Mwenyekiti Abdulrahaman A.Alli (shoto) akiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh.J.Bendera baada ya mazungumzo.

Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Mh.Abdulrahaman A.Alli alipata nafasi ya kumtembelea waziri Bendera nyumbani kwake,mwenyekiti alikuwa na mazungumzo marefu na Naibu waziri Bendera.
Mwenyekiti na naibu waziri walijadili jinsi ya kukuza vipaji vya michezo kwa vijana wa kitanzania wenyenye umri mdogo kwa kushirikiana kati ya Tanzania na Italia.

Pia katika mazungumzo hayo walijadili juu ya kuutambulisha utamaduni wa kitanzania nchini Italia pamoja na utalii. Vilevile mwenyekiti aliongea na waziri juu ya uwezekano wa kuwapa nafasi wasanii wa fani mbalimbali kutembelea Italia na kupata ubunifu zaidi na kuongeza masoko ya kazi zao.Waziri Bendera aliahidi kushirikiana na jumuiya ya watanzania Italia katika kufanikisha mikakati hiyo.
Toka shoto ni Mjumbe wa jumuiya ndugu A.Bendera,katibu wa jumuiya tawi la Napoli ndugu J.Mandai, Mjumbe wa jumuiya upande wa kina mama Bi Fatma Tandika, Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italia Mh.Abdulrahaman A.Alli

Jumuiya ya Watanzania Italia leo ilishiriki katika sherehe za canival zilizoandaliwa na Manispaa ya Villaricca-Napoli (Comune di Villaricca). Mwenyekiti aliwashukuru wote waliohudhuria na kusema kuwa hii ndio njia mojawapo ya kuonyesha ushirikiano na wenyeji wetu.

Pamoja na shukrani za mwenyekiti kwa watanzania waliohudhuria pia mwenyekiti alisikitishwa na mahudhurio madogo ya wadau.

Mwenyekiti alimaliza hotuba yake fupi kwa kuwataka watanzania kujitokeza zaidi pindi inapokuwepo sherehe za kitaifa kwani ushirikiano na wenyeji ni jambo la muhimu ili na sisi tupate fursa ya kutangaza nchi yetu na utamaduni wa kitanzania.

Mdau Kagutta N.M

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. angalau mngeonyesha watu ktk iyo jumuiya...

    na ao kina bendera mh!!naibu vekesheni nini?

    ReplyDelete
  2. mh viongozi wa jumuiya mh!!!

    mayb ndo sababu wau hawaonekani jumuiyani

    ReplyDelete
  3. Ni vema mgetoa link yenu ili wadau wa globu ya jamii waweze kuwasiliana nanyi, au ni lazima kupitia kwa Mh. Naibu Waziri?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...