Hello Ankaaaal, mzee wa libeneke

Napenda kuchukua nafasi hii, kukutumia picha za gari uniwekewee tangazo kwenye Globu yetu ya Jamii ambayo sio tu haina mshindani bali pia ni mkombozi wa wadau wa aina yoyote kuanzia JK hadi mdau wa Mwananyamala kwa Kopa. Hubagui, huchagui...Hongera Ankal!

Gari pichani, aina ya Toyota SIENNA, ya mwaka 1998, inafaa kwa familia inabeba abiria 7. ipo katika hali nzuri kama unavyoiona imetembea km 156,000.kwa yoyote atakayehitaji wasiliana kwa namba zifuatazo muda wowote ule we piga tu ama tuma SMS.

0755 364656
au
0712 968490

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. ebu na wewe tangaza biashara yako sio kumpaka ankal mafuta kwa mgongo wa chupa. michuzi, uchumi unao, unaukalia tu!

    ReplyDelete
  2. Utakufa masikini Ankal.huyo jamaa alitakiwa alipe tangazo na sio kukupamba tu ili aruke bure kutangaz biashara yake

    ReplyDelete
  3. Mdau ungetupa na bei kabisa ili ambao hatuwezi dau tusipoteze vocha.

    ReplyDelete
  4. DOOOO IMEZUNGUKA DUNIA ZAIDI YA MARA TANO, GARI NI ENGINE SI UZURI WA MUONEKANO WAKE.

    ReplyDelete
  5. Afrika bwana. Sasa kwa nini muuzaji asiweke wazi specs? Automatic/ manual transmission? Power locks/ power window? na upukupuku wote na bei! Make it easier kwa watu. Ili anayepiga simu ni serious buyer siyo wapiga mdomo tuu. Maana utapotezewa muda wa kujibu maswali ambayo yangejijibu yenyewe kwa kuweza specs za gari mtandaoni! Please update the information ili tukupigie simu

    ReplyDelete
  6. Mtaingia choo cha kike kimeo hicho, mwenyewe kishamshinda anataka awaingize mjini kati ha ha ha!! bongo bwana ka niuyeki vile

    ReplyDelete
  7. Kwani mwananyamala kwa kopa kuna nini? Kunguru jike wewe. Acha dharau hata wanaoishi huko ni binaaadamu tena wenye maana kuliko wewe.

    ReplyDelete
  8. Inamaanisha JK yuko juu sana na mtu anyeishi mwananyamala kwa kopa yupo chini saana, kama sijakosea. NI Maoni tuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...