Rais Mstaafu wa Chama cha Wanafunzi waishio Bangalore (TASABA) Bw. Baraka Kange akizungumza na waandishi wa habara mara wakati wakisubiri kupokea mwili wa Mwanafunzi aliyeuwa nchini India katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo. Kushoto kwake ni Babu wa marehemu, Balozi Abubakar Abrahim
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Imran Mtui likiingizwa kwenye gari tayari kwa kusafiri kwenda Moshi.
Dada wa marehemu na waombolezaji wakilia kwa uchungu wakati jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa kusafirisha mwili kwenda moshi Mjini kwa mazishi. Picha zote na Pete Masangwa

Habari Kamili ya msiba huu wa kusikitisha
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. RIP Imran- tunataka Govt. itoe tamko kuhusu kifo hiki.Inahuzunisha sana.

    ReplyDelete
  2. Membe waziri wa nje yuko wapi? naona katia kichwa kwapani anashindwa hata kulaani. Hivi hawa mawaziri wanje wanasubiri tu kuandamana na raisi? nchi hii bwana!

    ReplyDelete
  3. Innalillahi wainna ilayhi rajiun poleni sana wafiwa M/Mungu amlaze marehemu malazi mema peponi

    ReplyDelete
  4. Natoa pole kwa familia. Kweli ni huzuni usiosemekana.

    Mimi sikumfahamu huyu kijana wala familia yake siifahamu lakini imeniuma sana.

    Hizi ndo news za kuweka hewani mkieleza ufuatiliaji wa nani alifanya unyama huu na malipo (kama yapo) kwa familia iliyomtegemea huyu kijana kuliko kila siku kujadili sijui afande katamka eti 'elektronishi' au eti Jerry kumbe alinunua pingu sijui ya kunogesha mapenzi, upuuzi mtupu.

    Hiyo ni kesi kama zingine ambazo kuna wengi sana huko rumande na hata mafaili yao hayajakamilishwa eti upelelezi unaendelea.
    Sheria ichukuwe mkondo wake.

    Na ni aibu kusema eti kesi ya Jerry ikamilishwe mapema, je ni nani anayewasemea au kuongeza spidi kesi za wengine maskini tena walio rumande muda mrefu sasa ambao wengine wana mwaka na zaidi na hukumu bado. Vyombo vya dola haviko kwa ajili ya watu fulani wachache tu!

    Kwangu mashauri yenye kipaumbele ni kwa familia ya watu kama hawa na yule kijana (Fundikira?) aliyeuawa kwa kipigo na Wanajeshi, aliyeuwawa na Kiongozi kwa kukwaruza Prado na wengineo ambao wamekatishwa maisha yao kinyama na wale walioko magerezani wakihangaika kupata mlo toshelezi (not balanced), wakisukumana kupata nafasi ya kuweka ubavu na katika mazingira magumu ya kutengwa na jamii nyingine.

    Media, Mambo ya nje, Mambo ya ndani na Ubalozi tupeni habari ya kifo cha huyu kijana ambaye familia na Taifa lilimtegemea na tujuwe familia yake inasaidiwaje?

    Angalia mfano USA wanatua tu Haiti, pamoja na kutoa misaada wanaanza kutafuta Wamerekani waliojeruiwa au kuhangamia huko ili taratibu ya kuwatambuwa na mafao yanayopaswa yashughulikiwe kwa familia zao!

    Uhai wa Mtz ni kwanza popote alipo ndipo mambo mengine ya kurejesha hadhi ya mtu au kusafishana yafuatwe!

    Habari ndo hii!

    ReplyDelete
  5. MICHUZI EBU TULETEE HABARI NZI YA CHANZO CHA KIFO CHA MPENDWA WETU WENGINE HATUJAPA, JE NI AJALI AU KUNA MKONO WA MTU?

    ReplyDelete
  6. Inatia huzuni sana.Poleni waifiwa.
    M/Mungu amuweke mahala pema peponi. Amiin.

    Membe mwite balozi wa wahindi. Mpe huzuni ya Taifa kwa kuuliwa kijana wake. Tunaata taarifa kutoka serikali ya wahindi kupitia huyo balozi jinsi gani wanachukulia ulinzi wa vijana wetu huko. Hatua gani zinachukuliwa kukomesha mauaji ya vijana wetu huko.

    Mdau

    ReplyDelete
  7. Michuzi asante kwa kuendelea kutuhabarisha,lakini kapteni Ibrahim umemzeesha sana.

    ReplyDelete
  8. RIP brother Imran

    ReplyDelete
  9. Nimepata habari hizi hapa blog ya jamii kwa mshtuko mkubwa sana. Pole kwa sisi sote kwani Imran ni mdogo wangu tangu Majengo,Moshi; Mawenzi Sec. Kilimanjaro,kwenye fcbk ni rafiki yangu na nakumbuka hata tulipochat mara ya mwisho na kunifahamisha safari yako ya Moshi.Tupo nawe kiroho daima,tutaonana Mungu akipenda Imran.
    R.I.P IMRAN.
    DIDI VAVA.

    ReplyDelete
  10. r.i.p bro klm-tz(same struggle like og show us the way) promise for retaliation

    ReplyDelete
  11. Kwahiyo mwili umekuja bila kichwa? maana nilisikia hakikukutwa.
    So sad jamani. RIP comrade

    ReplyDelete
  12. mungu amlaze mahali pema peponi na awape familia nguvu. Nimesoma kwenye news kuwa balozi wa india tanzania kasema yeye hajasikia kitu kama kijana wa kitanzania kuuawa india bila hata kuonesha remorse kuwa atafuatalia au nini. je hii inawezekana kuwa honor killing maana wahindi wanajulikana sana kwa hizo na kuua waafrika au hata wahindi wenzao ambao ni lower cast wanapokua na wasichana wao au wanapotaka kuoana nao etc? au nini wenzake wanasema inaweza kuwa sababu?

    ReplyDelete
  13. we mtoa maoni Tarehe Fri Feb 05, 10:34:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous ur joking eh?

    ReplyDelete
  14. No mtoa maoni 10:34am is not joking. Hata mimi nimejiuliza swali kama hilo

    ReplyDelete
  15. kwa kweli jamani huku india we are very disappointed..the worst thing ni kwamba bado hatujui what happened...yani this issue is not anyway in the news wala newspapers,indians are full of shit na ni wabaguzi sana...jamani,tunaomba msaada huku cause ubalozi hata hautusikilizi...its not safe huku....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...