
FAMILIA YA MAREHEMU ALHAJ RASHIDI MFAUME KAWAWA INATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA; MHE. DKT. ALI MOHAMED SHEIN, MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA; MHE. AMANI ABEID KARUME, RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR; MHE. MIZENGO PETER PINDA , WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA; CHAMA CHA MAPINDUZI, NDUGU GEORGE YAMBESI, KAIMU KATIBU MKUU KIONGOZI WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (MWENYEKITI WA KAMATI YA MAZISHI) NA WAJUMBE WAKE, WANANCHI WOTE WATANZANIA WALIOKO NDANI NA NJE YA NCHI, JAMII YA KIMATAIFA NDANI NA NJE YA NCHI, MADAKTARI NA WATUMISHI WOTE WA SEKTA YA AFYA WA NDANI NA NJE YA NCHI , VYOMBO VYA HABARI VYA NDANI NA NJE YA NCHI, VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, MASHEIKH, MADHEHEBU MENGINE YOTE YA DINI NA VYAMA VYOTE VYA SIASA VYA UPINZANI NCHINI KWA MISAADA NA HUDUMA MBALIMBALI YA HALI NA MALI WALIYOITOA WAKATI WA KUMUUGUZA MZEE WAO MAREHEMU RASHIDI MFAUME KAWAWA HADI KIFO KILIPOMCHUKUA DISEMBA 31, 2009 KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI NA WAKATI WA MAZISHI YAKE YALIYOFANYIKA KWA HESHIMA ZOTE JANUARI 2, 2010 MADALE, DAR ES SALAAM.
SI RAHISI KUTAJA MAJINA YA WOTE WALIOWAFARIJI WAKATI WA MSIBA WA MZEE WAO ILA FAMILIA INATOA SHUKRANI ZAKE ZA DHATI KUPITIA SALAMU HIZI KWA KILA MMOJA WENU ALIYESHIRIKI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KUWAFARIJI WAKATI WA MSIBA MKUBWA WA MZEE WAO.
FAMILIA INAWAKARIBISHA WOTE KATIKA HITMA/AROBAINI YA MAREHEMU MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA ITAKAYOFANYIKA JUMAMOSI TAREHE 6 FEBRUARI 2010 SAA 7 MCHANA NYUMBANI KWAKE MADALE, DAR ES SALAAM.
MUNGU AILAZE ROHO YA
MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
AMIN.
INNAH LILLAH WA INNA ILLAHI RAJJIUN.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...