Mkurugenzi wa Bwagamoyo Sound, Muumini Mwinjuma (shoto) akiimba na kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta, Lwiza Mbutu wakati bendi ya African Stars ilipofanya onyesho maalum la "Usiku wa kurudi nyumbani" lililowashirikisha wanamuziki wa zamani waliowahi kutamba na bendi hiyo akiwemo Banza Stone. Onyesho hilo liliandaliwa na Kampuni ya First Entetainment na kufanyika katika ukumbi wa Koyanga uliopo Kiwalani jijini Dar usiku kuamkia leo
Home
Unlabelled
usiku wa kurudi nyumbani wafana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Barabara! Mwinjuma Muumin (MM), Mungu kakujalia sauti.
ReplyDeleteNakupongeza pia kwa kulinda viungo vyako vinavyokuwezesha kuitunza sauti yako maana wewe si mlevi (mvutaji wala mnywaji) kama walivyo wasanii wengi.
Nadhani bado tu hujapata meneja / mshauri mzuri wa kukusaidia katika maendeleo yako ndani ya fani hii ya muziki.
Jitahidi utulie na upange mikakati yako vyema katika mwaka huu 2010 na kuendelea na Mola atakujalia.
Kuhusu Lwiza (shemeji yako) sina cha kusema zaidi ya kumtunuku kwa jinsi anavyoendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa kujali kazi yake na kujituma kwa moyo wote.
Nyote mna taranta hadimu! Ingawa tuko mbali nanyi tunawaombea sana.
Nilifurahi kuongea kwa simu nawe MM ulipokuwa na Banza Stone hivi karibuni huko kanda ya Ziwa.
Kazi nzuri, Hongereni sana.
ReplyDeletekazi safi sana,kamatieni hapo hapo.
ReplyDeletewadau FFU