Mtangazaji Mashuhuri wa Tanzania Susanne Mungy akimfunda mtanzania Lilian Mduda anayeshiriki fainali za Mnet Face of Africa 2010 jijini Lagos. Binti huyu anatabiriwa na wengi kushinda shindano hili, na hata asipofanikiwa imeelezwa na wengi kuwa kwa alipofikia tayari ameonekana na wabunifu wengi wa mavazi waliofurika jijini Lagos na huenda akawa mmoja wa watakaofanikiwa kwa mwaka huu. Fainali za Mnet Face of Africa ni leo Jumamosi saa 3 usiku kwa saa za bongo kipitia channel ya Mnet. Usiku kuamkia leo kulikuwa na mnuso ulioandaliwa na Gavana wa jiji la lagos, Mh. saana Bw. Babatunde Raji Fashola (SAN) katika Hotel ya Eko Hotel Grand Ballroam kuwapongeza washiriki kumi waliofanikiwa kuingia fainali hizo. Lilian alishangiliwa sana jana alipotambulishwa kwa waalikwa wa mnuso huo wa Gavana.
Lilian akizungumza na CEO wa Multichoice Tanzania
Bw. Peter na mai waifu wake wakati wa mnuso huo.
Lillian akipozi na mdau Innocent na Suzzane Mungy
ambao nao wako Lagos kushuhudia fainali hizo za M-Net usiku huu
Mdau Innocent Mungy na mai waifu wake Suzanne
wakiwa na CEO wa MultiChoice Tanzania na mai waifu wake






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. na huku kama kwenye soka tu mrembo wetu ameshindwa kuingia tano bora ila analipa makapuni ya bongo mtumieni ili tusiue vipaji vya wadogo zao

    ReplyDelete
  2. Yaani hao waliomfunda hawakumpa cat walk skills, manake hakuwa akitembea kama modo anavyotakiwa kutembea on the cat walk na hicho ndicho kilichomuangusha. Otherwise nnampa hongera kufika finali.

    ReplyDelete
  3. KAMA MASHINDANO YAMEISHA ARUDISHWE CHUO MAPEMA KESHO(j3)MITIHANI INAANZA!!!

    ReplyDelete
  4. Mungi (Inno)fanya mazoezi bwana. Wewe bado yanki. Na pesa za Gym hazikushindi. Usijiachie.

    ReplyDelete
  5. Brother Mungy na Da Suzy mumependeza sana.

    Good to see you!!!

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  6. Hey Suzy and Innocent.. red carpet huh?..!..lookimng great and relaxed.Keep it up!
    T..Bonn

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Lily, mbali na kwamba hujashinda lakini hapo ulipofikia tayari umepiga hatua kubwa sana, na umeiwakilisha vyema nchi yako,kwa nidhamu ya hili ya juu uliyoonyesha,hongera sana..Mungu akuongoze uweze kumudu masomo yako vyema.

    ReplyDelete
  8. Duniani kweli hakuna mtu mwembamba, namkumbuka Suzan Mongy alipokuwa anatagaza ITV, alikuwa mwembamba kweli ,asa hivi tofauti

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...