Mheshimiwa anko Ankal,
Mimi ndugu zangu nipo hapa Uganda najibebesha maboksi yangu na ni mzaliwa wa mkoa wa Kagera lakini kama mjasiriamali kuna kitu hapa Uganda kimenikera na kunifumbua macho nakuona kuwa kweli Wabongo bado tumelala na wanzetu wanapiga kazi kwa kwenda mbele!

Issue yenyewe nikuwa waganda wanakuja kwetu Karagwe wananunua ndizi kwa bei ya kutupa na wao wanazipark vizuri zinapelekwa USA na UK kama organic food na wanauza kwa bei nzuri nafikiri lakini juu ya yote ndizi za KARAGWE na box zimeandikwa UGANDA PRODUCE! Shame on us!

Kwa kutambua uwezo wa wadau wa blog hii tukufu nawaomba wadau wan je na ndani wanipe mwanga jinsi yakupata masoko nje au wanipe link niweze kuzifuatilia nakuanza pia kuingiza bidhaa kama hizo nje kwani ndio njia pekee ya kujikwamua sisi wabeba box na nipo tayari kushiriki na mshirika yeyote ambaye yupo makini kwa kuwa huu ni ulimwengu wa e-business nina uhakika wadau mtaniunganisha ipasavyo ili nasisi tuonekane na bidhaa zetu sio watu wanatutumia tu.
Nihayo tu wadau kila la kheli Ankal!
MDAU
UG

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Mzee Mwijage!
    Hongera kwa kufumbua macho, sisi watanzania wengi tunajua siasa! Mimi sio mfanyabiashara, ila kwa mtazamo wangu wa haraka ni kwamba ni vyema kwa watanzania ambao wapo nje na wanafanya biashara wajitokeze ili wawe wadau sahihi wa kutafuta soko au kukuunganisha na soko, maana hao wenzetu ndivyo wanavyofanya. Nami nadhani kuna bidhaa nyingi tuu tunaweza kuzitoa TZ zikaletwa ulaya, cha ajabu unakuta hata ktk baadhi ya miji kuna maduka ya waghana, nigeria uganda kwa wingi zaidi. Ombi kwa wadau waishio nje ya nchi tuwe wabunifu wa biashara za bidhaa toka home maana kwa kufanya hivyo tutatengeneza pesa na kuongeza ajira. Ni mtazamo tuu wadau!

    ReplyDelete
  2. Wazo Zuri.

    Kusema ukweli kwa biashara za vyakula sina uhakika zinakwenda vipi ila kwa ninavyofahamu, lazma ujue unataka kupeleka nchi gani. Alafu ukishajjua hilo then serikali huwa inalist ya bidhaa ambazo zinaweza kupelekwa kwenye iyo nchi, yaani kuna agreements za International trade...kujua zaidi unawasiliana na ubalozi wa Tanzania katika hiyo nchi halafu wao wanatakiwa kukupa mwanga zaidi. Yaani, watakupa link au source za information ambazo zitakua ni kama dira ambayo inaelezea mahitaji ya mtu anaetaka kuuza bidhaa kwenye nchi hiyo then hapo ndio mwanzo ulivyo. Usitishike na hii theory, practically things happen simultaneously.

    ukishajua nchi unayotaka kujaribu kuuza bidhaa zako, tujulishe labda tunaweza kutoa msaada zaidi wa mawazo.

    Ni hayo tu

    ReplyDelete
  3. Bwana Mwijage

    kwanza nikupongeze kwa ujasiriamali ulikokuwa nao.

    Ndizi huuzwa huku kwa kama $0.60 kwa pound rejareja, wenye maduka hununua kwa kama $0.30 zisizo organic na kama $2 kwa pound for organic kwa pound. Gharama za kusafirisha perisheble bidhaa kutoka TZ hadi huku ni kama $3.00 per pound.

    Kwa data hizo za harakaharaka ni kwamba hata kama wewe unatapa ndizi zabure zitakugharibu $3 kufikisha huku amabayo iko juu.

    Ndizi nyingi za US hutoka nchi za karibu kama Mexico, Colombia etc.

    Huenda kuna nafasi nzuri ya kuuza Europe kuliko USA. Jaribu kuzungumza na ofisi ya Ubalozi wa US, kitengo cha biashara.

    Ama tafuta mtu atakayeweza kukufanyia utafiti huku kupitia rekodi za ofisi za biashara amabazo ni public information.

    Ni hayo tu na nakutakia kila la heri katika shughuli zako.

    (US Bogger)

    ReplyDelete
  4. Ni kweli hata huku UK,waganda ndio wanaoleta vyakula, na bidhaa nyingine kutoka East Africa,sisi wabongo tunaongoza kwa kuleta madawa ya kulevya.

    Mimi,uk.

    ReplyDelete
  5. Huu ndo ujinga wa serikali yetu hii, yaani fursa zinaenda kwa majirani na si sisi! Angalia mfano wa biashara ya maua Northern regions yaani Manyara, Arusha na Kilimanjaro! Wale wakina mama wamehangaika weee miaka nenda rudi sasa bishara imekua na imeanza pata recognition, baada tu ya kuweza ku-secure Cargo flights (with the assistance of USAID) from KIA watu wa TRA wamewabandika VAT 18% kwa bidhaa zinazotolewa KIA sasa najiuliza hao TRA na huyo Mh wetu Mkulo yaani waziri wa fedha walipokuwa wanapanga hiyo VAT hawakufikiria kuangalia mazingira ya ushindani yaani ni vp majirani zetu wanafanya (yaani Jomo Kenyatta Airport)? au ndo mambo ya kisiasa zaidi wenyeji wa huko wasifaidike?
    Jamani mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni wale wakina mama wa maua wamehangaika na msiwaangushe mnatakiwa kuwapa moyo hiyo mbiu ya Kilimo Kwanza mbona huyo Mkulo anaenda kinyume?

    ReplyDelete
  6. Si mnakataa dual citizenship? shauri yenu...

    ReplyDelete
  7. MZEE MWAIJAGE USISHANGAE, HIYO NDIO KAWAIDA YETU WADANGANYIKA, TUMEZOWEA KUTAFUNIWA, NA IKIWEZEKANA TUMEZEWE VILEVILE. DR. MBELE ALIJARIBU KUWAAMSHA WATU, LAKINI MATUSI ALIYOPATA NADHANI MWENYEWWE KAJUTA.
    HIYO YA NDIZI NI TRAILOR. NGOJA JUMUIYA YA EA ICHANGANYE NDIPO TUTAKAPO CHEZA MASANTULA BILA JASHO. WAKENYA HUKU UGHAIBUNI WANACHEKELEA, WANASEMA WATANZANIA HAWANA HARAKA, WANASEMA TUMEZOEA KUPUNGA MKONO WAKATI TUNATEMBEA; LABDA NDIO MATUNDA YA MAREHEMU MWALIMU AU LABDA HUO NDIO MUSTAKABALI WETU, SIJUI.
    KWA KWELI SAFARI YETU BADO NDEFU SANA.

    ReplyDelete
  8. ADILI NA NDUGUZEFebruary 19, 2010

    Ndugu Mwijage siyo ndizi tu. Kule wilaya ya Karatu about kilometa 300 hadi Nairobi and less than that to Namanga border, kuna eneo linaitwa Mang'ola ambapo vitunguu vinastawi sana. Wakenya huja na kununua na kupakia kwenye malori yao hadi Nairobi. Wakifika kule they sort and pack them and export to Dubai as Produce of Kenya. Hiyo ni mbinu ya marketing. Na hivi sasa tuko kwenye soko moja la Afrika Mashariki, Watz lazima tuamke.

    Si hio tu. Makampuni ya kitalii ya Afrika Kusini yanatangaza nchini Thailand kuwa ukitaka kwenda Kilimanjaro ni masaa matatu tu kutoka Joburg. Again it is a marketing gimmick. Kwa mtu wa Thailand anaamini kabisa kuwa Kilimajaro iko South Africa. Hiyo ndiyo biashara ndugu yangu.

    Tuache kulia ila tujue nafasi yetu ni ipi halafu tuchangamke. Na tuachane na mazoea ya kijinga ya kuilaumu serikali na kumlaumu JK kwa failure zetu wenyewe. Serikali imetengeneza mazingira tuyatumie. So Tanzania WAKE UP

    ReplyDelete
  9. Mdau ulietoa mada si ndizi peke yake tunazopoteza. Nenda Iringa wakenya kibao wamejaa wananunua mbao na magogo kwa bei che yanapelekwa Mombasa yanapigwa stamp Product Of kenya then wanaexport na kula dola zao safi. Kifupi ni kwamba sisi ni shamba la bibi.

    ReplyDelete
  10. mimi sioni tatizo liko wapi hapo. Waganda ni Watanzania na watanzania ni waganda. Hii ni kwa mtazamo wangu mimi kama mwafrika. Tukiwa na mitazamo kama hii, mwishowe tutaanza kusema, ..."kwanini wanyakyusa wanakuja kukunua nyumba Tanga?"

    mimi wala sioni kama tunaibiwa hapo, ukizingatia kwamba kama hao waganda wasingezinunua hizo ndizi, basi zingepikiwa pombe tuu na kuchangia kueneza ukimwi, na nyingine zingeoza tuu.

    Wanaotuibia ni wazungu makaburu. Makaburu wanachukua migodi, na kuajiri watanzania wachache wenye degree zisizokuwa na elimu na kuwapa mishahara minono sana. Hawa watanzania kwa mishahara wanayopewa hawana hata muda wa kukaa na kufikiri kwamba tunaibiwa tena tunaibiwa ile mbaya. Kama tunataka kuzuia wizi basi ni kwenye migodi, na wala siyo kwenye ndizi.

    ReplyDelete
  11. Mimi nafikiri watanzania tulishanasa pabaya, itatuchukua miaka miingi mno kutoka kwenye mtego huo. Ni sawa na triangle ya ujinga, umasikini na maradhi yanavyotegemeana. Ukishakuwa masikini utaendelea kuwa mjinga na huo ujinga utakufanya uwe mgonjwa kwa muda mrefu na utashindwa kufanya kazi zako kwa hiyo utakuwa maskini na kuendelea kutomudu gharama zote za lazima na utaendelea kuwa bwege na mzunguko utaendelea unless kuwe msukumo kutoka sehemu fulani.
    Kwa maana hii watanzania (walio wengi) ili watoke kwenye uzubaifu huu lazima kuwe na msukumo fulani, na mimi naona msukoma huu uko mikononi mwa viongozi wetu; waondoe vizingiti kama vya uraia mmoja, kuwe na masharti nafuu kwa wafanyabiashara, wazuie wizi wa waziwazi kama wa migodi yetu na mambo mengi mengine.

    Kazi ipo!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  12. us Bloger nimekukubali una data za nguvu endelea na moyo huo tutafika tu nafikiri mdau mwenye hoja kakupata vizuri tukaze buti

    ReplyDelete
  13. wala si uongo tunanunua hapa sweden pia kwenye mabox zimeandikwa made in uganda,box moja km kilo 7kr 300 ambayo ni sawa na 50000,kweli wabongo tunalala sio siri.watu wanaleta visamvu,matembele mihogo,kambale,viazi na kila kitu toka kwao afrika sisi tumekalia majungu tu na kuchomeana imigration kama yule hana karatasi,wabongo wachawi kwel kwel

    ReplyDelete
  14. we mtoa maada bongo kubwa msipende kutujumuisha watz wote kwenye mambo mliyoshindwa nyie kama kulala mmelala nyie wenyewe huko bukoba na musoma wanakoendekeza kuuana mimi nimeona wafanya biashara wanatoka makete wanapeleka mbao komoro watu kwingine wameamka tatizo lenu nyie shomile tangu zamani mlikuwa mnajifanya mko matawi.kumbuka banza stone aliimba UPATAPO FAHAMU JUA UMEPOTEA.

    ReplyDelete
  15. mjomba hapa kwetu ukitaka kupeleka bidhaa nje hizo kodi utazoletewa itakuwa ni siri yako, mara ooh hairuhusiwi kuuza chakula nje nk lkn wenzetu hawana mavipingamizi ya kipuuzi kuuza vitu nje

    ReplyDelete
  16. Sie tumezoea kulalamika tu kazi kujituma hatutaki,haya hao waganda wanawalazimisha hao jamaa zako wawauzie hizo ndizi? kumbuka ule usemi" panapo miti ni nadra kupata mjenzi" Tuombe pengine twaweza badilika na kuacha tabia yetu hii iliyojengeka miongoni mwetu ya kupenda vya rahisi. Nakushauri nawe ukanunue hizo ndizi ujaribu kuzipeleka kunako walaji uone kama ni rahisi hivyo kama hadithi yako.

    ReplyDelete
  17. Wabongo hatujalala wewe ila hao jamaa wengine ndio sio WAAMINIFU. Kama bidhaa zimetengenezwa Tanzania kisha wao wanasema ni za Uganda au Kenya hayo sio makosa yetu! kwani hao WaUganda wangekuwa waaminifu kwa wateja wao wangeeza kusema produce of Karangwe, Tanzania, Distributed by XYZ of Kampala, Uganda.

    ReplyDelete
  18. MDAI NI WAZO ZURI LAKINI INFASTRUCTURE YA KUFANYA BISHARA MBOVU. NIKUULIZE KUTOKA KARAGWE HADI UGANDA ENTEBE AIRPORT NI MUDA GANI UNACHUKUWA NA KUTOKA KARAGWE NADI DAR ESALAAM NI MUDA GANI. WMIMI NAKWENDA KARAGWE TAKRIBAN KILA MWAKA NA NAJUWA MAZINGIRA YA HUKO. INABIDI UWE NA CHAIN YA KUSAMBAZA IMARA...NDUGU YANGU HUKU UK NI GHALI SANA HIZO NDIZI KWASABU YA USAFIRISHAJI...

    ReplyDelete
  19. Mimi nadhani tusikatishane tamaa tulilaa na sasa tunaamka kila kitu kinawezekana. Tatizo ni msingi wetu ndo unatutatizo wa ujamaa amabo nia ni kujitosheleza kwanza. Hawa wanaokuja kununua hawafikili hili bali ni faida tu mwisho wa siku njaa mikoa yetu. Serikali ijitahidi kujenga miundo mbinu na kupunguza urasimu ili kurahisisha mauzo ya bidhaa zetu. Hawa kama ni wezi Bob marley anasema 'Time will tell' Dunia itajuwa kuwa hivi ni vya Tanzania. Mbeba mabox Uganda fanya search huko uliko ujuwe mbinu wanazotumia then uje uziemploy huku nyumbani..Ndivyo wachina wanavyofanya kokote waendako, akija kwetu anaona kinyago cha mpingo yeye anatengeneza cha plastic!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...