Ankal Michuzi,
hii nilikutumia asubuhi, lakini tumepata habari za uhakika juu ya sakata zima la kutaka kumnusuru huyu mwarabu Mohsen Shousha,Habari za uhakika tulizozipata kutoka duru za kipolisi ni kwamba inasemekana tayari rupia imeshapenyezwa pale Central na sasa kuna juhudi za makusudi zinazofanywa na askari anayeshikilia hilo jalada ili kumnusuru mwarabu huyo asifikishwe mahakamani kama ilivyotarajiwa.
Leo kijana aliyefungua kesi hiyo alishauriwa na askari amalizane na mtuhumwa kule kazini, lakini kijana akakataa akitaka shauri hilo lifikishwe mahakamni ili haki itendeke.
Baada ya kuona kijana kagoma ku-withdraw hayo mashtaka, huyo askari akamwambia aache namba ya simu ili wawasiliane, mchana huu amempigia simu akimtaka aachane na hiyo kesi kwa kuwa haina ushahidi, lakini kijana amesisitiza kuwa kesi ipelekwe mahakamani na mshahidi watajulikana huko na sio polisi.
Inaonekana kama kuna juhudu za makusudi za kutaka kumnasua mwarabu huyo baada ya kutembeza mlungula.
Mpaka sasa kijana bado ameshikilia msimamo wa kutaka mtuhumiwa afikishwe mahakamani na anayo RB ya kesi hiyo mkononi ambayo ni CD/RB/1169/2010.
Tunakuomba uiweke hii habari katika blog ya jamii ili wadau waone jinsi haki inavyotaka kunyongwa kwa sababu ya pesa.
-----------------------------------------------
MWARABU MTUKANA WATU WA MOVENPICK AFIKISHWA POLICE CENTRAL KWA MATUSI YA NGUONI.
Ankal Michuzi,
kwanza sisi wafanyakazi wa Hotel ya Movenpick Royal Palm Hotel Dar Es Salaam, tunatoa shukrani za pekee kwa blog ya jamii kwa kutupa nafasi katika blog hiyo kufikisha malalamiko yetu kwa jamii.
Kama unakumbuka juu ya malalamiko yetu kuhusiana na uongozi wa Hoteli hii hasa unaofanywa na mkurugenzi msaidizi ndugu Mohsen Shousha, mpaka kufikia kutaka kuajiri meneja rasilimali watu kutoka nchi jirani ili aweze kutunyanyasa vizuri.
Baada ya malalamiko yetu kutoka katika blog ya jamii, inasemekana vyombo husika vilianza kufuatilia, na kama kawaida meneja huyo msaidizi alitaka kupenyeza rupia lakini ikashindikana kutokana na labda mambo kuwa magumu. Hata hivyo amesisitiza kuwa atahakikisha anatumia kiasi chochote cha fedha kuhakikisha kuwa anatimiza azma yake hiyo.
Kutokana na hatua yake hiyo kukwama, ndugu Mohsen Shousha amegeuka kuwa mnyanyasaji mkubwa wa wafanyakazi na amekuwa akitumia matusi ya nguoni kuwanyanyasa wafanyakazi , bila sababu ya msingi. Kutokana na baadhi ya wafanyakazi kuwa waoga wa kupoteza ajira zao wamekuwa wastahimilivu huku wakiendelea kunyanyaswa ndani ya nchi yao.
Hivi nkaribuni kuna mfanyakazi mwenzetu mmoja ambaye ni kibarua, alikutwa na meneja huyo msaidizi akiwa anasafisha meza baada ya wageni kuondoka lakini meneja huyo bila sababu ya msingi akamwambia kwa kingereza, naomba ninukuu, ‘you casual if yo still my money, I will fuck you up’ mwisho wa kunukuu.
Akiwa ameshikwa na mshangao kijana huyo alimuuliza kosa lake lakini alisisitiza kauli yake na kumwambia aondoke nyumbani mpaka atakapoitwa, kisha akaondoka. Hiyo ndio kawaida yake kuwatukana wafanyakazi bila sababu za msingi hapa kazini, tena wakati mwingine huwadhalilisha kwa kuwaofokea mbele ya wateja.
Mfanyakazi husika alilifikisha swala hilo kwenye ofisi ya Human Resources hapa kazini lakini halikupewa uzito unaostahili, na baada ya kuona kuwa anaweza kupoteza haki yake akaona ni vyena alifikishe swala hili Police. Kwa kuwa Hoteli hii iko katikati ya jiji, kijana huyo alilifikisha swala lake Police Central na jana mtuhumiwa alikamatwa na kupelekwa Police Central kwa mahojiano, ambapo inasemekana alikanusha madai hayo.
Mtuhumiwa aliachiwa na kurudi kazini lakini kama kawaida, alitamba kusema kuwa hata tufanye nini hatumuwezi, kwani pesa inaongea. Aliongea kwa kujiamini sana na kutamba kusiko kawaida.
Sasa sisi wafanyakazi tunajiuliza kuwa ni watu gani hasa wanamlinda mwarabu huyu jeuri, na wanapata maslahi gani kwake?! Haiwezekani ndani ya nchi hii kuwe na mtu tena mgeni awe na jeuri kubwa kiasi hiki kiasi cha kutamba kuwa anaweza kutumia pesa kufanya atakalo.
Je mtu kuwa na pesa inahalalisha kuwa juu ya sheria, na kama ni hivyo basi wanyonge tumekwisha maana sasa, wanyonge hatuna pa kukimbilia. Ukweli ni kwamba huyu mwarabu siyo mwenye mali yeye ni mfanyakazi ambaye yupo kweny payroll kama mfanyakazi mwingine yeyote katika hoteli hii,mwenye mali mwenyewe yupo SAUDIA wala huyo mwenye mali hamjui Shousha hata kwa sura! Ni meneja wa mauzo tu ambaye amebadili cheo na kuwa meneja mkuu msaidizi ili apate kibali cha kuendelea kuishi na kufanya kazi nchini baada kibali cha kwanza kuisha muda wake!
Mpaka sasa kuna juhudi kubwa zinafanyika kutaka kuizima hiyo kesi, lakini mlalamikaji anasisitiza suala hilo lifikishwe mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake, upo uwezekano kesi hii ya aina yake ikatinga mahakamani kesho.
Tunaomba mamlaka husika hasa mkuu wa Police IGP Mwema na DCI Robert Manumba walifuatilie swala hili kwa undani ili wajue kiini cha jeuri hii, Mwarabu huyu anadhani kwa kuwa amemudu kuishika TIC kwa kuwapa rushwa anadhani anaweze kuishika serikali nzima, kwani yeye ni nani hasa ndani ya nchi hii kuwadhalilisha watu wazima kwa matusi ya nguoni.
Tunaomba kilio chetu kiwafikie wahusika ili hatua za kisheria dhidi ya mtuhumiwa zichukue mkondo wake vinginevyo tutaamini kuwa huyu bwana yuko juu ya sheria.
Ni sisi wafanyakazi wa
Movenpick Royal Palm Hotel
Dar Es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. kaka Wega ni hapa nchini anatuhuma za ubadhirifu juu ya ofice mpaka Mh Pinda akamsimamisha kazi kwa kula hele za miradi ya maendeleo ktk wilaya yake huyu jamaa anatumia mwaya huu kufanya serikali isahau mambo yake na kuweka usaniii mbele ya jamii imwonee uruma kwanini pcb waanze uchunguzi wa Jerry pamoja na huyu Wega kwa sababu wote ni watuhumiwa

    ReplyDelete
  2. sitafanya tena mikutano yangu hapo. that ii not a human rights

    ReplyDelete
  3. WEWE MFANYAKAZI ACHA MDOMO MKUBWA NA KULETA MAMBO YA KIBAGUZI! USITAKE KUPATA PUBLIC ATTENTION, HAYO NI MAMBO YA KAWAIDA YA KIKAZI EVERYWHERE IN THE WORLD, DEAL WITH IT WITHIN YOUR ORGANIZATION!
    KAMA VIPI HAMA KAZI, KWANI HAMNA MABOSS WA KISWAHILI WANAFANYA VITUKO KAMA HIVYO?
    SIO LAZIMA MLETE MAMBO YA WARABU NA UHINDI........

    ReplyDelete
  4. Mh! mbona maoni aliyotoa mdau hapo juu hayaendani na kisa cha hao wafanyakazi wa Movenpick!?.Mi naona sasa busara zitumike katika kutoa maoni,kama suala linamuhusu Jerry Muro changia katika habari inayomuhusu sio kuchanganya habari.
    Mdau-India

    ReplyDelete
  5. inabidi muwe mnarekodi kilalitu kuhusu hali itakayo tokea ili kuwe na ushahidi wakutosha sikuizi watu wanakuruka kama huna ushahidi wakutosha,sim zenu hizo ndio mtumie kwa matukio,watanzania wote wanatakiwa wajifunze kufanya hivi inasaidia kumkamta mhusika kiulaini,au fanyeni maandamano ya wafanyakazi asiogope mtu si unaona chuo kikuu wameandamana suluhu imepatikana nyinyi mnasubiri nini.

    ReplyDelete
  6. Hapo Movenpick inaonekana kuna tatizo kubwa sana la "morale", mahusiano kati ya manejimenti na watu wa chini si mazuri, hilo ndilo linataka litafutiwe ufumbuzi, kama kuna vibaka kati ya wafanyakazi inabidi manejimenti itumie mbinu nzuri kuelimisha wafanyakazi wote na wale vibaka wafanyiwe mfano adhabu. Maslahi ya wafanyakazi hodari yasipuuzwe kwa kujumlishwa na wale wabovu. Na hii manejimenti kutoka nje inabidii ielimishwe kuhusu mila na tabia za Mtazania. Na kuhusu mawasiliano kati ya wageni na wenyeji nafikiri suala la lugha litiliwe makazo kwani kuna uwezakano wa ufinyu wa uwelewaji wa lugha mdogo mtu akafikiria ametukanwa sana kumbe siyo hivyooo!! Namnukuu mwandishi "you casual if yo still my money, I will fuck you up". Sehemu ya kwanza ya sentesi ina matatizo kimuundo,lakini kama nitajitahidi kutafasiri ninavyohisi maana yake "Unakawaida ya kuiba,ukiiba pesa tena , nitakushughulikia". Sasa hili neno la " I will fuck you up" ndilo naona lawachanganya hawa watu wa Bongo, mimi silioni katika mantiki ya tusi la nguoni, huo ni msemo tu wa kutilia mkazo tishio lake. Kuna maneno kama hayo mfano "I will fire your ass" ambalo si tusi. Au " Get your lazy butt up to work".

    Anyway, nawatakia kila la kheri kutatua tatizo hilo kwa amani bila ya kupelekana mejela.

    Mdau

    ReplyDelete
  7. WEWE ANONI HAPO JUU NENO YOU CASUAL KATIKA MAMBO YA KAZI HASA WESTERN ENGLISH-USA, NI MFANYAKAZI ASIYE AJIRIWA NA HANA MKATABA KWA KIFUPI NI KIBARUA. CASUAL WORKERS, upo hapo? acha kiingereza chako cha form six hicho YOU CASUAL ETI ULIYE ZOEA KUIBA TETETETETEEEEEE!

    ReplyDelete
  8. haya mambo siyakibauguzi.ni kweli kuna watu wana abuse positions zao. mimi ningeshauri sana mambo kama haya mutumie mbinu za kupata shahidi na hasa kwenye
    kipindi hichi kigumu..kama kuna mtu yeyote anahitaji vifaa vya kurikodi mambo kama hayo kisiri kuna vifaa nnavyo naomba nitonyeni...tunataka rushwa ipotee..kwani ni adui wa taifa....

    ReplyDelete
  9. Washikaji nilikuwa bwiii tangu Ijumaa, hivi Misri na Ghana wametoka ngapi ngapi. Nasikia Ghana kampiga Mwarabu tatu mtungi?

    ReplyDelete
  10. HAPO ZAMANI ZA KALE PALITOKEA TAJIRI MMOJA GIRIKI KUTOKA VISIWA VYA CYPRUS,SIKU MOJA KATIKA VIKAO VYA BRANDY PALE SKY WAYS HOTEL{TANCOT HOUSE},AKAJI GAMBA KUWA SERIKARI YOTE YA TANZANIA KAIWEKA MFUKONI KWA PESA ZAKE,MEZA YA JIRANI SHUSHU AKAINYAKA VUUUUUUUUU!MPAKA KWA MWALIMU WEEEEEE!CHAMOTO ALIKIONA KEKO AKAWEKWA SELO MMOJA NA WAFUNGWA WA KIUME,KAOMBA MSAMAHA MPAKA KACHEZA BUZUKI WAPI JOMO KENYATA RAISI WA KENYA AKAMWOMBEA MSAMAHA,MWALIMU AKMWAMBIA KENYA NAKUHESHIMU USINIINGILIE,MPAKA ASKOFU MAKARIUS RAISI WAKE AKAMTUMIA UJUMBE MWALIMU KUOMBA MSAMAHA,ALIMSAMEHE KWA HESHIMA YA BABA ASKOFU,KWA SHARTI AKIMTOA KEKO MOJA KWA MOJA KWAO NA ASIKANYAGE TENA AFRIKA.MSIJALI MUDA SI MREFU ATASHUGHULIKWA KWA KUNYANYASA WANANCHI.

    ReplyDelete
  11. kulikuwa na jamaa mmoja akajiita OSAMA kwa kutukana watu wanamzaa sababu ni vibarua pale ok plast, wakubwa wakamtupilia nchi gani sijui ya wareno huko africa/kati/south ili kunusuru biashara na aibu kama hii!
    hawa jamaa wakija huku wanajiona kama miungu wakati ukiskia story zao huko wanakotoka masikini wa kutupwa! wanaletana huku na kupeana vyeo kwa vyeti fake!

    ReplyDelete
  12. mdau wa tatu umenena. mie sipendi nikikuta maneno mwarabu, mhindi, muasia, nk. mbona sie hatupendi kuitwa waswahili?

    ReplyDelete
  13. Tatizo lugha mbantu ukiambiwa neno fuck up!! Unapitiliiizaa! Umaona jamaa anania mbaya nami! Tena mwarabu!.... Fanyeni kazi mambo ya "SU"(mashirika ya umma) yatoweka sasa! Ama kweli JKT irudi tu.

    ReplyDelete
  14. Jamani wadau, swala nzima la kuaanza kuitana kwa majina eti yule mwarabu, au kale kazungu, hatutafika mbali.
    ni bahati mbaya sana kwamba kijana amejikuta amepakizwa matusi na "bosi" wake. lakini sijaona sehemu ambaye inaonyesha makosa aliyekosa yeye "Mswahili"?
    Katika mazingira ya kikazi hasa pale tunapokuwa na wadau kutoka ughaibuni tujifunze kushirikiana nao na kuwaelewa.

    Lakini tatizo la wadau wengine bwana ni kwamba akikosea hataki kuambiwa tena ukute huyu kijana ni mzembe kupita kiasi na sasa anatafuta namna ya kupata "cha Juu" kupita matusi aliyepewa kutokana na uzembe wake.
    Mwambie akue na ujifunze kufanya kazi kwa uadilifu!!!

    ReplyDelete
  15. UKWELI WA MAMBO WENGI WA WAFANYAKAZI WA KIGENI WANAWANYANYASA SANA WAFANYAKAZI WAZAWA,WAKITUMIA KIGEZO KUWA WATANZANIA WANA UPOLE WA KONDOO, MBONA WANAPOKWENDA KWENYE NCHI NYINGINE ZA KIAFRIKA HAWAFANYI UPUUZI KAMA HUO. KAMA NIMEIELEWA VIZURI HIYO HABARI NI KUWA HUYO MWARABU AMEMTIMUA KAZI HUYO KIBARUA KWA KUMTUHUMU MWIZI BILA HATA YA KUMPA HAKI YAKE YA MSINGI YA NATURAL JUSTICE YA KUSIKILIZA UTETEZI WA KIBARUA HUYO,PILI AMEMDHALILISHA MBELE YA WAGENI NA WAFANYAKAZI WENZAKE KWA KUMFOKEA, KWA HIYO HUYO KIJANA NI HAKI YAKE KUPELEKA SUALA LAKE KWENYE VYOMBO VYA SHERIA, KWA MATUKIO YA AINA HIYO YANAYOTOKEA MOVENPICK TUTAANZA KUYAKUMBUKA MANENO YA MWALIMU NYERERE KUWA UBEPARI NI UNYAMA!!

    ReplyDelete
  16. Allah SWT, Katujaalia makabila (mataifa) ili tujuane tu na mbora kwetu sote ni kwa yule anaemtii Allah swt kwa kuzifuata amri zake natoa nasiha kwa pande zote mbili 1). alie na kiburi aache kiburi kwa kunyanyasa watu kwani kwa Allah swt wote ni sawa kwake hamna ubaguzi akiwa mwarabu au asie mwarabu 2). na hawa wanatumia ubaguzi kwa kusema mwarabu pia waache maneno kama haya hayana faida ili kuzidisha chuki baina ya jamii na ubaguzi tu, kwani yote unayoyafanya binaadam kesho utakwenda kujibu mashtaka kwa Allah swt. na la mwisho anaepokea na anaetoa rushwa basi ameelaniwa na Allah swt. unaweza ukafanikiwa Duniani jee kesho akhera utafanya nini utakaposimamishwa na Allah swt kujibu kosa lako. kwa hivyo kwa yoyote asidai haki yake kijaahil kwa kusema mwarabu huyu kanifanya hivi au hivi ila adai kwa njia za sheria kwa kusema mimi huyu kanidhulumu hichi na hichi. shukran Abdulaziz.

    ReplyDelete
  17. Guys kuweni serious na kazi, tuache upumbavu hapa, hasa haya mambo ya kijinga ya kupelekana polisi.
    Mwenye mamlaka ya kufungua kesi mahakamani ni idara ya polisi, kwa niaba ya serikali au mwanasheria wa serikali au wakili na sio mlalamikaji.
    kama idara ya polisi, imeona hakuna haja ya kufungua kesi na imeomba kesi iishie ilikotoka ni kigezo tosha kwamba ushahidi ni finyu kudhibitisha mashtaka au kushinda kesi.
    Kwanza huyu mfanyakazi alitakiwa awe amefukuzwa kazi kwa kutokufuata sheria na ngazi za kazi pindi matatizo kama haya yanapotokea.
    jamani tujiulize kama wewe ukimtukana mtu au ukitukwanwa matusi ya nguoni basi lazima iwe kesi na lazima iende mahakamani hata kama polisi wamesema haya yaishe , au msameheane?
    Nyinyi Movenpick nilishawaona toka mwanzo mnalalamika ujinga tupu tena ushuzi na sasa mmedhibitisha hili wazi kabisa.
    Ndio maana nchi haiendelei kabisa, kwani hii ni kuharibu sifa ya hiyo hoteli nchi za nje, na mtakosa soko na mtakuwa hamna kazi nyinyi wenyewe.
    Nilishasema muondoke tu hamna lolote, mfukuziliwe mbali, ili mkaandamane ikulu mpigwe virungu.

    ReplyDelete
  18. Nyie wafanyakazi kama hamumtaki huyo Shousha mngejiunga wote mgome. Kaeni nje wote msifanyekazi hadi huyo Shousha aondoke. Hivyo kuandika tuu, kuandika tuu hakutasaidia. Mngeamua moja. Mngoeni katika hiyo Hotel.

    ReplyDelete
  19. ooo yes we will call them names tupendavo,mbona kwao wanatuita majina meengi tu ya dharau kubwa

    ila hii hotel wala sitakanyaga maana mmenitoa stimu kbs,izi tabia za kishenzy za waajiri tena mwarabu

    poa tu

    ReplyDelete
  20. JAMANI TANZANIA HATUJAFIKIA HATUA YA KUTUKANWA HIVYO KWENYE KAZI,TENA MBELE YA WAGENI,NYIE MNAOUNGA MKONO HAYA MATUSI AU MANENO YA KASHFA NA WABEBA MABOX HUKO ULAYA KWENU NYIE SAWA TU SI MNABEMBELEZA ILI MUENDELEE KUISHI HUKO,SISI HAPA KWETU HATUKO TAYARI KWA HILO NA TUTAENDELEA KUWAPELEKA POLISI TU...POLENI KWA MATUSI MNAYOPATA ILA SIWALAUMU SANA KWANI BADO MNAO USWAHILI NA MNATIMIZA MOJA YA NGUZO ZAKE YA MTAKA CHA UVUNGUNI.....

    ReplyDelete
  21. eeeh mungu naomba unisamee ilaa hawa viumbe kama kuna mwanadamu mjinga na mabae hajuiii ginsi ya kuishi na watu wengine ni mwaraabu.mwaraabu mbaguzi kuliko hata makaburu a.k.a mzungu.heshima kitu cha bure hata kama wee ni boss jua kwamba huo mfanyakazi pia ni binadhamu ka ww.mzungu mjanjaa maana hawezi kutukana hivo afu hadharani kwa sababu sheria zao zina nchaa kali naa anajuaa ukimburuza mahakamani lazima umfilisi na kiji hoteli chake so full respect inakuepo.buruza hilo taka mahakamani afu akitiwa hatiani pokonya kibali cha kuishi hapo residence maana utakua umecreat kazi kwa mzawa.ni hayo tu

    mdau kigali makzi boksini

    ReplyDelete
  22. Tatizo hili la unyanyasaji mbona sio movenpick peke yake ?

    Hawa wanaojiita ma expatriate hii ni kawaida yao kuja na ku abuse wananchi kwa kutumia loop hole za u- expatriate.Hasa huyu wa movenpick yeye anajifanya ndio ajent wa wanyanyasaji wenzake anatumia visenti yake kuhonga anatumia ma agent wa mtaani kumpatia kupata vibali vya kuendelea kufanya kazi nchini.ukweli hata vyeti vyao ni duni tunao watanzania kibao wenye uwezo kufanya kazi zao kwa ufanisi ila wanatunia udhaifu wa sheria zetu kutunyanyasa iwenye amalize muda wake halafu aongezewe muda tena just for changig his position ....hali tunao watanzania wenye uwezo ?

    ReplyDelete
  23. Hakuna sheria ya mwajiri kumtukana kibarua au mwajiriwa yeyeto hilo muelewe nyie mnao kurupuka nakusifia huyo muharabu kutukana matusi hadharani.

    Tena anamakosa sana ameitukana jamuhuri!

    Kama huwa mnatukanwa na waajiri wenu na mkasema "asante au pole boss" ni nyie tu na umbumbumbu wenu, huku wenzenu hatutaki kabisa upuuzi huo.

    Muharabu ajue kutukana mwajiriwa sio suruhisho. Na hao wanaopokea mrungura ipo siku zitawatokea puani we ngoja. Jitahidini kumshauri huyo muharabu aliekosa nidham na asiyejua administration kwa ujumla aende upya darasani.

    Kama huko kwao matusi kazini ni sehemu ya kazi bongo sivyo.

    ReplyDelete
  24. (1)Mtu akikutukana, ashitakiwe; lakini isiwe ndiyo sababu ya kueneza chuki za kikabila na kidini ambazo zimo ndani ya nyoyo ya baadhi ya binaadamu wanaongoja tu wapate sababu na fursa za kuzitapika chuki zao hadharani. Mandela, Nyerere na Reverand Martin Luther King waliotumia maisha yao wako sawa : "Fight the racist, not the race". (2) Sisi wazawa pia tuonyeshe mfano bora kwa kutendeana haki wenyewe kwa wenyewe; katika ajira, polisi, mahakama, n.k. (3) Kusoma Injili kunaweza kusaidia kuondoa utata wa "Nani alaumiwe: mkosaji au kundi lake lote?" Wote mnaosoma makala hii mbarikiwe.

    ReplyDelete
  25. nimeona watu wengi wanajaribu kurekebisha lugha aliyoitumia mr shousa kiukweli sio tatizo la uelewa kokote kule ulimwenguni kuna rights za employer na employee moja wapo ambayo ni global maana ipo nchi yeyote ile ni kuheshimiana... na maana ya kuheshimiana pia ni kuchagua lugha za kutamka hata kwenye nchi zilizoendelea swearing is prohibited especially kama mtu anakufokea kama hivyo maana kwenye story za kawaida haina neno ila ikifikia hapo lazima mtu atakimbilia kwenye vyama vya wafanyakazi na hata tribunal na kudai fidia au re instatement.. mimi sidhani kama tatizo ni uelewa kabisa, huyo mtu kajaribu njia zote mpaka kwenda HR ila inaonekana huyo shousa anaogopwa hata na ma director wenzie sasa aende wapi ? akapigane nae? haki yake ataipata mahakamani na kuna anony mmoja amesema kama polisi wamesema wakamalizane basi hamna ushahidi na anatakiwa a withdraw hiyo kesi sio kweli hata yeye ingawa sio mwanasheria anaweza kumtuhumu mtu na shauri likaenda mahakamani ila polisi wanaweza kukushauri kutokana na kama ukishindwa unaweza daiwa fidia .... ni hayo tu waungwana

    ReplyDelete
  26. sasa ikiwa wewe ni mfanyakazi wa kuhudumu tena ni mwenye wadhifa ya chini kabisa .umechukua madaraka ya kumhukumu meneja wako. unaonekana kuwa hiyo kazi huiwezi nakushauri katafute kazi ya ukubwa unaonekana unataka kazi ya uongozi. lakini kumbuka kuwa uongozi una maadui wengi unataka ustahmilifu mkubwa ambao ni subira. MWARABU

    ReplyDelete
  27. HAKUNA KITU KIBAYA DUNIANI KAMA KIBURI TENA KIBURI AMBACHO CHA MTU MJINGA. SASA WATAPATAPA NA WATAFUTA WAFUASI UWALAGHAI NA IKIWA NI WAJINGA KAMA WEWE UTAPATA WENGI MASHABIKI AMBAO WENGI NI WASHANGILIAJI WAPIGA DEBE LA KUVUMA BILA KUZAA MATUNDA.

    ReplyDelete
  28. I really think it is becoming a big issue for the past 3 days. are we sure of all the infomration we hear? i look at the positive and negatives and I am not really sure of this guy? was he really sweared at? was he really stealing? is he trying to make some money? big question marks for me? and need answers from brothers.

    ReplyDelete
  29. I am Tanzanian and I am in the USA and I can say something, we have dignaty and pride and we shouldn't leave our rights brothers but also we have to see our mistakes it is not good for anybody to prove we are what they say about us, that we steal and we are lazy at work place. but we can not get all emotional here. I agree to find out the truth and who is wrong. did the brother is trying to save his dignaty or he is just trying to cover somthing? can the police investigate this to see the witness? is it really he is inocent? and why this shoshan acuse him? does he know him? is this shosha someone who treat tanzanian with bad intension? or he is just doing his job? I search hom on the net and he seem not bad and he want to help tanzanian. we just have to be sure to protect our reputation as tanzanian.

    ReplyDelete
  30. I work with shousha in the hotel and I say he is a good guy and trying to help all. we make more money because of the service charge and he is working hard he defend our money by some bad employees who steel our money and they take it for them self why we acuse him of hate tanzanian now he is working for 3 years now and he was always good with us and support us, why now we say he is arab and bad. i write in English to support him and say that we are 300 emolyees some are bad but many are good and we are support him and we tell him we are with you you are fare man. please who are steal money I ask you to stop this way, you are hurting us all and our reputataion as tanzanian, we are not stealers and you make all look bad you are gangs and what you do is bad shousha we ask you to catch all stealer and clean the hotel we are honest and you help the hotel to get more busnes and guests so we can make more money i want my children to have better future and be honest mens you are working so hard and we want to learn from you.

    ReplyDelete
  31. now that the investigation is over and the Shousha is innocent and no witness with the brother was true I say what is happen is wrong. this is the reputation of us Tanzanian and it is not good to look liars. and to all brothers we have to stop the steeling because it comes from our money because they are not stuiped they take the stolen things from our money. please stop the lay and the steal we are Tanzanian and good people we have to prove this way. the manager befoe was not good and now we have a good manager and he is fair so we have to be good and stop going after people who are trying and trying to push us to do wrong things because they want to make troble and make money from us. I say we have to work hard and come down and do our job good. we should not make 3 or 4 poeple push our thoughts and our actions because at the end they are not good tanzanian people.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...