUMBUI.
ReplyDeletenyambaff sana hajasema anataka gesti au hoteli anataka apatimenti huo ushuzi wenu mnaouandika sijui gesti haihusu eleweni swali raha ya apatimenti uko huru zaidi ya hivyo vigesti vyenu unajipikilisha kwa sana kama vile mtu uko hm tuu na mtu anapoomba ushauri mijitu mingine inaleta pumba zao ovyo sana hivi hamkui tuu ebo!!
ReplyDeletemweeee yani ulivo na matusi unataja kianzio kwa SIKU ekfu 50???
ReplyDeletehaki ya nani wee aya weee,una bahati ujasema jisnia yako
Wala usiangike nitakupati hiyo appatimenti karibu kabisa na katikati ya jiji tena kwa bei poa kabisa. Shilingi 5900/= kwa siku. ila uwe na ujuzi wa kuogelea kwani appartmeny yangu ipo katika bonde la jangwani na mwezi huo ni wa mvua kubwa Hivyo lazima ukae kimachale. Huduma nyingine zote zipo
ReplyDelete